Naibu
Katbu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Dkt. Yahaya
Simba akizungumza na washiriki wa Mkutano wa Afrikawa wa Usalama wa
Mtandao katika ufunguzi wa mkutano huo kwa Niaba ya Waziri waUjenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa, kwenye Hoteli ya Hyatt
Regency jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Kampuni ya Oracle System Ltd Janusz Naklicki, akitoa Mada
kwenye Mkutano wa Afrika wa Usalama wa Mtandao uliofanyika kwenye Hoteli
ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Msanifu
wa Mifumo ya Mtandao kutoka Kampuni Oracle Enterprise Architecture,
Alexander Smirnov akiwasilisha Mada kwenye Mkutano wa Afrika wa Usalama
wa Mitandao uliofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es
Salaam.
Baadhi
ya washiriki wa Mkutano wa Afrika wa Usalama wa Mtandao kutoka kutoka
nchi mbalimbali wakifuatilia ufunguzi wa mkutano huo wenye lengo la
kupata elimu juu ya usalama wa taarifa na mifumo ya Teknolojia ya
HabarinaMawasiliano (TEHAMA).
Naibu
Katbu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Dkt. Yahaya
Simba (kushoto) akiwa na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Oracle System Ltd
Janusz Naklicki (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa Nchi za Kusini mwa
Jangwa la Sahara wa Kampuni ya Oracle System Ltd, wakifuatilia Mada
kwenye Mkutano wa Afrika wa Usalama wa Mtandao uliofanyika kwenye Hoteli
ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
CHOICE FM NA AFRICAN LYON WAINGIA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO KATIKA KUKUZA VIPAJI NA KUBORESHA MISINGI YA UENDESHAJI WA TIMU.
Mtangazaji wa
Choice Fm cha Dar es Salaam, Jimmy Kabwe (katikati), akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa hafla yakuingia
makubaliano kati ya Timu ya mpira wa miguu ya African Lyon inayoshiriki
ligi kuu Tanzania Bara (Vodacom Premier League) na kituo cha radio cha
Choice FM 102.5, juu ya ushirikiano katika kukuza vipaji na kuboresha
misingi ya uendeshaji wa timu, wengine kushoto kwake alievaa kanzu ni Mmiliki wa klabu ya African Lyon, Rahim Kangezi, na Mkuu wa Vipindi Choice FM, Antonio Nugaz, Mkuu wa Masoko na Mauzo wa Choice FM .
Mkuu wa Vipindi Choice FM, Antonio Nugaz (kulia) akitolea ufafanuzi makubaliano hayo ambapo amesema yanalenga kujenga mazingira ya kuweza kutambua na kuvikuza vipaji vya wanamichezo hasa wale wa mpira wa miguu (kushoto), Mmiliki wa klabu ya African Lyon, Rahim Kangezi
Amesema makubaliano hayo yataiwezesha Africani Lyon yenye masikani yake Mbagala kushirikiana na Choice FM katika kuandaa mashindano na programm zinginezo ambazo zitaleta mvuto kwa vipaji vya wanamichezo wa Kike na Kiume.
Mmiliki wa klabu ya African Lyon, Rahim Kangezi (katikati), akitoa neno la shukrani kwa kituo cha radio cha Choice FM 102.5 mara baada ya kuingia makubaliano .
Mmiliki wa klabu ya African Lyon, Rahim Kangezi, na Captain African
Lyon, Baraka Jafari (Nyaka) wakikabidhiwa jezi wakati wa hafla
yakuingia makubaliano kati ya Timu ya mpira wa miguu ya African Lyon
inayoshiriki ligi kuu Tanzania Bara (Vodacom Premier League) na kituo
cha radio cha Choice FM 102.5, juu ya ushirikiano katika kukuza vipaji
na kuboresha misingi ya uendeshaji wa timu.
Naibu Spika Dkt. Tulia akabidhiwa ripoti ya uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 Bungeni mjini Dodoma
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa
akisalimiana na Mmbunge wa Nkasi Ali Kessy Bungeni Mjini Dodoma Mapema
leo.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akihutubia
Bunge Mapema leo mjini Dodoma wakati wa kuhitimisha mkutano wa Tatu wa
Bunge la kumi na moja la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki
akiteta jambo na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce
Ndalichako Bungeni Mjini Dodoma leo.
Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva akiongoza
ujumbe wa tume hiyo kwenye viwanja vya Bunge leo wakati wa Ziara ya
kutembelea Bunge na kuwasilisha ripoti ya Uchaguzi mkuu wa mwaka 2015
kwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.
Tulia Ackson.
Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia
Ackson akisisitiza jambo kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi
Jaji Mstaafu Damiani Lubuva na ujumbe wake uliotembelea Bunge ili
kumkabidhi Naibu Spika Ripoti ya Uchaguzi mkauu wa mwaka 2015.
WAZIRI MKUU: SERIKALI ITATOA WARAKA JUU YA UKUSANYAJI MAPATO KUPITIA MAWAKALA
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema Halmashauri zitaelekezwa kwa waraka ni
vyanzo vipi vitahitaji kutumia wawakala wa ukusanyaji mapato kwani siyo
kila chanzo cha mapato ya Halmashauri kitakusanywa kwa ufanisi kwa
kutumia au kwa kutotumia mawakala.
Waziri
Mkuu ametoa agizo hilo leo mchana (Alhamisi, Juni 30, 2016) wakati
akitoa hoja ya kuhitimisha mkutano wa tatu wa Bunge la 11 la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.
Amesema
katika ukusanyaji wa mapato, baadhi ya vyanzo vitapaswa kukusanywa na
Halmashauri zenyewe kwa kuzingatia miongozo iliyotolewa na Serikali.
“Moja ya miongozo hiyo ni kwamba kuanzia sasa, iwe kwa kutumia mawakala
au Halmashauri zenyewe ni lazima fedha zinazokusanywa ziwekwe kwenye
akaunti ya Halmashauri na kutumia mifumo ya kielektroniki ili kupunguza
au kumaliza kabisa masuala ya kutumia malipo kwa fedha taslimu (cash
transactions),” alisema.
Amesema
katika kutekeleza agizo hilo, Halmashauri itabidi zikubaliane na wakala
ni kiasi gani cha asilimia ya makusanyo kitalipwa kwa wakala na malipo
yafanyike baada ya kukusanya na kuingizwa kwenye akaunti ya Halmashauri.
Amesema
Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa Sura ya 290, inazipa uwezo Mamlaka
za Serikali za Serikali za Mitaa kutoza na kukusanya kodi, ushuru na
ada mbalimbali kama vyanzo vya mapato vya Mamlaka za Serikali za Mitaa.
“Sheria
hiyo pia inazipa mamlaka hizo kuteua mawakala wa kukusanya mapato hayo
kwa niaba ya Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kuzingatia sheria, kanuni
na taratibu. Lakini Serikali imebaini changamoto za kiufundi katika
kufanya tathmini ya vyanzo vya mapato; ugumu katika kupata mawakala
wenye weledi katika ukusanyaji mapato na kubuni vyanzo vipya vya mapato,
na wakati mwingine watumishi wenyewe kujipa uwakala kinyume na taratibu
zinazomzuia mtumishi kufanya biashara na taasisi yake,” alisema.
Amesema
hatua ya Mamlaka za Serikali za Mitaa kutumia mawakala ni miongoni mwa
mikakati ya kuboresha ukusanyaji mapato na pia kutoa muda mwingi zaidi
kwa watumishi wa mamlaka hizo kushughulika na majukumu ya msingi ya
Halmashauri na hasa utoaji wa huduma kwa wananchi na usimamizi wa miradi
ya maendeleo.
MAJALIWA AKUTANA NA WAJUMBE WA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva katika mazungumzo kati yake na wajumbe wa
Tume ya Taifa ya Uchaguzi yaliyofanyika kwenye makazi yake mjini
Dodoma Juni 30, 2016.
