Meneja
Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele, (kulia), akiwasaidia
wanakijiji hawa wa Ikwiriri, Wilayani Rufiji mkoani Pwani, kutuma michango kwa
njia ya mtandao wa simu, wakati wa kuandikisha wanachama chini ya mpango wa
Wote Scheme kwenye chuo cha Maendeleo ya Jamii, Ikwiriri, Oktoba 3, 2016. Takriban wanakijiji 395
wakiwemo, wakulima, wafuga nyuki, wavuvi na waendesha bodaboda, wamekabidhiwa
kadi za uanachama kupitia mpango huo unaoruhusu mtu yeyote aliye kwenye sekta
rasmi na isiyo rasmi kujiunga kwa kuchangia kila mwezi kima cha chini shilingi
20,000.
Meneja
wa PPF, Kanda ya Temeke, Erica Sendegeya, (kulia), akimkabidhi kadi ya
uanachama wa Mfuko huo kupitia mpango wa uchangiaji wa Hiari, (Wote Scheme),
wakati wa kuandikisha wanachama na kugawa kadi kwenye viwanja vya chuo cha
ufundi Ikwiriri, wilayani Rufiji mkoa wa Pwani, Oktoba 3, 2016.
Zawadi Hamza Sule, (kushoto), ambaye ni mkulima huko Ikwiriri, akipokea kadi yake ya uanachama wa PPF kupitia Wote Scheme
NA
MWANDISHI WETU, IKWIRIRI
MFUKO
wa Pensheni wa PPF, kupitia mpango wa Uchangiaji wa Hiari, “Wote Scheme”,
umesajili karibu wanachama 400 huko
Ikwiriri wilayani Rufiji mkoa wa Pwani.
Akizungumza
na waandishi wa habari wakati wa zoezi la usajili na ugawaji kadi za uanachama
kwenye viwanja vya chuo cha Ufundi Ikwiriri, (IFDC), Oktoba 3, 2016, Meneja wa
PPF Kanda ya Temeke, Erica Meshack Sendegeya, alisema, wanakijiji hao wajasiriamali walihamasika
kujiunga na mpango huo baada ya Kanda yake kutoa elimu juu ya umuhimu wa
wananchi kujiunga na Mfuko huo kwani kuna manufaa mengi.
“Tuliwaeleza,
mpango huu wa Wote Scheme umebuniwa ili kutoa fursa ya wananchi walioajiriwa au
waliojiajiri wenyewe, wakiwemo wakulima, wavuvi, wafugaji, Boda boda na mama lishe, kujiunga na Mfuko kwa kuchangia
kima cha chini cha shilingi 20, 000 kila mwezi. “Fedha hizo unaweza kuzitoa kwa
mkupuo au kwa awamu kulingana na uwezo wa mwanachama,” alifafanua Sendegeya.
Akielezea
faida za kuwa mwanachama, Meneja huyo alisema, “Mwanachama atafaidika na fao la
Afya ambapo atapatiwa bima ya afya kupitia NHIF baada ya kuchangia shilingi
elfu 60,000 tu.” Alisema na kuongeza kuwa faida nyingine ni pamoja na
mwanachama kujipatia mkopo wa maendeleo ambapo sharti kuu la kupata mkopo huu
ni mwanachama kuchangia Mfuko kwa kipindi cha miezi sita, mkopo wa elimu,
lakini pia fao la uzeeni, alisema Meneja huyo.
Kuhusu
namna mwanachama anavyoweza kuchangia baada ya kujiunga na Mpango huo, Meneja
Uhusiano wa PPF, Lulu Mengele alisema, “Kuna njia rahisi ya kuwasilisha
michango, ambayo ni kutumia mitandao ya simu, Airtel Money, Tigo Pesa na
M-Pesa.” Alisema.
Baadhi
ya wanakijiji waliojiunga na Mpango huo, wameipongeza PPF kwa kutoa elimu
ambayo imewafanya wajiunge na Mfuko huo na ni matarajio yao utasaidia kuboresha
shughuli zao.
“Mimi
ni mfuga nyuki, kilichonivutia ni jinsi Mfuko huu unavyoweza kutoa mikopo ya
maendeleo,” alisema Erasto Joseph, ambaye pia ni mwalimu wa shule.
Naye
Ishara Ibrahim ambaye ni mkulima, alisema, ni matarajio yake kuwa kujiunga na
PPF, basi ataweza kumudu kupata huduma ya afya kupitia Bima ya Afya.” Alisema.
Zawadi Hamza Sule, akionyesha kadi yake baada ya kukabidhiwa
Seif M. Mgumba akionyesha kadi yake ya uanachama wa PPF, kupitia Wote Scheme
Khadija R. Kitango, akionyesha kadi yake
Meneja wa PPF, Kanda ya Temeke, Erica
Sendegeya, akizungumza na wanachama hao wapya wa PPF huko Ikwiriri,
wilayani Rufiji mkoa wa Pwani Oktoba 3, 2016
Wanachama wapya wa PPF, wakiwasikiliza viongozi wa PPF
Wanachama hawa wapya wakionyeshana kadi zao za uanachama baada ya kukabidhiwa
Wanachama wakisubiri utaratibu wa kukabidhiwa kadi zao na kufanya malipo ya michango ya awali
Wanachama wapya wa PPF, wakihudumiwa
Meenja wa PPF, Kanda ya Temeke, Erica
(kushoto), na Meneja Uhusiano wa Mfuko huo, Lulu Mengele, wakiwasaidia
wanachama hao kutumia simu zao za mkononi kuweka michango yao
Erica, akiwasaidia kuwaelekeza namna ya kutuma michango kupitia simu za mkononi
Erica (kulia) na Lulu, wakimsikiliza mwanachama huyu wa Ikwiriri baada ya zoezi la kuwapatia kadi za uanachama Oktoba 3, 2016
Erica, akisoma majina ya wanachama wapya waliojiunga na PPF kupitia Wote Scheme
Meneja Uhusiano wa PPF, Lulu Mengele, akiwaarifu waandishi wa habari kuhusu shughuli nzima ilivyokwenda
Lulu akisalimiana na wanachama hawa wenye furaha
Wanakijiji wa Ikwiriri wakisubiri
kupatiwa kadi zao za uanachama baada ya kujiunga na PPF kupitia
uchangiaji wa Hiari, (Wote Scheme) Oktoba 3, 2016
ACT YAZINDUA HARAMBEE YA UJENZI WA KANISA JIJINI DA
Kanisa la All-
Nations Christian Tabernacle (ACT) linaloendesha shughuli zake katika ukumbi wa
Utoji, Sinza Mapambano jijini Dar limezindua harambee ya kuchangia ujenzi wa
kanisa hilo rasmi .
Akizungumza
katika misa iliyofanyika eneo hilo, mchungaji wa kanisa hilo Pastor Sos Mabele
alisema kuwa harambee hiyo imezinduliwa kanisani hapo kwa waumini na watu
mbalimbali kuweka ahadi au kuchangia moja kwa moja fedha kwa ajili ya ujenzi wa
kanisa unaotarajiwa kuanza mwisho wa mwaka huu.
Mbali na
hayo Mchungaji huyo aliwataka watu mbalimbali wajitokeze kuchangia ujenzi wa kanisa hilo bila kujali madhehebu
au dini, kwa kuwa Mungu ni wa wote ambapo
pia alisema kuwa zoezi la harambee
litaisha tarehe 25 mwezi huu kwa walioahidi wote kutimiza ahadi zao.
“Sisi kanisa
letu kama linavyosema kuwa ni All- Nations Christian Tabernacle yaani hekalu la
makanisa ya mataifa yote, hivyo hatubagui mtu kwa dhehebu wala dini na wote
wanakaribishwa kila jumapili kwenye ibada zetu,” alisema Pastor Sos na kuwataka
watu waendelee kuwasiliana naye kwa ahadi na michango kupitia namba 0784935855.
Naye
mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Kanisa hilo, bwana Ibrahimu Chanikicha,
aliwashukuru wote wanaoendelea kuchangia kwa hali na mali na kuwaomba waendelee
kuwa na moyo huohuyo.
Mchungaji wa Kanisa la All- Nations Christian Tabernacle (ACT) Sos Mabele akisali wakati akifungua Ibada hiyo iliyokuwa ni ya ufunguzi wa Harambee ya uchangiaji wa ujenzi wa Kanisa
Mmoja ya waumini akisoma neno la Mungu wakati Mchungaji akiwaongoza
Waumini wakimsikiliza kwa makini Baba Mchungaji akifundisha neno
Katibu wa kamati ya ujenzi Debora Simon (wa kwanza Kulia) pamoja na waumini mwengine wakifuatilia neno
Mchungaji
wa Kanisa
la All- Nations Christian Tabernacle (ACT) Sos Mabele akiendelea kutoa
mahubiri wakati wa Ibada hiyo ya uzinduzi wa Harambee ya uchangiaji kwa
ajili ya ujenzi wa Kanisa
Mweka Hazina wa Kanisa hilo Bwana Geofrey Raymond akifuatilia Ibada kwa makini
Waumini wakiendelea kufuatilia Ibada kwa makini
Mmoja wa watoto akisoma Neno la Mungu wakati wa Ibada hiyo ya Uchangiaji kwa ajili ya Ujenzi wa Kanisa
Wakijiandaa Kumtukuza Mungu
Baadhi ya watoto wakiwa Ibadani
Mchungaji
wa Kanisa
la All- Nations Christian Tabernacle (ACT) Sos Mabele akiimba nyimbo za Sifa
Mweka Hazina wa Kanisa hilo Bwana Geofrey Raymond akizungumza neno wakati wa Ibada hiyo
Ibrahim Chanikicha Mwenyekiti wa kamati ya Ujenzi akizungumza jambo
Waimbaji wakiendelea kumtukuza Mungu kwa njia ya Nyimbo za Sifa
Waumini wakiimba nyimbo za Sifa
Muda wa Maombezi ulifika ambapo Mchungaji
wa Kanisa
la All- Nations Christian Tabernacle (ACT) Sos Mabele aliwaombea watumishi mbali mbali
Wakiendelea kusifu na Kuabudu
Picha zote na Fredy Njeje
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akizungumza na Mgeni wake Makamu wa Rais wa Cuba Mh. Salvador Valdes
Mesa wakati alipokutana naye Ikuu leo kwa mazungumzo ambapo
wamezungumzia jitihada za Serikali hizi mbili ya Cuba na Tanzania
katika kuendelea kuimarisha na kudumisha mahusiano mazuri yaliyopo kwa
manufaa ya wananchi wa nchi hizi mbili.(PICHA KWA HISANI YA OFISI YA
MAKAMU WA RAIS)
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
na Mgeni wake Makamu wa Rais wa Cuba Mh. Salvador Valdes Mesa wakiwa
katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Tanzania na Cuba.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akimkabidhi zawadi ya picha ya mnyama Chui anayepatikana katika mbuga
za wanyama za Tanzania Mgeni wake Makamu wa Rais wa Cuba Mh. Salvador
Valdes Mesa.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akipokea zawadi ya picha kutoka kwa Mgeni wake Makamu wa Rais wa Cuba
Mh. Salvador Valdes Mesa , Kulia ni Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa.
................................................................................................
Na. Immaculate Makilika- MAELEZO
Serikali
ya Tanzania na Cuba zimeahidi kuendeleza ushirikiano uliopo, ambao
umeasisiwa na viongozi wa mataifa hayo Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
wa Tanzania pamoja na Fidel Castro Rais mstaafu wa Cuba.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Ikulu leo jijini Dar es salaam, Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu, amesema kuwa
Makamu wa Rais wa Cuba, Mhe. Salvador Valdes Mesa ameitikia mwaliko huo
wa kuja nchini kwa vile nchi hizo mbili zimekua na ushirikiano na
mahusiano mazuri kwa muda mrefu.
“Ziara
hii ni moja ya jitihada za Serikali hizi mbili ya Cuba na Tanzania
katika kuendelea kuimarisha na kudumisha mahusiano mazuri yaliyopo kwa
manufaa ya wananchi wa nchi hizi mbili ili kuhakikisha mahusiano
yaliyopo yanaimarika zaidi” alisema Makamu wa Rais
Katika
ziara hiyo ya Makamu wa Rais wa Cuba nchini, mambo mbalimbali
yalijadiliwa ikiwemo masuala ya Afya, Elimu, Michezo, na Utamaduni,
ambapo katika sekta ya afya nchi ya Cuba imepiga hatua na kuahidi
kushirikiana na Tanzania ili kujenga kiwanda cha kisasa cha
kutengeneza madawa ya binadamu.
Aliongeza
kuwa Tanzania imeomba Serikali ya |Cuba kuendelea kusaidia sekta hiyo
kwa kufundisha wataalamu wa afya, ambapo tayari madaktari 24 kutoka Cuba
wako nchini kwa ajili ya kusaidia kutoa huduma za kitabibu na mafunzo
katika mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Visiwani.
Masuala mengine yaliyojadiliwa katika ziara hiyo ni pamoja na ushirikiano katika sekta ya elimu, biashara, utalii na uwekezaji.
Ambapo
pia Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Suluhu
amesisitiza nia ya Serikali ya Tanzania kudumisha ushirikiano huo ikiwa
ni pamoja kupongeza jitihada za kuboresha uhusiano wa Cuba na Marekani.
Kwa
upande wake, Makamu wa Rais wa Cuba, Mhe. Salvador Antonio Valdes Mesa
ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kuonesha ushirikiano kwa
nchi yake na kuahidi kuendelea kutoa msaada kwa Tanzania.
“Tumeamua
kuendelea kuboresha mahusiano yetu na Tanzania kwa kuongeza ushirikiano
wetu katika sekta nyingine ambazo hatukuwa tunashirikiana hapo awali
kama vile sekta ya utalii” alisema Makamu wa Rais wa Cuba
Aidha,
Mhe. Mesa ameiomba Tanzania kuendelea kuiunga mkono Cuba katika masuala
ya kimataifa ili kuendeleza ushirikiano na kukuza uchumi kwa nchi zote
mbili.
Makamu
wa Rais wa Cuba aliwasili nchini jana jioni kwa ziara ya siku tatu
ambapo alipata fursa ya kuonana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa John Magufuli .
No comments:
Post a Comment