Mwakilishi wa benki ya NMB, Doris
Kilale, (Kushoto), akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi
Milioni 10, kwa Mwenyekiti wa muda wa TBN, Joachim Mushi wakati wa hafla
hiyo fupi iliyofanyika Desemba 2, 2016 kwenye ukumbi wa Idara ya habari
Maelezo jijini Dar es Salaam.
NA MWANDISHI MAALUM
BENKI
ya NMB imetoa shilingi Milioni 10, kwa Mtandao wa Wamiliki/Waendesha Mitandao
ya Kijamii nchini Tanzania, (TBN), jijini Dar es Salaam, Desemba 2, 2016.
Akizungumza
kwenye mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo
jijini Dar es Salaam, mwakilishi wa benki hiyo, Doris Kilale alisema, NMB
inatambua kuwa TBN ni wadau wakubwa na benki hiyo katika kuhabarisha umma, kwa
hivyo benki imeona isaidie ili kufanikisha mkutano huo unaotarajiwa kuanza
Jumatatu Desemba 5 jijini Dar es Salaam.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa muda wa TBN, Joachim Mushi alisema, TBN ambayo ilisajiliwa rasmi na Serikali Aprili mwaka
jana, 2015 kwa kushirikiana na wataalam wa masuala ya habari na mitandao ya
kijamii imeandaa semina kwa wanahabari hawa wa mitandao ya kijamii hasa
'Bloggers' wapatao 150 kutoka bara na visiwani.
Alisema
mkutano huo ambao utaenda sambamba na mafunzo kwa wana TBN yatakayolenga
kujenga uwezo juu ya uendeshaji mitandao ya jamii kwa manufaa, upashaji habari
kwa kutumia mitandao yao kwa kuziangatia maadili na namna ya kunufaika na
mitandao hiyo kwa waendeshaji (kujipatia kipato).
Mhandisi wa umeme wa Shirika la Umeme nchuini Tanzania TANESCO, akiwa kazini jijini Dar es Salaam
SHIRIKA la Umeme
Tanzania (TANESCO) linawatangazia wateja wake wa Mikoa ya Dodoma, Singida,
Shinyanga, Tabora, Mwanza, Geita, Mara,
Simiyu na na baadhi ya maeneo ya Mikoa ya
Arusha, Manyara, Kilimanjaro na
Tanga na baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Dar es Salaam (Tazara, Mlimani City,
Mandela Road, Ubungo na Kimara, Sinza, Mabibo) kuwa yatakosa Umeme siku ya
Jumapili DESEMBA 04, 2016 kuanzia saa 02:00 Asubuhi hadi saa 11.00 Jioni.
SABABU: Kuruhusu
Mkandarasi anayejenga Njia Kuu ya Kusafirisha Umeme ya Msongo Mkubwa ya
Kilovolti 400 maarufu kama (Backbone Transmission Line 400 kV) kutoka Iringa
hadi Shinyanga.
SABABU: Kuzimwa
kwa njia ya Umeme ya Msongo wa Kilovolti 33 Kituo cha Ubungo Dar es Salaam
ilikumruhusu Mkandarasi kufanya matengenezo.
Matengenezo hayo
yanalenga kuboresha na kuimarisha hali ya upatikanaji wa Umeme Nchini.
Uongozi unaomba
radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
Imetolewa na;
Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao
Makuu
Mhe.Waziri Balozi Dkt.Mahiga akivalishwa skafu maalum |
Mhe.Waziri Balozi Dkt. Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mhe.Abdulla Ibrahim Ghanim Alsuwaidi |
Wageni waalikwa wakifuatilia jambo |
Balozi wa Taifa la Umoja wa Falme za Kiarabu Mhe.Abdulla Ibrahim Ghanim Alsuwaidi akizungumza wakati wa maadhimisho |
Mhe. Waziri Balozi Dkt. Mahiga akitoa hutuba fupi wakati wa maadhimisho ya sherehe hizo |
Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati Balozi Abdalla Kilima akisalimiana na Mhe. Balozi wakati wa sherehe za maadhimisho |
Tanzania
na Umoja wa Nchi za Kiarabu (UAE) zimepiga hatua kubwa za ushirikiano
hususan wa kiuchumi ambapo kwa takwimu za Kituo cha Uwekezaji Tanzania
(TIC) hadi Juni, 2015 Makampuni 67 kutoka UAE yamewekeza hapa nchini
katika sekta mbalimbali kwa mtaji wa thamani ya Dola za Marekani
milioni 497.12 na kuajiri Watanzania zaidi ya 9,044.
Hayo
yalibainishwa jana katika sherehe za kuadhimisha Siku ya Kitaifa ya UAE
zilizofanyika jijini Dar Es Salaam ambapo Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga alikuwa
Mgeni Rasmi.
Tanzania
na UAE zinatarajiwa kufanya Mkutano wa Kwanza wa Tume ya Pamoja ya
Kudumu ya Ushirikiano (JPC) ambao utakuwa chachu ya kuimarisha mahusiano
baina ya nchi hizi mbili hususan ya kiuchumi.
Akiongea
katika hafla hiyo, Mhe. Waziri alilipongeza taifa hilo kwa kuadhimisha
siku yake ya Kitaifa ikiwa imepiga hatua kubwa ya kimaendeleo ya
kichumi, kijamii na kisiasa. Mhe. Waziri alisema kuwa siku hiyo ni
inatoa fursa pia ya kutathmini mahusiano mazuri yaliyopo baina ya
Tanzania na UAE.
Kwa upande wake, Balozi wa UAE hapa nchini, Mhe. Abdulla Ibrahim Ghanim Alsuwaidi aliishukuru
Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano mkubwa inayotoa kwa Ubalozi huo
ambao unamwezesha kutekeleza majukumu yake kwa wepesi ikiwa ni pamoja na
kuimarisha mahusiano ya nchi hizi mbili. Mhe. Balozi aliahidi
kuendeleza ushirikiano huo hususan katika kutimiza azma ya Serikali ya
Awamu ya Tano ya Kuifanya Tanzania kuwa nchi ya Viwanda.
Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) unajumusha falme saba ambazo ni Abu Dhabi, Dubai, Sharjah, Ras Al Khaimah, Fujairah, Ajman na Umm al-Quwain huadhimisha siku yake ya Kitaifa tarehe 02 Disemba ya kila mwaka tokea mwaka 1971.
Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Allen Kijazi, (katikati), akiwa na Meneja Utalii na masoko wa Tanapa, Ibrahimu Musa kushoto na Mkurugenzi wa kampuni ya Zara, Zainabu Ansell wakati wa mkutano wao na waandisi wa habari juu ya maandalizi ya miaka 55 ya uhuru ambayo yanatarajiwa kufanyika Desemba 9, 2016
katikati ni Mkurugenzi wa Tanapa Allen Kijazi (wakwanza kushoto), akizungumza na waandishi wa habari. kushoto ni Meneja Utalii na masoko wa Tanapa, Ibrahimu Musa. Kulia ni Meneja uhusiano wa Tanapa, Paschal Shelutete
Habari Picha na Woinde Shizza,Arusha
Aliyekuwa
mkuu wa majeshi na mwenyekiti wa bodi ya tanapa jenerali msataafu
geogre waitara anatarajiwa kuongoza msafara wa zoezi la kupanda mlima
kilimanjaro desemba 5 hadi kumi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka
55 ya uhuru wa tanzania,
Aidha
katika msafara huo wa kupanda mlima kilimanjaro watakuwepo pia
wanajeshi kutoka jeshi la wananchi tanzania pamoja na wanahabari ambao
watakuwa wanahabarisha jamii kuhusiana na tukio hilo.
Akizungumza
na vyombo vya habari mkurugenzi mkuu wa tanapa allan kijazi alisema
kuwa mwaka huu tanzania itaadhimisha miaka 55 ya uhuru na hivyo shrikia
hilo imeshirikiana na kampuni ya utalii ya zara pamoja na bodi ya utalii
(ttb) kuandaa zoezi la kupanda mlima kilimnajro ili kuweza kuhamasisha
watanzania kuvifahamu vifutio vya utalii.
Alisema
kuwa zoezi hilo la upandaji mlima litahusissha baadhi ya viongozi
mashuhuri wa jeshi awastaafu akiwemo aliyekuwa mkuu wa majeshi ili
kuhamasisha watanzania waweze kupanda mlima ambapo tukio hilo
litajulikana kama Uhuru Epedition .
