Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye(katikati) akishiriki kukimbia na
vijana wa Jogging club Mjini Dodoma leo March 1,2017 wa pili kushoto ni
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri
Mkuu kazi Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akiwapongeza vijana wa
Jogging club na wakazi wa Dodoma kwa kushirki michezo mara baada ya
kufanya mazoezi ya pamoja yenye nia ya kuimarisha afya na kuendeleza
michezo nchini yaliyofanyika katika Uwanja wa Jamhuri leo March 1,
2017.
Katibu Mkuu Wizara wa Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akiwashukuru
wakazi na vijana wa Jogging club kwa mapokezi mazuri ya Wizara yake
mara baada ya kufanya mazoezi ya pamoja yenye nia ya kuimarisha afya na
kuendeleza michezo nchini yaliyofanyika katika Uwanja wa Jamhuri Mjini
Dodoma leo March 1, 2017.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya
Michezo Nchini Bw. Omary Singo akitoa hamasa kwa wakazi na vijana wa
Jogging club kushiriki michezo katika kuimarisha afya na kuendeleza
michezo nchini mara baada ya kufanya mazoezi ya pamoja yaliyofanyika
katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma leo March 1, 2017.
Katibu Mkuu Wizara wa Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel( wa pili Kulia)
akishiriki mazoezi na na vijana wa Jogging club Mjini Dodoma leo March
1,2017 kulia ni Naibu Waziri Ofisi ya waziri Mkuu kazi Vijana na Ajira
Mhe. Anthony Mavunde.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye pamoja na viongozi wengine wa Serikali
na Mkoa wa Dodoma wakishiriki mazoezi yaliyofanyika katika Uwanja wa
Jamhuri leo March 1, 2017.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na Vijana
wa Jogging Club, viongozi wengine wa Serikali na Mkoa wa Dodoma mara
baada ya kushiriki mazoezi yaliyofanyika katika Uwanja wa Jamhuri leo
March 1, 2017.
No comments:
Post a Comment