Eng. Athu Chulla akifafanua jambo
kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani
(wa pili kulia), mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba
zinazojengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), katika eneo la
Magomeni jijini Dar es Salaam. Pembeni kwa Naibu Waziri ni Mratibu wa
Ujenzi wa nyumba hizo, Arch. Christina Shayo.
Mratibu wa Ujenzi wa nyumba
zinazojengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Arch. Christina Shayo
(wa kwanza kushoto), akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani, mara baada ya kukagua
maendeleo ya ujenzi wa nyumba katika eneo la Magomeni jijini Dar es
Salaam.
Muonekano wa moja ya nyumba za
wananchi zinazojengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) katika eneo la
Magomeni ikiwa katika hatua ya msingi, Nyumba hizo zinatarajiwa
kuhudumia kaya 656 zitakapokamilia Septemba mwaka huu.
Mafundi wa Wakala wa Majengo
Tanzania (TBA), wakiendelea na ujenzi wa nyumba za wananchi katika eneo
la Magomeni. Nyumba hizo zinatarajiwa kuhudumia kaya 656 zitakapokamilia
Septemba mwaka huu.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
No comments:
Post a Comment