Pages

Wednesday, March 1, 2017

TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE KWA KUSHIRIKIANA NA TAASISI YA SAVE CHILD HEART YA NCHINI ISRAEL YAWAPELEKA WATOTO NANE KUTIBIWA MAGONJWA YA MOYO NCHINI HUMO


 Baadhi ya wazazi ambao watoto wao wamekwenda nchini Israel kwa ajili ya matibabu ya magonjwa ya moyo wakifuatilia kwa karibu mkutano wa waandishi wa Habarai uliofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).
 Kaimu Mkurugenzi wa Huduma ya Uuguzi  kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Robert Mallya akiwaongoza watoto
wanaokweda kutibiwa magonjwa ya moyo  nchini Israel kuingia kwenye gari kwa ajili ya kwenda uwanja wa ndege kuanza
safari ya kuelekea nchini humo. Serikali kupitia JKCI  kwa kushirikiana na Serikali ya Israel kupitia Taasisi ya Save Child Heart imewapeleka watoto nane (8) nchini humo kwa ajili ya matibabu ya moyo. 
 Wataalamu wa Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) , ndugu na watoto wanaokwenda kutibiwa nchini Israel wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa safari ya watoto hao ya kuelekea nchini humo kwa ajili ya
matibabu ya moyo.
 Mkutano na waandishi wa Habari kuhusu watoto nane  wanaokwenda kutibiwa magonjwa ya moyo  nchini Israel ukiendelea leo katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) . Serikali kupitia JKCI  kwa kushirikiana na Serikali ya Israel kupitia Taasisi ya Save Child Heart imewapeleka watoto nane (8) nchini Israel kwa ajili ya matibabu ya moyo. 
 Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo kwa watoto kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Godwin Sharau akiongea na waandishi wa habari kuhusu watoto nane wanaokwenda  nchini Israel kwa ajili ya matibabu ya moyo. Hili ni kundi la nne la watoto kwenda kutibiwa nchini humo tangu mwaka 2015 ambapo JKCI ilianza ushirikiano  na Taasisi ya Save Child Heart  ya kuwapeleka wagonjwa nchini Israel hadi sasa watoto 40 wameshatibiwa na wanaendelea vizuri. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi
wa Huduma ya Uuguzi   Robert Mallya.

No comments:

Post a Comment