Pages

Thursday, June 30, 2016

Ugandan scientist among $250,000 World Food Prize winners

Orange sweet potato shredded for making chips. It is said to be rich in Vitamin A. PHOTO | MORGAN MBABAZI 
By NELSON WESONGA
A Ugandan is among four scientists who have won the $250,000 World Food Prize for their effort in fighting malnutrition.

Millya, Mbilinyi, Kubenea served 5-10-sitting Bunge ban

NELLY MTEMA in Dodoma
THREE MPs on CHADEMA ticket, Mr James Millya (Simanjiro), Mr Joseph Mbilinyi (Mbeya Urban) and Mr Saidi Kubenea (Ubungo) have been banned from attending between five and ten parliamentary sittings from yesterday for misconduct.

Mkutano wa Afrika wa Usalama wa Mitandao WAFANYIKA DAR ES SALAAM

A1 
Naibu Katbu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Dkt. Yahaya Simba akizungumza na washiriki wa Mkutano wa Afrikawa wa Usalama wa Mtandao katika ufunguzi wa mkutano huo kwa Niaba ya Waziri waUjenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa, kwenye Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
A2 
Makamu wa Rais wa Kampuni ya Oracle System Ltd Janusz Naklicki, akitoa Mada kwenye Mkutano wa Afrika wa Usalama wa Mtandao uliofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
A3 
Msanifu wa Mifumo ya Mtandao kutoka Kampuni Oracle Enterprise Architecture, Alexander Smirnov akiwasilisha Mada kwenye Mkutano wa Afrika wa Usalama wa Mitandao uliofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
A4 
Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Afrika wa Usalama wa Mtandao kutoka kutoka nchi mbalimbali wakifuatilia ufunguzi wa mkutano huo wenye lengo la kupata elimu juu ya usalama wa taarifa na mifumo ya Teknolojia ya HabarinaMawasiliano (TEHAMA).
A5 
Naibu Katbu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Dkt. Yahaya Simba (kushoto) akiwa na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Oracle System Ltd Janusz Naklicki (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa Nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara wa Kampuni ya Oracle System Ltd, wakifuatilia Mada kwenye Mkutano wa Afrika wa Usalama wa Mtandao uliofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

WAZIRI MKUU Kassim MAJALIWA AHITIMISHA BUNGE

J1 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa hoja ya kuahirisha bunge, bungeni mjini Dodoma  Juni 30,  2016.
J2 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipongezwa na wabunge baada ya kutoa hoja ya kuahirisha bunge, bungeni mjini Dodoma Juni 30, 2016.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

CHOICE FM NA AFRICAN LYON WAINGIA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO KATIKA KUKUZA VIPAJI NA KUBORESHA MISINGI YA UENDESHAJI WA TIMU.

2
1Mtangazaji  wa Choice Fm cha Dar es Salaam, Jimmy Kabwe (katikati), akizungumza na waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam wakati wa hafla yakuingia makubaliano kati ya Timu ya mpira wa miguu ya African Lyon inayoshiriki ligi kuu Tanzania Bara (Vodacom Premier League) na kituo cha radio cha Choice FM 102.5, juu ya ushirikiano katika kukuza vipaji na kuboresha misingi ya uendeshaji wa timu, wengine kushoto kwake alievaa kanzu ni Mmiliki wa klabu ya African Lyon, Rahim Kangezi, na Mkuu wa Vipindi Choice FM, Antonio Nugaz, Mkuu wa Masoko na Mauzo wa Choice FM .3 
Mkuu wa Vipindi Choice FM, Antonio Nugaz (kulia) akitolea ufafanuzi makubaliano hayo ambapo amesema yanalenga kujenga mazingira ya kuweza kutambua na kuvikuza vipaji vya wanamichezo hasa wale wa mpira wa miguu (kushoto), Mmiliki wa klabu ya African Lyon, Rahim Kangezi
Amesema  makubaliano hayo yataiwezesha Africani Lyon yenye masikani yake Mbagala kushirikiana na Choice FM katika kuandaa mashindano na programm zinginezo ambazo zitaleta mvuto kwa vipaji vya wanamichezo wa Kike na Kiume.
4 
Mmiliki wa klabu ya African Lyon, Rahim Kangezi (katikati), akitoa neno la shukrani kwa kituo cha radio cha Choice FM 102.5 mara baada ya kuingia makubaliano .
5 
Mmiliki wa klabu ya African Lyon, Rahim Kangezi, na Captain African Lyon, Baraka Jafari (Nyaka) wakikabidhiwa jezi wakati wa hafla yakuingia makubaliano kati ya Timu ya mpira wa miguu ya African Lyon inayoshiriki ligi kuu Tanzania Bara (Vodacom Premier League) na kituo cha radio cha Choice FM 102.5, juu ya ushirikiano katika kukuza vipaji na kuboresha misingi ya uendeshaji wa timu.

Naibu Spika Dkt. Tulia akabidhiwa ripoti ya uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 Bungeni mjini Dodoma

K1 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akisalimiana na Mmbunge wa Nkasi Ali Kessy Bungeni Mjini Dodoma Mapema leo.
K2 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akihutubia Bunge Mapema leo mjini Dodoma wakati wa kuhitimisha mkutano wa Tatu wa Bunge la kumi na moja la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
K3 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki akiteta jambo na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako Bungeni Mjini Dodoma leo.
K9Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva akiongoza ujumbe wa tume hiyo kwenye viwanja vya Bunge leo wakati wa Ziara ya kutembelea Bunge na kuwasilisha ripoti ya Uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson.
K4 
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson akisisitiza jambo kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damiani Lubuva na ujumbe wake uliotembelea Bunge ili kumkabidhi Naibu Spika Ripoti  ya Uchaguzi mkauu wa mwaka 2015.

WAZIRI MKUU: SERIKALI ITATOA WARAKA JUU YA UKUSANYAJI MAPATO KUPITIA MAWAKALA

MAJALIWA 
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Halmashauri zitaelekezwa kwa waraka ni vyanzo vipi vitahitaji kutumia wawakala wa ukusanyaji mapato kwani siyo kila chanzo cha mapato ya Halmashauri kitakusanywa kwa ufanisi kwa kutumia au kwa kutotumia mawakala.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo mchana (Alhamisi, Juni 30, 2016) wakati akitoa hoja ya kuhitimisha mkutano wa tatu wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.
Amesema katika ukusanyaji wa mapato, baadhi ya vyanzo vitapaswa kukusanywa na Halmashauri zenyewe kwa kuzingatia miongozo iliyotolewa na Serikali. “Moja ya miongozo hiyo ni kwamba kuanzia sasa, iwe kwa kutumia mawakala au Halmashauri zenyewe ni lazima fedha zinazokusanywa ziwekwe kwenye akaunti ya Halmashauri na kutumia mifumo ya kielektroniki ili kupunguza au kumaliza kabisa masuala ya kutumia malipo kwa fedha taslimu (cash transactions),” alisema.
Amesema katika kutekeleza agizo hilo, Halmashauri itabidi zikubaliane na wakala ni kiasi gani cha asilimia ya makusanyo kitalipwa kwa wakala na malipo yafanyike baada ya kukusanya na kuingizwa kwenye akaunti ya Halmashauri.
Amesema Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa Sura ya 290, inazipa uwezo Mamlaka za Serikali za Serikali za Mitaa kutoza na kukusanya kodi, ushuru na ada mbalimbali kama vyanzo vya mapato vya Mamlaka za Serikali za Mitaa.
“Sheria hiyo pia inazipa mamlaka hizo kuteua mawakala wa kukusanya mapato hayo kwa niaba ya Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu. Lakini Serikali imebaini changamoto za kiufundi katika kufanya tathmini ya vyanzo vya mapato; ugumu katika kupata mawakala wenye weledi katika ukusanyaji mapato na kubuni vyanzo vipya vya mapato, na wakati mwingine watumishi wenyewe kujipa uwakala kinyume na taratibu zinazomzuia mtumishi kufanya biashara na taasisi yake,” alisema.
Amesema hatua ya Mamlaka za Serikali za Mitaa kutumia mawakala ni miongoni mwa mikakati ya kuboresha ukusanyaji mapato na pia kutoa muda mwingi zaidi kwa watumishi wa mamlaka hizo kushughulika na majukumu ya msingi ya Halmashauri na hasa utoaji wa huduma kwa wananchi na usimamizi wa miradi ya maendeleo.

MAJALIWA AKUTANA NA WAJUMBE WA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

C1 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva   katika mazungumzo kati yake na wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi  yaliyofanyika kwenye  makazi yake mjini Dodoma Juni 30, 2016.
C2 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  akimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva katika mazungumzo kati yake ya Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi yaliyofanyika  kwenye makazi yake mjini Dodoma Juni 30, 2016.
C3 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva Taarifa ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi wa Rais na Wabunge wa 2015 kwenye makazi yake mjini Dodoma Juni30, 2016.
C4 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wajumbe wa Tume ya taifa ya Uchaguzi kwenye Makazi yake  mjini Dodoma Juni 30, 2016. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Damian Lubuva.
C5 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi baada ya kuzungumza nao kwenye makazi yake mjini Dodoma Juni 30, 2016. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Damiana Lubuva.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Wawekezaji wazawa wana haki kuwekeza kwenye gesi, mafuta

D1Afisa Habari, Mhandisi  Yisambi Shiwa (kushoto) na Mkaguzi wa Madini Mwandamizi Jeremiah Hango (kulia) kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini Nchini (TMAA), wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kuwahudumia wateja katika  Maonesho ya Kimataifa  ya Saba Saba (Dar es Salaam International  Trade  Fair)  yanayoendelea katika  Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
D2Afisa Habari, Mhandisi  Yisambi Shiwa (kulia) kutoka  Wakala wa Ukaguzi wa Madini Nchini (TMAA) akielezea madini ya dhahabu yanavyochenjuliwa kwa mteja aliyeshika sampuni ya madini hayo kwenye banda la TMAA katika maonesho hayo.
D3 
Mtaalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Phillip Mathayo  (kushoto) akielezea majukumu ya Wizara  kwa mteja aliyetembelea banda  hilo  katika Maonesho ya Kimataifa  ya Saba Saba (Dar es Salaam International  Trade  Fair)  yanayoendelea katika  Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
D5 
Mmoja wa wateja (kushoto) akitoa maoni yake kwenye banda la Shirika la Madini la  Taifa (STAMICO) kwenye Maonesho ya Kimataifa  ya Saba Saba (Dar es Salaam International  Trade  Fair)  yanayoendelea katika  Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

MASHINDANO YA ORYX ENERGIES RALLY OF TANZANIA 2016 KUTIMUA VUMBI JULAI 08 - 10, BAGAMOYO PWANI

Viongozi wakuu na waandaaji wa mashindani ya mbio za Magari wakiwa katika mkutano huo wa waandishi wa habari leo Juni 30 Jijini Dar es Salaam katika hotel ya Southern Sun.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo Tanzania, Bwana Mohamed Kiganja azungumza katika mkutano huo
Rais wa chama cha Magari Tanzania (AAT), Bwana Nizar Jivani akizungumza katika mkutano huo
Bwana Satinder Birdi ambaye ni mwandaaji wa shindano hilo akizungumza katika tukio hilo
Sehemu ya waandishi wa Habari.
TAASISI YA UTAWALA BORA NA DEMOKRASIA NCHINI TANZANIA YAWAKUTANISHA WADAU WA MAZINGIRA.
Jimmy Luhende, Mkurugenzi wa Taasisi ya Utawala Bora na Demokrasia nchini (ADLG), akizungumza katika Mjadala wa Mwezi June uliofanyika hii leo Jijini Mwanza.

Taasisi ya ADLG huendesha mijadala tofauti tofauti kila mwisho wa mwezi ambapo wadau mbalimbali hukutana na kujadili mada husika. Mjada wa mwezi june umeangazia Fursa, changamoto na athari za kimazingira zitokanazo na shughuli za migodini.

Katika mjada huo, wadau wameishauri serikali kupia Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEC, kuboresha sheria ya usimamizi wa mazingira ili kuweza kuwafanyia tathmini za uchafunzi wa mazingira wachimbaji wadogo kwa kuwa baadhi yao wamekuwa wakichangia uchafunzi wa mazingira nchini.
Jamal Baruti ambae ni Mratibu wa Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC, Kanda ya Ziwa, akiwasilisha mada juu ya tathmini ya athari za mazingira zitokanazo na shughuli za uchimbaji wa madini.

Amesema tathimini ya uchafuzi wa mazingira imekuwa ikifanyika kwa wachimbaji wakubwa wa madini kabla na baada ya uchimbaji lakini wachimbaji wadogo wamekuwa hawaguswi na tathmini hiyo kutokana na kutojumuishwa katika tathimini hiyo kwa mjibu wa sheria ya mazingira.
Mmoja wa washiriki akichangia mada
Mmoja wa washiriki akichangia mada

WAZIRI MKUU: SERIKALI ITATOA WARAKA JUU YA UKUSANYAJI MAPATO KUPITIA MAWAKALA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Halmashauri zitaelekezwa kwa waraka ni vyanzo vipi vitahitaji kutumia wawakala wa ukusanyaji mapato kwani siyo kila chanzo cha mapato ya Halmashauri kitakusanywa kwa ufanisi kwa kutumia au kwa kutotumia mawakala.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo mchana (Alhamisi, Juni 30, 2016) wakati akitoa hoja ya kuhitimisha mkutano wa tatu wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.

Amesema katika ukusanyaji wa mapato, baadhi ya vyanzo vitapaswa kukusanywa na Halmashauri zenyewe kwa kuzingatia miongozo iliyotolewa na Serikali. “Moja ya miongozo hiyo ni kwamba kuanzia sasa, iwe kwa kutumia mawakala au Halmashauri zenyewe ni lazima fedha zinazokusanywa ziwekwe kwenye akaunti ya Halmashauri na kutumia mifumo ya kielektroniki ili kupunguza au kumaliza kabisa masuala ya kutumia malipo kwa fedha taslimu (cash transactions),” alisema.

Amesema katika kutekeleza agizo hilo, Halmashauri itabidi zikubaliane na wakala ni kiasi gani cha asilimia ya makusanyo kitalipwa kwa wakala na malipo yafanyike baada ya kukusanya na kuingizwa kwenye akaunti ya Halmashauri.

Amesema Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa Sura ya 290, inazipa uwezo Mamlaka za Serikali za Serikali za Mitaa kutoza na kukusanya kodi, ushuru na ada mbalimbali kama vyanzo vya mapato vya Mamlaka za Serikali za Mitaa.

“Sheria hiyo pia inazipa mamlaka hizo kuteua mawakala wa kukusanya mapato hayo kwa niaba ya Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu. Lakini Serikali imebaini changamoto za kiufundi katika kufanya tathmini ya vyanzo vya mapato; ugumu katika kupata mawakala wenye weledi katika ukusanyaji mapato na kubuni vyanzo vipya vya mapato, na wakati mwingine watumishi wenyewe kujipa uwakala kinyume na taratibu zinazomzuia mtumishi kufanya biashara na taasisi yake,” alisema.

Amesema hatua ya Mamlaka za Serikali za Mitaa kutumia mawakala ni miongoni mwa mikakati ya kuboresha ukusanyaji mapato na pia kutoa muda mwingi zaidi kwa watumishi wa mamlaka hizo kushughulika na majukumu ya msingi ya Halmashauri na hasa utoaji wa huduma kwa wananchi na usimamizi wa miradi ya maendeleo.

“Pamoja na dhamira nzuri ya hatua hizo, tunayo mifano ya baadhi ya Halmashauri kama vile Nzega ambayo baadhi ya wahusika wameshinikiza wakitaka zabuni zote wapewe madiwani. Jambo hili halikubaliki na tena ni kinyume cha maadili ya utumishi,” alisisitiza.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameziagiza Halmashauri zote nchini kwamba kuanzia Julai Mosi, 2016 zihakikishe zinatumia mifumo ya kielektroniki katika kukusanya mapato, katika kulipa, kuweka na kutekeleza kikamilifu mikakati madhubuti ya kuboresha makusanyo iwe yanakusanywa na Halmashauri au na wakala.

Amesema Mamlaka za Serikali za Mitaa zina wajibu wa kutoa taarifa kwa wananchi kuhusu mapato na matumizi ya Serikali pamoja na michango ya wananchi licha ya kuwa uzoefu unaonesha kuwa mamlaka hizo zina tatizo la kukaa na fedha kwa muda mrefu kabla ya kuzielekeza kwenye matumizi yaliyokusudiwa.

“Kuchelewesha kutoa fedha zilizotengwa kwa shughuli zilizopangwa ni kuchelewesha kufikisha huduma muhimu kwa wananchi. Napenda kuhimiza uzingatiaji wa utaratibu wa kutoa taarifa kwa wananchi kuhusu mapato na matumizi ya fedha za Serikali katika ngazi zote ili kuongeza uwazi na uwajibikaji katika sekta ya umma,” aliongeza.

Mkutano huo wa tatu wa Bunge ulioanza Aprili 19, 2016 ulikuwa mahsusi kwa ajili ya kujadili na kupitisha bajeti ya kwanza ya Serikali ya Awamu ya Tano pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2016/2017. Bunge limeahirishwa hadi Septemba 6, mwaka huu litakapokutana tena mjini Dodoma.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
DODOMA.
ALHAMISI, JUNI 30, 2016
 
 
AFC FUELS EXPANSION AT NEW AGE WITH NEW INVESTMENT
                                                                               Andrew Alli, President and CEO of AFC

LAGOS, Nigeria, 30 June 2016 -/African Media Agency (AMA)/- Africa Finance Corporation ('AFC') is acting as lead arranger for an up to US$425 million senior mezzanine facility for New Age (African Global Energy) Limited ('New Age'), a privately held oil and gas exploration, development, and production company with assets primarily across Africa, to enable the company to further develop its existing assets and expand operations. AFC is investing US$75 million in the deal. 

AFC and the lender consortium are disbursing an initial US$350 million of the facility immediately, with an accordion feature to allow for an additional US$75 million of capital to follow. The investment will allow New Age to refinance an existing loan facility and develop projects in Nigeria, the Republic of Congo, and to expand operations in several other African countries. The lenders include amongst other EIG Global Energy Partners, and a Middle East based Sovereign Wealth Fund.

This loan will enable New Age to ramp up production in its high quality portfolio across the continent. New Age has made significant steps in achieving its growth objectives. As an example, New Age as the technical operator of the Aje field in OML 113 in Nigeria has attained first oil production targeting 11,000 barrels per day, making Lagos state officially an oil producing state. 


The Aje field is also targeted to be a significant gas supplier to Lagos power and industrial projects. In addition, New Age has achieved first production within the last two years at the Litchendjili and Nene marine fields in offshore Congo-Brazzaville.

Andrew Alli, President & CEO of AFC commenting on the announcement said:

"While the recent volatility in the oil industry has been challenging, AFC believes the current market provides opportunities for long-term investors across the value chain.

New Age has enjoyed considerable operational success in recent years across its Pan African portfolio and we would like to help them build on these foundations for the future. 


The company's well capitalised existing shareholder base, now complemented by a new financing from top tier financial institutions with a long history of investing in global oil and gas projects, is a testament to the confidence in the business model and provides comfort on New Age's ability to successfully execute future large scale capital projects. 

The lenders in the consortium are also working with New Age to further enhance the company's existing robust corporate governance.

AFC is pleased and excited to be able to help the company grow and thrive, especially in this difficult environment. The significance of this investment, is in the linkages between the company's gas production and the power sector in Nigeria in particular, and, the replicability for the development of an energy infrastructure network across continental Africa".

Distributed by African Media Agency (AMA) on behalf of Africa Finance Corporation (AFC).

Mombasa nanny caught breastfeeding employer’s baby









Breastfeeding-III  
By EVELYNE MUSAMBI

A police officer in Mombasa is the latest victim of house help drama after she caught the house help breastfeeding her four-month old baby.

Cost of living rises in June on higher food and fuel costs

The cost of living for the month of June rose for the first time since the beginning of the year.
  Traders at a food market. The rate of inflation stood at 5.27 per cent in April 2016. FILE
Traders at a food market. Official data shows that inflation increased to 5.80 per cent in June from 5.0 per cent a month earlier. PHOTO | FILE 
By NEVILLE OTUKI, notuki@ke.nationmedia.com
The cost of living for the month of June rose for the first time since the beginning of the year helped by rising prices of food, petroleum and house rent.

Wawekezaji wazawa wana haki kuwekeza kwenye gesi, mafuta

D1 
Afisa Habari, Mhandisi  Yisambi Shiwa (kushoto) na Mkaguzi wa Madini Mwandamizi Jeremiah Hango (kulia) kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini Nchini (TMAA), wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kuwahudumia wateja katika  Maonesho ya Kimataifa  ya Saba Saba (Dar es Salaam International  Trade  Fair)  yanayoendelea katika  Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
D2 
Afisa Habari, Mhandisi  Yisambi Shiwa (kulia) kutoka  Wakala wa Ukaguzi wa Madini Nchini (TMAA) akielezea madini ya dhahabu yanavyochenjuliwa kwa mteja aliyeshika sampuni ya madini hayo kwenye banda la TMAA katika maonesho hayo.
D3 
Mtaalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Phillip Mathayo  (kushoto) akielezea majukumu ya Wizara  kwa mteja aliyetembelea banda  hilo  katika Maonesho ya Kimataifa  ya Saba Saba (Dar es Salaam International  Trade  Fair)  yanayoendelea katika  Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
D5 
Mmoja wa wateja (kushoto) akitoa maoni yake kwenye banda la Shirika la Madini la  Taifa (STAMICO) kwenye Maonesho ya Kimataifa  ya Saba Saba (Dar es Salaam International  Trade  Fair)  yanayoendelea katika  Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Ulinzi vituo vya DART kuimarishwa

DARAJANI 
Benjamin Sawe Maelezo
—————————–
Baadhi ya abiria wanaotumia usafiri wa mabasi yaendayo kasi maarufu kama mwendo kasi wameilalamikia kampuni hiyo kwa kushindwa kudhibiti vitendo vya wizi vinavyoendelea katika baadhi ya vituo hivyo.
Bw. Juma Ally mkazi wa Kimara mwisho anasema vitendo hivyo hutokea nyakati za usiku kwa baadhi ya vijana kujifanya nao ni miongoni mwa watumiaji daraja hilo na kupelekea abiria kuibiwa vitu vyao ikiwa ni pamoja na kujeruhiwa.
Aliongezea kuwa walinzi wa kituo hicho wamekuwa wakifanya kazi ya kuwapanga abiria na kusahau majukumu yao ya kulinda usalama wa kituo hicho pamoja na mali zao.
“Tunashangaa hawa walinzi wanaolinda vituo hivi, abiria wamekuwa wakilalamika kila siku kuibiwa nyakati za usiku lakini tunaona abiria wakiendelea kuibiwa sijui wahusika wapo wapi?”Aliuliza Bw. Ally.
Nae Bi. Herrieth Shangaa aliongezea kuwa licha ya vitendo vya wizi vinavyoendelea katika vituo hivyo kuna baadhi ya vitendo vikiwemo vya kujisaidia katika madaraja hayo hivyo kupelekea uchafuzi wa mazingira
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi msimamizi wa vituo hivyo ambae hakutaja kutajwa jina lake amesema kuna baadhi ya vituo ni vikubwa na wanawalinzi wachache hivyo wamejipanga kuongeza ulinzi ikiwa ni pamoja na kufunga mfumo wa kidigitali wa kudhibiti wahalifu
Mradi wa mabasi yaendayo haraka ulioanza rasmi terehe 10, mei, 2016 umeonesha ni jinsi gani kero ya foleni itakavyopungua kwa kuwa mabasi hayo yanatumia njia yake ambayo ni miundombinu  iliyojengwa kwa  gharama kubwa  sana.

siku ya mwisho wa zoezi la kuhakiki silaha

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
TZ 
TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI
Ndugu zangu waandishi wa habari,
Leo tarehe 30.6.2016 ndiyo tarehe na siku ya mwisho wa zoezi la kuhakiki silaha. Kwa mujibu wa takwimu za silaha tulizonazo inaonyesha kwamba wapo baadhi ya wamiliki wa silaha ambao hawajatekeleza agizo la kuhakiki silaha wanazozimiliki.
Kufutia hali hiyo, natoa angalizo kwa wale wote ambao hawajahikiki silaha zao kwamba muda wowote kuanzia sasa tutaanza operesheni maalum ya kutafuta silaha ambazo hazijahikikiwa.  Ifahamike kwamba yeyote atakaye kutwa na silaha ambayo haijahakikiwa atachuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo  kupoteza sifa ya kuwa mmiliki halali wa silaha hiyo.
Tunatoa agizo kwa wamiliki binafsi wa maghala ya silaha waziwasilishe silaha hizo pamoja na nyaraka zake katika vituo vya karibu vya Polisi kwa ajili ya uhakiki.
Imetolewa:-
Nsato M. Mssanzya – CP
Kamishina wa Polisi Operesheni na Mafunzo
Makao Makuu ya Polisi

BARAZA LA WAFANYAKAZI MUHIMBILI LAFANYA KIKAO CHAKE CHA 16, WAJUMBE WATAKIWA KUWA MFANO KWA WATUMISHI WENGINE.

M1 
Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la Hospitali ya Taifa Muhimbili   Profesa Lawrence Museru  akifungua kikao cha 16 cha Baraza hilo kilichofanyika  leo Juni 30, 2016  katika ukumbi wa NACTE Mikocheni jijini Dar es salaam. Kulia ni Katibu wa Baraza hilo Dk. Kisah Mwambene na kushoto ni Katibu Msaidizi Enezer Msuya.
M2 
Katibu wa TUGHE mkoa Bwana.  Gaudence  Kadyango   akiwasilisha mada kuhusu umuhimu wa mikataba ya hali bora za kazi na faida zake.
M3 
Bwana.  Andrew Mwalwisi  kutoka Tume ya Usuluhishi  -CMA-   akiwasilisha mada  katika kikao cha Baraza la wafanyakazi  wa MNH .
M4Mwenyekiti wa TUGHE  Tawi la Muhimbili Mziwanda Salum Chimwege akiuza swali   kwa viongozi wa Baraza  la MNH  katika kikao hicho  .
M5Mjumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa- MNH -Alex   Samweli  akitoa hoja katika kikao hicho  kilichofayika leo.

SABMiller kuendelea kufanya biashara zenye kuleta manufaa kwa jamii

indexMkurugenzi wa Mazingira wa SABMiller Africa,Muzi Chonko katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
———————————————————–
Na Mwandishi wetu
Kampuni ya kimataifa ya SABMiller inayomiliki viwanda vya kutengeneza vinywaji sehemu mbalimbali duniani itaendelea kufanya biashara zenye mwelekeo wa kubadilisha maisha ya jamii mbalimbali kuwa bora bila kusahau kuzingatia utunzaji wa mazingira.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Mazingira wa kampuni hiyo kanda ya Afrika Bw.Muzi Chonco,alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ambapo alipata wasaa wa kuelezea kanuni zinazoongoza utendaji wa kazi wa kampuni kwa ajili ya kuleta mabadiliko endelevu sehemu zote ilikowekeza duniani.
Chonco alisema kuwa tangu kampuni ianze kutumia kanuni hizo ambazo zinashahabiana na malengo ya umoja wa mataifa tayari mafanikio mbalimbali yameanza kupatikana na yapo matumaini ya kufikia mafanikio makubwa katika siku za usoni.
“Tunapoongelea biashara  endelevu tunamaanisha kuwawezesha wanachi kiuchumi kama ambavyo tumekuwa tukifanya kazi na wakulima kupitia mpango wetu wa Go Farming,kuwakwamua wanawake kiuchumi,kuendeleza wajasiriamali,kutunza vyanzo va maji na kuwekeza katika miradi ya maji bila kusahau utunzaji wa mazingira”.Alisema Chonco.
Alitoa mfano wa kampuni  ya TBL Group ambayo iko chini ya kampuni hiyo kwa jinsi ilivyoweza kufanya uwekezaji ambao umeleta mabadiliko nchini ambapo serikali na taaasisi mbalimbali zinatambua mchango wake kwa kuitunukia tuzo mbalimbali ambazo imekuwa ikishinda mwaka hadi mwaka.
Chonco alizichambua kanuni zinazoongoza kampuni na kuleta mabadiliko kwenye jamii kuwa ni dunia yenye nuru njema,dunia changamfu,dunia imara,dunia iliyo  safi na dunia yenye nguvu kazi.
Alisema wakati umefika kwa wawekezaji mbalimbali kufanya uwekezaji wenye kuleta mabadiliko kwenye jamii badala ya kunufaisha upande mmoja  “uwekezaji unaoleta ajira za kila aina kwa wananchi,unaowawezesha kujipatia mapato kwa kuuza bidhaa kwa kampuni iliyowekeza,kutunza mazingira na kuwapatia wananchi elimu ya utunzaji wa mazingira na vyanzo vva maji,kusaidia makundi mbalimbali kwenye jamii yaliyoachwa nyuma ukizingatiwa kwa vyovyote utaleta mabadiliko”.Alisisitiza.
Alitoa mfano kuwa ukimwezesha mkulima ataweza kupata kipato na kujenga nyumba nzuri ya kuishi,watoto wake kusoma vizuri,familia yake kupata lishe bora na kuongeza pato la familia kwa ujumla na maisha kubadilika kutoka hali duni kuwa bora kama ambavyo imetokea kwa wakulima na makundi mengine yanayoshirikiana na kampuni hiyo sehemu mbalimbali duniani.

Bodaboda waiomba serikali kuwachukulia hatua kali abiria wanaokataa kuvaa helmeti

bodaBoda 
Jonas Kamaleki, Maelezo
——————————
WAAENDESHA pikipiki maarufu kama bodaboda wameiomba serikali kuwachukulia hatua kali abiria wanaokataa kuvaa kofia ngumu (Helmet) ili kutoa fundisho kwa watu wengine wasihatarishe maisha yao.
Akiongea katika mahojiano maalum, mwendesha pikipiki, Nathanael Kiula wa Dar es Salaam amesema kuwa abiria wanaokataa kuvaa helmeti wachukuliwe hatua kali ikiwepo kutozwa faini isiopungua Tsh. 30,000/=  ili liwe fundisho kwa wengine.
“Mimi nina helmeti mbili ya kwangu na abiria lakini abiria wengi hawataki kuvaa helmeti hasa akina mama kwa madai kuwa nywele zao zinaharibika pia wanadai kuwa zina uchafu.”alisema Kiula.
Kiula alisema kuwa elimu itolewe kwa abiria na waendesha pikipiki juu ya umuhimu wa kuvaa helmeti kwani ni kwa manufaa yao wanapopata ajali wasiumie sana au kupoteza maisha na si kwa ajili ya kuwakwepa matrafiki.
Mwendesha pikipiki aliyejitambulisha kwa jina la Isaac William alisema abiria wanaokataa kuvaa helmeti waadhibiwe vikali ili kukomesha tabia hii isiokubalika katika suala zima la usafirishaji.
“Abiria wangu baadhi wanakubali kuvaa helmeti lakini walio wengi hukataa kuzivaa kwa madai kuwa wanaogopa magonjwa ya kuambukizwa kupitia vifaa hivyo,”alisema William.
Naye abiria wa bodaboda ambaye ni mkazi wa Dar es Salaam, Bi Fatuma Abdallah amesema yeye hawezi kuvaa helmeti kwani zinatumiwa na watu wengi hivyo anaogopa kupatwa na magonjwa.
“Siwezi kuvaa mikofia yao kwani inatumiwa na watu wengi huwezijua wana magonjwa ya ngozi kiasi gani, kamwe sintoyavaa ng’o,”alisema Fatuma.
Kwa upande wake Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchi, Mohamed Mpinga alisema kuwa uvaaji wa kofia ngumu kwa waendesha pikipiki ni lazima. Anayekaidi amri hiyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Helmet Vaccine Initiative Tanzania Foundation, Bw. Alpherio  Nchimbi alisema matumizi ya Helmeti hayaepukiki kwa usalama wa mwendesha pikipiki na abiria.
“Kwa umuhimu huo, Taasisi yetu inatoa msaada wa kiufundi kwa Jeshi la Magereza nchini kwa ajili ya uanzishwaji wa kiwanda cha kutengeneza kofia ngumu kwa kufuata viwango vya Shirika la Viwango nchini (TBS) na pia tunatoa elimu kwa bodaboda kuhusu matumizi ya kofia ngumu na madhara yatokanayo na kutovaa kofia hizo kuanzia ngazi ya familia hadi Taifa kwa ujumla,” alisema Nchimbi.
Kuhusu suala la kuvaa helmeti, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alisema kuwa mwendesha pikipiki na abiria ni lazima wavae helmeti na ifikapo Julai 1, 2016 hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya abiria au mwendesha pikipiki atakayekaidi amri hiyo.
“Nawaambia, hatutamvumilia mtu yeyote, mwendesha pikipiki na abiria asiyevaa helmeti tunawahesabu kuwa wana mpango wa kujiua,”alisema Makonda wakati wa Uzinduzi wa Mpango wa Taifa wa Usalama wa raia wa Jeshi la Polisi.
Suala la kuvaa kofia ngumu au helmeti kwa waendesha pikipiki na biria wao limekuwa likipuuzwa kwa muda mrefu ndio maana serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam kwa kushirikiana na Jeshi la polisi wameandaa utaratibu wa kuwafuatilia na kuwachukulia hatua za kisheria kwa ajili ya kunusuru maisha yao. Mpango huu unaanza rasmi tarehe 1, 2016.

SERIKALI YATANGAZA KIAMA CHA WAUZA DAWA NA VIPODOZI HATARI MITANDAONI

TZ 
Na Fatma Salum (MAELEZO)
——————————
Serikali kupitia Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imesema hivi karibuni itaanza msako mkali wa kuwatafuta na kuwakamata wauzaji wa dawa zinazokatazwa pamoja na vipodozi vikali ambao wanajitangaza kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii.
Hayo yamesemwa na Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Umma kutoka TFDA Bi. Gaudensia Simwanza wakati wa mahojiano na mwandishi wa habari hii kuhusu kuibuka kwa watu wanaotangaza  biashara ya dawa na vipodozi ambavyo Serikali imevipiga marufuku.
Akitaja bidhaa hizo Bi. Simwanza alisema ni pamoja na dawa za kuongeza ukubwa wa viungo vya mwili, kupunguza uzito wa mwili na vipodozi vyenye kemikali za kuchubua ngozi bidhaa ambazo zinasababisha madhara makubwa kwa binadamu ikiwemo ugonjwa wa Saratani.
“Kumezuka wafanyabiashara holela wanaotumia mitandao ya kijamii kama vile Instagram, Facebook, Whatsup Groups na kwengineko  kutangaza biashara ya dawa na vipodozi vyenye kemikali hatari ambavyo vimepigwa marufuku na TFDA hivyo wanaohusika wajiandae, hivi karibuni tutaanza kuwashughulikia.” Alisema Simwanza.
Alibainisha kuwa bidhaa hizo nyingi hazijathibitishwa na kupewa kibali na TFDA hivyo wauzaji wanakiuka Sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi Sura ya 219 inayowataka wafanyabiashara wote wa bidhaa hizo kuzisajili kabla hazijaenda kwa  mtumiaji na kutofanya hivyo ni kwenda kinyume na Sheria.
Alieleza kuwa TFDA kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi wameandaa mkakati madhubuti wa kuhakikisha wanawabaini na kuwakamata wafanyabiashara wote wanaouza dawa na vipodozi hivyo kupitia mitandao na kuwachukulia hatua ikiwemo kuwafikisha mahakamani au kuwatoza faini.
“Wengi wa wafanyabiashara hao hawaweki anuani za maeneo wanayopatikana na hawana maduka rasmi bali huweka namba za simu za mkononi lakini kwa kutumia vyombo vya dola tutawabaini tu na kuwatia mbaroni.” Alisisitiza Simwanza.
Kwa upande wake Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Innocent Mungy amewatahadharisha watumiaji wa huduma za mawasiliano hasa matangazo ya biashara kuwa makini na matangazo hayo kwani baadhi ya wafanyabiashara hizo wanaweza kuwa ni watu wenye nia mbaya.
Hivi karibuni kumeibuka wimbi la wafanyabiashara wa dawa mbalimbali pamoja na vipodozi ambao wanajitangaza kupitia mitandao ya kijamii na kuna baadhi ya watu wananunua bidhaa hizo bila ya kuhakikisha usalama wake jambo ambalo ni hatari kwa afya zao.

