-Maofisa wa TFDA wakuta uzalishaji umesitishwa
Kampuni
ya TDL maarufu kama konyagi imesitisha utengenezaji za pombe kwa
kutumia vifungashio vya plastiki kwa mujibu wa agizo la serikali ambapo
mwisho wa kusambaza pombe hizo ulikuwa jana.
Maofisa
kutoka Mamlaka ya kusimamia vyakula na Madawa (TFDA) na NEMC, TRA
Pamoja na POLISI wamefika kiwandani leo na kukuta hakuna uzalishaji wa
vinywaji hivyo unaoendelea kama ambavyo kuna taarifa za kupotosha kwenye
mitandao ya kijamii zinazoeleza kuwa TDL imekaidi agizo la serikali na
imekutwa ikiendelea kufanya uzalishaji kwa kutumia vifungashio
vilivyopigwa marufuku na serikali.
TDL
siku zote imekuwa ikiendesha shughuli zake za kibiashara kwa kufuata
miongozo na sheria za serikali kupitia taasisi zake mbalimbali hivyo
haiwezi kukaidi na kuendelea na uzalishaji wa kutumia vifungashio vya
plastiki wakati vimepigwa marufuku bali inajipanga kutumia teknolojia ya
kutumia vifungashio vilivyotengenezwa kwa malighafi ya kioo ambavyo
vina ubora wa hali ya juu na salama kwa kuwa sio rahisi kuviigiza
No comments:
Post a Comment