CHANZO BBC
Bastian Schweinsteiger hataihama
klabu ya Manchester United na atajumuishwa kwenye kikosi cha klabu hiyo
kinachocheza ligi ndogo ya Ulaya, Europa League, kwa mujibu wa meneja
Jose Mourinho.
Kiungo huyo wa kati wa miaka 32 alifunga wakati wa ushindi wa United wa 4-0 Kombe la FA dhidi ya Wigan Jumapili.
Hiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kuanza mechi katika klabu hiyo tangu Januari 2016.
Schweinsteiger aliachwa nje ya
kikosi cha Europa League msimu huu na Mourinho na akalazimishwa
kushiriki mazoezi na kikosi cha wachezaji wasiozidi umri wa miaka 23
mwanzoni mwa msimu.
Msimamo wa ligi ya EPL 2016/17
Mourinho amesema mchezaji pekee ambaye huenda akaondoka mwezi huu ni Ashley Young.
Mourinho amesema mchezaji pekee ambaye huenda akaondoka mwezi huu ni Ashley Young.
“Ataenda kucheza Europa League
kwa sababu tumeachwa na nafasi za kujaza kutokana na kuondoka kwa
[Memphis] Depay na [Morgan] Schneiderlin.”
Schneiderlin aliuzwa Everton mnamo 12 Januari, naye Depay akajiunga na Lyon siku nane baadaye.
United watakutana na
Saint-Etienne hatua ya 32 bora Old Trafford tarehe 16 Februari, na mechi
ya marudiano itachezwa wiki moja baadaye.
No comments:
Post a Comment