Mkuu
wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues
akifuatilia kwa makini darasa lililokuwa likiendeshwa na mwanafunzi wa
kidato cha pili (hayupo pichani).
Mradi
mkubwa wa kijiji cha digitali cha Ololosokwan, Loliondo umezinduliwa
rasmi mwishoni mwa wiki, miaka miwili tangu kutiwa saini kwa uanzishwaji
wake kati ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni
(Unesco) na kampuni ya Samsung.
Hiki
kitakuwa ni kijiji cha nne cha digitali barani Afrika cha kwanza kikiwa
nchini Afrika Kusini huku kingine kikiwa Gabon na Ethiopia.
Kijiji
hicho cha digitali ni nadharia ya Samsung katika kurejesha faida kwa
umma na kina huduma mbalimbali ambazo zikiunganishwa na haja ya wananchi
zitasaidia kubadili maisha ya wamasai na kuondokana na utegemezi wa
mifugo pekee.
Uzinduzi
rasmi wa kijiji hicho umefanywa na Mkuu wa mkoa Arusha Mrisho Gambo kwa
niaba yaWaziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na watoto
Ummy Mwalimu.
Kijiji
hicho cha digitali kina shule yenye tehama ikiwa na maunganisho ya
intaneti, kiliniki ya kisasa ikiwa na kituo cha teknolojia ya
mawasiliano yenye kuwezesha utabibu (telemedicine) na jenereta
linalotumia nguvu za jua.
Mradi
huo ambao ulishuhudiwa utiaji saini na Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya
Taifa ya UNESCO, Bi. Leah Kihimbi kutoka Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo na Dkt. N. Iriya kutoka Shirika la Afya Duniani
(WHO) Dar es Salaam na wafanyakazi wa UNESCO mwaka 2014, kukamilika
kwake kunawezesha UNESCO na serikali ya Tanzania kuwapatia wakazi wa
eneo hilo huduma bora za afya na vijana wa Kimasai nafasi ya kupata
elimu kutokana na ukweli kuwa kwa utamaduni na kazi zao za ufugaji
wamekuwa wakipata shida ya kupata elimu.
Utiaji
saini wake katika mwaka huo ulifanywa na Mkuu wa ofisi na Mwakilishi
Shirika la UNESCO nchini Bi. Zulmira Rodrigues na Mkurugenzi wa Samsung
Electronics nchini Tanzania, Bw. Mike Seo .
Kupitia
kijiji hicho vijana wataendelea na masomo hata kama wanachunga mifugo
yao kutokana na kupatiwa tablet ambazo zitawawezesha kujifunza hata
wakiwa nje wakichunga mifugo yao.
Aidha
miongoni mwa manufaa makubwa yatakayopatikana katika mradi huo wa
kijiji cha digitali ni kuweza kupata nishati rahisi na iliyo rafiki kwa
mazingira kwa kuwepo na jenereta linalotumia nishati ya jua.
Kuwepo
kwa kijiji hicho kunataka kudhihirisha ni kwa namna gani teknolojia
inaweza kutumika kuleta mabadiliko chanya yanayotakiwa kwa ajili ya
maendeleo ya wananchi waliopo vijijini.
Kijiji
hicho cha Loliondo ambacho kitakuwa cha nne katika vijiji vya
kidigitali barani Afrika kimeelezwa naMkuu wa mkoa wa Arusha Mheshimiwa
Mrisho Gambo kama utekelezaji wa Sera ya Tiba Mtandao kutokana na
kuzinduliwa kwa Kliniki Mtandao iliyopo katika Kijiji hicho.
Katika uzinduzi wa mradi huo kwa ujumla
wake, kliniki ndicho kitu ambacho kinaonekana kwenda karibu zaidi na
wananchi wa Ololosokwan kwani itakuwa inatoa huduma za afya, bora za
kisiasa na za haraka kwa wakazi wa kata za Soitsambu naa Oloipiri,
Wilayani Ngorongoro.
Katika
hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa mkoa wa Arusha ,Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na watoto Mhe Ummi Mwalimu
wakati wa uzinduzi wa kliniki hiyo,alisema kuwa Tiba Mtandao imekua ni
miongoni mwa Vipaumbele vya Wizara yake ili wananchi wote Tanzania
waweze kupata huduma stahiki za matibabu pasipo kujali changamoto za
Kijiografia zinazotukabili,
Pamoja
na kufanya uzinduzi huo katika hotuba yake Mkuu wa mkoa wa Arusha,
Mrisho Gambo aliwashukuru wote walioshiriki kuleta Mradi huo wa maana
kwa mkoa wa Arusha kwani wangeweza kupeleka sehemu nyingine yeyote na
kuongeza kuwa ni deni kubwa sana lazima tuhakikishe huduma hiyo
imefanikiwa.
Akizungumzia
masuala ya afya kama kipaumbele katika mradi huo wenye lengo la
kuhifadhi utamaduni wa kimasai huku wakitumia teknolojia ya kisasa
kuleta maendeleo katika elimu na kuhifadhi mazingira, Mkuu huyo wa mkoa
akizungumza kwa niaba ya Waziri alisema kuwa kutokana na umuhimu wa
sekta ya afya kwa kila Mtanzania ,serikali itaelekeza nguvu katika
Kliniki hiyo ili kuiwezesha kutoa huduma stahiki na Kwa muda mrefu kwa
wananchi wa maeneo haya.
"Kliniki
hii ni ya kwanza Tanzania na itaweza kutoa huduma bora na za kisasa kwa
njia ya mtandao kwa wananchi zaidi ya elfu kumi kutoka katika maeneo
ambayo hapo awali wananchi walikuwa wanatembea umbali mrefu zaidi ya
Kilomita 50 kufuata huduma za afya".
"
Hii inadhihirisha kwamba mwananchi wa Ololosokwan na maeneo ya jirani
anaweza kuhudumiwa na daktari bingwa aliyeko Muhimbili au kokote Duniani
kupitia Klinik hii;na mfumo wa Mtandao uliopo unaruhusu upatikanaji wa
huduma hizi kwa kipindi chote cha mwaka mzima".
Aidha
aliitaka Halmashauri kutenga Bajeti kwa ajili ya kuongeza hadhi ya
zahanati hiyo kuwa Kituo cha Afya ambapo itaenda sambamba na kuongeza
majengo Pamoja na wataalam watakaoweza kutoa huduma stahiki Kwa
wananchi.
Upatikanaji
wa kituo cha Afya katika eneo hilo huku kukiwepo na kliniki mtandao
kutasaidia kuokoa maisha ya wananchi ambao wengi wao waliamini kupona
magonjwa makubwa ni mpaka uende KCMC au Muhimbili tu.
Awali
akizungumza katika uzinduzi huo Mkuu Shirika la Umoja wa mataifa
linaloshigulikia Elimu na Sayansi (UNESCO) nchini Tanzania Bi. Zulmira
Rodrigues alisema kijiji hicho ni ushuhuda tosha wa ukuaji wa teknolojia
unaenda sambamba na maono ya shirika la Unesco la kutoa kipaumbele
katika miradi ya sayansi inayosaidia wananchi wenye mahitaji moja kwa
moja.
Alisema
kwa kutambua adha waliyokuwa wanaipata wananchi wa Ololosokwan
walitengeneza mradi ambao sehemu mojawapo ni kliniki Mtandao ili kuleta
mabadiliko ya afya za watu kwa njia ya kisayansi.
Naye
mkurugenzi wa Tiba Kutoka Wizara ya Afya Dr. Margareth Evelyne Mhando
alishukuru Unesco kusaidia kutekeleza malengo ya Wizara kupitia Mradi
huu wa kijiji cha digitali na kuongeza kuwa ni hatua nzuri katika sekta
ya afya Kwa sababu hivi sasa wananchi waliombali na vituo vya Afya
kupitia Mradi huu watapata huduma bora kutoka Kwa matabibu wabobezi.
Uzinduzi
wa Mradi huu ulihudhuriwa pia na Balozi wa Switzerland Nchini Tanzania
Bi. Florence Mattli, Wawakilishi wa Samsung ambao ndio waliotoa fedha na
Teknolojia pamoja na wawakilishi kutoka Umoja wa Ulaya (EU).
