Zaidi
ya watu milioni moja wa Uingereza wamesaini barua ya kutoa shinikizo
kwa serikali ya Uingereza kusitisha ziara rasmi iliopangwa baadaye mwaka
huu ya rais Donald Trump.
Barua hiyo iliyoandikwa kufuatia
agizo la rais Trump dhidi ya wahamiaji, inaeleza kuwa kuja kwake
kutamuaibisha Malkia Elizabeth.
Idadi ya watu wanaoendelea
kusaini kupinga Mwaliko wa Trump nchini Uingereza inaendelea kuongezeka,
tangu Marekani kuweka vikwazo dhidi ya wageni hatua iliyozua ghadhabu
kote duniani. Amri ya Trump: Ni nani anaathirika?
No comments:
Post a Comment