CHANZO BBC
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Chad Moussa Faki amechaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa tume ya Muungano wa Afrika AU.
Faki anachukua mahala pake Dlamini Zuma kutoka Afrika Kusini ambaye kipindi chake cha kuhudumu kimekamilika.
Mshindani ,mkuu wa bwana Faki
katika duru ya mwisho ya upigaji kura, wakati wa kikao cha AU mjiji
Addis Ababa, Ethiopia, alikuwa ni waziri wa mashauri ya nchi za kigeni
wa Kenya Amina Mohamed.
Wagombea watano waliokuwa
wakiwania wadhifa huo ni pamoja na waziri wa mambo ya nchi za kigeni wa
Kenya Amina Mohammed, mwanadiplomasia Abdoulaye Bathily kutoka Senegal,
waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Chad Moussa Faki Mahamat,
mwanasiasa mkongwe kutoka Botswanda Pelonomi Venson-Moitoi na aliyekuwa
wakati mmoja mshauri wa rais wa Equatorial Guinea Mba Mokuy
No comments:
Post a Comment