=Katika kuitikia agizo la
Serikali kuhamia Dodoma, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Mheshimiwa Ummy A. Mwalimu amefika kwenye Ofisi za
Wizara yake iliyopo eneo la Chuo Kikuu cha Dodoma, sehemu ya Kitivo cha
Sanaa na Sayansi ya Jamii na kukutana na watumishi wa Wizara yake.
Mhe. Ummy alipokelewa kwa shangwe
na bashasha na watumishi wa Wizara yake – Idara Kuu ya Afya na Idara
Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakiongozwa na
Katibu
Mkuu wa Wizara Bibi Sihaba Nkinga. Waziri alipata muda wa kusalimiana
na watumishi 106 waliotangulia kuhamia Dodoma katika Awamu ya kwanza ya
Uhamisho na kujiridhisha na ari waliyonayo watuimishi.
Akiwa hapa UDOM, Waziri Ummy
alitembelea Hospitali ya Benjamin Mkapa kwa lengo la kuhakikisha kuwa
huduma za matibabu ya kibigwa kwa wagonjwa zinapatikana kupitia
Hospitali hiyo iliyoko eneo la Chuo Kikuu cha Dodoma, ambayo imefungwa
vifaa vya kisasa ili kukabiliana na magonjwa mbalimbali yaliyoshidikana.
Akiongea na waandishi wa habari,
Mhe. Waziri alifafanua kuwa katika kuhakikisha Serikali inasogeza huduma
za afya kwa wananchi wake, wanafunzi na viongozi wanaohamia Dodoma,
Hospitali ya Benjamini Mkapa imekamilisha kufunga vifaa vya kisasa vya
matibabu ikiwa ni ‘MIR’ mashine ya ‘mamography’ inayotumika kuchunguza
magonjwa ya saratani ya akinamama, na kwamba mashine hiyo inapatikana
hapo hospitalini pekee hapa nchini.
Kufuatia kuwepo kwa changamoto ya
upungufu wa madaktari, wahuguzi na watumishi wa kada mbalimbali, Wizara
itaangalia uwezekano wa kufanya uhamisho wa ndani ili kupunguza uhaba
wa watumishi uliopo katika hospitali hiyo. Aidha, Wizara imeahidi
kuwasiliana na Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora ili kupata watumishi wakutosha kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya
watumishi.
Na Erasto T. Chingoro- Msemaji Kitengo cha Mawasilino Serikalini, WAMJJW
No comments:
Post a Comment