Kijazi
alifafanua kuwa pamoja na kuadhimisha uhuru wa nchi ,lakini madhumuni
mengine ya zoezi hilo ni kuhamasisha utalii na kuhimiza uhifadhi wa
mazingira kwani bado watanzania wengi hawana muamko wa kutembelea
vufutio vya utalii hivyo kujikuta asilimia kubwa ya watalii ni kutoka
nje ya nchi.
"Katika
maadhimisho haya tuna malengo ya kuhamasisha watanzania ili wajitokoze
kupanda mlima kilimanajaro pamoja na kutembela hifadhi mbali mbaki kwani
tunavyo vivutio 16 ambavyo vipo ndani ya tanzania na vinahitaji
watanzania wote wanufaike navyo sio tu wageni kutoka nje ya nchi bali
hata wa hapa wajue wanazo fursa "aliongeza kijazi.
Kwa
upande wake mkurugenzi wa zara Zainabu Ansell alisema kuwa watanzania
wanapaswa kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo la kihistoria kwani
wengi wao wamekuwa na mawazo potofu ya kufikiria wanaopaswa kupanda
mlima na kutembelea hifadhi ni wazungu tu na wageni kutoka nje ya nchi
hali inayowafanya watanzania kupoteza haki yao.
Kauli mbiu ya zoezi la kupanda mlima kilimanjaro mwaka huu ni endelea kuweka mazingira safi na salama ya fahari ya afrika.
So fresh and so clean.
Mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafuri akizungumza na wananchi wa Mjini Njombe katika mkutano wake wa Hadhara
Baadhi ya wakazi mjini njombe wakisikiliza mkutano wa mkuu wa wilaya ambapo walipata nafasi ya kutoa maoni yao
WANANCHI
halmashauri ya Mji wa Njombe wamemuomba mkuu wa wilaya hiyo Ruth
Msafiri kuiamuru halmashauri hiyo kuwagawia wananchi viwanja
vilivyopimwa ambapo katika halmashauri hiyo tangu mwaka 2012 hakujapimwa
tena viwanja.
Wananchi
wanatoa kero zao wakati wa mkutano wa kwanza wa mkuu wa wilaya na
wananchi ambapo ni kitu cha kwanza kufanyika wilayani hapo.
Nestori
Kigae akitoa kero yake kwa mkuu wa Wilaya ya Njombe alisema kuwa
halmashauri hiyo haigawi viwanja kwa vijana na kuwa sasa ni muda mrefu
viwanja havijagawiwa na kusasabisha wananchi kukosa maeneo ya kujenga.
Alisema kuwa vijana wapo tayari kujenga makazi yao lakini halmashauri hiyo haipimi viwanja na kuvigawa kwa wananchi.
Mkuu wa wilaya alitoa nafasi kwa afisa wa Ardhi kujibu masuala yanayo husu ardhi yaliyo ulizwa na wananchi.
Afisa
ardhi Taday Kabonge alisema kuwa halmashauri yake ilipima viwanja mwaka
2012 lakini mpaka sasa haijawahi kupima na kuwa kuna viwanja ambavyo
mpaka leo bado vipo havijachukuliwa.
Alisema
kuwa viwanja vinavyo gawiwa na halmashauri vinauzwa na havigawiwi bure
kwa wananchi na kuwa vinatolewa kwa wananchi wote wa halmashauri hiyo.
Katika
hotuba ya mkuu wa wilaya ya Njombe ya lisaa limoja kwa wananchi anasema
kuwa serikali itahakikisha kero kwa wananchi zinaondoka na kuishi kwa
amani bila bughuza.
Hata
hivyo aliitaka halmashauri hiyo kuhakikisha kuwa inapima viwanja mara
kwa mara ili wananchi wake kuendelea kupata maeneo ya kujenga na
kuachana na kujenga maeneo ambayo hayahusiki.
Alisema
kuwa haiwezekani halmashauri ikapima viwanja kila mara na sio baada ya
miaka minne, na kuwa wananchi wanajenga kila wakati.
Hata
hivyo diwani wa kata ya Njombe Mjini, Agrey Mtambo alilalamika viwanja
vinavyo pimwa na halamshauri kuuzwa bei ghari na kusababisha wananchi
kushindwa kuvimiliki.
