Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Ndg. Athumani Kihamia akitoa maelekezo wakati wa Kikao cha Baraza la Madiwani
- Mstahiki Meya wa Jiji Mhe. Kalisti Lazaro(kushoto) akiteta jambo na Naibu Meya wa Jiji Mhe. Viola Lazaro Likindikoki wakati wa Kikao cha Baraza.
Madiwani na wataalam wakifuatilia kikao cha Baraza la Madiwani robo ya Pili.
Afisa
Utumishi Mkuu wa Jiji. Ndg. Baltazari Ngowi(Kushoto) akiwa na Kaimu
Mwanasheria wa Jiji Fabiola Kisarika wakati wa Kikao cha Baraza.
Katibu
wa Mwenezi wa CCM Arusha Mjini Gasper Kishumbua(kushoto) akiteta jambo
na Katibu wa Chadema Wilaya ya Arusha Innocent Kisanyage wakati wa Kikao
cha Baraza (kulia).
………………………………………………………….
Nteghenjwa Hosseah, Arusha
Kikao cha Baraza la Madiwani Jiji
la Arusha kilichoketi kwa robo ya pili kwa mujibu wa kanuni kimepitisha
taarifa mbalimbali za shughuli za maendeleo, kuidhinisha mapendekezo ya
Sheria ndogo za Jiji za mwaka 2006 pamoja kupokea taarifa mbalimbali
kutoka kwa Taasisi za Serikali zinazotoa huduma kwa wananchi wa Jiji la
Arusha.
Akifungua Kikao hicho Mstahiki
Meya wa Jiji la Arusha Mhe. Kalisti Lazaro amewataka wajumbe wa Kikao
kuwa makini katika kujadili na hoja mbalimbali zilizowasilishwa katika
Baraza ili kuweza kuleta Tija kwa wananchi wa Jiji na wanaotegemea
kupata maendeleo kupitia vikao.
Naye Mkurugenzi wa Jiji Ndg.
Athumani Kihamia alisema kwa kushirikiana na Menegiment amehakikisha
kwamba maazimio yote ya vikao vya awali yamezingatiwa na miradi
imetekelezwa kwa kiwango cha juu huku thamani ya Fedha ikionekana.
Kutoka katika taasisi
zilizoalikwa katika kikao hicho Mkurugenzi wa AUWSA Eng Ruth Koya alieza
changamoto kubwa inayowakabili wananchi kwa sasa kuwa ni uhaba wa Maji
na kusema kuwa wanategemea kuanza utekelezaji wa mradi mkubwa ambao
utawezesha upatikanaji wa maji Lita Mil 200 wakati mahitaji ni Mil 94
tofauti na sasa ambapo kiasi kinachohitahjika ni Lita Mil 35 tu ambacho
hakitoshelezi hata nusu ya mahitaji ya wananchi, hivyo kinachohitajika
ni ushirikiano wa wadau na wananchi ili kuweka kufanikisha utekelezaji.
Akiendelea kujibu maswali ya Wah.
Madiwani waliyohoji maji yanayopatikana kuwa na Chumvi Eng. Koya
alisema maji ya kisima yanayopatikana Arusha kwa kiasi kikubwa yana
uwekezekano wa kuwa na chumvi kidogo lakini na hayana Flouride tofauti
nay ale ambayo wananchi wanadai ni matamu huwa ni ya yanatokana na
Chemchem ambayo hayapatikani kwa wingi na athari zake ni kuwa na
Flouride ambayo mtumiaji huwezi kuigundua kwa kunywa lakini athari zake
huonekana kwenye meno nk.
Kutoka Tanesco Mhandishi wa
Mipango na Ubunifu Eng.Beatus Rwegoshora alifafanua tatizo la kukatika
umeme mara kwa mara kuwa Tanesco iko katika maboresho ya huduma kwa
wateja nahivyo tatizo hilo litapungua na pia shirika lipo katika mpango
mahususi wa kuwafanya wananchi waweze kupata taarifa zote za msingi
kupitia simu za kiganjani ambapo huduma hiyo itawafanya wananchi
kufuatilia na kupata taarifa kwa wakati na muda wote popote walipo.
Meneja wa Sumatra Mkoa wa Arusha
Bw. Allen Mwani amesema kwa sasa Mamlaka hiyo ipo katika upembuzi
yakinifu wa mradi wa kuondoa usafiri wa daladala maarufu, ‘Vifodi’
ambazo hazina viwango katika usafirishaji wa abiria hivyo mpango uliopo
ni wadau kukaa pamoja na kuleta magari makubwa ya usafirishaji wa
abiria(City Bus) katika jiji la Arusha.
Mkurugenzi wa Fedha na Utawala
AICC Ndg. Savo Mng’ong’o aliwatoa shaka Madiwani waliolalamikia Hospital
ya Kituo hicho kutopokea Kadi za Bima ya Afya (NHIF) ilihali wananchi
wanahimizwa kujiunga na mfuko huu ili kurahisisha upatikanaji wa huduma
za matibabu kwa alifafanua kuwa huduma hiyo itarejea mwezi Oktoba.
Katika kikao hiki pia Baraza
limepitia na kuidhinisha Sheria ndogo za Halmashauri ambapo sasa
zitawasilishwa Mkoani kisha Tamisemi kwa ajili ya kuidhinisha kisha
kuanza kutumika rasmi. Sheria hizi ni muhimu sana kwa jiji kwa kuwa
zinazotumika sasa ni zile za mwaka 2003.
No comments:
Post a Comment