Pages

Wednesday, March 1, 2017

WAFANYAKAZI WA ZANTEL-ZANZIBAR WACHANGIA DAMU KUISAIDIA BENKI YA DAMU SALAMA NCHINI


1
Mfanyakazi wa kampuni ya Zantel -Zanzibar Kassim Bakari Zuberi akichangia damu wakati wa zoezi lililowahusisha wafanyakazi wa kampuni hiyo kwa upande wa Zanzibar ikiwa ni njia ya kuokoa maisha ya watanzania wenye uhitaji mkubwa wa huduma hiyo. Zoezi hilo limefanyika jana mjini Unguja. Kushoto ni ofisa kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama-Zanzibar Gabriel Laurent.
2
Mfanyakazi wa kampuni ya Zantel -Zanzibar Mohamme Ali akichangia damu wakati wa zoezi lililowahusisha wafanyakazi wa kampuni hiyo kwa upande wa Zanzibar ikiwa ni njia ya kuokoa maisha ya watanzania wenye uhitaji mkubwa wa huduma hiyo. Zoezi hilo limefanyika jana  mjini Unguja. Kushoto ni Khairia Ali Hamad, mtoaji damu kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama-Zanzibar.
3
Afisa mdhibiti wa Rasilimali watu wa kampuni ya Zantel -Zanzibar Said Habibu akichangia damu wakati wa zoezi lililowahusisha wafanyakazi wa kampuni hiyo ikiwa ni njia ya kuhamasisha jamii kuchangia damu kwa hiari. Zoezi hilo limefanyika jana mjini Unguja. Kushoto ni Khairia Ali Hamad, mtoaji damu kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama-Zanzibar.
4
Mfanyakazi wa kampuni ya Zantel -Zanzibar Salum Habib Mohammed akichangia damu wakati wa zoezi lililowahusisha wafanyakazi wa kampuni hiyo kwa upande wa Zanzibar ikiwa ni njia ya kuokoa maisha ya watanzania wenye uhitaji mkubwa wa huduma hiyo. Zoezi hilo limefanyika jana mjini Unguja. Kushoto ni Khairia Ali Hamad, mtoaji damu kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama-Zanzibar.
5
Mkurugenzi wa Ofisi Kuu ya Kampuni ya Zantel-Zanzibar Mohamed Musa Baucha akijiandaa kuchangia damu wakati wa zoezi la uchangiaji damu kwa hiari lilloandaliwa na kampuni hiyo ikiwa ni njia ya kuhamasisha jamii kuchangia damu kwa hiari. Zoezi hilo
limefanyika jana mjini Unguja. Kushoto ni ofisa kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama-Zanzibar Gabriel Laurent.
………………………………………….
Katika kuisaidia benki ya damu hapa nchini, wafanyakazi wa Zantel-Zanzibar wamejitokeza kwa wingi na kujitolea kuchangia damu katika kuendeleza mwitikio huo kwa jamii ulioanzishwa na Kampuni hiyo wiki iliyopiata katika makao makuu yake jijini Dar es Salaam.
Zoezi hili ambalo linaratibiwa na Kitengo cha uwajibikaji kwa jamii (CSR) cha Kampuni hiyo, limelenga kusambaza upendo kupitia shughuli hii ya uchangiaji damu ili kuiwezesha benki ya damu sambamba na kuokoa maisha ya Watanzania wenzetu.
Shughuli hiyo ya uchangiaji iliyofanyika katika makao makuu ya Ofisi za Zantel-Zanzibar, ilishuhudia mwitikio mkubwa kutokana na wingi wa wafanyakazi wa Zantel kujitokeza, pamoja na baadhi ya wananchi wakishiriki kuchangia damu.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo la uchangiaji damu, Mkurugenzi wa Ofisi kuu ya Zantel-Zanzibar, Bw. Mohamed Musa Baucha aliwashukuru watu wote walioshiriki na kutoa rai kwa makampuni mbalimbali pamoja na wananchi kuwa tayari kujitolea kwenye shughuli kama hizo wanapotakiwa  kufanya hivyo.
“Tunayo furaha kwa mwitikio huu wa kukubali kuokoa maisha ya Watanzania wenzetu kwa kuonyesha upendo hususan wafanyakazi wa Zantel Zanzibar. Niwaombe muendelee na moyo huu huu wa kujitolea pindi mnapohitajika kushiriki kwenye shughuli nyingine kama hizi,”alisema.
Kwa upande wake, Afisa Uhamasihaji wa Mpango wa damu salama Zanzibar Bw. Omar Said Omar alisema kwamba zoezi la uchangiaji damu limefanyika kwa mafanikio makubwa na amefurahishwa na moyo wa kujitolea ulioonyeshwa na wafanyakazi wa Zantel-Zanzibar. Hata hivyo aliongeza kuwa, bado mahitaji ya damu ni makubwa ikilinganishwa na kiwango kilichokusanywa ambapo kwa mwaka huu wa 2017 walijiwekea lengo la kukusanya chupa 12,000.
Alisema kwamba shughuli ya kukusanya damu ni zoezi endelevu la kujitolea, benki ya damu imekuwa ikiomba makampuni na jamii kwa jumla kutambua umuhimu wa kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wananchi.
“Ni watu wachache sana ambao wamekuwa wakijitokeza kuchangia damu, hivyo tunaamini kuwa zoezi hili litaendelea kuwahamasisha watu wengi kujitokeza kushiriki,” alisema.

No comments:

Post a Comment