Pages

Tuesday, January 31, 2017

WAANDISHI WA HABARI ANDIKENI HABARI BILA WOGA, RC GAMBO


GAMBO-1-1
Na Mahmoud Ahmad Arusha
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo Amewataka waandishi wa habari
kuandika habari zao bila wooga na wasiandike habari zinazowafuarahisha
viongozi pekee, badala yake kuandika kwa uhuru, lakini pia kuandika
habari za kweli  wala wasitake kuwafurahisha viongozi ilimradi habari

hizo ziwe za ukweli
 Aidha akazitaka taasisi za Serikali  na umma mkoani hapa  kutoa
taarifa kwa wakati ilikuondoa kero na kuweka majibu sawa kwa jamii
yatakayosaidia kuondoa manung’uniko yanaweza kumalizwa kwa kutoa
taarifa sahihi na kwa wakati kwa wananchi.
Hayo yamebainishwa na mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo wakti
akifungua kikao cha wadau wa habari na taasisi za serikali lengo
likiwa ni kupata taarifa za mkoa wa Arusha kuhusu utendaji kazi kwa
kipindi cha nusu mwaka .
Ameongeza kuwa migogoro ya Ardhi mingi inachangiwa na wanasiasa
wanaotaka kuomba kura na mingine inachangiwa na wenyeviti wa vijiji
hali inayoonyesha kuwapo kwa migogoro isiyo isha maeneo yote mkoani
petu.
“ Naombeni Andikeni kwa uhuru habari zenu lakini za kweli wala hakuna
atakayewabugudhi,tukosoweni wala msitake kuwafurahisha viongozi,
lakini andikeni Ukweli kumekuwepo uandikaji habari nzuri za viongozi
tu andikeni habari za kukosoa ilikuweza kujisahihisha”.aliongeza Gambo
Ameongeza kuwa wananchi kupeleka malalamiko ya migogoro kwa viongozi
wa mkoa ni wazi  kuwa watendaji wa ngazi za chini kuanzia ngazi ya
wilaya na ngazi zingine hawafanyikazi ipasavyo,ambapo serikali itaanza
kuwashughulikia vinara wa migogoro ya Ardhi mkoani petu.
Ameongeza kuwa waandishi wa habari waandike habari zenye ukweli
zitakazo saidia kuondoa kero nao kuweza kujisahihisha zenye mwelekeo
wa kuwatumikia wananchi kwa kuacha Alama ya uongozi.
Ameutaka mfuko wa hifadhi ya Bima ya Afya kuhakikisha wateja wao
wanapata huduma bora na kujua matatizo wanayopata wateja wao kwenye
hospitali ya selian na kukaa na uongozi wa Selian kujua ni namna gani
mtayapatia ufumbuzi malalamiko yao, pia tembeleeni kwenye vyuo vikuu
vyote mkoani petu ili kujua malalamiko ya wanavyuo kuhusu huduma zenu.
“Watendaji wa serikali  timizeni  wajibu wenu katika kuwahudumia
wananchi na waelezeni ukweli hatua zinazochukuliwa kuondoa kero mbali
mbali na serikali yao kwani itasaidia kukuza ushirikiano na kuweza
kukuza maendeleo kwa wananchi”aliongeza Gambo
Nae  mkuu wa  wilaya ya Arusha  Gabriel Daqarro amewataka wanahabari
kuandika habari zao kwa weledi bila kumung’unya kwani zitaisaidia
serikali kuweza kutambua kero za wananchi na kuzipatia majawabu
yatakayosaidia kukuza na kuweza kujiletea maendeleo.
Ameongeza kuwa ushirikiano kati ya idara za serikali na wanahabari
zitasaidia kuweza kutoa taarifa ya utendaji wa serikali na
kijitathmini wapi tulipo na wapi tunakosea katika

No comments:

Post a Comment