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva katika mazungumzo kati yake ya Wajumbe wa
Tume ya Taifa ya Uchaguzi yaliyofanyika kwenye makazi yake mjini Dodoma
Juni 30, 2016.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa
ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva Taarifa ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi wa
Rais na Wabunge wa 2015 kwenye makazi yake mjini Dodoma Juni30, 2016.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wajumbe wa Tume ya taifa ya
Uchaguzi kwenye Makazi yake mjini Dodoma Juni 30, 2016. Kulia kwake ni
Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Damian Lubuva.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Tume
ya Taifa ya Uchaguzi baada ya kuzungumza nao kwenye makazi yake mjini
Dodoma Juni 30, 2016. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji
Damiana Lubuva.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Wawekezaji wazawa wana haki kuwekeza kwenye gesi, mafuta
Afisa
Habari, Mhandisi Yisambi Shiwa (kushoto) na Mkaguzi wa Madini
Mwandamizi Jeremiah Hango (kulia) kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini
Nchini (TMAA), wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kuwahudumia
wateja katika Maonesho ya Kimataifa ya Saba Saba (Dar es Salaam
International Trade Fair) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu
Nyerere jijini Dar es Salaam.
Afisa
Habari, Mhandisi Yisambi Shiwa (kulia) kutoka Wakala wa Ukaguzi wa
Madini Nchini (TMAA) akielezea madini ya dhahabu yanavyochenjuliwa kwa
mteja aliyeshika sampuni ya madini hayo kwenye banda la TMAA katika
maonesho hayo.
Mtaalam
kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Phillip Mathayo (kushoto)
akielezea majukumu ya Wizara kwa mteja aliyetembelea banda hilo
katika Maonesho ya Kimataifa ya Saba Saba (Dar es Salaam International
Trade Fair) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini
Dar es Salaam.
Mmoja wa wateja (kushoto) akitoa maoni yake kwenye banda la Shirika la
Madini la Taifa (STAMICO) kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Saba Saba
(Dar es Salaam International Trade Fair) yanayoendelea katika
Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
MASHINDANO YA ORYX ENERGIES RALLY OF TANZANIA 2016 KUTIMUA VUMBI JULAI 08 - 10, BAGAMOYO PWANI
Viongozi
wakuu na waandaaji wa mashindani ya mbio za Magari wakiwa katika
mkutano huo wa waandishi wa habari leo Juni 30 Jijini Dar es Salaam
katika hotel ya Southern Sun.
TAASISI YA UTAWALA BORA NA DEMOKRASIA NCHINI TANZANIA YAWAKUTANISHA WADAU WA MAZINGIRA.
Jimmy
Luhende, Mkurugenzi wa Taasisi ya Utawala Bora na Demokrasia nchini
(ADLG), akizungumza katika Mjadala wa Mwezi June uliofanyika hii leo
Jijini Mwanza.
Taasisi ya ADLG huendesha mijadala tofauti tofauti kila mwisho wa mwezi ambapo wadau mbalimbali hukutana na kujadili mada husika. Mjada wa mwezi june umeangazia Fursa, changamoto na athari za kimazingira zitokanazo na shughuli za migodini.
Katika mjada huo, wadau wameishauri serikali kupia Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEC, kuboresha sheria ya usimamizi wa mazingira ili kuweza kuwafanyia tathmini za uchafunzi wa mazingira wachimbaji wadogo kwa kuwa baadhi yao wamekuwa wakichangia uchafunzi wa mazingira nchini. Jamal Baruti ambae ni Mratibu wa Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC, Kanda ya Ziwa, akiwasilisha mada juu ya tathmini ya athari za mazingira zitokanazo na shughuli za uchimbaji wa madini.
Amesema tathimini ya uchafuzi wa mazingira imekuwa ikifanyika kwa wachimbaji wakubwa wa madini kabla na baada ya uchimbaji lakini wachimbaji wadogo wamekuwa hawaguswi na tathmini hiyo kutokana na kutojumuishwa katika tathimini hiyo kwa mjibu wa sheria ya mazingira.
Taasisi ya ADLG huendesha mijadala tofauti tofauti kila mwisho wa mwezi ambapo wadau mbalimbali hukutana na kujadili mada husika. Mjada wa mwezi june umeangazia Fursa, changamoto na athari za kimazingira zitokanazo na shughuli za migodini.
Katika mjada huo, wadau wameishauri serikali kupia Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEC, kuboresha sheria ya usimamizi wa mazingira ili kuweza kuwafanyia tathmini za uchafunzi wa mazingira wachimbaji wadogo kwa kuwa baadhi yao wamekuwa wakichangia uchafunzi wa mazingira nchini. Jamal Baruti ambae ni Mratibu wa Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC, Kanda ya Ziwa, akiwasilisha mada juu ya tathmini ya athari za mazingira zitokanazo na shughuli za uchimbaji wa madini.
Amesema tathimini ya uchafuzi wa mazingira imekuwa ikifanyika kwa wachimbaji wakubwa wa madini kabla na baada ya uchimbaji lakini wachimbaji wadogo wamekuwa hawaguswi na tathmini hiyo kutokana na kutojumuishwa katika tathimini hiyo kwa mjibu wa sheria ya mazingira.
Mmoja wa washiriki akichangia mada
Mmoja wa washiriki akichangia mada
WAZIRI MKUU: SERIKALI ITATOA WARAKA JUU YA UKUSANYAJI MAPATO KUPITIA MAWAKALA
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema Halmashauri zitaelekezwa kwa waraka ni
vyanzo vipi vitahitaji kutumia wawakala wa ukusanyaji mapato kwani siyo
kila chanzo cha mapato ya Halmashauri kitakusanywa kwa ufanisi kwa
kutumia au kwa kutotumia mawakala.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo mchana (Alhamisi, Juni 30, 2016) wakati akitoa hoja ya kuhitimisha mkutano wa tatu wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.
Amesema katika ukusanyaji wa mapato, baadhi ya vyanzo vitapaswa kukusanywa na Halmashauri zenyewe kwa kuzingatia miongozo iliyotolewa na Serikali. “Moja ya miongozo hiyo ni kwamba kuanzia sasa, iwe kwa kutumia mawakala au Halmashauri zenyewe ni lazima fedha zinazokusanywa ziwekwe kwenye akaunti ya Halmashauri na kutumia mifumo ya kielektroniki ili kupunguza au kumaliza kabisa masuala ya kutumia malipo kwa fedha taslimu (cash transactions),” alisema.
Amesema katika kutekeleza agizo hilo, Halmashauri itabidi zikubaliane na wakala ni kiasi gani cha asilimia ya makusanyo kitalipwa kwa wakala na malipo yafanyike baada ya kukusanya na kuingizwa kwenye akaunti ya Halmashauri.
Amesema Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa Sura ya 290, inazipa uwezo Mamlaka za Serikali za Serikali za Mitaa kutoza na kukusanya kodi, ushuru na ada mbalimbali kama vyanzo vya mapato vya Mamlaka za Serikali za Mitaa.
“Sheria hiyo pia inazipa mamlaka hizo kuteua mawakala wa kukusanya mapato hayo kwa niaba ya Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu. Lakini Serikali imebaini changamoto za kiufundi katika kufanya tathmini ya vyanzo vya mapato; ugumu katika kupata mawakala wenye weledi katika ukusanyaji mapato na kubuni vyanzo vipya vya mapato, na wakati mwingine watumishi wenyewe kujipa uwakala kinyume na taratibu zinazomzuia mtumishi kufanya biashara na taasisi yake,” alisema.
Amesema hatua ya Mamlaka za Serikali za Mitaa kutumia mawakala ni miongoni mwa mikakati ya kuboresha ukusanyaji mapato na pia kutoa muda mwingi zaidi kwa watumishi wa mamlaka hizo kushughulika na majukumu ya msingi ya Halmashauri na hasa utoaji wa huduma kwa wananchi na usimamizi wa miradi ya maendeleo.
“Pamoja na dhamira nzuri ya hatua hizo, tunayo mifano ya baadhi ya Halmashauri kama vile Nzega ambayo baadhi ya wahusika wameshinikiza wakitaka zabuni zote wapewe madiwani. Jambo hili halikubaliki na tena ni kinyume cha maadili ya utumishi,” alisisitiza.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameziagiza Halmashauri zote nchini kwamba kuanzia Julai Mosi, 2016 zihakikishe zinatumia mifumo ya kielektroniki katika kukusanya mapato, katika kulipa, kuweka na kutekeleza kikamilifu mikakati madhubuti ya kuboresha makusanyo iwe yanakusanywa na Halmashauri au na wakala.
Amesema Mamlaka za Serikali za Mitaa zina wajibu wa kutoa taarifa kwa wananchi kuhusu mapato na matumizi ya Serikali pamoja na michango ya wananchi licha ya kuwa uzoefu unaonesha kuwa mamlaka hizo zina tatizo la kukaa na fedha kwa muda mrefu kabla ya kuzielekeza kwenye matumizi yaliyokusudiwa.
“Kuchelewesha kutoa fedha zilizotengwa kwa shughuli zilizopangwa ni kuchelewesha kufikisha huduma muhimu kwa wananchi. Napenda kuhimiza uzingatiaji wa utaratibu wa kutoa taarifa kwa wananchi kuhusu mapato na matumizi ya fedha za Serikali katika ngazi zote ili kuongeza uwazi na uwajibikaji katika sekta ya umma,” aliongeza.
Mkutano huo wa tatu wa Bunge ulioanza Aprili 19, 2016 ulikuwa mahsusi kwa ajili ya kujadili na kupitisha bajeti ya kwanza ya Serikali ya Awamu ya Tano pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2016/2017. Bunge limeahirishwa hadi Septemba 6, mwaka huu litakapokutana tena mjini Dodoma.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
DODOMA.
ALHAMISI, JUNI 30, 2016
LAGOS,
Nigeria, 30 June 2016 -/African Media Agency (AMA)/- Africa Finance
Corporation ('AFC') is acting as lead arranger for an up to US$425
million senior mezzanine facility for New Age (African Global Energy)
Limited ('New Age'), a privately held oil and gas exploration,
development, and production company with assets primarily across Africa,
to enable the company to further develop its existing assets and expand
operations. AFC is investing US$75 million in the deal.
AFC and the lender consortium are disbursing an initial US$350 million of the facility immediately, with an accordion feature to allow for an additional US$75 million of capital to follow. The investment will allow New Age to refinance an existing loan facility and develop projects in Nigeria, the Republic of Congo, and to expand operations in several other African countries. The lenders include amongst other EIG Global Energy Partners, and a Middle East based Sovereign Wealth Fund.
This loan will enable New Age to ramp up production in its high quality portfolio across the continent. New Age has made significant steps in achieving its growth objectives. As an example, New Age as the technical operator of the Aje field in OML 113 in Nigeria has attained first oil production targeting 11,000 barrels per day, making Lagos state officially an oil producing state.
The Aje field is also targeted to be a significant gas supplier to Lagos power and industrial projects. In addition, New Age has achieved first production within the last two years at the Litchendjili and Nene marine fields in offshore Congo-Brazzaville.
Andrew Alli, President & CEO of AFC commenting on the announcement said:
"While the recent volatility in the oil industry has been challenging, AFC believes the current market provides opportunities for long-term investors across the value chain.
New Age has enjoyed considerable operational success in recent years across its Pan African portfolio and we would like to help them build on these foundations for the future.
The company's well capitalised existing shareholder base, now complemented by a new financing from top tier financial institutions with a long history of investing in global oil and gas projects, is a testament to the confidence in the business model and provides comfort on New Age's ability to successfully execute future large scale capital projects.
The lenders in the consortium are also working with New Age to further enhance the company's existing robust corporate governance.
AFC is pleased and excited to be able to help the company grow and thrive, especially in this difficult environment. The significance of this investment, is in the linkages between the company's gas production and the power sector in Nigeria in particular, and, the replicability for the development of an energy infrastructure network across continental Africa".
Distributed by African Media Agency (AMA) on behalf of Africa Finance Corporation (AFC).
No comments:
Post a Comment