Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na vijana wa Jogging club
Mjini Dodoma mara baada ya kufanya mazoezi ya pamoja yenye nia ya
kuimarisha afya na kuendeleza michezo nchini yaliyofanyika katika Uwanja
wa Jamhuri Mjini Dodoma leo March 1, 2017.
………………………………………………………………………………………………………….
Na Raymond Mushumbusi WHUSM Dodoma.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye amewahakikishia wapenzi wa Mpira Mjini
Dodoma kuwa timu za Mpira Mkoani humo zitashiriki Ligi Kuu ili
kuwapa
raha ya Ligi hiyo mashabiki wa mpira na michezo kwa ujumla.
Amezungumza hayo mara baada ya
kukutana na kufanya mazoezi na Vijana kutoka Jogging Club mbalimbali
Mjini Dodoma ikiwa ni ishara rasmi ya Wizara yake kuhamia katika Makao
Makuu ya nchi.
Mhe. Nape Nnauye amesema kuwa
haitawezekana Serikali ikahamia Dodoma na kusiwe na timu inayoshiriki
Ligi kuu ya Mpira wa Miguu Tanzania Bara hivyo yeye kama Waziri
anayehusika na Michezo kwa kushirikiana na wadau wa Michezo atahakikisha
Timu zinafanya vizuri na kushiriki Ligi hiyo.
“Haiwezekani Rais akawa hapa na
Makamu wa Rais na Mawaziri tukakosa ladha na furaha ya Ligi kuu hapa
Dodoma nitahakikisha timu za hapa zinashiriki Ligi kuu”alisistiza Mhe.
Nnauye.
Kwa upande wake Naibu Waziri
Ofisi ya Waziri Mkuu kazi Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde
amewapongeza vijana wa Jogging club na wakazi wa Dodoma kwa kushiriki
michezo na kuhimiza kujituma zaidi kwa timu za michezo hasa mpira wa
miguu ili kushiriki Ligi kuu Tanzania Bara.
Naye Katibu Mkuu Wizara wa Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel amewaomba wakazi
wa Dodoma kufanya michezo kuwa ni Utamaduni wao wa kila siku ili kujenga
Taifa la wapenda michezo kwa nia ya kuimarisha afya na kuendeleza
michezo nchini.
Aidha Mkurugenzi wa Maendeleo ya
Michezo Nchini Bw. Omary Singo amewahakikishia wakazi na wapenzi wa
Michezo ushirikiano katika kuendeleza na kukuza michezo hasa katika
makao makuu ya nchi Dodoma
No comments:
Post a Comment