Mkurugenzi wa Singita Grumeti Stephen Cunliffe (kulia)
akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Mara Dk. Charles Mlingwa msaada wa madawati 500
yenye Thamani ya Tshs Milioni 112 kwa ajili ya Wilaya za Serengeti na Bunda
katika hafla iliyofanyika Shule ya Msingi Makundusi Wilayani Serengeti.
MFUKO wa Singita Grumeti umeendelea kuwa mstari wa
mbele katika kuboresha hali ya elimu katika Wilaya za Serengeti na Bunda.
Hii
imedhihirika kwenye halfa ya kukabidhi madawati 500 kwa Mkuu wa Mkoa wa Mara Dk.
Charles Mlingwa ili kupunguza uhaba wa madawati katika Wilaya hizo. Aidha
Grumeti wamekabidhi nyumba ya kuishi mwalimu iliyojengwa katika Shule ya Msingi
Makundusi.
“Tuko
hapa kukabidhi madawati haya 500 yenye thamani ya Tshs Milioni 112 kwa Wilaya
za Serengeti na Bunda pamoja na nyumba hii yenye thamani ya Tshs Milioni 86” alisema Richard Ndaskoi
ambae ni Mkuu wa Huduma za Jamii toka Mfuko wa Singinta Grumeti.
Akipokea
misaada hiyo, Dk. Mlingwa alisema “Nawashukuru Singita Grumeti kwa Msaada huu
wa madawati pamoja na nyumba hakika mchango wenu katika Mkoa wa Mara unaoneka”
Dk Mlingwa amewataka wawekezaji wengine katika Mkoa wa Mara kuchangia madawati
katika Wilaya za Serengeti na Bunda kwani bado zina uhaba wa madawati.
Aidha
Dk. Mlingwa ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti kwa kuwa na
mahusiano mazuri na wawekezaji waliopo katika Wilaya hiyo “Tukiwawekea
mazingira mazuri ya kufanya shughuli zao hata wananchi pia watanufaika na uwepo
wa wawekezaji hawa” alisema Dk. Mlingwa.
Naye
Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Bunda,
Lydia Bupilipili wote kwa nyakati tofauti wameushukuru Mfuko wa Singita Grumeti
kwa msaada huo wa madawati na kuuomba mfuko huo kuendelea kuchangia katika
shughuli za maendeleo katika Wilaya za Serengeti na Bunda. “Wilaya hii ina
wawekezaji wengi lakini wamekuwa nyuma katika kuchangia shughuli za maendeleo,
nawapongeza kwa kuwa mstari wa mbele kusaidia jamii inayowazunguka pamoja na
kuchangia katika maendeleo ya Wilaya ya Serengeti” alisema Nurdin Babu.
Aidha
Bi. Bupilipili ameuomba Mfuko huo kuanzisha kampeni maalumu ya kuongeza kiwango
cha ufaulu kwa watoto wa kike kwa shule za sekondari Wilayani Bunda.
Singita
Grumeti wamekuwa wawekezaji wenye tija kwa wananchi wa Wilaya za Serengeti na
Bunda licha ya kuwa mstari wa mbele kuchangia katika shughuli za maendeleo,
kampuni hiyo pia imekuwa ikitoa ajira kwa wakazi toka wilaya hizo mbili pamoja
na kutoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi toka wilaya hizo.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiwasha mshumaa ikiwa
ni ishara ya ufunguzi wa Mkutano wa Mawaziri wa Nchi zinazopakana na Bahari ya
Hindi wa Kudhibiti Biashara na Usafirishaji wa Dawa za Kulenya kwa njia ya
bahari. Mkutano huo unafanyika mjini Colombo nchini Sri Lanka. Picha zote na WMNN.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akisikiliza
mada zilizokuwa zinatolewa katika Mkutano wa Mawaziri wa Nchi zinazopakana na
Bahari ya Hindi wa Kudhibiti Biashara na Usafirishaji wa Dawa za Kulenya kwa
njia ya bahari unaofanyika mjini Colombo nchini Sri Lanka
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza katika
Mkutano wa Mawaziri wa Nchi zinazopakana na Bahari ya Hindi wa Kudhibiti
Biashara na Usafirishaji wa Dawa za Kulenya kwa njia ya bahari unaofanyika
mjini Colombo nchini Sri Lanka
No comments:
Post a Comment