- Tigo na Ericson wazindua maeneo ya kwanza ya 3G katika miundombinu ya ushirikiano ya GSMA inayojielekeza kuunganisha maeneo ya vijijini nchini Tanzania.
- Mfumo wa Redio wa Ericsson kwa mara ya kwanza utawapatia wateja huduma bora ya mtandao wa simu, huduma iliyo na ubora ambayo kampuni ya simu za mkononi ya Tigo imekuwa ikiitoa kwa wateja mbalimbali.
- Katika ushirikiano huu, kampuni ya Tigo itakuwa na asilimia 40 katika uendeshaji wa mtandao.
Ericsson (NASDAQ:ERIC) na mtandao
wa simu unaoendeshwa Tanzania Tigo wameungana katika kuzindua maeneo
ya minara ya mfano katika maeneo ya vijijini itakayotoa huduma za
simu kwa maeneo ya Chiwale na Mingumbi katika mikoa ya Lindi na
Mtwara ambayo yamo ndani vijijini na awali yalikuwa hayajaunganishwa.
Shughuli hiyo ni mwanzo wa
miundombinu ya mfano ya kushirikiana kunakofanywa na GSMA pamoja na
Tigo, serikali ya Tanzania na waendeshaji wawili wakubwa wa mtandao wa
simu kwa kuunganisha zaidi ya watu binafsi zaidi ya milioni 13
wanaoishi sehemu za maeneo ya vijijini hapa nchini.
Miundombinu ya kushirikiana na
kuihusisha serikali katika kupunguza kodi katika mikoa
hiyo kunawaruhusu waendeshaji kupunguza gharama za kuendesha mitandao
mipana katika maeneo ambayo awali ilikuwa haifikiwi na huduma za simu.
Tigo na Ericson zimetoa nafasi
katika ushirikiano huu kwa kuzindua eneo la kwanza linalofanya kazi
kwa kutumia mfumo wa Redio wa Ericson wa kizazi kipya wenye viwango
vingi. Seti hiyo ya suluhisho inawezesha kuwepo kwa uwezo unaotakiwa
katika kupunguza gharama za jumla za umiliki hadi asilimia 40 pindi
eneo la suluhisho la jumla kwa uwanda mpana wa simu wa Ericsson
utakapoanza kufanya kazi. Hii inafanya uwekezaji unaokuwepo katika
masoko kuwa na wastani wa chini wa mapato kwa kila mtumiaji.
Suluhisho hili litaiwezesha Tigo
na washirika wake kuweza kuyabaini kwa urahisi maeneo yasiyo na
huduma katika mkoa, kuharakisha kuanzisha au kuboresha uzoefu wa
watumiaji wengine wa uwanda mpana wa simu ndani ya jamii hizi za
vijijini. Huu ni uzinduzi wa kwanza kibiashara kwa suluhisho hilo
katika Afrika, Kusini mwa jangwa la Sahara.
Fundi Mkuu na Ofisa wa Teknolojia
ya Habari, Jerome Albou wa Tigo Tanzania alisema, “ndani ya Tigo
ni dira yetu kuongoza katika kupokea intaneti na mtindo wa maisha ya
kidijitali nchini Tanzania. Kufikiwa kwa uwanda mpana wa simu za
mkononi kutazifungua jumuia hizi za vijijini katika huduma ambazo
awali walikuwa hawazipati kama vile huduma ya fedha kwa njia ya simu,
huduma za afya kielektroniki, elimu kielektroniki, na serikali mtandao,
hivyo kubadilisha namna ambavyo watu wanacheza, kujifunza na kufanya
biashara kwa ujumla”.
Mkuu wa Ericsson Kanda ya Afrika,
Kusini mwa jangwa la Sahara Jean-Claude Geha, alisema; “Sisi ni wapiga
mbiu vinara wa mchango wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama)
katika kuwezesha utambuzi wa seti mpya na za jumla za Malengo Endelevu
ya Milenia (SDGs). Washirika wetu kwa pamoja wanatafuta masuluhisho ya
kuleta faida zinazopatikana katika teknolojia ya simu za mkononi kwa
kila mtu kwa kuunda ulimwengu ambao ni endelevu na jumuishi zaidi”.
Muunganiko huo mpya wa suluhisho
unajumuisha; program ya Ericsson inayosimamia eneo, pamoja na program ya
kudhibiti eneo, ambavyo ni Redio 2219, Redio iIiyounganishwa na
Antenna, AIR 2488, MINI-LINK 6363, MINI-LINK 6651 ambacho ni kifaa cha
ndani na nyongeza mpya kwa ajili ya kuunganisha mitambo hii ya Ericsson.
Hali kadhalika inajumuisha programu mpya iliyoboreshwa katika Zero
Touch WCDMA na masuluhisho ya mtiririko wa watumiaji
No comments:
Post a Comment