Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye ameteua Kamati Maalum ya Hamasa
kuelekea Mashindano ya AFCON chini ya umri wa miaka 17 yatakayofanyika
mwezi May 2017 nchini Gabon ambapo Tanzania inawakilishwa na Timu ya
Taifa ya Mpira wa Miguu ya Vijana (Serengeti Boys).
Kamati hiyo ya watu kumi(10)
itaongozwa na Mwenyekiti Charles Hillary kutoka Azam Tv na
Katibu wake
Selestine Mwesigwa ambaye pia ni katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) na wajumbe wa kamati hiyo ni Dkt Hassan Abass
Mkurugenzi Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Ruge
Mutahaba Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji kutoka Clouds Media Group,
Hoyce Temu Mrembo wa Tanzania mwaka 1999, Maulid Kitenge Mtangazaji
kutoka EFM, Beatrice Singano Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania,
Erick Shigongo Mkurugenzi wa Global Publishers na wasanii wa muziki wa
kizazi kipya Ali Kiba na Naseeb Abdul (Diamond Platinumz).
Lengo kuu la Kamati hii ni
kuhamasisha watanzania kuiunga mkono Timu ya Serengeti Boys na juhudi za
Serikali katika kuhakikisha wanarudi na ushindi katika mashindano hayo.
Imetolewa na
Zawadi Msalla
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo.
28/02/2017
No comments:
Post a Comment