MAKAMU WA RAIS AFUTURU NA WATOTO YATIMA


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa Nasaha maalum mara baada ya kumaliza kufuturu na watoto Yatima
kwenye viwanja vya Karimjee iliyoandaliwa na kampuni ya Chocolate Princess inayoandaa kipindi television cha Mboni Show.
Mkuu wa Wilaya ya kinondoni Mhe. Ally Hapi (kushoto) akiwa kwenye dua pamoja na wageni waalikwa wengine.
Watoto Yatima wakiswali wakati wa tafrija ya kufuturisha watoto Yatima iliyoandaliwa na kampuni ya Chocolate Princess inayoandaa kipindi cha televisheni cha Mboni Show ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na kufanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Samia Suluhu Hassan (kushoto) akisalimiana na Mkuu mpya wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema (kulia)
mwingine pichani ni Mkurugenzi wa kampuni ya Chocolate Princess inayotengeneza kipindi cha television cha Mboni Show Bi. Mboni Masimba  wakati wa tafrija
ya kufuturisha watoto yatima iliyofanyika kwenye viwanja vya Karimjee.
Mkurugenzi wa kampuni ya Chocolate Princess kinachoandaa kipindi cha The Mboni Show akizungumza wakati wa kufuturisha watoto yatima .
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda akizungumza kwenye tafrija ya kufuturisha Watoto Yatima  iliyoandaliwa na kampuni ya Chocolate Princess inayoandaa na kipindi cha television Mboni Show ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan .(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Watoto wakipewa juisi wakati wa Tafrij ya Futari.
Naibu Mufti Mkuu Sheikh Hamid Jongo akizungumza kwenye tafrija hiyo.

GAZET LA MTANZANIA LA ZINDUA MWEONEKA MPYA “MTANZANIA LIMEBORESHWA

004
005 
Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari (2006)Ltd, Absalom Kibanda, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusu uzinduzi wa mwonekano mpya wa Gazeti la Mtanzania lenye kauli mbiu ya “Mtanzania Limeboreshwa”.Kulia ni Mhariri Mtendaji wa  Mtanzania, Dennis Msacky na Meneja Masoko wa kampuni hiyo.
???????????????????????????????????? 
Mhariri wa Gazeti la Mtanzania, Dennis Msacky.akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana. kuhusu uzinduzi wa mwonekano mpya wa Gazeti la Mtanzania lenye kauli mbiu ya “Mtanzania Limeboreshwa”Katikati ni Mhariri Mtendaji Kampuni ya New Habari(2006)Ltd, Absalom Kibanda na Meneja Masoko wa Kampuni hiyo, Michael Bugidira.
Picha na Mpiga Picha Wetu

WAFANYAKAZI WA ABANA WAANDAMANA KUDAI MIL 400 WANAZODAI

ma1Wafanyakazi wa kiwanda cha kuchapisha vitabu cha ABANA Printers ltd,kilichopo kata ya Mapinga wilayani Bagamoyo mkoani Pwani,wakiandamana kudai mishahara na mafao yao wanayodai kwa kipindi cha miaka miwili na nusu ambayo yamefikia mil 400 .
(Picha na Mwamvua Mwinyi) 
———————————————————–
Na Mwamvua Mwinyi,Bagamoyo
WAFANYAKAZI wa kiwanda cha uchapishaji vitabu(ABANA Printers Ltd) kilichopo kata ya Mapinga wilayani Bagamoyo mkoani Pwani ,wanadai fedha za mishahara na mafao yao kiasi cha sh.mil.400 tangu mwaka 2014 bila mafanikio.
Aidha wafanyakazi hao waiomba serikali ya awamu ya tano kuingilia kati tatizo hilo kwani wameshapigania haki zao kupitia mahakamani ,wizara,idara na vyama vinavyojishughulisha kutetea haki za wafanyakazi lakini hakuna msaada walioupata.
Wameeleza kuwa hadi sasa wanaishi katika maisha magumu  huku wengine wakiwa wamefukuzwa kwenye nyumba walizopanga  na wenzao watatu wamefariki kutokana na ugonjwa wa moyo.
Hayo yamejiri jana baada ya wafanyakazi hao kuchukua hatua ya kufanya maandamano nje ya kiwanda hicho na kisha kumfikishia kilio chao mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi (CCM)Bagamoyo,alhaj Abdul Sharif ili aweze kuwasaidia kulipwa haki zao.
Mwenyekiti wa tawi la chama cha wafanyakazi tawi la ABANA printers Wilbard Ikigo ,alidai kuwa mmiliki wa kampuni hiyo anajigamba kwa kusema serikali ipo mkononi mwake hivyo hawezi kuchukuliwa hatua yoyote.
Alisema ni miaka miwili na nusu sasa tangu watelekezwe na mwajiri wao hali iliyosababisha kuingia katika mgogoro na mmiliki huyo.