Waziri wa Maliasili na
Utalii,Prof.Jumanne Maghembe (katikati) akizungumza na wananchi kwenye
siku ya kilele cha Maadhimisho ya miaka 110 ya vita vya Maji Maji na
uzinduzi wa Makumbusho ya Hayati Rashidi Kawawa yaliyofanyika mkoani
Ruvuma katika wilaya ya Songea. Wengine ni Mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Dkt.
Binilis Mahenge ( wa pili kulia) Mbunge wa viti maalum wa Ruvuma,
Jacquiline ngonyani ( wa kwanza kulia) Balozi wa Ujerumani nchini
Tanzania, Egon Kochanke ( wa kwanza kushoto) pamoja na Chifu wa wangoni,
Emanuel Zulu (wa pili kushoto) .
Waziri wa Maliasili na Utalii,
Prof.Jumanne Maghembe akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Dkt. Binilis
Mahenge wakiangalia baadhi ya Nishani alizokuwa akitunukiwa Dkt. Rashid
Mfaume Kawawa katika kulitumikia taifa kwa uzalendo mara baada ya
kuzinduzia jana Makumbusho ya Hayati Rashidi Kawawa yaliyofanyika mkoani
Ruvuma katika wilaya ya Songea.
Balozi wa Ujerumani nchini
Tanzania, Egon Kochanke akiweka taji kwenye mnara wa kumbukumbu ya
mashujaa waliouawa kwa kunyongwa na wakoloni kwenye siku ya kilele cha
Maadhimisho ya miaka 110 ya vita vya Maji Majiyaliyofanyika mkoani
Ruvuma katika wilaya ya Songea.
No comments:
Post a Comment