➤Asema Rais ameshatimiza wajibu wake kwa kutoa fedha za mikopo
➤Chanzo cha Wanafunzi hewa awatupia lawama Bodi ya Mikopo
➤Chanzo cha Wanafunzi hewa awatupia lawama Bodi ya Mikopo
Na Bashir Nkoromo
Wadau
wa elimu wametakiwa kutomlaumu Rais Dk. John Magufuli kuhusu kero
zinazohusiana na mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kwa kuwa
ameshatekeleza wajibu wake kwa kutoa fedha, zinazokadiriwa kuwa Sh.
bilioni 483 mwaka huu ambapo ni ongezeko la kadirio la sh. Bilioni 130,
kutoaka kadirio la sh. Bilioni 350 la mwaka jana.
Hayo
yamesemwa na Kaimu Katibu Mtendaji wa Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya
Juu-CCM, Katibu Msaidizi wa CCM, Daniel Zenda wakati akifungua mkutano
mkuu wa uchaguzi wa Shirikisho hilo, tawi la Chuo Kikuu cha Dar es
Salam, uliofanyika leo katika ukumbi wa DDC, Mwenge na kuongeza kuwa
wanapaswa kulaumiwa ni watendaji wa serikali waliopewa jukumu la
kuratibu na kutoa mikopo hiyo.
Zenda
amesema, Rais Dk. John Magufuli, amekuwa akionyesha kiu ya kuhakikisha
hali ya huduma katika sekta ya elimu kwenye vyuo vikuu inakuwa bora
ikiwemo kuhakikisha kila mwanafunzi anayestahili kupata mikopo anapata
bila vikwazo, lakini watendaji wamekuwa wanaonekana kutoishauri serikali
vizuri na hivyo kusababisha kujitokeza kwa utata na vikwazo vya mara
kwa mara hasa katika utoaji mikopo.
“Mimi
ninavyoona kuna baadhi ya watumishi serikalini hasa pale Bodi ya mikopo
ambao wangpenda Serikali ya Rais Dk. John Magufuli isifanikiwe katika
azma yake ya kutaka kuboresha sekta mbalimbali ikiwemo elimu, kwa mfano
inakuwaje watu waliopewa dhama ya kushauri wanaweka kipengele kama cha
mlemavu asipewe mkopo hata akipata alama nzuri kwenye masomo yasiyo ya
kipaumbele vya mikopo na wakati huo huo, kushauri kwamba ulemavu ni
kipaumbele ni sifa mojawapo ya mwanafunzi kupata mikopo?”, Zenda alihoji
na kuongeza;
“Yaani
hawa washauri wamekuwa wakielekeza mambo ya ajabu sana, sasa tazama
hivi sasa wamekuja na sheria kwamba mwanafunzi atakayekuwa na umri wa
miaka kuanzia 30 asipewe mkopo, wakati kila mmoja anajua wapo Watanzania
wanaoweza kuchaguliwa kusoma vyuo vikuu wakiwa na umri huo, kwa kuwa
katika kuchaguliwa kwenda vyuo vikuu hakuna kigezo cha umri”.
Zenda
aliwatupia lawama Bodi ya Mikopo akisema, kwamba migogoro mingi kuhusu
mikopo huanzia kwao akitoa mfano kwamba, hata suala la kuwepo wanafunzi
hewa kunatokana na ujanjaujanja wa watumishi katika bodi hiyo ili waweze
kujipatia fedha za bure.
Aliwataka
wanafunzi wa vyuo vikuu kuachana na tabia ya kudhani maandamano ni
suluhisho la kuweza kupata mikopo wanapoikosa, na badala yake,
inapotokea watumie Shirikisho hilo, kufikisha hoja zao kwa viongozi hadi
ngazi ya taifa ambako bila shaka ufumbuzi hatimaye utapatikana.
“Sasa
wewe unashawishiwa kuandamana, unakubali, haya ukishaandamana ndiyo
unapata mkopo. acheni kabisa ujinga huu, ninyi ni wasomi mnachotakiwa ni
kujenga hoja na kuzifikisha kunakohitajika”, alisema Zenda.
Kuhusu
uchaguzi huo aliwataka wajumbe kuchagua viongozi kwa kufuata sifa za
kuwa wapambanaji kwa hoja, ni si kuchagua viongozi kwa kufuata urafiki
au kupewa rushwa.
Kaimu
Katibu Mtendaji wa Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu-CCM, Katibu
Msaidizi wa CCM, Daniel Zenda wakati akifungua mkutano mkuu wa uchaguzi
wa Shirikisho hilo, tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salam, uliofanyika leo
katika ukumbi wa DDC, Mwenge Dar es Salaam. Picha na Bashir Nkoromo wa
theNkoromo Blog. /Picha zaidi/>>BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment