Pages

Tuesday, October 4, 2016

RAIS JOSEPH KABILA ATUA NCHINI, APOKELEWA NA MWENYEJI WAKE RAIS JOHN MAGUFULI

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa kimataifa wa Ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere JNIA.(PICHA NA IKULU)
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na mgeni wake wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila wakati nyimbo za Taifa za mataifa yote mawili zikipigwa kabla ya ukaguzi wa gwaride lililoandaliwa kwa ajili ya heshima yake.
 Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila akikagua gwaride la heshima lililoandaliwa kwa ajili yake mara baada ya kuwasili uwanjani hapo.
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila akipunga mkono wakati kikundi cha ngoma za asili kilipokuwa kinatumbuiza uwanjani hapo

No comments:

Post a Comment