Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongea katika
ufunguzi wa majadala kuhusu ukatili wa kijinsia dhidi ya waanawake na
wasichana unavyokuwa kikwazo cha ukombozi wa wanawake kiuchumi katika
kuadhimisha siku ya wanawake duniani leo jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu
akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa majadala kuhusu
ukatili wa kijinsia dhidi ya waanawake na wasichana unavyokuwa kikwazo
cha ukombozi wa wanawake kiuchumi katika kuadhimisha siku ya wanawake
duniani leo jijini Dar es Salaam.
Na Anthony Ishengoma- MOHCDGEC
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu amesema Serikali
inakusudia kuanzisha kampeni ya kitaifa kumfikia mtoto wa kike popote
Nchini ili aweze kujitambua yeye ni nani ikiwemo umuhimu wa kujitambua
kiafya na
kujijengea ufahamu wa kujiendeleza kitaaluma kwani ndiyo nguzo
muhimu ya kujiletea maendeleo ya kiuchumi.
Waziri Ummy Mwalimu mesema hayo
wakati akifungua mjadala kuhusu ukatili dhidi ya wanawake na wasichana
unavyokuwa kikwazo cha ukombozi wa wanawake kiuchumi katika kuadhimisha
siku ya wanawake duniani. Mjadala huo unaendelea katika ukumbi wa
mikutano wa shirika la Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP) na kilele
cha maadhimisho hayo ni Machi 8, mwaka huu.
Aidha aliwaambia washiriki wa
mkutano huo kuwa serikali haina tatizo katika kutunga sera na sheria
zinazolenga kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na wasichana bali kuna
baadhi ya changamoto zinazoitaji msukumo ambazo ameziita za
kiutekelezaji akisema kila awamu ya serikali imekuwa ikifanyia masuala
mbalimbali yanayohusiana na sheria na sera hizo.
Waziri Mwalimu aliendelea kusema
kuwa kwa kuzingatia hilo, serikali imefanya jitihada mbalimbali za
kuwawezesha wanawake kiuchumi kwa kutunga sera, sheria na miongozo
mbalimbali, pamoja na kuweka mipango na mikakati ya Kitaifa na Kisekta
ili kuhakikisha kuwa wanawake wanapatiwa fursa mbalimbali za kuwawezesha
kiuchumi.
Waziri alongeza kuwa katika
kuwezesha wanawake kiuchumi pia Serikali imeanzisha Benki ya Wanawake,
mifuko mbalimbali ikiwemo Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake na Majukwaa ya
kuwezesha Wanawake Kiuchumi, ili kuwawezesha wanawake kupata mikopo
yenye masharti nafuu.
Akifafanua kuhusu mfuko wa
maendeleo ya wanawake Waziri amesema Wizara imeendelea kuhamasisha
Halmashauri kuchangia asilimia tano (5%) ya mapato yao ya ndani kwa
ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake ambapo kwa kipindi cha Mwezi
Julai, hadi Disemba, 2016 kiasi cha Shs 6,222,164,982 zilitolewa na
Halmashauri 101 kwa ajili ya kuwakopesha wa wanawake wajasiriamali.
Aidha aliongeza kuwa idadi ya
Wanawake wanaoshiriki katika mifumo rasmi ya kifedha imeendelea
kuongezeka ingawa kiwango chao cha ushiriki bado ni cha chini
ikilinganishwa na wanaume.
Aidha aluambia mkutano huo kuwa
wanawake wanaotumia huduma rasmi za kifedha waliongezeka kutoka
asilimia ya 44.5 mwaka 2009 hadi kufikia asilimia 84 mwaka 2016
ikilinganishwa na wanaume waliongezeka kutoka asilimia 44.4 mwaka 2009
hadi kufikia asilimia 88 mwaka 2016.
Aliendelea kusema kuwa dhamira ya
serikali ni kuhakikisha kuwa uwezeshwaji huu unawafikia wanawake wengi
zaidi hususan wanaoishi pembezoni huku akibainisha kwamba ni dhahiri
kuwa uchumi kwa mwanamke unaleta mabadiliko ya haraka ndani ya familia,
jamii na Taifa kwa ujumla.
Akiongelea fursa za kisiasa na
nafasi za juu katika ajira Waziri amesema anatambua bado kuna kazi kubwa
ya kufanya ili kufikia usawa 50/50. Kwasasa tumeweza kuweka usawa
kikatiba kwa kuwa na asilimia 36 ya uwakilishi wa wanawake bungeni. Pia,
usawa katika usaili wa wanafunzi katika shule za msingi, hata hivyo,
bado changamoto zipo katika utendaji na nguzo za kimahakama, pamoja na
kupata nafasi za juu serikalini.
Naye Barozi wa Sweden hapa Nchini
Tanzania Katrina Rangnitt aliwaambia awajumbe wa mkutano huo kuwa ni
muhimu jamii ya Tanzania ikaachana na mila potofu zinazoendelea
kumkandamiza mwanamke na kutaka kuwepoa kwa usawa wa kijinsia unaomfanya
mwanamke kuwa huru kimaamzi.
Aliongeza kuwa ana taarifa kuwa
Tanzania ina sera shirikishi za ajira na wigo wa elimu umetanuliwa ili
kuongeza nafasi za masomo kwa wanawake hapa nchini.
Katika juhudi kutokomeza ukatili
wa kijinsia hapa chini Serikali tayari imezindua mpango mpango wa miaka
mitano wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
No comments:
Post a Comment