ESRF YAKUTANISHA WADAU KUIJADILI BAJETI YA 2016/2017 KATIKA SEKTA ZA ELIMU NA KILIMO
Taasisi
ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) imewakutanisha wadau mbalimbali
wa maendeleo nchini kuijadili bajeti ya Tanzania ya mwaka wa fedha
2016/2017 ambao unaelekea kuisha.
Akizungumza katika mkutano huo,
Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt. Tausi Kida alisema mdahalo huo ni
sehemu ya shughuli ambazo zinafanywa na ESRF ili kutazama ni njinsi gani
Taasisi inaweza kuisaidia Serikali kuweka mipango thabiti kwa ajili ya
maendeleo ya nchi.
Dkt. Kida alisema mdahalo huo ulihusu bajeti
ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia kwa kuangalia utekelezaji wa bajeti zilizopitishwa kwa mwaka
wa fedha 2016/2017, changamoto zilizopo na nini kifanyike katika bajeti
ya 2017/2018.
Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt. Tausi Kida akitoa neno la ufunguzi.
“ESRF
imekuwa ikishirikiana na wadau ili kuangalia ni jinsi gani tunaweza
kusaidia mchakato wa maendeleo wa nchi yetu kwa njia ya utafiti
mbalimbali, uchambuzi na utayarishaji wa sera na kuongeza wadau uwezo
kupitia mafunzo mbalimbali.
“Kama jinsi mnavyojua nchi yetu
imekuwa na mipango ya maendeleo ambayo inatekelezwa kupitia bajeti kwa
kuangalia mambo yenye umuhimu kwa Taifa, bajeti imekuwa ikipangwa kila
mwaka kwa kuzingatia maeneo ya kuyapa kipaumbele ili kuleta maendeleo
kwa nchi.” alisema Dkt. Kida.
Kwa upande wa mtoa taarifa ya
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Joviter Katabaro (Mkufunzi
katika, shule ya Elimu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam) alisema pamoja na
serikali kutoa elimu bure katika ngazi fulani ya elimu nchini lakini
bado kuna changamoto mbalimbali katika elimu ambazo zinahitaji
kutafutiwa ufumbuzi katika bajeti ya 2017/2018.
Mhadhiri
Mwandamizi wa Shule Kuu ya Elimu Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Dk.
Joviter Katabaro akitoa taarifa kuhusu Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia.
“Pamoja na jitihada kubwa ya Serikali katika elimu
bado kuna upungufu wa majengo 10,000 ya shule nchini kitoke, kuna
upungufu wa maktaba 15,000, vyoo bado havitoshi,” alisema Dk.
Katabaro.
Kwa upande wake, Prof. Haidari Amani (Mtafiti Mshirki
mwandamizi ESRF) ambaye alitoa taarifa kuhusu Wizara ya Kilimo, Mifugo
na Uvuvi alisema pamoja na sekta ya kilimo kuwa na changamoto ambazo
zinajitokeza serikali inatakiwa iweke mfumo mzuri kuanzia wakulima
wadogo ili waweze kunufaika na kilimo ambacho wanakifanya.
Mtafiti Mwenza wa ESRF, John Shilinde akitoa taarifa kuhusu Bajeti ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
Mtafiti Mwenza Kiongozi wa ESRF, Prof. Haidari Amani akijibu maswali ya baadhi ya washiriki waliohudhuria.
Mkurugenzi
Mtendaji wa ESRF, Dkt. Tausi Kida akifafanua jambo wakati wa kuijadili
bajeti ya 2016/2017 katika sekta za Elimu na Kilimo.
No comments:
Post a Comment