Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mwenyeji wake Rais wa
Kenya, Uhuru Kenyatta wakiserebuka na wanakwaya katika eneo la Karen mara baada
ya kufungua barabara “mchepuko” ya (Nairobi Southern Bypass), nchini Kenya
Novemba 1, 2016. (PICHA NA IKULU)
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mwenyeji wake Rais wa
Kenya Uhuru Kenyatta, Naibu Rais wa Kenya William Rutto pamoja na viongozi
wengine, wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa barabara ya kupunguza msongamano
ya Nairobi Southern Bypass nchini Kenya.
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata maelezo kutoka kwa Bi.
Lucy Karuga kuhusu usindikaji wa mazao ya chakula katika kiwanda cha Maziwa cha
Eldoville katika eneo la Karen nchini Kenya.
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia usindikaji wa Samli
katika kiwanda hicho cha maziwa cha Eldoville nchini Kenya.
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mama Ngina
Kenyatta mama mzazi wa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakati alipomtembelea
nyumbani kwake Nairobi nchini Kenya.
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Mama
Ngina Kenyatta mama mzazi wa Rais Uhuru Kenyatta pamoja na Rais Uhuru
Kenyatta wakati alipomtembelea mama huyo
nyumbani kwake Nairobi nchini Kenya.
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais wa
Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na Mke wa Rais wa Kenya Mama Margaret Kenyatta
katika dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Rais Kenyatta kwenye Ikulu ya Nairobi, usiku wa kuamkia leo Novemba 1, 2016
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo huku akiwa
amewashika mikono kwa pamoja Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, Naibu Rais wa Kenya
William Ruto na Mke wa Rais wa Kenya Mama Margaret Kenyatta katika dhifa hiyo
ya kitaifa.
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mabalozi
mbalimbali wa Kenya waliohudhuria katika dhifa hiyo ya Kitaifa. (PICHA NA IKULU)
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akigonganisha glass na
mwenyeji wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta katika Ikulu ya Nairobi nchini
Kenya.
Rais wa Kenya
Uhuru Kenyatta akizungumza katika dhifa ya Kitaifa aliyomuandalia mgeni wake
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika Ikulu
ya Nairobi.
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza katika dhifa ya
Kitaifa aliyoandaliwa na mwenyeji wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta katika
Ikulu ya Nairobi.
Dusntan Tido Mhando, Mkuruhenzi wa Azam TV
K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
MTANGAZAJI
mkongwe nchini Dunstan Tido Mhando, “atamkabili” Rais John Pombe Magufuli,
katika mahojiano ya moja kwa moja yatakayofanyika Novemba 4, 2016 kuanzia saa 4
asubuhi.
Tido ambaye ni
Mkurugenzi wa Azam TV, na mwenye uzoefu wa karibu miaka 40 katika utangazaji,
atashirikiana na Mkurugenzi wa TBC, Dkt. Ayoub Ryoba kwenye mahojiano hayo
ambayo pia yatashirikisha wahariri wengine wa vyombo vya habari na kupeperushwa
moja kwa moja kupitia runinga.
Tido Muhando
ambaye awali alikuwa nchini Uingereza akifanyia kazi Shirika la Habari la Uingereza
BBC, kama mkuu wa Idhaa ya Kiswahili, anauzoefu mkubwa wa kufanya mahojiano “interview”
na marais mbalimbali barani Afrika.
Miongoni mwa
Maris aliowahi kuwafanyia mahojiano ni pamoja na hayati Rais Laurent Kabila wa
DRC, Rais mstaafu Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi, Rais
Mstaafu Jakaya Kikwete, na Hayati Mwalimu Nyerere
Tido anasifika
kwa ufundi wa kuuliza maswali yenye mantiki na bila woga. Kwa mujibu wa
wachambuziwa masuala ya habari, hii itakuwa fursa nzuri ya Rais Dkt. John Pombe
Magufuli, kuelezea tathmini yake ya utawala katika kipindi cha mwaka mmoja tangu
aingie madarakani Novemba iliyopita.
Akihojiwa na
mtangazaji mwingine gwiji wa Azam TV, Charles Hillary kwenye taarifa ya habari
ya saa mbili usiku Oktoba 31, 2016, Tido alsema, anatarajia mahojiano hayo
yatakuwa mazuri. “Baada ya jitihada nyingi tulizofanya za kufanya mahojiano na
Mheshimiwa Rais Magufuli kugonga mwamba mara kadhaa, safari hii Ikulu
imetukubalia na ninahakika yatakuwa mahojiano mazuri na motomoto,” Alisema
Tido.
Rais Dkt. John Pomba Magufuli, akiwa
amekamata ngao na mkuki siku alipoapishwa kushika madaraka yakuiongoza
Tanzania Novemba 2016.
Mkurugenzi wa TBC, Dkt. Ayoub Ryoba
Tido akifanya mahojiano na Rais mstaafu Jakaya Kikwete
Tido akifanya mahojiano na Hayati
Laurent Kabila, aliyekuwa Rais wa DRC. Inaelezwa kuwa mahojiano haya
ndiyo yalikuwa ya mwisho kwa rais huyo kuhojiwa na vyombo vya habari
hadi mauti yalipomkuta
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni (mwenye
mpama), "akikata kiu" kwenye nyumba moja, wakati wa ziara yake ya
nyumbakwa nyumba kuhamasisha wananchi kuondokana na umasikini kupitia
operesheni aliyoanzisha ya "Vumbua Utajiri".
RAIS wa Uganda,
Yoweri Kaguta Museveni, ameanza kampenio ya nyumba kwa nhyumba aliyoipa jina la
“Vumbua utajiri” ikiwa na lengo la kuhamasisha umma kuondokana na umasikinikwa
kutumia mazingira yanayowazunguka.
Ili kuthibitisha
kuwa yeye ndiye anaanza na wengine wanafuata kwenye operesheni hiyo ya “Wealth
creation), Rais Museveni alichapisha picha kadhaa kwenye ukurasa wake wa
Facebook Oktoba 31, 2016 akiwa kwenye Kawaumu wilaya ya Luweero, ambapo
alionekana akikokota baiskeli iliyokuwa na dumu, akitoka kuchota maji ili
akamwagilie shamba lake la kahawa na ndizi.
Katika maneno
yake aliyochapisha kwenye ukurasahuo Rais alisema “Leo ni sikuya tatau ya
operesheni yangu ya Uvumbuzi wa utajiri hapa Luweero, Asubuhi hii nimechota
maji na kuyabeba kwenye baskeli yangu kwa nia ya kuonyesha umwagiliaji kwenye
shamba la Kahawa na Migomba ambayo nimepanda kwenye ekari 24 hivi karibuni nilizopewa
na serikali hapa Luweero. Nitaendelea na kampeni yangu ya mlango kwa mlango
kuhamasisha na kusisitiza juu ya operesheni “Vumbua Utajiri.”Alisema Rais
Museveni kwenye ukurasa huo wa Facebook.
No comments:
Post a Comment