Mratibu wa Milele Zanzibar
Foundation Ali Bakari Amani akitoa maelezo ya Mradi wa Champion in
Health utakavyowasaidia wanafunzi watakaojiunga na mradi huo katika
kipindi cha miaka mitatu wakati wa utiaji saini katika Chuo cha Taaluma
za Sayansi za Afya kiliopo Mbweni Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Taaluma za
Sayansi za Afya Zanzibar Dkt. Amina Abdulkadir akitiliana saini na
Mkurugenzi Mtendaji wa Milele Zanzibar Foundation Yusouf Luiz mkataba
wa maridhiano ya kuimarisha huduma za Afya vijijini kupitia mradi wa
Champion in Health.
Baadhi ya wanachama wa Champion
in Health wakifuatilia utiaji saini mkataba wa maridhiano kati ya Milele
Zanzibar Foundation na Chuo cha Taaluma za Sayansi za Afya Zanzibar
katika sherehe zilizofanyika Chuoni Mbweni nje kidogo ya mji wa
Zanzibar.
Picha ya pamoja ya viongozi wa
Milele Zanzibar Foundation na Chuo cha Taaluma za Sayansi za Afya
Zanzibar na baadhi ya wanafunzi watakaofaidika na mradi wa Champion in
Health baada ya sherehe za utiaji saini kumalizika katika chuo hicho.
Picha na Makame Mshenga.
………………
Na Ramadhani Ali/Maelezo Zanzibar
Milele Zanzibar Foundation
imetiliana saini mkataba wa maridhiano na Chuo cha Taaluma za Sayansi za
Afya Zanzibar mradi wa kuboresha kiwango cha ubora wa utoaji wa huduma
za afya katika maeneo ya vijijini.
Mradi huo wa miaka mitatu
ujulikanao kwa jina la Champion in Health utaangalia changamoto za Afya
vijijini ambako kunaupungufu mkubwa wa wafanyakazi kutokana na vijana
wengi kukosa hamu ya kufanyakazi katika maeneo hayo.
Akizungumza wakati wa kutia saini
mradi huo katika Chuo cha Taaluma za Sayansi za Afya Mbweni, Mratibu wa
Milelele Foundation Zanzibar Ali Bakari Amani alisema vijana 98 wakiwemo
waliomaliza masomo mwaka huu 2016 na wengine wanaoendelea na masomo
Chuoni hapo watafaidika.
Aliyataja masharti ya wanafunzi
kuingia katika mradi huo kuwa ni wale waliofanya vizuri katika masomo,
wawe tayari kufanya kazi vijijini baada ya kumaliza masomo na wazee
wawe hawana uwezo wa kuwasomesha.
Ameyataja maeneo makuu ya Mradi
kuwa ni kuwapatia nafasi za masomo nje ya nchi wanafunzi walioteuliwa
kuingia katika mradi, kuwaendeleza na kuwajengea uwezo.
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Taaluma za
Sayansi za Afya Zanzibar Dkt. Amina Abdulkadir amewataka wanafunzi
walioingia katika maradi huo kuutumia vizuri msaada huo na amewashauri
kufuata sharti la kuwa tayari kufanya kazi sehemu yeyote watakayo
pangiwa.
Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya
Dkt Fadhil Abdalla aliipongeza Milele Zanzibar Foundation kwa kuangali
changamoto zinazoikabili jamii hasa vijijini na kuzitafutia ufumbuzi
unaofaa.
Amesema Wizara hivi sasa inatilia
mkazo kuimarisha ubora wa utoaji huduma vijijini baada ya maeneo mengi
kuwa na vituo vya afya na Milele Zanzibar Foundation imekuwa ikitoa
msukumo mkubwa katika sula hilo tokea kuanzishwa kwake miaka minne
iliyopita.
Mradi wa Champion in Health
umetiwa saini na Kaimu Mkuu wa Chuo cha Taaluma za Sayansi za Afya
Zanzibar DKT. Amina Abdulkari na Mkurugenzi Muendeshaji wa Milele
Zanzibar Foundation Yusouf Luiz Caires.
No comments:
Post a Comment