Bi.
Mattli alisema kwamba wataendelea kusaka wadau wengine kuhakikisha
kwamba mradi huo unaendelea kutanuka na kufanikiwa kwa kujazia maeneo
ambapo panahitaji nguvu nyingine.
Mkuu
wa Wilaya ya Ngorongoro, Rashid Taka akizungumza machache kabla ya
kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (kushoto aliyeketi)
kuhutubia wageni waalikwa na wanakijiji wa Ololosokwan wilayani
Ngorongoro kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa kijiji cha kidigitali chenye
kituo cha huduma maalum za afya pamoja na kituo cha elimu kwa njia ya
mtandao uliofanyika mwishoni mwa wiki mkoani Arusha.
Pichani
juu na chini ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akisoma hotuba
katika hafla ya uzinduzi wa kijiji cha kidigitali chenye kituo cha
huduma maalum za afya pamoja na kituo cha elimu kwa njia ya mtandao kwa
niaba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh.
Ummy Mwalimu uliofanyika kwenye kijiji cha Ololosokwan, wilayani
Ngorongoro mkoani Arusha.
Pichani
juu na chini ni baadhi ya wanakijiji wa Ololosokwan na wageni waalikwa
wakimsikiliza mgeni rasmi RC Gambo kwenye hafla ya uzinduzi wa kijiji
cha kidigitali chenye kituo cha huduma maalum za afya pamoja na kituo
cha elimu kwa njia ya mtandao uliofanyika mwishoni mwa wiki, wilayani
Simanjro, mkoani Arusha.
Mkuu
wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues
akizungumzia ukuaji wa teknolojia ambayo inaenda sambamba na maono ya
shirika lake kwenye hafla uzinduzi wa kijiji cha kidigitali chenye kituo
cha huduma maalum za afya pamoja na kituo cha elimu kwa njia ya mtandao
uliofanyika mwishoni mwa wiki, wilayani Simanjro, mkoani Arusha.
Mkuu
wa Masoko wa Kampuni ya Samsung Afrika Mashariki, Patricia Kingori
akizungumza kwenye hafla uzinduzi wa kijiji cha kidigitali cha Samsung
(Samsung Digital Village) kinachotumia umeme wa jua chenye kituo cha
huduma maalum za afya pamoja na kituo cha elimu kwa njia ya mtandao
uliofanyika mwishoni mwa wiki, wilayani Simanjro, mkoani Arusha.
Balozi
wa Uswisi nchini, Mh. Florence Tinguely Mattli akizungumza kwenye
uzinduzi wa kijiji cha kidigitali cha Samsung (Samsung Digital Village)
kinachotumia umeme wa jua ambacho kina kituo cha huduma maalum za afya
pamoja na kituo cha elimu kwa njia ya mtandao kilichopo katika kijiji
cha Ololosokwan, wilayani Simanjro mkoani Arusha.
Mkurugenzi
wa Tiba Wizara ya Afya, Dr. Margaret Mhando akitoa neno ambapo
aliwashukuru Unesco kusaidia kutekeleza malengo ya wizara kupitia mradi
huu wa kijiji cha kidigitali cha (Samsung Digital Village) unaoratibiwa
na Shirika la UNESCO kwenye kijiji cha Ololosokwan, wilayani Ngorongoro,
mkoani Arusha.
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akimsikiliza kwa makini Balozi wa
Uswisi nchini, Mh. Florence Tinguely Mattli wakati wa hafla ya uzinduzi
wa kijiji cha kidigital cha Samsung chenye kituo cha huduma maalum za
afya pamoja na kituo cha elimu kwa njia ya mtandao (Samsung Digital
Village) uliofanyika kwenye kijiji cha Ololosokwan, wilayani Ngorongoro
mkoani Arusha.
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akijipanga kuzindua rasmi moja ya kituo
cha huduma maalum za afya huku Mkuu wa Masoko wa Kampuni ya Samsung
Afrika Mashariki, Patricia Kingori (katikati) Balozi wa Uswisi nchini,
Mh. Florence Tinguely Mattli (kushoto), Mkurugenzi wa Tiba Wizara ya
Afya, Dr. Margaret Mhando (kulia), Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues (wa pili kushoto)
wakishuhudia tukio hilo.
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akikata utepe kuzindua rasmi moja ya
kituo cha huduma maalum za afya huku Mkuu wa Masoko wa Kampuni ya
Samsung Afrika Mashariki, Patricia Kingori (katikati) Balozi wa Uswisi
nchini, Mh. Florence Tinguely Mattli (wa pili kushoto), aibu Katibu Mkuu
wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nuru Milao (kushoto),
Mkurugenzi wa Tiba Wizara ya Afya, Dr. Margaret Mhando (kulia), Mkuu wa
Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues (wa pili
kushoto) wakishuhudia tukio hilo.
Mganga
Mkuu wa Wilaya Ngorongoro, Dk. Omari Sukari akitoa maelezo ya huduma
mbalimbali za Afya zitakazokuwa zikipatikana ndani ya moja ya makontena
ya kijiji cha Kidigitali cha Samsung (Samsung Digital Village) kwa Mkuu
wa Mkoa wa Arusha, Mh. Mrisho Gambo (kulia) wakati wa uzinduzi wa kituo
cha huduma maalum za afya uliofanyika katika kijiji cha Ololosokwan,
wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha, Mh. Mrisho Gambo akifanya kipimo cha B.M.I ndani ya
kituo cha huduma maalum za afya kilichopo katika kijiji cha Ololosokwan,
wilayani Ngorongoro mkoani Arusha mara baada ya kukizundua rasmi.
Mganga
Mkuu wa Wilaya Ngorongoro, Dk. Omari Sukari akimsoea majibu ya BMI Mkuu
wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ndani ya kituo cha huduma maalum za
afya kilichopo katika kijiji cha Ololosokwan, wilayani Ngorongoro mkoani
Arusha ambacho kimezinduliwa rasmi mwishoni mwa juma.
Mkuu
wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues
(kushoto) akifurahi jambo wakati Mganga Mkuu wa Wilaya Ngorongoro, Dk.
Omari Sukari (katikati) akimsoma majibu ya BMI Mkuu wa Mkoa wa Arusha,
Mrisho Gambo.
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (kulia) akiwa ndani ya Kliniki hiyo ya
Kidigitali ya Samsung akifanya uchunguzi wa kupima uwezo wake wa kusikia
kwa kutumia kifaa maalum.
Mratibu
wa Telemedicine kutoka Wizara wa Afya ,Maendeleo ya jamii, Jinsia,Wazee
na Watoto, Dk. Liggy Vumilia akifafanua kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha,
Mrisho Gambo (hayupo pichani) jinsi kituo cha huduma maalum za afya cha
kijiji cha Ololosokwan, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha kinavyoweza
kufanya mawasiliano na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa njia ya
mtandao na kupata ufumbuzi wa tatizo la mgonjwa katika hafla fupi ya
uzinduzi wa kituo hicho. Kulia ni Stella Kairuki kutoka Samsung.
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akitoa mkono wa pongezi kwa Mkuu wa
Masoko wa Kampuni ya Samsung Afrika Mashariki, Patricia Kingori kwa
kusogeza huduma muhimu za afya kwa wanakijiji wa Ololosokwan mara baada
ya kuzindua kituo hicho cha afya wilayani Ngorongoro mwishoni mwa juma.
Mkuu
wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akimpongeza Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues kwa kuratibu mradi huo
utakaowasaidia wanakijiji wa Ololosokwan katika huduma za afya na elimu
kwa njia ya mtandao.
Kutoka
kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Nuru Milao, Mkuu wa Masoko wa Kampuni ya Samsung Afrika
Mashariki, Patricia Kingori pamoja na Afisa Utawala na Fedha wa Shirika
la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni
(UNESCO) nchini, Spencer Bokosha wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye
hafla ya uzinduzi wa kituo cha huduma maalum za afya uliofanyika katika
kijiji cha Ololosokwan, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
Televisheni
ya Samsung iliyopo nje ya kituo hicho cha huduma za afya ikionyesha
kipindi maalum cha kuelimisha jamii ya wafugaji (Wamasai) wa kijiji cha
Ololosokwan iliyotafsiriwa Kimasai kuhusiana na masuala ya afya na usafi
wakati wakisubiri kupata huduma za afya.
Mkuu
wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues
akifafanua jambo kwa wageni waalikwa nje ya kituo cha huduma ya meno na
maabara ya kijiji cha kidigitali wakati wa uzinduzi wa kituo cha huduma
maalum za afya pamoja na kituo cha elimu kwa njia ya mtandao (Samsung
Digital Village) uliofanyika kijiji cha Ololosokwan, wilayani Ngorongoro
mkoani Arusha.
Mkuu
wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues
akibadilishana mawazo na Mkuu wa Masoko wa Kampuni ya Samsung Afrika
Mashariki, Patricia Kingori kwenye hafla ya uzinduzi wa kituo cha huduma
maalum za afya uliofanyika katika kijiji cha Ololosokwan, wilayani
Ngorongoro mkoani Arusha.
Mgeni
rasmi Mkuu wa Mkoa wa Arusha kwenye picha ya pamoja na wadau
waliofanikisha mradi wa Samsung Digital Village pamoja na baadhi ya
wanakijiji wa Ololosokwan watakaonufaika na mradi huo.
Mkuu
wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues (wa pili
kushoto) Mkuu wa Masoko wa Kampuni ya Samsung Afrika Mashariki,
Patricia Kingori (kushoto) Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Unesco
(NATCOM), Dkt Moshi Kimizi (wa pili kulia) pamoja na Naibu Katibu Mkuu
wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nuru Milao (kulia)
wakiwasili kwenye eneo la kituo cha elimu kwa njia ya mtandao kwa ajili
ya uzinduzi rasmi katika kijiji cha Ololosokwan, wilayani Ngorongoro
mkoani Arusha.
Balozi
wa Uswisi nchini, Mh. Florence Tinguely Mattli (wa pili kushoto) akiwa
ameambatana na Wawakilishi kutoka Umoja wa Ulaya (EU), Olivier Couplex
(wa pili kulia) pamoja na Anna Costantine wakiwasili ene la tukio.
Mkuu
wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues na
Balozi wa Uswisi nchini, Mh. Florence Tinguely Mattli wakifurahia jambo
kwenye hafla ya uzinduzi huo.
Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akikaribishwa kwa ngoma za kimasai katika eneo la tukio.
Mkuu
wa Masoko wa Kampuni ya Samsung Afrika Mashariki, Patricia Kingori
akizungumza machache jengo la kituo cha elimu kwa njia ya mtandao ambalo
limetengenezwa na Samsung kabla halijazinduliwa rasmi kwenye kijiji cha
Ololosokwan, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
Mkuu
wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues akitoa
neno wakati wa jengo la kituo cha elimu kwa njia ya mtandao kabla
kuzinduliwa rasmi kwenye kijiji cha Ololosokwan, wilayani Ngorongoro
mkoani Arusha. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (wa pili kulia) akikata utepe kuashiria
uzinduzi wa kituo cha elimu kwa njia ya mtandao kinachotumia umeme wa
jua (Solar Power Internet School) uliofanyika katika kijiji cha
Ololosokwan, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha. Wanaoshuhudia tukio hilo
ni Mkuu wa Masoko wa Kampuni ya Samsung Afrika Mashariki, Patricia
Kingori (wa tatu kushoto) Balozi wa Uswisi nchini, Mh. Florence Tinguely
Mattli (wa kwanza kushoto), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nuru Milao (wapili kushoto), Mkuu wa Ofisi
na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues (kulia).
Mwanafunzi
wa Shule ya Sekondari Emanyata ya Loliondo, Kenneth Pascal wa kidato
cha pili akitoa elimu kwa njia ya mtandao kupita programu ya Shule
Direct kwa wanafunzi wenzake wa darasa la kompyuta waliojumuika na mgeni
rasmi Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo wakati wa sherehe ya
uzinduzi wa kituo hicho uliofanyika katika kijiji cha Ololosokwan,
Wilayani Ngorongoro, mkoani Arusha.
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (katikati), Balozi wa Uswisi nchini,
Mh. Florence Tinguely Mattli (kushoto) pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nuru Milao wakiwa ndani
ya kituo cha elimu kwa njia ya mtandao kinachotumia umeme wa jua (Solar
Power Internet School) mara baada ya kukizindua katika kijiji cha
Ololosokwan, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
Darasa la kompyuta kwa njia mtandao likiendelea huku wageni wakishuhudia.
Mkuu
wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues
akifuatilia kwa makini darasa lililokuwa likiendeshwa na mwanafunzi wa
kidato cha pili (hayupo pichani).
Mafunzo kwa vitendo yakiendelea.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa
Kiuchumi na Kijamii, (ESRF), Dkt. Tausi Mbaga Kida, (kulia), akizungumza
kwenye Warsha ya majadiliano ya wadau kuhusu nafasi ya sekta binafsi
katika kutekeleza mpango wa pili wa maendeleo wa miaka mitano (FYDPII),
kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Anthony Mtaka
Naibu Katibu Mkuu Tume ya Mipango, kutoka Wiraza ya Fedha na Mipango, Dkt. Maduka Paul Kessy(kushoto), akizungumza kwenye warsha hiyo. |
Mkurugenzi
wa Huaduma kwa Wanachama, Taasisi ya Sekta Binafsi, (TPSF), Bw. Louis
Accaro, akitoa mada yake juu ya sekta za kipaumbele ambazo zinapaswa
kujadiliwa ili kufanyiwa kazi, sekta hizo ni kutoka zao la Pamba na kuwa
nguo, kutoka ngozi na kuwa mazao yatokanayo na ngozi, na pia viwanda
vya madawa
Baadhi yawashiriki wa warsha wakifuatilia mjadalaBaadhi ya washiriki
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Anthony Mtaka, akizungumza wakati wa warsha hiyo |
NA
K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID
WADAU kutoka kada mbalimbali wamekutana kujadiliana
jinsi sekta binafsi itakavyoshiriki katika utekelezaji thabiti wa mpango wa
pili wa miaka mitano wa maendeleo ya Tanzania kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF
jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa
Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii, (ESRF), Dkt. Tausi Mbaga Kida,
amesema sekta binafsi inao umuhimu mkubwa katika kushiriki kuandaaa na kujadili
mipango mbalimbali ya maendeleo.
Dkt. Kida aliyasema
hayo katika hotuba yake aliyoitoa kwenye Warsha ya majadiliano kuhusu nafasi ya
sekta binafsi katika kutekeleza mpango wa pili wa miaka mitano wa maendeleo ya
Tanzania, (FYDP II) iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar
es Salaam.
Warsha hiyo iliyoandaliwa
kwa pamoja na ESRF, Serikali kupitia Tume ya Mipango na Mpango wa Kusaidia
Mabadiliko ya Kiuchumi, (SET), iliwakutanisha wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja
na Taasisi ya Sekta Binafsi nchini, (TPSF), CEO roundtable, Suma JKT, Taasisi ya Biashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA) ,
wadau wa maendeleo kutoka Jumuiya ya Ulaya, mashirika yasiyo ya kiserikali
(NGOs) na wasomi.
Dkt. Kida
alisema, Majadiliano hayo nimatokeo ya juhudi zilizoanza tangu 1998-200, ambapo ESRF ilishiriki katika
uanzishwaji wa mpango wa Taifa wa Vision 2025 uliolenga kuitoa Tanzania kwenye
kundi la nchi masikini hadi zile zenye uchumi wa Kati, (Middle income coutry.
“Mwaka 2011
ESRF ilifanya mkakati wa kupitia mpango huo wa vision 2015 na kubaini masuala
kadhaa ambayo yalihitaji kuelezewa kama kweli taifa linaelewa mpango huo wa
kipindi kirefu.” Alisema na kuongeza ni hivi karibuni sisi katika ESRF
tulifanya mapitio ya mkakatiwa kwanza wa Maendeleo wa Miaka Mitano (FYDPI), na
MKUKUTA II, mapitio ambayo yamechangia kuingia katika Mpango huu wa pili wa
Maendeleo wa Miaka Mitano, (FYDP II), Alisema Mkurugenzi huyo Mtendaji wa ESRF.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Tume ya
Mipango, kutoka Wiraza ya Fedha na Mipango, Dkt. Maduka Paul Kessy alisema, “Kuna
mambo matatu muhimu ya kuzingatia katika mkakati huu ambayo wajumbe mtalazimika
kuyafanyia kazi kwa kina ambayo ni pamoja na kutambua kwamba nchi yetu imedhamiria
kuingia kwenye uchumi wa viwanda, kwa hivyo rasilimali tulizonazo tuhakikishe
zinalisha viwanda vyetu mfano tunapaswa tujadiliane ni kwa namna gani tunafikia
hatua ya kuchakata pamba na ngozi hapa hapa nchini, na utengenezaji wa madawa.”,
aliwaambia washiriki wa warsha hiyo.
Ili
kutekeleza hilo, Viongozi wa Wilaya na Mikoa hawana budi kushirikiana na sekta
binafsina kujadili namna ya kutekeleza maswala haya ili kusudi ifikapo mwishoni
mwa Novemba mwaka huu, tutakapokutana tujue nini kilicho mbele yetu,
alifafanuaDkt. Kessy.
Akitoa
mada yake kuhusu ushirikishwaji wa sekta binafsi katika maendeleo ya nchi, Mkuu
wa mkoa wa Simiyu Bw. Anthony Mtaka alisema, “Wakati umefika sasa, watanzania
kuanzisha viwanda vidogo vya kuongeza thamani ya mazao na mifugo ili kuboresha
maisha na kuondokana na tatizo la vijana kukosa kazi.
Akitolea
mfano, Mkuu huyo wa mkoa ambaye ameteuliwa na Rais John PombeMagufuli kuogoza
mkoa huo akitokea wilayani Mvomero mkoani Morogoro, alisema. “Sisi Simiyu
tumepiga hatua, hivi sasa tunatengeneza chaki sisi wenyewe kwa matumizi ya
shule, na tunataka pamba tunayolima ambapo Simiyu ndio mkoa unaoongoza kwa
uzalishaji wa zao hilo, tuanze kutengeneza vifaa vya hospitalini vinavyotokana
na zao la pamba. “ Alifafanua Mkuu huyo wa Mkoa kijana.
Bw.
Mtaka pia alisema, asilimia 50 ya mifugo inatoka mkoani Simiyu na moja ya
mkakati alioufanya kuwashirikisha SIDO na wadau wengine katika kuanzisha
kiwanda kidogo cha kuongeza thamani ya maziwa na kutengeneza bidhaa mbalimbali zitokanazo
na maziwa na nia yetu ni kusambaza viwanda vya aina hii kwenye kila wilayani
Mkurugenzi
wa Mpangowa kusaidia mabadiliko ya kiuchumi, (SET), Dkt.Dirk Willem te Velde,
akizungumza kwenye warsha hiyo
Mtafiti Mkuu wa Taasisi
ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii, (ESRF), Profesa Samwel Wangwe,
akitoa mada kuhusu masuala ya utekelezaji wa mpango huo na mapungufu,
kutokana na funzo la mipango iliyopita
Katibu Mtendfaji wa CEO-Roundtable, Bi. Santona Benson, akifungua warsha hiyo kwa niabaya wa Taasisi hiyo, Bw. Ali Mufuruki.
Mjumbe akipitia machapishowakati wa warsha hiyo
Mjumbe akipitia machapisho
Maafisa kutoka SUMA-JKT nao walikuwepo
Katibu Mtendfaji wa CEO-Roundtable, Bi.
Santona Benson(kushoto), akifafanua baadhi ya mambo. Katikati ni Mkuu
wa mkoa wa Simiyu, Bw. Anthony Mtaka, na Mkurugenzi wa ESRF, Dkt. Tausi
Mbaga Kida
Dkt. Kida, akipeana mikono na Mkuu wa Mkoa, Bw. Anthony Mtaka
Dkt.Dirk akitoa mada juu ya misingi ya utekelezaji thabiti ya mikakati ya utekelezaji wa mpango huo
Baadhi ya washiriki waliohudhuria warsha hiyo
Picha ya pamoja |
No comments:
Post a Comment