Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais – Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akiongea na Diwani wa
Kata ya Buguruni Mhe. Adam Fugame (katikati) wakati wa ziara ya kikazi
ya kukagua ujenzi wa mfereji wa maji taka katika eneo la Ilala Bungoni
Sehemu ya Mfereji wa Maji taka
unaojengwa eneo la Ilala Bungoni chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais
kupitia Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi na unafadhiliwa na
Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira (UNEP).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais – Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akiongea na Wananchi
wakazi wa Ilala Bungoni, mara baada ya
kukagua ujenzi wa mrefeji wa maji taka
Bw. Gervas wa Kampuni ya Dezo
Civil Contractors Co. Ltd (kulia) akifanunua jambo kwa Waziri wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba
katika eneo la Temeke – Mtoni kwa Azizi Ali ambapo Kampuni hiyo imepewa
kazi ya kusafisha na kujenga mfumo wa maji taka.
Mwakilishi wa UNOPS Bw Bernard
Omondi akifanunua jambo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais –
Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba katika eneo la Temeke – Mtoni
kwa Azizi Ali ambapo kazi ya kusafisha na kujenga mfumo wa maji taka
inaendelea.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa
Rais Prof. Faustin Kamuzora ( wa tatu kutoka kulia) akifafanua jambo kwa
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira Mhe.
January Makamba mara baada ya ziara ya kukagua hatua za ujenzi kwa
miradi inayosimamiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais. Kulia ni Bw. Kanizio
Manyika Afisa Mazingira Mkuu na Msimamizi wa Mradi na Bw. Richard
Muyungi Kaimu Mkurugenzi wa Mazingira.
……………..
Na Lulu Mussa
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais – Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba hii leo amefanyia
ziara ya kikazi ya kukagua hatua za ujenzi katika miradi inayofadhiliwa
na Ofisi yake.
Akiwa katika Wilaya ya Ilala,
Waziri Makamba ametembelea ujenzi wa Mfereji wa kupitishia maji taka
katika eneo la Ilala Bungoni na kuongea na wananchi wa eneo hilo.
Waziri Makamba ameugiza uongozi wa
Dezo Civil Constractors Co. Ltd kuhakikisha ujenzi wa Miundombinu ya
maji taka katika Manispaa za Ilala na Temeke unakamilika kwa muda
uliopangwa na kwa ubora wa hali ya juu kwa kuzingatia makubaliano
yaliyopo katika mkataba.
“Nataka mradi huu uwe wa mfano kwa
ubora na viwango vya hali ya juu, ikiwa ni jitihada za kukabiliana na
athari za mabadiliko ya Tabianchi, kwa kuweka mfumo mzuri wa kukusanya
maji taka na kuyaelekeza sehemu stahiki” Makamba alisisitiza.
Aidha, Waziri Makamba amewataka
wakazi wanaozuka eneo hilo kuacha mara moja utupaji wa taka maji na taka
ngumu katika mfereji huo unaojengwa, na kumuagiza Mkurugenzi wa
Manispaa ya Ilala Bw. Palela Msongela kutoa adhabu kali kwa yeyote
atakayekiuka agizo hilo.
“Kwa kupitia kamati za Mazingira
za vitongoji na sheria ndogo ndogo mlizojiwekea hakikisheni kuwa hifadhi
ya mazingira inazingatiwa kwa mstakabali wa vizazi vya sasa na vizazi
vijavyo.”
Pia, Waziri Makamba amemuagiza
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kuhakikisha Wakandarasi wanaopewa kazi
za ukusanyaji wa taka, wanakuwa na vifaa na uwezo wa kutosha kwa
kuhakikisha taka zote zinazolewa kwa wakati ili kuepuka mrundikano wa
taka katika makazi ya watu.
“Natoa wito pia kwa vijana wa
maeneo haya kuunda vikundi vidogo vya kuzoa taka ili kuwa chanzo cha
ajira kwenu.” Makamba alisisitiza.
Waziri Makamba ameliagiza Baraza
la Taifa La Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira – NEMC kutembelea eneo
hilo la Ilala Bungoni na kutoa maelekezo kwa Gereji bubu zinazokiuka
hifadhi na usimamizi wa Mazingira kwa kufanya shughuli zao pembezoni mwa
mfereji unaojengwa.
Ujenzi wa Ukuta wa (Obama/Ocean
Road na Kigamboni) na Miundombinu ya maji taka katika Manispaa za Ilala
na Temeke unatekelezwa chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais kupitia Mradi
wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi na unafadhiliwa na Shirika la Umoja
wa Mataifa kuhusu Mazingira (UNEP). Aidha, Kampuni ya Dezo Civil
Contractors ndio inafanya kazi ya ujenzi huu na kazi zinatarajiwa
kukamilika mwezi Julai 2017.
Waziri Makamba katika ziara yake
hii leo ametembelea Ilala Bungoni, Mtoni kwa Azizi Ali, Chuo cha
Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na Kutembelea eneo la Ujenzi wa Ukuta
Barabara ya Obama.
No comments:
Post a Comment