Pages

Tuesday, October 4, 2016

MAJALIWA AKUTANA NA MBUNGE WA MSALALA NA MADIWANI WAKE


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige (wapili kulia), Ofisini kwake mjini Dodoma Oktoba 3, 2016. Kushoto ni makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Msalala, Bebedicto Manuari (kushoto) na Diwani wa Kata ya Isaka, Gerlard Mwanzia. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MAKAMU WA RAIS WA CUBA AONDOKA ZANZIBAR.

cu1
Makamu wa Rais wa Cuba Salvador Antonio Valdes Mesa kushoto akioneshwa jambo na Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo kulia wakati akifanya matembezi katika mji Mkongwe wa Zanzibar,kabla ya kuondoka leo na kurejea nyumbani.
cu2
Makamu wa Rais wa Cuba Salvador Antonio Valdes Mesa katikati akipita katika baadhi ya maeneo ya mji Mkongwe wa Zanzibar kabla ya kuondoka leo na kurejea nyumbani.
cu3
Makamu wa Rais wa Cuba Salvador Antonio Valdes Mesa katikati akipata maelezo kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo Dk, Amina Ameri kulia wakati akitembelea maeneo ya mji Mkongwe wa Zanzibar kabla ya kuondoka leo na kurejea nyumbani.
cu4
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi Kushoto akiwa pamoja na Makamu wa Rais wa Cuba Salvador Antonio Valdes Mesa wakikagua Gwaride rasmi katika Uwanja wa Ndege wa Zanzibar kabla ya kuondoka leo na kurejea nyumbani.
cu5
Ndege iliompakia Makamu wa Rais wa Cuba Salvador Antonio Valdes Mesa ikiacha aridhi na kuingia mawinguni baada ya kumaliza Ziara ya kikazi ya Siku moja Zanzibar. PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

KIM KARDASHIAN ALIHOFIA WEZI WALIOMVAMIA HOTELINI PARIS WANGEMBAKA


Kim Kardashian alihofia kuwa huenda angebakwa, wakati taarifa za kuhuzunisha zikiibuka kuwa alifungwa mikono na kuachwa kwenye bafu katika hoteli ya kifahari Jijini Paris na kuibiwa vito vya mamilioni ya dola.

Wakati tukio hilo likitokea jana asubuhi Kim alikuwa amelala na mara akashtuka baada ya kuwasikia wezi hao waliokuwa wamevalia mavazi ya polisi na kufunika sura zao wakipanda ngazi za kwenye jengo alilokodi kwenye hoteli.

Kim, aliwaomba wezi hao wasimuue na kuwaambia kuwa anawatoto wawili wakati wezi hao watano walipomkamata mikono na kumfunga na kumziba mdomo kwa kumfunga na  gundi ya kufungia vifurushi 'duct tape' na kisha kumuacha bafuni.
     Muonekano wa ndani wa jengo la hoteli ambalo Kim alikuwa amelipia kwa malazi Jijini Paris 
               Kim Kardashian akiwa na mumewe Kanye West baada ya kurejea nchini Marekani

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA RAIS KABILA WA DRC KWA MAZUNGUMZO RASMI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimlaki Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 4, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitambulisha viongozi kwa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 4, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 4, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 4, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 4, 2016

MAJALIWA AKUTANA NA MWENYEKITI WA BARAZA LA UDOM

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Gaudencia Kabaka kabla ya mazungumzo yao, Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dodoma Oktoba 3, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM), Gaudencia Kabaka (kulia kwake) na ujumbe wake, Ofisini kwake mjini Dodoma Oktoba 3, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

TYSON FURRY AMESEMA BADO ATAENDELEA NA MCHEZO WA NGUMI


Bingwa wa Uzito wa Juu duniani Tyson Furry amesema bado anaendelea na ngumi, baada ya awali kuashiria kuwa amejiuzulu mchezo huo.



Bondia huyo Muingereza ambaye alijiondoa katika pambano la Oktoba 29 la dhidi ya Wladimir Klitschko kutokana na masuala ya kiafya, alituma twitti isemayo “Mimi ni bora na nimejiuzulu."



Hata hivyo saa tatu baadaye Fury, 28, alirejea katika mitandao ya jamii na kusema alikuwa anatania, bado hajajiuzulu.

RAIS WA FIFA GIANNI INFANTINO APENDEKEZA KUONGEZWA TIMU KOMBE LA DUNIA

Rais wa Fifa Gianni Infantino amependekeza kuongeza timu zinazoshiriki fainali za kombe la dunia kuwa 48 ikiwa ni idadi kubwa kuliko ahadi aliyoitoa wakati wa uchaguzi.

Infantino amependekeza idadi hiyo na kusema kuwa timu 16 zitatolewa baada ya mzunguko mmoja wa kwanza wa mtoano, kabla ya kuingia hatua ya makundi.

Baada ya hapo michuano hiyo itaendelea kama kawaida kwa kuwa na timu 32 zikichuana katika hatua ya makundi na baadae kufikia hatua ya mtoano.

RIGOBERT SONG BAHANAG ALAZWA BAADA YA KUPATWA NA KIHARUSI

Mchezaji mkongwe wa zamani wa timu ya taifa ya Cameroon, Rigobert Song Bahanag, amepatwa na tatizo la kiharusi na kulazwa katika kituo cha Yaoundé Emergency.

Song ambaye pia aliwahi kuwa kapteni wa timu ya taifa ya Cameroon, alianza kuugua siku ya jumapili, kwa mujibu wa chanzo cha karibu na familia yake.

Raia wa Cameroon wametumia mitandao ya kijamii kumuombea Song apone haraka, ambapo tangu alazwe bado yupo katika hali ya mahututu.

Beki huyo mwenye nguvu aliwahi kuzichezea timu za Ligi Kuu ya Uingereza za Liverpool na West Ham, vile vile alizichezea Metz na Lens za Ufaransain France na Galatasaray ya Uturuki.

CHAMA CHA WATU WENYE UALIBINO MKOANI MWANZA CHATOA KILIO CHAKE KWA RAIS MAGUFULI.

                                                                                                     Na BMG
 

Chama cha watu wenye ualibino mkoani Mwanza, kimemuomba Rais John Pombe Magufuli, kukemea vikali vitendo vya ukatili ikiwemo kutekwa na kuuawa kwa watu hao kama anavyokemea masuala ya rushwa na ufisadi kwenye mikutano yake mbalimbali.

Mwenyekiti wa chama hicho, Alfred Kapole, ametoa ombi hilo Jijini Mwanza wakati akizungumzia juhudi zinazofanywa na chama hicho ili kuhakikisha vitendo vya utekaji, ukataji viungo pamoja na mauaji kwa watu wenye ualibino nchini vinatokomezwa.

Amesema pamoja na juhudi zinazofanywa na vyombo vya ulinzi na usalama kwa kushirikiana na wanajamii katika kutokomeza vitendo hivyo, bado watu wenye ualibino nchini wanaishi kwa wasiwasi mkubwa kwani wamekuwa wakiwindwa na baadhi ya watu wenye imani potofu za kishirikina hivyo Rais Magufuli anapaswa kukemea vikali hali hiyo.

Mkoa wa Mwanza ni miongoni mwa mikoa yenye rekodi zisizoridhisha za matukio ya kutekwa, kukatwa viungo na kuuawa kwa watu wenye ualibino hapa nchini ambapo kesi tatu kati ya kesi 27 zilizoripotiwa mahakamani zimetolewa hukumu yake na wahusika kuhukumiwa adhabu ya kunyongwa.

"MRADI WA GREEN VOICES UMEONYESHA MAFANIKIO, UTAWAKOMBOA WANAWAKE TANZANIA"

Makamu wa Rais mstaafu wa Hispania na Rais wa Taasisi ya Women for Africa Foundation, Mama Maria Tereza Fernandez de la Vega, akisalimiana na maofisa wa ulinzi na usalama mara baada ya kuwasili katika bandari ya Nansio, Ukerewe hivi karibuni kuzindua mradi wa kilimo cha viazi lishe unaofadhiliwa na taasisi yake ya inayoshughulikia maendeleo ya Wanawake wa Afrika.
Mama Getrude Mongella (waliosimama katikati mwenye blauzi nyekundu) akifafanua jambo kwa Mkamu wa Rais mstaafu wa Hispania na Rais wa Taasisi ya Women for Africa Foundation, Mama Maria Tereza Fernandez de la Vega, wakati walipotembelea mradi wa kilimo cha viazi lishe wilayani Ukerewe. Kushoto kwa Mama Mongella ni Bi. Leocadia Vedastus, ambaye ni mshiriki kiongozi wa mradi huo.
Makamu wa Rais mstaafu wa Hispania na Rais wa Taasisi ya Women for Africa Foundation, Mama Maria Tereza Fernandez de la Vega, akiangalia bidhaa zilizo mbele yake ambazo zinatokana na viazi lishe katika kuongeza mnyororo wa thamani. Hii ni wakati alipokwenda kuuzindua mradi huo wilayani Ukerewe katika Mkoa wa Mwanza.

MRATIBU wa mradi wa akinamama wapambanao na mazingira wa Green Voices, Alicia Cebada, amesema kwamba wamefarijika na mradi huo kwa kuwa umeonyesha mafanikio makubwa nchini Tanzania.

Akizungumza wakati wa kuhitimisha ziara yao ya kutembelea miradi mitano kati ya 10 inayotekelezwa na wanawake wa Tanzania,hivi karibuni mratibu huyo kutoka taasisi ya Women for Africa Foundation, alisema hawakutegemea kama miradi waliyoianzisha akinamama hao ingeweza kufanikiwa katika kipindi kifupi tangu kuwapatia mafunzo.
 
“Ni kipindi kifupi tangu wanawake hawa walipopatiwa mafunzo nchini Hispania, lakini kwa hakika miradi waliyoibuni imeonyesha mafanikio, ni endelevu, rafiki wa mazingira na italeta tija kwao na taifa kwa ujumla,” alisema Alicia.
 
Aidha, alieleza kwamba, changamoto pekee ambayo ipo mbele yao ni kuhakikisha miradi hiyo inasimama na kuwafundisha wanawake wengi kadiri wawezavyo ili kuhakikisha wanajiletea maendeleo katika maeneo yao kiuchumi na kijamii.
 
“Tumewaona wanawake wa Ukerewe wanavyolima viazi lishe na kuongeza mnyororo wa thamani, tumewaona wanawake wa Kijiji cha Kitanga huko Kisarawe wakiongozwa na ‘Malkia wa Muhogo’ Abia Magembe, tumewatembelea akinamama wanaofuga nyuki kupambana na ukataji wa misitu huko Kisarawe, pia tumewaona wanawake wa Morogoro namna wanavyokausha mboga na kuwa na uhakika wa akiba ya chakula, na hapa (Bunju) tumeshuhudia jinsi kilimo cha uyoga kilivyo na faida, ni miradi mizuri, endelevu na rafiki mkubwa wa mazingira,” alisema.

CUBA KUISAIDIA ZANZIBAR KATIKA SEKTA YA AFYA

Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Cuba Bwana Salvador Antonio Valdes Mesa wa Tatu upande wa Kushoto na ujumbe wake akizungumza na mwenyeji wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wa kwanza kulia ofisini kwa Balozi Seif Vuga Mjini Zanzibar.
Balozi Seif akimuonyesha mgeni wake Bwana Salvador baadhi ya vitu vya utamaduni kama kanga pamoja na vyakula vya viungo alivyomuandalia kama zawadi ya uwepo wake Visiwani Zanzibar.
Balozi Seif akimkabidhi zawadi ya Kasha Makamu wa Rais wa Cuba Bwana Salvador likisheheni vuti vya utamaduni na vyakula vya viungo mara baada ya kumaliza mazungumzo yao.
Balozi Seif wa Nne kutoka Kulia na Mgeni wake Bwana Salvador wanne kutoka kushoto wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine walioshiriki kwenye mazungumzo yao ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kulia akimuaga mgeni wake Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Cuba Bwana Salvador Antonio Valdes Mesa mara baada ya mazungumzo yao. Picha na – OMPR – ZNZ.

Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Cuba Bwana Salvador Antonio Valdes Mesa ameahidi kwamba Nchi yake itaongeza nguvu za uhusiano na Jamuhuri ya Muungano wa Tanazania ili kizazi kipya kipate fursa pana ya kurithi Historia ya muda mrefu iliyopo ya pande hizo mbili.

Alisema anafarajika kuona Sekta ya Afya imepanua zaidi mafungamano ya pande hizo mbili kufuatia kundi kubwa la Madaktari wazalendo kumaliza mafunzo yao ya muda mrefu chini ya usimamizi wa Wataalamu wa Cuba.

Bwama Salvardo Antonio Valdes Mesa alieleza hayo wakati wa mazungumzo yake na Mwenyeji wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hapo Ofisini kwa Balozi Seif Vuga akiuongoza Ujumbe wa Viongozi kadhaa katika ziara yake ya siku mbili Visiwani Zanzibar.

Bwana Salvardo alisema kundi hilo la Madaktari wazalendo waliopata mafunzo hayo litasaidia kuongeza kasi za utoaji wa huduma za Afya kwa Wananchi katika maeneo mbali mbali kama azma na matarajio ya Zanzibar yalivyokusidiwa.

MAKAMO WA RAIS WA CUBA AKUATANA NA DK.SHEIN

cb1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba Salvador Antonio Valdes Mesa mara alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo jioni,akiwa katika ziara ya siku mbili na ujumbe aliofuatana nao,[Picha na Ikulu.] 03/10/2016.
cb2
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba Salvador Antonio Valdes Mesa mara alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo jioni akiwa katika ziara ya siku mbili na ujumbe aliofuatana nao,[Picha na Ikulu.] 03/10/2016.
cb3
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba Salvador Antonio Valdes Mesa (wa tatu kulia) mara alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo jioni akiwa katika ziara ya siku mbili na ujumbe wake,[Picha na Ikulu.] 03/10/2016.
cb4
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba Salvador Antonio Valdes Mesa (kushoto) mara alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo jioni akiwa Nchini kwa ziara ya siku mbili na ujumbe wake,[Picha na Ikulu.] 03/10/2016.

MAKONDA AZITAKA TAASISI NA MASHIRIKA YA UMMA KUTUMIA TTCL

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (wa pili kulia) akikata keki kuashiria uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja wa TTCL leo kwenye duka la huduma kwa wateja na bidhaa za TTCL lililopo Makao Makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Waziri Waziri Kindamba pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Biashara TTCL Kanda ya Dar es Salaam, Bi. Jane Mwakalebela (kulia) wakishuhudia tukio hilo. Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Waziri Waziri Kindamba (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto) wakigonganisha glasi za mvinyo mara baada ya mkuu huyo wa mkoa kuzinduwa Wiki ya Huduma kwa Wateja wa TTCL leo kwenye duka la huduma kwa wateja na bidhaa za TTCL lililopo Makao Makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akimlisha keki Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Waziri Waziri Kindamba kwenye uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja wa TTCL leo.

MAFISA WA TAASISI YA OPEC NA TASAF WAFURAHISHWA NA MIRADI YA KUNUSURU KAYA MASKINI JIJINI ARUSHA

Afisa Mwandamizi kutoka Idara ya Kimataifa ya Mfuko wa misaada ya OPEC unaofadhili miradi mbalimbali chini Mfuko wa Tasaf nchini,Solomon Amieyeofori kutoka Vienna ,Austria(kushoto)akiwa na maafisa wa Mfuko wa Tasaf nchini kukagua miradi katika Jiji la Arusha. 

Ujumbe huo ukakagua ujenzi wa madarasa mawili katika Shule ya Msingi Azimio jijini Arusha.
Mmoja wa wanakikundi cha Ushonaji eneo la Kambi ya Fisi Kata ya Ngarenaro,Bupe Anyingise ambaye ni miongoni mwa wanufaikaji wa kunusuru Kaya maskini akishona nyumbani kwake ,Tasaf imewanunulia Vyerehani,Meza na vifaa mbalimbali kuwawezesha kujipatia kipato vilivyogharimu zaidi ya sh 28 milioni.
Afisa Mwandamizi kutoka Idara ya Kimataifa ya Mfuko wa misaada ya OPEC unaofadhili miradi mbalimbali chini Mfuko wa Tasaf nchini,Solomon Amieyeofori kutoka Vienna ,Austria( wa pili kushoto)akiwa na maafisa wa Mfuko wa Tasaf nchini kukagua miradi katika Jiji la Arusha katika Shule ya Msingi Azimio,Kata ya Elerai.

WATANZANIA WATAKIWA KUJENGA MOYO WA KUJITOLEA

  Mmoja wa wanakikundicha Marafiki wa Batuli aliyejulikana kwa jina la Tausi Swalehe akiwa anakabidhi anagawa peniseli kwa baadhi ya wanafunzi ambao ni yatima wanaosoma katika shule ya msingi Ngarenaro ilipo katika kata ya Sokoni one ndani ya jiji la Arusha
  Wanakikundi wa kikundi cha marafiki wa batuli wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi waliowagawia msaada wa sare za shule ,penseli ,madaftari na kalamu ikiwa ni moja ya mchango wao kama wao wanakikundi .
                                                                                                Na Woinde Shizza Arusha
 

Wazazi na watanzania wameaswa kujenga moyo Wa kujitolea kwa makundi maalumu yasiojiweza nakuwapa kile mungu alichowajaalia nakuondoa ubaguzi kwa watoto yatima waliochiwa na ndugu zao.
Hayo yalisemwa na Tausi swalehe baada ya kikundi cha marafiki Wa batuli kufika kutoa msaada kwenye shule za unga ltd,na Sahel zilizopo kata ya Sokon 1 jijini Arusha nakuwata jamii kuwa na moyo huo wa kusaidia yatima na makundi yasiojiweza.
Alisema kuwa msaada waliotoa unathamani ya tsh.700,000 vikiwemo madaftari'sare za shule,penseli na pen ambazo zitawapunguzia adha watoto wenye uhitaji wakiwemo yatima na wasiojiweza ambao wameshindwa kujihudumia na kufikia malengo.
Alisema kuwa ni vizuri kwa jamii kuendelea kuzijali familia zisizojiweza na mayatima iliwaweze kufikia malengo yao yakupata elimu itayowasaidia kujikwamua kimaisha na kuondokana na utegemezi.
 

''Sio wote wenye kuweza kujiendesha kimaisha yatupasa kama jamii kujipanga nakuweza kuwasaidia wenye uhitaji natusingoje kuiachia serikali pekee''alisema Tausi.
Akipokea msaada huo kwa niaba ya wanafunzi hao wenye uhitaji mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Unga Ltd Rachel Mussa alisema kuwa wapo wengi katika jamii wenye fedha lakini wamekuwa hawatumii vipato vyao katika kusaidia makundi yenye uhitaji.
Akatoa rai kwa makampuni na wenye kuguswa kuweza kujitolea kwa kile kidogo mungu alichowajaalia kwani wapo watoto wenye uhitaji nao wajitokeza kuwasaidia.
 

Nae Mwanafunzi mwenye uhitaji kwa niaba ya wenzake 86 Konsolata Michael alisema kuwa wanashukuru sana kwa msaada huo kwani umukuja wakati muufaka na kuwataka kuendelea kusaidia watoto yatima na wasiojiweza na mungu awazidishie pale mlipopunguza kwa ajili yetu.

WAZIRI MKUU AKAGUA MAENEO YA UJENZI DODOMA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea maeneo yaliyopendekezwa kujengwa mji wa Serikali na kujiridhisha kuwa yanatosha kwa ajili ya ujenzi wa makao makuu.

Katika ziara hiyo aliyoifanya leo mchana (Jumatatu, Oktoba 3, 2016) Waziri Mkuu amesema ameridhishwa na ukubwa wa maeneo hayo ambayo pia yanatosha kujenga miundombinu inayohitajika.

Katika ziara hiyo Waziri mkuu ameridhishwa na maeneo yaliyotengwa na Mamlaka ya Ustawishaji wa Makao Makuu(CDA) yanayofaa kuwekeza kwa ujenzi wa miundombinu ya biashara kama masoko na hoteli na viwanda na tumejirishisha kuwepo kwa ardhi ya kutosha.

Wakati huo huo Waziri Mkuu amekaribisha wawekezaji wa miradi mbalimbaliya maendeleo ikiwemo ya ujenzi wa nyumba za watumishi ambao watajenga nyumba za makazi na kuziuza kwa watumishi wa umma na wananchi.

Aidha amebainisha kuwa muwekezaji atakayekuwa tayari awasiliane na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana ambaye ndiye anayeratibu shughuli hiyo huku akikaribisha wawekezaji wa ujenzi wa hoteli za kitalii na kawaida kwa kuwa wanatarajia kupata wageni wengi.

“Tumekaribisha pia wawekezaji wa ujenzi wa viwanda tumeiona ardhi inatosha na uzalishaji ni mkubwa Kanda ya kati kwa mkoa wa Dodoma wenyewe, Manyara, Singida na mikoa ya jirani ya Iringa na Morogoro inaweza kunufaika na fursa hizo,” amesema.

Awali Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA), Mhandisi Paskasi Muragili alisema maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya ujenzi huo ambayo Waziri Mkuu alimeyatembelea ni Chigongwe lenye hekta 11,297, Kikombo hekta 13,275 na Nyankali hekta 2,370.
 

IMETOLEWA NA: 
OFISI YA WAZIRI MKUU 
S. L. P. 980, 
DODOMA. JUMATATU, OKTOBA 3, 2016

RAIS DKT. MAGUFULI AMTEUA PROF. LAWRENCE MUJUNGU MUSERU KUWA MKURUGENZI MTENDAJI WA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI

MKURUGENZI ARUSHA AFAFANUA TUHUMA ZA UBADHIRIFU WA JENGO LA UTAWALA KALIUA

Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Arusha, Athumani Kahamia
                                                                                                
                                                                                          Na Woinde Shizza,Arusha 

Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Arusha, Athumani Kahamia ametoa ufafanuzi kuhusu tuhuma ya matumizi mabaya ya fedha kiasi cha sh, 500 milioni zilizotengwa kwa ajili ya ujenzi wa jengo la utawala katika halmashauri ya Kaliua na kusema kwamba fedha hadi anahamishwa fedha hizo hazikuwahi kuletwa katika halmashauri hiyo kutoka serikali kuu.

Hivi karibuni kumekuwa na tuhuma mbalimbali zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii nchini ambapo Kahamia anatuhumiwa kutumia kiasi hicho cha fedha zilizotengwa kwa ajili ya ujenzi wa jengo la utawala katika halmashauri ya Kaliua wakati akiwa mkurugenzi wa Kaliua kabla ya kuhamishiwa jijini Arusha.

Akihojiwa na mwandishi Wa Habari hizi Kahamia alisema kwamba aliripoti mnamo febuari 2015 katika halmashauri hiyo na kukuta ujenzi wa jengo la utawala ukiendelea ambapo katika bajeti ya halmashauri ya Kaliua mwaka wa fedha 2015/16 waliomba fedha hizo kwa ajili ya kukamilisha ujenzi huo katika awamu ya kwanza lakini serikali haikuleta pesa hizo.

Alisema ya kwamba lakini pamoja na kutenga bajeti ya fedha hizo halmashauri hiyo haikupokea kiasi hicho kutoka serikali kuu na kusisitiza kwamba hadi anaondoka Kaliua fedha hizo hazikuwahi kuzipokea.

"Hadi tarehe 30 juni mwaka huu hizo fedha tulikuwa bado hatujazipokea mpaka leo tunavyoongea hizo fedha hazijapokelewa taarifa kwamba nimezitafuna zinalenga kunichafua "alisema Kahamia

Hatahivyo, alifafanua tuhuma kwamba tayari ameandikiwa barua ya kurudishwa Kaliua ili kujibu tuhuma zinazomkabili na kusema si kweli kwani hadi sasa hajapokea barua yoyote wala wito kutoka mamlaka yoyote kumtaka arudi kujibu madai hayo.

Hata hivyo, alifafanua tuhuma za kumwingilia mkandarasi kutoka kampuni ya Saram Company Limited iliyopewa zabuni ya kujenga jengo hilo la utawala na kusema yeye kama mwajiri alivunja mkataba na kampuni hiyo kwa mujibu wa sheria kwa kuwa mkandarasi huyo alionekana kusuasua katika majukumu yake.

Alisema kwamba baada ya mkandarasi huyo kuonyesha udhaifu katika mkataba wake walimpa onyo na kisha nitosi kabla ya kuvunja mkataba wake ambapo alikimbilia mahakamani lakini walimshinda kesi hiyo.

"Huyu mkandarasi alipaswa kumaliza kazi mwezi Mei mwaka 2015 lakini hadi Septemba mwaka huo alikuwa bado hajamaliza kazi yake ndipo tukavunja mkataba wake Akakimbilia mahakamani tukamshinda akakata rufaa tukamshinda tena mchezo ukaishia hapo hapo "alisema Kahamia

Alisema kwamba wakati wa kuvunja mkataba na mkandarasi huyo zoezi hilo lilisimamiwa na timu ya wanasheria wa halmashauri ya Kaliua pamoja na mkaguzi wa ndani chini ya usimamizi wa mkuu wa mkoa wa Tabora wakati huo, Ludovick Mwananzila.

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kaliua, Haruna Kasele alipoulizwa kuhusu tuhuma hizo kwa njia simu alisema kwamba ni kweli halmashauri hiyo katika bajeti ya mwaka 2015/16 waliomba kiasi cha sh,500 milioni kwa ajili ya ujenzi wa jengo hilo lakini hadi mwaka wa fedha wa serikali unakwisha hawakuwahi kupokea fedha hizo.

Hatahivyo,alithibitisha taarifa za halmashauri hiyo kuvunja mkataba na mkandarasi huyo chini ya baraza la madiwani na kusema sababu iliyopelekea ni baada ya mkandarasi huyo kusuasua na kushindwa kumaliza kazi aliyopewa kwa wakati mwafaka. 


Kuhusu madai ya Kahamia kuandikiwa barua ya kuitwa ili kuhojiwa kuhusu tuhuma hizo mwenyekiti huyo alisema kwamba hakuna jambo kama hilo na wala hawajaandika barua ya kumwita kumhoji mkurugenzi huyo.

WATU 52 WAMEKUFA NA WENGINE WENGI KUJERUHIWA KWENYE GHASIA NCHINI ETHIOPIA

Watu wapatao 52 wamekufa na wengine wengi wamejeruhiwa katika mkoa wa Oromia nchini Ethiopia baada ya kufanyika maandamano wakati wa tamasha la kidini.

Serikali ya Ethiopia imesema baadhi ya watu wamekufa baada ya kukanyagana baada ya polisi kufyatua mabomu ya machozi, kurusha risasi za mipira na kutumia virungu.

Waziri Mkuu Hailemariam Desalegn amesema waandamanaji walipanga kufanya ghasia walizofanya na kusababisha watu kuanguka kwenye bonde na kufa.
    Waandamanaji wakiangaliana uso kwa uso na askari wakati wa maandamano hayo
                      Askari wakitumia mabomu ya machozi kuwasambaratisha waandamanaji

TANESCO DODOMA YAOMBA KUPEWA HADHI YA MKOA MAALUM

MENEJA wa Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa Dodoma, Mhandisi Zakayo Temu amesema ni vema mkoa huo ukapewa hadhi ya mkoa maalum ili uweze kukabiliana na changamoto za ujio wa Serikali Dodoma.

Ametoa ombi hilo jana jioni (Jumapili, Oktoba 2, 2016) wakati akitoa taarifa ya utendaji wa TANESCO Mkoa wa Dodoma mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye alifika kwenye kituo cha kupozea umeme cha Zuzu nje kidogo ya mji wa Dodoma, kukagua mahitaji halisi ya umeme ikilinganishwa na ujio wa watumishi mkoani humo.

Mhandisi Temu alisema: “Tunaomba mkoa wetu wa Dodoma ambao ni Makao Makuu uangaliwe kwa jicho la pekee na kupewa hadhi ya mkoa maalum kama ilivyo kwa Dar es Salaam ambako kuna mikoa minne ya ki-TANESCO.”

“Dar es Salaam ina mikoa minne ya Ilala, Kinondoni, Temeke na Mikocheni. Mkoa wetu unatakiwa kubeba majukumu yote ya Serikali kama yanavyofanyika hivi sasa katika Jiji la Dar es Salaam. Hivyo, tunaomba tupewe kipaumbele kwenye rasilmali watu, usafiri na vitendea kazi,” alisema.

Alisema TANESCO inabidi iende kwa kasi zaidi ili kumudu wimbi la wafanyakazi wanaohamia Dodoma.

Akifafanua kuhusu uboreshaji wa miundombinu iliyopo, Mhandisi Temu alisema kukamilika kwa njia ya kusafirisha umeme wa kilovolti 400 kutoka Iringa mpaka Shinyanga kupitia Dodoma, kumeboresha upatikanaji wa umeme kwenye mji wa Dodoma.

“Umeme unapatikana ukiwa na voltage nzuri na hauchezichezi na hivi sasa tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara limepungua kwa kiasi kikubwa. Kukamilika kwa njia hii kunaleta uwezekano wa kufanya matengenezo kwenye njia moja ya umeme bila kuathiri upatikanaji wa umeme kama ilivyokuwa awali,” alisema.

Alisema kazi inayoendelea hivi sasa ni kubadilisha nguzo za umeme zilizochakaa; kubadilisha njia za msongo wa kilovolti 11 kwenda kilovolti 33 zenye urefu wa km. 85 na transforma 74 ili kupunguza upotevu wa umeme na kuingiza njia hizo kwenye njia mpya ya 132/33kV katika maeneo ya manispaa ambayo yanapata umeme kupitia njia za 11kV.

Alisema mbali ya kusambaza umeme kwa njia ya mzunguko wa mji (ring circuit), wataongeza vituo vikubwa viwili vya kupozea umeme katika maeneo ya Msalato na Kikombo.

Mhandisi Temu alisema wameanza kuboresha miundombinu ya umeme ili kuwezesha baadhi ya wilaya za mipakani zipate umeme kutoka mikoa ya jirani wakati wa matengenezo au kukiwa na hitilafu za umeme.

“Tunapanga wilaya ya Gairo ipate umeme kutoka Morogoro; Bahi ipate umeme kutoka Manyoni; Mpwapwa hasa maeneo ya Chipogolo yapate umeme kutoka Ruaha Mbuyuni ambako ni karibu zaidi. Pia tunataka wilaya ya Kiteto ipate umeme kutoka Dodoma badala ya Babati kama ilivyo hivi sasa,” alisema.

Alimhakikishia Waziri Mkuu kwamba umeme unaozalishwa na kituo cha Zuzu unatosha mahitaji ya sasa na hata baadaye kwani wanazalisha megawati 48 wakati mahitaji ya juu ni megawati 25 na hivyo kubakiwa na ziada ya megawati 23.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliwaagiza viongozi wa TANESCO mkoa wa Dodoma wahakikishe wanapeleka miundombinu ya umeme kwenye maeneo yanayopimwa viwanja ili wanaonunua wakute huduma hiyo ipo tayari.

“Nimeongea na watu wa idara ya maji, nimewaambia wapeleke miundombinu yao katika maeneo yanayopimwa viwanja. Na ninyi pia mfanye hivyo kama ambavyo watu wa TAMISEMI walijenga barabara za lami katika viwanja vipya vya makazi ili watu wakienda kununua wakute huduma hiyo ipo tayari,” alisema.

“Nimefarijika kukuta kwamba Dodoma hatuna shida ya umeme, hatuna mgao, kwa hiyo endelezeni kazi hii nzuri mnayoifanya,” alisema Waziri Mkuu.

IMETOLEWA NA: 

OFISI YA WAZIRI MKUU, 
S. L. P. 980, 
DODOMA. 
JUMATATU, OKTOBA 3, 2016

No comments:

Post a Comment