Kaimu Kamishna Jenerali wa
Magereza, Dkt. Juma Malewa akitoa hotuba yake fupi ya kufunga mwaka 2016
na kuukaribisha mwaka mpya 2017 kwenye Baraza la Maafisa na Askari
kutoka vituo mbalimbali vya Magereza Mkoani Dar es Salam Desemba 30,
2016 katika Bwalo Kuu la Maafisa Magereza Ukonga.
Naibu Kamishna wa Magereza, Edith
Mallya akimkaribisha Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma
Malewa(katikati aliyeketi) kabla ya kuongea na Maafisa na Askari wa
Jeshi la Magereza Mkoa wa Dar es Salaam katika Baraza Maalum la kufunga
mwaka 2016 na kuukaribisha mwaka mpya 2017(kushoto) ni Mkuu wa Magereza
Mkoa wa D ar es Salaam, SACP. Augustine Mboje. Baraza hilo limefanyika
Bwalo Kuu la Maafisa Magereza Ukonga, Dar es Salaam Desemba 30, 2016.
Kaimu Kamishna Jenerali wa
Magereza, Dkt. Juma Malewa akijibu kero mbalimbali zilizoulizwa na
Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Dar es Salaam(hawapo
pichani) katika Baraza Maalum la kufunga mwaka 2016 na kuukaribisha
mwaka mpya 2017
Askari wa Jeshi la Magereza kutoka
vituo mbalimbali vya Magereza ya Mkoa wa Dar es Salaam wakisikiliza
hotuba ya Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(hayupo
pichani) katika Baraza Maalum la kufunga mwaka 2016 na kuukaribisha
mwaka mpya 2017.
Afisa Utumishi wa Jeshi la
Magereza, Mrakibu wa Magereza Elmas Mgimwa akitolea ufafanuzi kuhusiana
na masuala ya kiutumishi yaliyoulizwa na Maafisa na Askari wa Jeshi la
Magereza Mkoa wa Dar es Salaam(hawapo pichani) katika Baraza hilo.
No comments:
Post a Comment