Frank Mvungi-Maelezo
Serikali kununua meli mpya ili kuongeza tija katika utoaji wa huduma za usafirishaji ndani ya Ziwa Victoria.
Akizungumza wakati wa kipindi cha
Tunatekeleza kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC)
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi )
Dkt. Leonard Chamuriho alisema kuwa ujenzi wa meli hiyo ni utekelezaji
wa ahadi ya Serikali kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa.
“Bajeti yetu ni takribani
trilioni 2.5 hivyo, inatuwezesha kutekeleza mikakati yetu ya kuhakikisha
kuwa sekta ya uchukuzi inachochea ujenzi wa uchumi wa Viwanda
nchini”Alisisitiza Dkt. Chamuriho.
Akizungumzia mikakati
yakuendeleza sekta hiyo Dkt. Chamuriho alisema kuwa Bajeti waliyotengewa
inawawezesha kuanza ujenzi wa reli kwa viwango vya Kimataifa (Standard
gauge) ambayo itajengwa kwa awamu tano ambapo awamu ya kwanza
itahusisha eneo la Dar es salaam na Morogoro.
Pia alifafanua kuwa ,upanuzi wa
bandari ya Dar es salaam, Mtwara na Mwanza utachochea ukuaji wa uchumi
hasa katika eneo la Bandari ya Mtwara itochochea ukuaji wa Sekta ya
gesi na Viwanda.
“Jambo Jingine ni kukarabati meli
zote katika ziwa Victoria na Tanganyika ili kusaidia kuboresha
usafirishaji wa abiria na mizigo katika maeneo mbalimbali” alisisitiza
Dkt. Chamuriho.
Aidha Dkt.Chamuriho alibainisha
kuwa Serikali imepanga kujenga Bandari ya Bagamoyo kwa kuwatumia
wawekezaji ili kuchochea ukuaji wa uchumi wa Viwanda katika eneo la
Bagamoyo na maeneo mengine kwa kuwa itatumika kusafirisha bidhaa
zinazozalishwa na malighafi kutoka nje ya nchi kwa ajili ya viwanda.
Katika hatua hiyo Dkt Chamuriho
alisema kuwa Mikakati mingine iliyopo ni kuimarisha shirika la ndege
Tanzania (ATCL) kwa kufunga mfumo madhubuti wa kielektroniki
utakaosaidia kuondoa tatizo la upotevu wa mapato hali itakayochangia
kukuza shirika hilo kwa manufaa ya Taifa.
Sekta ya uchukuzi ni mhimili wa
ujenzi wa Uchumi wa Viwanda hapa nchini kwa kuwaungainisha wazalishaji
wa bidhaa, malighafi na wananchi katika maeneo mbalimbali ndani na nje
ya nchi.
No comments:
Post a Comment