Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akikagua gwaride la heshima
lililoandaliwa na maafisa na askari wa Jeshi la Magereza, Makao Makuu,
jijini Dar es Salaam wakati kiongozi huyo alipofanya ziara ya kikazi
katika Jeshi hilo leo. Masauni mara baada ya kumaliza ziara yake
aliagiza Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Idara ya Uhamiaji nchini,
kuanzia sasa sare zote za askari na maafisa wa Idara hizo zitashonwa
katika Kiwanda cha Magereza, Ukonga, jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akimpa maelekezo Mratibu wa Mradi wa
Ujenzi wa Nyumba za Makazi ya Askari wa Jeshi la Magereza, Julius Chego
(kulia), wakati kiongozi huyo alipofanya ziara katika eneo la Ujenzi wa
nyumba hizo 9,500, Ukonga, jijini Dar es Salaam leo, ambazo Rais Dk.
John Magufuli ametoa Shilingi Bilioni kumi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba
hizo. Katikati ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo, Dk Juma
Malewa.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa suti) akiiikagua moja ya
nyumba za askari wa Jeshi la Magereza zinazojengwa Ukonga, jijini Dar es
Salaam. Jumla ya nyumba 9,500 zinatarajiwa kujengwa katika eneo hilo
mara baada ya Rais Dk John Magufuli kutoa shilingi Bilioni Kumi kwa
ajili ya ujenzi wa nyumba hizo. Masauni alifanya ziara ya kikazi katika
maeneo mbalimbali ya Jeshi hilo, na alitoa agizo kwa Jeshi la Zimamoto
na Uokoaji pamoja na Idara ya Uhamiaji, kuhakikisha kuwa, sare za idara
hizo kuanzia sasa zitakuwa zinashonwa katika Kiwanda cha Magereza,
Ukonga. Mbele kushoto ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza
nchini, Dk Juma Malewa.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akitoka katika Jengo la
Useremala mara baada ya kukagua mashine mbalimbali zinazotumika kuranda
na kuchana mbao kwa ajili ya utengenezaji wa samani katika Kiwanda cha
Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, Dk Juma Malewa, na kulia ni Mkuu
wa Kiwanda hicho, Ismail Mlawa.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akikiangalia kikapu kilichoshonwa na
wafungwa katika Kiwanda cha Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam.
Masauni alifanya ziara katika kiwanda hicho na kujionea vitu mbalimbali
vinavyotengenezwa na wafungwa kiwandani hapo. Watatu kulia ni Kaimu
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, Dk Juma Malewa, kulia ni
Mkuu wa Kiwanda hicho, Ismail Mlawa.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akiviangalia viti
vilivyotengenezwa na wafungwa katika Kiwanda cha Magereza Ukonga, jijini
Dar es Salaam, huku Mkuu wa Kiwanda hicho, Ismail Mlawa akitoa maelezo
ya utengenezaji wa viti hivyo. Masauni alifanya ziara katika kiwanda
hicho na kujionea vitu mbalimbali vinavyotengenezwa na wafungwa
kiwandani hapo.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa suti) akikiangalia kitanda
kilichotengenezwa na wafungwa katika Kiwanda cha Magereza Ukonga, jijini
Dar es Salaam, huku Mkuu wa Kiwanda hicho, Ismail Mlawa (kushoto)
akitoa maelezo ya utengenezaji wa kitanda hicho. Masauni alifanya ziara
katika kiwanda hicho na kujionea vitu mbalimbali vinavyotengenezwa na
wafungwa kiwandani hapo. Wapili kulia ni Kaimu Kamishna Jenerali wa
Jeshi la Magereza nchini, Dk Juma Malewa.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiiangalia moja ya nguo iliyoshonwa na
wafungwa katika Kiwanda cha Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam, huku
Mkuu wa Kiwanda hicho, Ismail Mlawa (kulia) akitoa maelezo ya
utengenezaji wa nguo hiyo. Masauni alifanya ziara katika kiwanda hicho
na kujionea vitu mbalimbali vinavyotengenezwa na wafungwa kiwandani
hapo. Kushoto ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, Dk
Juma Malewa. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment