Afisa
Habari, Mhandisi Yisambi Shiwa (kushoto) na Mkaguzi wa Madini
Mwandamizi Jeremiah Hango (kulia) kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini
Nchini (TMAA), wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kuwahudumia
wateja katika Maonesho ya Kimataifa ya Saba Saba (Dar es Salaam
International Trade Fair) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu
Nyerere jijini Dar es Salaam.
Afisa
Habari, Mhandisi Yisambi Shiwa (kulia) kutoka Wakala wa Ukaguzi wa
Madini Nchini (TMAA) akielezea madini ya dhahabu yanavyochenjuliwa kwa
mteja aliyeshika sampuni ya madini hayo kwenye banda la TMAA katika
maonesho hayo.
Mtaalam
kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Phillip Mathayo (kushoto)
akielezea majukumu ya Wizara kwa mteja aliyetembelea banda hilo
katika Maonesho ya Kimataifa ya Saba Saba (Dar es Salaam International
Trade Fair) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini
Dar es Salaam.
Mmoja wa wateja (kushoto) akitoa maoni yake kwenye banda la Shirika la
Madini la Taifa (STAMICO) kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Saba Saba
(Dar es Salaam International Trade Fair) yanayoendelea katika
Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Ulinzi vituo vya DART kuimarishwa
Benjamin Sawe Maelezo
—————————–
Baadhi ya abiria wanaotumia
usafiri wa mabasi yaendayo kasi maarufu kama mwendo kasi wameilalamikia
kampuni hiyo kwa kushindwa kudhibiti vitendo vya wizi vinavyoendelea
katika baadhi ya vituo hivyo.
Bw. Juma Ally mkazi wa Kimara
mwisho anasema vitendo hivyo hutokea nyakati za usiku kwa baadhi ya
vijana kujifanya nao ni miongoni mwa watumiaji daraja hilo na kupelekea
abiria kuibiwa vitu vyao ikiwa ni pamoja na kujeruhiwa.
Aliongezea kuwa walinzi wa kituo
hicho wamekuwa wakifanya kazi ya kuwapanga abiria na kusahau majukumu
yao ya kulinda usalama wa kituo hicho pamoja na mali zao.
“Tunashangaa hawa walinzi
wanaolinda vituo hivi, abiria wamekuwa wakilalamika kila siku kuibiwa
nyakati za usiku lakini tunaona abiria wakiendelea kuibiwa sijui
wahusika wapo wapi?”Aliuliza Bw. Ally.
Nae Bi. Herrieth Shangaa
aliongezea kuwa licha ya vitendo vya wizi vinavyoendelea katika vituo
hivyo kuna baadhi ya vitendo vikiwemo vya kujisaidia katika madaraja
hayo hivyo kupelekea uchafuzi wa mazingira
Akizungumza na mwandishi wa habari
hizi msimamizi wa vituo hivyo ambae hakutaja kutajwa jina lake amesema
kuna baadhi ya vituo ni vikubwa na wanawalinzi wachache hivyo
wamejipanga kuongeza ulinzi ikiwa ni pamoja na kufunga mfumo wa
kidigitali wa kudhibiti wahalifu
Mradi wa mabasi yaendayo haraka
ulioanza rasmi terehe 10, mei, 2016 umeonesha ni jinsi gani kero ya
foleni itakavyopungua kwa kuwa mabasi hayo yanatumia njia yake ambayo ni
miundombinu iliyojengwa kwa gharama kubwa sana.
siku ya mwisho wa zoezi la kuhakiki silaha
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI
Ndugu zangu waandishi wa habari,
Leo tarehe 30.6.2016 ndiyo tarehe
na siku ya mwisho wa zoezi la kuhakiki silaha. Kwa mujibu wa takwimu za
silaha tulizonazo inaonyesha kwamba wapo baadhi ya wamiliki wa silaha
ambao hawajatekeleza agizo la kuhakiki silaha wanazozimiliki.
Kufutia hali hiyo, natoa angalizo
kwa wale wote ambao hawajahikiki silaha zao kwamba muda wowote kuanzia
sasa tutaanza operesheni maalum ya kutafuta silaha ambazo
hazijahikikiwa. Ifahamike kwamba yeyote atakaye kutwa na silaha ambayo
haijahakikiwa atachuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kupoteza sifa
ya kuwa mmiliki halali wa silaha hiyo.
Tunatoa agizo kwa wamiliki binafsi
wa maghala ya silaha waziwasilishe silaha hizo pamoja na nyaraka zake
katika vituo vya karibu vya Polisi kwa ajili ya uhakiki.
Imetolewa:-
Nsato M. Mssanzya – CP
Kamishina wa Polisi Operesheni na Mafunzo
Makao Makuu ya Polisi
BARAZA LA WAFANYAKAZI MUHIMBILI LAFANYA KIKAO CHAKE CHA 16, WAJUMBE WATAKIWA KUWA MFANO KWA WATUMISHI WENGINE.
Mwenyekiti
wa Baraza la Wafanyakazi la Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa
Lawrence Museru akifungua kikao cha 16 cha Baraza hilo kilichofanyika
leo Juni 30, 2016 katika ukumbi wa NACTE Mikocheni jijini Dar es
salaam. Kulia ni Katibu wa Baraza hilo Dk. Kisah Mwambene na kushoto ni
Katibu Msaidizi Enezer Msuya.
Katibu
wa TUGHE mkoa Bwana. Gaudence Kadyango akiwasilisha mada kuhusu
umuhimu wa mikataba ya hali bora za kazi na faida zake.
Bwana. Andrew Mwalwisi kutoka Tume ya Usuluhishi -CMA- akiwasilisha mada katika kikao cha Baraza la wafanyakazi wa MNH .
SABMiller kuendelea kufanya biashara zenye kuleta manufaa kwa jamii
Mkurugenzi wa Mazingira wa SABMiller Africa,Muzi Chonko katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
———————————————————–
Na Mwandishi wetu
Kampuni ya kimataifa ya SABMiller
inayomiliki viwanda vya kutengeneza vinywaji sehemu mbalimbali duniani
itaendelea kufanya biashara zenye mwelekeo wa kubadilisha maisha ya
jamii mbalimbali kuwa bora bila kusahau kuzingatia utunzaji wa
mazingira.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi
wa Mazingira wa kampuni hiyo kanda ya Afrika Bw.Muzi
Chonco,alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ambapo
alipata wasaa wa kuelezea kanuni zinazoongoza utendaji wa kazi wa
kampuni kwa ajili ya kuleta mabadiliko endelevu sehemu zote ilikowekeza
duniani.
Chonco alisema kuwa tangu kampuni
ianze kutumia kanuni hizo ambazo zinashahabiana na malengo ya umoja wa
mataifa tayari mafanikio mbalimbali yameanza kupatikana na yapo
matumaini ya kufikia mafanikio makubwa katika siku za usoni.
“Tunapoongelea biashara endelevu
tunamaanisha kuwawezesha wanachi kiuchumi kama ambavyo tumekuwa
tukifanya kazi na wakulima kupitia mpango wetu wa Go Farming,kuwakwamua
wanawake kiuchumi,kuendeleza wajasiriamali,kutunza vyanzo va maji na
kuwekeza katika miradi ya maji bila kusahau utunzaji wa
mazingira”.Alisema Chonco.
Alitoa mfano wa kampuni ya TBL
Group ambayo iko chini ya kampuni hiyo kwa jinsi ilivyoweza kufanya
uwekezaji ambao umeleta mabadiliko nchini ambapo serikali na taaasisi
mbalimbali zinatambua mchango wake kwa kuitunukia tuzo mbalimbali ambazo
imekuwa ikishinda mwaka hadi mwaka.
Chonco alizichambua kanuni
zinazoongoza kampuni na kuleta mabadiliko kwenye jamii kuwa ni dunia
yenye nuru njema,dunia changamfu,dunia imara,dunia iliyo safi na dunia
yenye nguvu kazi.
Alisema wakati umefika kwa
wawekezaji mbalimbali kufanya uwekezaji wenye kuleta mabadiliko kwenye
jamii badala ya kunufaisha upande mmoja “uwekezaji unaoleta ajira za
kila aina kwa wananchi,unaowawezesha kujipatia mapato kwa kuuza bidhaa
kwa kampuni iliyowekeza,kutunza mazingira na kuwapatia wananchi elimu ya
utunzaji wa mazingira na vyanzo vva maji,kusaidia makundi mbalimbali
kwenye jamii yaliyoachwa nyuma ukizingatiwa kwa vyovyote utaleta
mabadiliko”.Alisisitiza.
Alitoa mfano kuwa ukimwezesha
mkulima ataweza kupata kipato na kujenga nyumba nzuri ya kuishi,watoto
wake kusoma vizuri,familia yake kupata lishe bora na kuongeza pato la
familia kwa ujumla na maisha kubadilika kutoka hali duni kuwa bora kama
ambavyo imetokea kwa wakulima na makundi mengine yanayoshirikiana na
kampuni hiyo sehemu mbalimbali duniani.
Bodaboda waiomba serikali kuwachukulia hatua kali abiria wanaokataa kuvaa helmeti
Jonas Kamaleki, Maelezo
——————————
WAAENDESHA pikipiki maarufu kama
bodaboda wameiomba serikali kuwachukulia hatua kali abiria wanaokataa
kuvaa kofia ngumu (Helmet) ili kutoa fundisho kwa watu wengine
wasihatarishe maisha yao.
Akiongea katika mahojiano maalum,
mwendesha pikipiki, Nathanael Kiula wa Dar es Salaam amesema kuwa abiria
wanaokataa kuvaa helmeti wachukuliwe hatua kali ikiwepo kutozwa faini
isiopungua Tsh. 30,000/= ili liwe fundisho kwa wengine.
“Mimi nina helmeti mbili ya kwangu
na abiria lakini abiria wengi hawataki kuvaa helmeti hasa akina mama
kwa madai kuwa nywele zao zinaharibika pia wanadai kuwa zina
uchafu.”alisema Kiula.
Kiula alisema kuwa elimu itolewe
kwa abiria na waendesha pikipiki juu ya umuhimu wa kuvaa helmeti kwani
ni kwa manufaa yao wanapopata ajali wasiumie sana au kupoteza maisha na
si kwa ajili ya kuwakwepa matrafiki.
Mwendesha pikipiki
aliyejitambulisha kwa jina la Isaac William alisema abiria wanaokataa
kuvaa helmeti waadhibiwe vikali ili kukomesha tabia hii isiokubalika
katika suala zima la usafirishaji.
“Abiria wangu baadhi wanakubali
kuvaa helmeti lakini walio wengi hukataa kuzivaa kwa madai kuwa
wanaogopa magonjwa ya kuambukizwa kupitia vifaa hivyo,”alisema William.
Naye abiria wa bodaboda ambaye ni
mkazi wa Dar es Salaam, Bi Fatuma Abdallah amesema yeye hawezi kuvaa
helmeti kwani zinatumiwa na watu wengi hivyo anaogopa kupatwa na
magonjwa.
“Siwezi kuvaa mikofia yao kwani
inatumiwa na watu wengi huwezijua wana magonjwa ya ngozi kiasi gani,
kamwe sintoyavaa ng’o,”alisema Fatuma.
Kwa upande wake Kamanda Mkuu wa
Kikosi cha Usalama Barabarani nchi, Mohamed Mpinga alisema kuwa uvaaji
wa kofia ngumu kwa waendesha pikipiki ni lazima. Anayekaidi amri hiyo
hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Kwa upande wake, Afisa Mtendaji
Mkuu wa Taasisi ya Helmet Vaccine Initiative Tanzania Foundation, Bw.
Alpherio Nchimbi alisema matumizi ya Helmeti hayaepukiki kwa usalama wa
mwendesha pikipiki na abiria.
“Kwa umuhimu huo, Taasisi yetu
inatoa msaada wa kiufundi kwa Jeshi la Magereza nchini kwa ajili ya
uanzishwaji wa kiwanda cha kutengeneza kofia ngumu kwa kufuata viwango
vya Shirika la Viwango nchini (TBS) na pia tunatoa elimu kwa bodaboda
kuhusu matumizi ya kofia ngumu na madhara yatokanayo na kutovaa kofia
hizo kuanzia ngazi ya familia hadi Taifa kwa ujumla,” alisema Nchimbi.
Kuhusu suala la kuvaa helmeti,
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alisema kuwa mwendesha
pikipiki na abiria ni lazima wavae helmeti na ifikapo Julai 1, 2016
hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya abiria au mwendesha pikipiki
atakayekaidi amri hiyo.
“Nawaambia, hatutamvumilia mtu
yeyote, mwendesha pikipiki na abiria asiyevaa helmeti tunawahesabu kuwa
wana mpango wa kujiua,”alisema Makonda wakati wa Uzinduzi wa Mpango wa
Taifa wa Usalama wa raia wa Jeshi la Polisi.
Suala la kuvaa kofia ngumu au
helmeti kwa waendesha pikipiki na biria wao limekuwa likipuuzwa kwa muda
mrefu ndio maana serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam kwa kushirikiana na
Jeshi la polisi wameandaa utaratibu wa kuwafuatilia na kuwachukulia
hatua za kisheria kwa ajili ya kunusuru maisha yao. Mpango huu unaanza
rasmi tarehe 1, 2016.
SERIKALI YATANGAZA KIAMA CHA WAUZA DAWA NA VIPODOZI HATARI MITANDAONI
Na Fatma Salum (MAELEZO)
——————————
Serikali kupitia Mamlaka ya
Chakula na Dawa (TFDA) imesema hivi karibuni itaanza msako mkali wa
kuwatafuta na kuwakamata wauzaji wa dawa zinazokatazwa pamoja na
vipodozi vikali ambao wanajitangaza kupitia mitandao mbalimbali ya
kijamii.
Hayo yamesemwa na Meneja
Mawasiliano na Uhusiano wa Umma kutoka TFDA Bi. Gaudensia Simwanza
wakati wa mahojiano na mwandishi wa habari hii kuhusu kuibuka kwa watu
wanaotangaza biashara ya dawa na vipodozi ambavyo Serikali imevipiga
marufuku.
Akitaja bidhaa hizo Bi. Simwanza
alisema ni pamoja na dawa za kuongeza ukubwa wa viungo vya mwili,
kupunguza uzito wa mwili na vipodozi vyenye kemikali za kuchubua ngozi
bidhaa ambazo zinasababisha madhara makubwa kwa binadamu ikiwemo ugonjwa
wa Saratani.
“Kumezuka wafanyabiashara holela
wanaotumia mitandao ya kijamii kama vile Instagram, Facebook, Whatsup
Groups na kwengineko kutangaza biashara ya dawa na vipodozi vyenye
kemikali hatari ambavyo vimepigwa marufuku na TFDA hivyo wanaohusika
wajiandae, hivi karibuni tutaanza kuwashughulikia.” Alisema Simwanza.
Alibainisha kuwa bidhaa hizo
nyingi hazijathibitishwa na kupewa kibali na TFDA hivyo wauzaji
wanakiuka Sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi Sura ya 219 inayowataka
wafanyabiashara wote wa bidhaa hizo kuzisajili kabla hazijaenda kwa
mtumiaji na kutofanya hivyo ni kwenda kinyume na Sheria.
Alieleza kuwa TFDA kwa
kushirikiana na Jeshi la Polisi wameandaa mkakati madhubuti wa
kuhakikisha wanawabaini na kuwakamata wafanyabiashara wote wanaouza dawa
na vipodozi hivyo kupitia mitandao na kuwachukulia hatua ikiwemo
kuwafikisha mahakamani au kuwatoza faini.
“Wengi wa wafanyabiashara hao
hawaweki anuani za maeneo wanayopatikana na hawana maduka rasmi bali
huweka namba za simu za mkononi lakini kwa kutumia vyombo vya dola
tutawabaini tu na kuwatia mbaroni.” Alisisitiza Simwanza.
Kwa upande wake Meneja Mawasiliano
wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Innocent Mungy
amewatahadharisha watumiaji wa huduma za mawasiliano hasa matangazo ya
biashara kuwa makini na matangazo hayo kwani baadhi ya wafanyabiashara
hizo wanaweza kuwa ni watu wenye nia mbaya.
Hivi karibuni kumeibuka wimbi la
wafanyabiashara wa dawa mbalimbali pamoja na vipodozi ambao
wanajitangaza kupitia mitandao ya kijamii na kuna baadhi ya watu
wananunua bidhaa hizo bila ya kuhakikisha usalama wake jambo ambalo ni
hatari kwa afya zao.
MAKAMU WA RAIS AFUTURU NA WATOTO YATIMA
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akitoa Nasaha maalum mara baada ya kumaliza kufuturu na watoto Yatima
kwenye viwanja vya Karimjee iliyoandaliwa na kampuni ya Chocolate Princess inayoandaa kipindi television cha Mboni Show.
kwenye viwanja vya Karimjee iliyoandaliwa na kampuni ya Chocolate Princess inayoandaa kipindi television cha Mboni Show.
Mkuu wa Wilaya ya kinondoni Mhe. Ally Hapi (kushoto) akiwa kwenye dua pamoja na wageni waalikwa wengine.
Watoto
Yatima wakiswali wakati wa tafrija ya kufuturisha watoto Yatima
iliyoandaliwa na kampuni ya Chocolate Princess inayoandaa kipindi cha
televisheni cha Mboni Show ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na kufanyika
kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kushoto) akisalimiana na Mkuu mpya wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema (kulia)
mwingine pichani ni Mkurugenzi wa kampuni ya Chocolate Princess inayotengeneza kipindi cha television cha Mboni Show Bi. Mboni Masimba wakati wa tafrija
ya kufuturisha watoto yatima iliyofanyika kwenye viwanja vya Karimjee.
Mkurugenzi
wa kampuni ya Chocolate Princess kinachoandaa kipindi cha The Mboni
Show akizungumza wakati wa kufuturisha watoto yatima .
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda akizungumza kwenye tafrija
ya kufuturisha Watoto Yatima iliyoandaliwa na kampuni ya Chocolate
Princess inayoandaa na kipindi cha television Mboni Show ambapo mgeni
rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan .(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan .(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Watoto wakipewa juisi wakati wa Tafrij ya Futari.
Naibu Mufti Mkuu Sheikh Hamid Jongo akizungumza kwenye tafrija hiyo.
GAZET LA MTANZANIA LA ZINDUA MWEONEKA MPYA “MTANZANIA LIMEBORESHWA
Mhariri
Mtendaji wa Kampuni ya New Habari (2006)Ltd, Absalom Kibanda,
akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusu uzinduzi wa
mwonekano mpya wa Gazeti la Mtanzania lenye kauli mbiu ya “Mtanzania
Limeboreshwa”.Kulia ni Mhariri Mtendaji wa Mtanzania, Dennis Msacky na
Meneja Masoko wa kampuni hiyo.
Mhariri
wa Gazeti la Mtanzania, Dennis Msacky.akizungumza na waandishi wa
habari Dar es Salaam jana. kuhusu uzinduzi wa mwonekano mpya wa Gazeti
la Mtanzania lenye kauli mbiu ya “Mtanzania Limeboreshwa”Katikati ni
Mhariri Mtendaji Kampuni ya New Habari(2006)Ltd, Absalom Kibanda na
Meneja Masoko wa Kampuni hiyo, Michael Bugidira.
Picha na Mpiga Picha Wetu
WAFANYAKAZI WA ABANA WAANDAMANA KUDAI MIL 400 WANAZODAI
Wafanyakazi
wa kiwanda cha kuchapisha vitabu cha ABANA Printers ltd,kilichopo kata
ya Mapinga wilayani Bagamoyo mkoani Pwani,wakiandamana kudai mishahara
na mafao yao wanayodai kwa kipindi cha miaka miwili na nusu ambayo
yamefikia mil 400 .
(Picha na Mwamvua Mwinyi)
———————————————————–
———————————————————–
Na Mwamvua Mwinyi,Bagamoyo
WAFANYAKAZI
wa kiwanda cha uchapishaji vitabu(ABANA Printers Ltd) kilichopo kata ya
Mapinga wilayani Bagamoyo mkoani Pwani ,wanadai fedha za mishahara na
mafao yao kiasi cha sh.mil.400 tangu mwaka 2014 bila mafanikio.
Aidha
wafanyakazi hao waiomba serikali ya awamu ya tano kuingilia kati tatizo
hilo kwani wameshapigania haki zao kupitia mahakamani ,wizara,idara na
vyama vinavyojishughulisha kutetea haki za wafanyakazi lakini hakuna
msaada walioupata.
Wameeleza
kuwa hadi sasa wanaishi katika maisha magumu huku wengine wakiwa
wamefukuzwa kwenye nyumba walizopanga na wenzao watatu wamefariki
kutokana na ugonjwa wa moyo.
Hayo
yamejiri jana baada ya wafanyakazi hao kuchukua hatua ya kufanya
maandamano nje ya kiwanda hicho na kisha kumfikishia kilio chao
mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi (CCM)Bagamoyo,alhaj Abdul Sharif ili
aweze kuwasaidia kulipwa haki zao.
Mwenyekiti
wa tawi la chama cha wafanyakazi tawi la ABANA printers Wilbard Ikigo
,alidai kuwa mmiliki wa kampuni hiyo anajigamba kwa kusema serikali ipo
mkononi mwake hivyo hawezi kuchukuliwa hatua yoyote.
Alisema
ni miaka miwili na nusu sasa tangu watelekezwe na mwajiri wao hali
iliyosababisha kuingia katika mgogoro na mmiliki huyo.
No comments:
Post a Comment