Waziri wa Fedha, Dk. Philip Mpango
(kulia), akikata utepe kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
kuashiria kuzindua rasmi Kituo cha Taaluma ya Uhasibu (APC), kilichopo
Bunju jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa
ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), Profesa Isaya Jairo na
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa GEPF, Joyce Shaidi.
Mwonekano wa baadhi ya majengo ya kituo hicho.
Mwonekano wa ukumbi wa mikutano wa kituo hicho.
Katika hafla ya kufungua kituo hicho nyama choma zilikuwepo ingawa mimi sikubahatika kupata walau finyango moja.
Waziri wa Fedha, Dk. Philip Mpango, akisalimiana na
wageni waalikwa.
Waziri wa Fedha,
Dk. Philip Mpango (wa tatu kushoto), akiwa na viongozi wengine akitoka
kukagua vyumba vya kupumzikia vya kituo hicho.
Wanataalumu ya Uhasibu wakiwa kwenye hafla hiyo ya ufunguzi wa kituo hicho pamoja na kongamano lao la 2016 la siku tatu.
Wasanii Mpoto Mrisho na Banana Zoro wakitoa burudani
kwenye hafla hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), Profesa Isaya Jairo, akitoa taarifa fupi.
Mkutano ukiendelea.
Mwenyekiti wa Bodi wa GEPF Joyce Shaidi akitoa shukrani kwa mgeni rasmi.
Picha ya pamoja na mgeni rasmi na viongozi wa bodi ya NBAA na Mfuko wa GEPF
Picha ya pamoja.
Na Dotto Mwaibale
SERIKALI imeitaka Bodi ya Taifa ya
Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) kutoa hadharani majina ya wahasibu
wabadhilifu ili jamii iweze kuwatambua.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha
Dk.Philip Mpango kwa niaba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati
akizindua Kituo cha Taaluma ya Uhasibu (APC), kilichopo Bunju na
Kongamano la Uhasibu la 2016 la siku tatu Dar es Salaam leo.
"Ni vizuri mkaanza kutoa hadharani majina ya wahasibu wasio waadilifu ili jamii iweze kuwajua" alisema Mpango.
Mpango alisema kukamilika kwa ujenzi wa
kituo hicho kutaisaidia serikali kuelekeza fedha zilizokuwa zikitumika
na bodi hiyo kukodi kumbi kwa kazi zake mbalimbali kupelekwa kufanya
kazi zingine za maendeleo.
"Nawaombeni mkitunze kituo hiki ili kitimize malengo yake ya kuleta manufaa kwa wananchi na taifa kwa ujumla" alisema Mpango.
Aliwataka wahasibu nchini kutumia
taaluma yao kuisaidia serikali hasa katika kipindi hiki cha nchi
kuelekea kwenye uchumi wa viwanda badala ya wao kushirikiana na
wafanyabishara wasio waaminifu kuiibia serikali.
Mpango alisema kuwa serikali itaendelea
kuwatumbua watumishi wasio waaminifu na wahasibu bila ya kumuonea
muhusika huruma na kuwa atakayebainika atapelekwa mahakama ya mafisadi
iliyofunguliwa.
Mkurugenzi Mkuu wa NBAA Pius Maneno
alisema katika kipindi cha maiaka 12 iliyopita walikuwa wakitumia sh.
biliobi 1.5 kwa ajili ya gharama za kulipia kumbi hivyo ujenzi wa kituo
hicho utaondoa changamoto hiyo na kuwa kitakuwa ni chanzo cha mapato.
Mwenyekiti wa Bodi ya NBAA Profesa Isaya
Jairo alisema kituo hicho kimejengwa kwa mkopo wa sh.bilioni 15 kutoka
Shirika la Hifadhi ya Taifa (NSSF), Mfuko wa GEPF bilioni 10 na Wahasibu
na Wakaguzi walichangia Bilioni 8.
Alisema awali walikadiria ujenzi huo
ungekamilika kwa gharama za sh. bilioni 14 lakini kutokana na sababu
mbalimbali kukamilika kwake kumefikia sh. bilioni 33 zaidi ya kiasi
kilichokuwa kimepangwa.
Mwenyekiti wa Bodi wa GEPF Joyce Shaidi
aliishukuru serikali kwa ushirikiano na mifuko ya jamii na NBAA hasa
katika suala zima la kusukuma maendeleo ya nchi ikiwa na kuzitaka
taasisi zake kwenda kukodi ukumbi wa kituo hicho cha kimataifa ili
kusaidia kurejesha fedha zilizokopwa kukijengea.
Mwenyekiti Mteule wa Chama cha Afya ya
Jamii Tanzania (TPHA), Shaibu Mashombo (wa nne kushoto), akiwa na
viongozi wenzake wateule waliochaguliwa katika mkutano mkuu wa chama
hicho 2016 jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Dismas Vyagusa,
Violeth Shirima, Dk. Godfrey Swai, Dk.Nderineia Swai, Dk. Feliciana
Mmasi, Dk. Mwanahamisi Hassan na Dk.Elihuruma Nangawe ambaye alikuwa
Mwenyekiti wa chama hicho aliyemaliza muda wake.
Mwenyekiti wa Chama cha Afya ya Jamii
Tanzania (TPHA), aliyemaliza muda wake Dk.Elihuruma Mangawe (katikati),
akiongoza kikao cha mkutano mkuu wa chama hicho. Kushoto ni Katibu Mkuu
wa TPHA, Fabian Magoma na kulia ni Ofisa Utawala wa chama hicho, Erick
Goodluck.
Mwenyekiti
Mteule wa Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA), Shaibu Mashombo
(kulia) akiwaelekeza jambo wajumbe kabla ya kufanyika kwa uchaguzi
uliompa nafasi hiyo.
Wajumbe wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Wajumbe wa mkutano huo.
Usikivu katika mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Na Dotto Mwaibale
CHAMA cha Afya ya Jamii (TPHA) kimepata viongozi wapya ambapo kimemchagua Dk. Shaibu Mashombo kuwa Mwenyekiti.
Mashombo alishinda nafasi hiyo kwa kupata kura 35 na kumbwaga Feliciana Mmassy aliyepata kura 10 na kura moja ikiharibika.
Katika nafasi ya Mhariri Mkuu Dk.Godfrey
Swai aliibuka kidedea dhidi ya Ndeniria Swai aliyepata kura 15 na kura
tisa zilikataa ambapo katika nafasi ya Katibu Mwenezi wagombea walikuwa
wawili Elizabeth Nchimbi aliyepata kura 15 na Ndeniria Swai ambaye
aliibuka mshindi kwa kupata kura 29 huku kukiwa hakuna kura iliyopotea.
Katika nafasi ya Mtunza Fedha licha ya
kuwepo na ushindani makali aliyeibuka mshindi ni Mwanahamisi Hassan
ambaye alipata kura kura 20 dhidi ya mgombea mwenzake Violeth Shirima
aliyepata kura 24.
Nafasi ya Katibu wa Mipango ilikwenda
kwa Dk. Mwanahamisi Hassan aliyepata kura 38 dhidi ya Othman Shem
aliyeambulia kura tano huku Feliciana Mmasi na Dismas Vyagusa wakishinda
nafasi ya wajumbe wa kamati ya utendaji.
Wakati
wanachuo wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) cha mjini Mbeya
wakiahidi kupeleka vijijini kampeni ya malengo ya maendeleo endelevu
(SDGs) Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez amesema
kwamba utekelezaji wa malengo hayo uko mikononi mwa vijana zaidi.
Alisema nchini Tanzania zaidi ya nusu ya watu wake ni vijana hivyo
wakielewa malengo hayo itakuwa rahisi kushawishi wengine kuhuisha
maendeleo hayo na shughuli zao za kila siku huku wakitunza mazingira.
Alisema shauri kwanini malengo yamekuwa mengi wakati yale ya Milenia
yalikuwa nane tu, Mratibu huyo alisema kwamba suala si uwingi wa malengo
bali maana yake na haja ya utekelezaji.
Mkuu
wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) cha jijini Mbeya, Dr. Daniel
Mosses akimkaribisha na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa
nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez
aliyemtembelea ofisini kwake mjini Mbeya.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)
Alisema
MDGs (Malengo ya Millennia) iliacha masuala kadhaa bila uelekeo ikiwamo
suala la mazingira na mabadiliko ya tabia nchi na hivyo kuwapo kwake
kunahakikisha uwapo wa maendeleo endelevu kwa kuwa kila kitu kinategemea
sana mabadiliko ya tabia nchi kwa sasa. Alisema ni matumaini yake
kwamba kuzinduka kwa jamii ya vijana itasaidia kukabiliana na changamoto
hizo za sasa za dunia. Kauli ya mratibu huyo iliungwa mkono na wanachuo
hao ambao walisema kwamba wanaona uhalisia wa mahitajhi ya sasa na
kwamba watawasilisha kampeni hiyo maeneo wanayotoka ili kuwapo na
mabadiliko.
Mkuu
wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) cha jijini Mbeya, Dr. Daniel
Mosses akiwa kwenye mazungumzo na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro
Rodriguez aliyeambatana na Mtaalam wa Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa
Mataifa nchini, Hoyce Temu.
Kwa
kuwa wengi ni vijana na kwa kuwa asilimia 75 ya vijana wanaishi
vijijini, itakuwa heri kama walivyofundishwa na Umoja wa Mataifa
kupeleka salamu vijijini ili kukabiliana na tatizo la mazingira na
mabadiliko ya tabia nchi ambayo yanafumua misimu ya kilimo na
upatikanaji wa mvua. Kushirikisha vijana ni suala la msingi sana, hasa
ikizingatiwa kwamba sehemu kubwa ya vijana wanatoka vijijini ambako
malengo ya maendeleo endelevu yana maana zaidi kwa umma, alisema Kidai
Kabula Shaban, Mwanafunzi anayesomea Shahada ya Sanaa, Sosholojia na
Kazi za Jamii.
Mkuu
wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) cha jijini Mbeya, Dr. Daniel
Mosses akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez kuendesha semina ya malengo ya dunia
(Global Goals) kwa wanafunzi wa chuo hicho iliyofadhiliwa na Umoja wa
Ulaya (EU).
Amesema
amefurahishwa mno na mpango huo wa kuelimisha vijana hasa utunzaji wa
mazingira ili kukabiliana na tabia nchi. Alisema yeye alivyoelimishwa
basi atahakikisha anawaelimisha wengine kuwa watekelezaji wa maendeleo
hayo. Akirejea mazungumzo ya mwanafunzi huyo kwa niaba ya wenzake.
Alvaro alisema amefurahishwa na mwamko wa vijana wa kutaka kujua malengo
hayo na ni imani yake kwamba kwa kuwakujua wao basi jamii itaerevuka
mapema zaidi.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akiendesha semina kuhusu malengo
ya maendeleo endelevu (SDGs) kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Teofilo
Kisanji (TEKU) cha jijini Mbeya iliyofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU).
Mtaalam
wa Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu
akiwapiga msasa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji jijini Mbeya
wakati wa semina kuhusu malengo ya maendeleo endelevu (SDGs)
iliyofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU).
Mtaalam
wa Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu
akifafanua jambo wakati wa semina ya malengo ya maendeleo endelevu
(SDGs) kwa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji jijini Mbeya iliyofadhiliwa na
Umoja wa Ulaya (EU).
Mwalimu
wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji cha jijini Mbeya, Furaha Komoro
akiuliza swali kuhusu juhudi za Umoja wa Mataifa katika kuhakikisha
usawa wa kijinsia unakuwa na uwiano sawa pande zote.
Mwanafunzi
wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji akishiriki kutoa maoni kwenye semina
ya malengo ya dunia iliyoandaliwa na Umoja wa Mataifa na kufadhiliwa na
Umoja wa Ulaya (EU).
Mwanafunzi
anayesomea Shahada ya Sanaa, Sosholojia na Kazi za Jamii chuoni hapo,
Kidai Kabula Shaban akiuliza swali kwa mkufunzi (hayupo pichani) wa
malengo ya maendeleo endelevu (SDGs).
Pichani
juu na chini ni sehemu ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji
jijini Mbeya walioshiriki semina ya malengo ya maendeleo endelevu (SDGs)
iliyofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU).
Mmoja
wa washiriki akipitia kijarida cha malengo ya maendeleo endelevu (SDGs)
katika semina iliyofanyika Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji jijini Mbeya.
Picha
juu na chini ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini
na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez katika
picha ya pamoja na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji cha
jijini Mbeya waliohudhuria semina ya malengo ya dunia (Global Goals)
iliyofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU).
Pichani
juu na chini ni semina maalum ya mabalozi wa malengo ya maendeleo
endelevu (SDGs Champions/Global Goals Champions) wakipigwa msasa wa SDGs
na Mtaalam wa Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce
Temu (hayupo pichani).
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akikabidhi cheti kwa Balozi wa
Malengo ya Maendeleo Endelevu (Global Goals Champion) Manafunzi wa Chuo
Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) ambaye pia ni mrembo wa taji la Miss
Mbeya 2016, Eunice Robert.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na mabalozi
wa malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) Global Goals Champions wakiwa
wameshikilia vyeti vyao mara baada ya kuhitimisha semina maalum kwa
mabalozi hao.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na mabalozi
wa malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) Global Goals Champions wa Chuo
Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) cha jijini Mbeya wakiwa wameshikilia
baadhi ya SDGs.
Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla amelishukuru Shirika la Umoja wa Mataifa
kwa misaada na ushirikiano kwa serikali ya Tanzania ikiwemo huduma kwa
kambi za wakimbizi, Mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana yenye kauli mbiu
ya Vijana - Fursa na misaada mingi katika shughuli za maendeleo Hayo
ameyasema wakati wa mazungumzo na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro
Rodriguez aliyemtembelea Mkuu huyo wa mkoa ofisini kwake. RC Makalla
amewahakikishia ushirikiano zaidi kwa mradi wa Vijana kutambua fursa na
kuzitumia utakaotekelezwa Mkoa wa Mbeya mwakani.
Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla (kushoto) akisalimiana na Mratibu Mkazi
wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo
(UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez aliyemtembelea ofisini kwake na kufanya
mazungumzo ya kuboresha ushirikiano baina ya Serikali na Umoja wa
Mataifa jijini Mbeya.(Picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog)
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akisaini kitabu cha wageni
ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla alipomtembelea ofisini
kwake na kufanya mazungumzo ya kuimarisha ushirikiano baina ya Serikali
na Umoja wa Mataifa jijini Mbeya.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akielezea dhumuni la safari
yake mkoani Mbeya kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla wakati
alipomtembelea Mkuu huyo wa mkoa na kufanya naye mazungumzo kwa lengo la
kuimarisha ushirikiano baina Umoja wa Mataifa na Serikali.
Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akielezea mipango aliyonayo ya kuinua
uchumi wa mkoa wake na kutatua tatizo la ajira kwa vijana ambalo limekua
changamoto kubwa nchini kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro
Rodriguez (katikati) aliyemtembelea ofisini kwake akiwa ameambatana na
Mtalaam wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu (kushoto).
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akitoa taarifa
zilizomo kwenye Ripoti ya Umoja wa Mataifa ya Mpango wa misaada ya
Maendeleo UNDAP II 2016-2021 kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla
alipomtembelea ofisini kwake na kufanya naye mazungumzo kwa lengo la
kuimarisha ushirikiano baina ya Umoja wa Mataifa na Serikali.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akimkabidhi
rasmi Ripoti ya Umoja wa Mataifa ya Mpango wa misaada ya Maendeleo UNDAP
II 2016-2021 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla alipomtembelea ofisini
kwake jijini Mbeya.
Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla katika picha ya pamoja na Mratibu Mkazi
wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyeambatana na
Mtalaam wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu (kulia)
nje ya jengo la ofisi za mkuu huyo wa mkoa.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez na Mkuu wa
mkoa wa Mbeya, Amos Makalla katika picha ya pamoja na "Orange car" ikiwa
ni wiki ya maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia:
'Elimu kwa wote" nje ya ofisi za mkuu huyo wa mkoa.
Mkuu
wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akiagana na Mratibu Mkazi wa Mashirika
ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la
Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyemtembelea ofisini kwake
na kufanya naye mazungumzo jijini Mbeya.
--
Zainul A. Mzige,
Operation Manager,
MO BLOG,
www.modewjiblog.com
+255714940992.
No comments:
Post a Comment