Usiku
wa 31,December 2016 kuamkia mwaka mpya 2017 ndipo wanamitindo
mbalimbali walikutana na kusherekea kwa pamoja Usiku wa Khanga yaani
“Khanga Party”. Tukio hili kama lilivyo kuwa limetaarifiwa awali
limefanyika Regency Park Hotel. Design mbalimbali za vazi la Khanga
kutoka kwa wanamitindo zilioneshwa kwenye stage na kuzikonga mioyo za
wadau pamoja na wahudhuriaji usiku huo.
Kumbuka
Party hii imeandaliwa na Mama wa Mtindo maarufu kama Asya Idarous
Khamsin, mbali na burudani zilizo kuwepo pia kulikuwa na Red Carpet
yenye sifa kubwa ya kuwakutanisha mastaa na mashabiki wao kuweza kupiga
picha za pamoja kwa ajili ya kumbukumbu. Tunawatakia mwendelezo mwema na
wenye baraka wadau na wanamitindo kutoka hapa Tanzania. (Cheers 2017)
No comments:
Post a Comment