Badhi ya watumishi wa halmashauri ya Mji
Makambako wakimsikiliza mkuu wa mkoa alipo fika katika Halmashauri yao
kujia shina ma matatizo yao
Mkuu wa mkoa wa njombe Dr Rehema Nchimbi Akizungumza na wafanyakazi wa halmashauri ya Makambako
SERIKALI mkoani Njombe imetoa ruhusa ya kujenga nyumba mama
mjane ambaye amezuiriwa na Jeshi la polisi wilaya ya kipolisi Makambako
kutokana na eneo hilo kuwa na mgogoro baina yake na jeshi hilo kwa kuwa
majirani wa mama huyo wameruhusiwa kujenga.
Kauli hiyo inatolewa na mkuu wa mkoa wa Njombe Dr. Rehema
Nchimbi baada ya kupata taarifa za kuwapo kwa mkanganjiko wa kiwanja cha mjane
huyo na kuwapo kwa mvutano mrefu baina ya yake na jeshi la polisi wakati akiwa
na mkotano na watumishi wa halmashauri ya mji Makambako ambako yupo katika ziara
ya kikazi mkoani humo.
Dr. Nchimbe anasema kuwa mama huyo ajenge kama majirani zake
walivyo ruhusiwa kujenga maeneo hayo na wakati watakavyo bomoa kwa majirani
wengine basi wabomoe kwa wao wote.
Alisema kuwa haiwezekani mama huyo akazuiliwa kujenga wakati
wajirani zake wameruhusiwa kujenga na kuwa kwa kuwa watu hao walijenga kiholele
basi hata mama huyo ajenge kiholela.
Hata hivyo mkuu wa mkoa aliingia katika majibizano ya maswali
na majibu na afisa mipango walipo kuwa akimuhoji afisa mipango wa halmashauri
hiyo Ephahim Mkambo.
Mkuu wa mkoa: kwanini mama huyo haruhusiwi kujenga.
Afisa mipango: mama huyo yupo katika eneo la polisi na
haruhusiwi kujenga eneo hilo.
Mkuu wa mkoa: Kwanini majirani zake waliruhusiwa kujenga,
eneo hilo.
Afisa mipango: Hawa wengine walijenga kiholela na wenye eneo
walishindwa kudhibiti mikapa yao.
Mkuu wa Mkoa: sasa naamuru naye huyu mama ajenge eneo hilo
kihilele na watakapo kuwa wakibomoa wabomolewe wote haiwezekani akazuiwa mmoja
na wengine wakaruhusiwa.
Mkuu wa mkoa baada ya kutoa ruhusa ya ujenzi kwa mjane huyo
alimuonya mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Makambako Paulo Malala kuto saini
karatasi za watu wa ardhi kwa kuwa wamekuwa wakishindwa kufanya kazi zao kwa
usahihi na kufanya kwa ujanja ujanja.
“Nakuonya Mkurugenzi wewe usisaini karatasi za watu wa ardhi
watakuingiza matatani hawa ni wajanja wajanja kuwa majini nao,” alisema Dr.
Nchimbi.
Katika mkutano wake huo na maafisa na wakuu wa Idara walitoa
maoni yao mbalimbali na changamoto zao ambazo zinawakabili kutekeleza majukumu
yao na kufanya kazi za wananchi.
Afisa utumishi wa halmashauri hiyo Frederick Kazikuboma alisema
kuwa halmashauri hiyo inaupungufu wa magari, na rasisimali watu ambapo kuna
idara zinawafanyakazi wacheche.
Hata hivyo Dr. Kyunga Ernest, ni Afisa afya na ustawi wa
jamii Halmashauri ya Makambako alisema kuwa pamoja na kuwa na kituo cha afya
katika halmashauri hiyo changamoto kubw ani kuto kuwapo kwa chumba cha upasuaji
licha ya kuanza ujenzi wake na baadhi ya vifaa kuwanavyo.
Alisema kuwa pamoja na changamoto hiyo halmashuri imekuwa
ikipokea fedha za kituo cha afya huku huduma zinazotolewa zikiwa ni za
hospitali kutokana na watu wanaofika Hospitalini hapo.
No comments:
Post a Comment