Pages

Saturday, December 31, 2016

MATUKIO MBALIMBALI YA PICHA YAKIONYESHA WAZIRI MKUU MAJALIWA AKICHANGISHA FEDHA ZA UJENZI WA SEKONDARI MPYA RUANGWA


mju1
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya Shilingi milioni sita kutoka kwa Mkurugenzi wa kampuni ya Pacco GEMS Limited, Bw. Mahendra Bardiya katika harambee  ya kuchangia ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari wilayani Ruangwa ambapo jumla ya shilingi milioni 138.26 zilichangwa. Harambee hiyo ilifanyika sambamba na  mkutano wa hadhara uliohutubia wa Waziri Mkuu mjini Ruangwa, Desemba 30, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
mju2 mju3
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea cheti maalum cha kutambua mchango wake katika kukijenga na kukiimarisha Chama cha Mapinduzi wilayani Ruangwa kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Lindi, Ali Mtopa katika mkutano wa hadahara aliouhutubia mjini Ruangwa Desemba 30, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
mju4
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha Cheti Maalum  cha kutambua mchango wake katika kukijenga na kukiimarisha Chama cha Mapinduzi wilayani Ruangwa alichokabidhiwa na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Lindi, Ali Topa   (kulia) katika mkutano wa hadhara aliouutubia mjini Ruangwa Desemba 30, 2016. Kushoto ni Katibu wa CCM wa wilaya ya Ruangwam Issa Njinjo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
mju5
 Wananchi wa Ruangwa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia mkutano wa hadhara mjini Ruangwa, Desemba 30, 2016. (Picha na Ofisi  ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment