Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme
nchini Tanzania, (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba, (aliyenyoosha
kidole), akifafanua jambo wakati wahariri na waandishi wa habari kutoka
vyombo mbalimbali vya habari walipotembelea kituo cha kupoza na
kusambaza umeme cha Ilala-Mchikichini jijini Dar es Salaam, wakati wa
ziara ya wahariri kutembelea miradi ya ukarabati wa miundombinu ya
usambazaji umeme jijini Dar es Salaam, Desemba 3, 2016.
Mhandisi Mramba akiwa na wahariri na waandishi kwenye kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha City Centre
NA
K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
WAHARIRI
wa vyombo vya habari nchini, wametembelea miradi ya ukarabati wa miundombinu ya
usambazaji umeme jijini Dar es Salaam leo Desemba 3, 2016, ili kujionea hatua
zinazochukuliwa na shirika hilo katika kuboresha hali ya upatikanaji umeme
jijini.
Akiongea
wakati wa ziara hiyo ambayo iliwawezesha wahariri hao kutembelea vituo vya
kupoza na kusambaza umeme vya Muhimbili, kituo kipya cha City Centre, kituo cha
Sokoine Drive, kituo cha Ilala Mchikichini na kituo cha kuratibu na kudhibiti
mifumo ya umeme jijini kilichoko Mikocheni.
“Dhana
ya kujenga uchumi wa viwanda ni dhana inayotekelezeka na ushahidi wa wazi ni
kiasi cha uwekezaji uliowekwa na serikali kwenye sekta ya umeme,” alisema
Mhandisi Mramba.
Alisema
hivi miradi hiyo ya kuboresha miundombinu ya umeme jijini Dar es Salaam
inayotekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo imehusisha
ufungaji wa vifaa vipya kabisa.
“Tumeona
kituo hiki cha Ilala, upanuzi mkubwa unafanyika hapa kwa ushirikiano na
serikali ya Japan, City centre kinatekelezwa kwa ushirikiano na serikali ya Japan
na Finland, kituo cha Sokoine kwa ushirikiano na African Development Bank,
kituo kipya cha Muhimbili kwa ajili ya kutoa huduma kwenye hospitali ya taifa
Muhimbili, Taasisi ya Moi na Taasisi ya Jakaya Kikwete, pamoja na chuo kikuu
cha Muhimbil Kituo cha kudhibiti mifumo ya umeme cha Mikocheni kinachosimamia
mifumo yote ya umeme kwa jumla ukilinganisha
vituo vyote vya distribution, (usambazaji), ukaunganisha na vituo vya
uzalishaji umeme kama vile Kinyerezi I na II, ukaunganisha na vituo vya transmission
(kusafirisha) Backborne, Makambako-Songea na miradi mingine mingi, vitafanya
nchi yetu iweze kupata umeme wa kutosha.” Alifafanua.
Mhandisi
Mramba pia aliwaambia wahariri hao kuwa agizo alilolitoa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, wa kupeleka umeme kwenye kiwanda cha
Bakhresa kilichoko Mwandege tayari umeme umeshafika.
Mhandisi
Mramba amesema, kwa sasa TANESCO inatekeleza miradi mbalimbali ya umeme kote
nchini ili kuhakikisha taifa linapata umeme wa uhakika na ulio bora.
Miradi
hii ya Dar es Salaam, itakamilika ifikapo Aprili mwakani, alisema Mhandisi
Mramba.
Akielezea
lengo la ziara hiyo, Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Muhaji alisema, ni
kuwawezesha wahariri kuona na kuwafahamisha wananchi jinsi serikali ilivyofanya
uwekezaji mkubwa wa katika sekta ya umeme. “Mnaweza kuona kwamba umeme
unaopatikana sasahivi ni bora zaidi ukilinganisha na ule uliokuwa ukipatikana
miaka michache ya nyuma,” Alisema.
Aidha
Mhandisi Mramba alisema miradi ya TANESCO inayotekelezwa hivi sasa nchi nzima
ina thamani ya zaidi ya shilingi Trilioni 5 za kitanzania.
Meneja
Mwandamizi wa Usambazaji Umeme wa Shirika la
Umeme Tanzania, (TANESCO), ambaye pia ndiye Meneja wa Mradi wa
kuimarisha
miundombinu ya Umeme, Injinia Theodory Bayona, (kulia), akielezea hatua iliyofikiwa
hadi sasa ya uboreshaji miundombinu ya umeme jijini Dar es Salaam
Meneja
Mwandamizi wa Shirika hilo kanda ya Dar es Salaam na Pwani Mhandisi, Mahende
Mgaya.
Meneja
Mwandamizi wa Miradi ya Usafirishaji na Usambazaji Umeme wa Shirika hilo,
Mhandisi Gregory Chegere
Kituo cha City Centre.
Mhandisi Mramba akiwa na wahariri na waandishi wa habari kwenye gari wakati wa ziara hiyo
Mhandisi Mramba, akifafanua jambo wakati wahariri na waandishi walipotembelea kituo cha City Centre.
Tarehe 1 Desemba kila mwaka ni siku ya
maadhimisho ya Ukimwi Duniani,mwaka huu 2016 Kampuni ya Uchimbaji Madini
ya dhahabu ya Acacia kupitia mgodi wa Buzwagi uliopo wilayani Kahama
mkoani Shinyanga imeadhimisha siku hiyo kwa kuzindua Mashindano ya mpira
wa miguu na pete “Mahusiano Cup” ili kuhamasisha jamii inayozunguka mgodi huo kupima virusi vya Ukimwi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na
wafanyabiashara wa Arusha kwenye Kituo cha Mikutano cha Arusha (AICC) Desemba
2, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
|
No comments:
Post a Comment