Baadhi ya Watendaji wa Kampuni ya
Pan- African Energy, wakimsikiliza Waziri wa Nishati, Profesa Sospeter
Muhongo (katikati), wakati wa kikao chake na kampuni hiyo inayozalisha
gesi ya Songosongo. Wengine ni watendaji kutoka Shirika la Maendeleo ya
Petroli Tanzania (TPDC) na Wizara ya Nishati na Madini.
Mkurugenzi wa Mkondo wa Chini wa
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dkt. Wellington Hudson
akieleza jambo wakati wakati wa kikao baina ya Waziri wa Nishati na
Madini, TPDC na Kampuni ya Pan- African Energy.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya
Dodsal Hyrdocarbons Pilavullathil Surendran akiwasilisha taarifa kuhusu
maendeleo ya shughuli za Kampuni hiyo inayotafiti gesi katika Bonde la
Mto Ruvu. Wanaofuatilia ni Watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini,
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), na baadhi ya
wawasilishi ya kampuni hiyo.
Waziri wa Nishati na Madini,
Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akiongea jambo katika kikao baina
yake na kampuni ya Dodsal Hydrocarbons inayotafiti gesi katika Bonde la
Mto Ruvu. Wengine ni Watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini, TPDC
na wawakilishi wa kampuni hiyo.
Wawakilishi wa Kampuni ya Pan-
African Energy inayozalisha gesi ya Songosongo, wakimsikiliza Waziri wa
Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo wakati wa kikao baina yake
na kampuni hiyo. Wengine wanafuatilia ni Watendaji kutoka Wizara ya
Nishati na Madini na TPDC.
………………………..
Waziri wa Nishati na Madini,
Profesa Sospeter Muhongo, kwa nyakati tofauti leo tarehe 2 Desemba,
2016, amekutana na kampuni zinazofanya Utafiti na Uchimbaji wa Gesi na
Mafuta nchini za Pan-African Energy and Dodsal Hydrocarbons ikiwa ni
utaratibu wa kukutana na kampuni zote zinazofanya shughuli hizo kila
baada ya miezi mitatu, kwa lengo la kujadili maendeleo ya utekelezaji wa
shughuli za kampuni hizo nchini.
Kampuni ya Dodsal Hydrocarbons
inafanya utafiti wa gesi katika Bonde la Mto Ruvu na kampuni ya Pan-
Africa Energy inazalisha gesi ya SongoSongo.
No comments:
Post a Comment