Pages

Monday, November 30, 2015

Steps on TRA show President Magufuli as a principled leader


Editorial Cartoon
An earthquake of sorts has gripped the hearts and minds of many Tanzanians, not only from the steps taken so far by President John Magufuli since he took office, but, even more poignantly, the measures he took against the Tanzania Revenue Authority management on Friday.

Raw deal for Tanzania in global remittances as Kenya tops region

President Uhuru Kenyatta and his Chinese counterpart Xi Jinping shake hands during a deal signing ceremony. Some African countries may seek to renegotiate repayment of existing debts to China as a way of helping their economies hit by lower crude and commodity prices. PHOTO | AFP
President Uhuru Kenyatta and his Chinese counterpart Xi Jinping shake hands during a deal signing ceremony. Some African countries may seek to renegotiate repayment of existing debts to China as a way of helping their economies hit by lower crude and commodity prices. PHOTO | AFP 

 Whether it is for supplementing household incomes or remitted as gift or for investment, money sent home by relatives and friends living abroad has today become a pivotal aspect of life and national economies in the poor world.

Two Hadzabe villages earn 38 million/- from Carbon Tanzania in six months

The Hadzabe are one of the remaining gatherers and hunters in the world. (File photo)

Two little known Hadzabe villages in Arusha Region earned 38m/- from Carbon Tanzania Limited as payment for their forests carbon sequestration during the first half of this year.

One stop border posts will make a more tangible integration – Shyrose (EALA MP)

Shyrose Bhanji Tanzania�s MP at EALA
 The snail paced implementation of the East Africa Community (EAC) One Stop Border Posts (OSBP) Bill that was passed some two years ago (2013) has been cited as a factor undermining the very essence of the integration, to ease movement of people and goods across the EAC boarders.

'Government all out to ensure collection all of its revenues'


The Prime Minister, Majaliwa Kassim Majaliwa
 The Prime Minister, Majaliwa Kassim Majaliwa has said the fifth-phase government was determined to ensure that all revenues were collected and spent for the benefit of Tanzanians and not for individuals.
 

Missing containers saga: more to be arrested

Deputy Inspector General of Police (DIGP) Abdulrahmani Kaniki
 More Tanzania Revenue Authority (TRA) officials and their accomplices from the private sector implicated in the ‘missing containers’ saga will be arrested and prosecuted in an ‘ongoing’ exercise to bring sanity to the tax office.

How Kenya can attract investment in mining despite global slowdown

Opinion and Analysis
 
(L-R) France's Minister of Ecology and the Environment Segolene Royal and France's Foreign Affairs Minister Laurent Fabius greet US President Barack Obama as France's President Francois Hollande greets US Secretary of State John Kerry during the arrivals for the COP21 United Nations Climate Change Conference on November 30, 2015 in Le Bourget, outside Paris. PHOTO | CHRISTOPHE ENA |  AFP

By CLIFF OTEGA


As representatives from Kenya’s two Houses of Parliament come together in a mediation committee to finalise the Mining Bill 2014, it is prudent to consider the current state of the global mining industry, some of the key risks faced by both investors and governments in this sector and how they might impact the industry in Kenya.

NMG’s digital plan takes shape as new press starts rolling

Nation Media Group CEO Joe Muganda. PHOTO | FILE

Nation Media Group CEO Joe Muganda. PHOTO | FILE 
By HERBLING DAVID, hdavid@ke.nationmedia.com
In Summary
  • NMG's digital business currently accounts for about five per cent of revenue, riding on the flagship portal , www.nation.co.ke, which has an average of 90 million views every month.
  • The company now plans to leverage on this Internet traffic and 15 other websites to turn its online audiences into sustainable revenue streams.
  • NMG has nearly 120,000 e-paper subscriptions every month across its stables, helped by the availability of its print publications on e-paper formats — PDF, Android and iPad. 

Nation Media Group is banking on its large online presence and a revamped digital plan to double its revenues from advertising and e-papers, the management said.

Canada’s Simba Energy sued over sale of firm

Corporate News
 Geothermal now accounts for 29 per cent of Kenya’s energy mix, up from the previous 13 per cent four years ago. PHOTO | FILE
A geothermal well at the Menengai Crater. Geothermal now accounts for 29 per cent of Kenya’s energy mix, up from the previous 13 per cent four years ago. PHOTO | FILE 
By BRIAN WASUNA


An Isle of Man mining firm has sued Canada’s Simba Energy Incorporated for allegedly failing to honour a 2011 $1.5 million (Sh150 million) deal involving the sale of a company prospecting for oil in Kenya.

Miner ventures into power generation with 140MW plant

Corporate News
Geothermal now accounts for 29 per cent of Kenya’s energy mix, up from the previous 13 per cent four years ago. PHOTO | FILE
A geothermal well at the Menengai Crater. Geothermal now accounts for 29 per cent of Kenya’s energy mix, up from the previous 13 per cent four years ago. PHOTO | FILE 
By MUGAMBI MUTEGI
In Summary
  • Olsuswa Energy is seeking to construct a geothermal power plant in Turkana at a cost of Sh42.8 billion, with planned transmission into the national electricity grid.
  • The energy firm says it will begin exploratory work in the first quarter of 2016, drilling a year later and planned transmission of the first phase of the 70MW expected to happen in 2022.

A Kenyan gold explorer is the latest investor seeking to get into power production with the planned construction of a 140 megawatts (MW) geothermal plant in Turkana County.

Uchumi battles to recover Sh2bn from landlords

Corporate News
Uchumi Supermarkets branch in Kisumu. The retailer has started selling its non-core assets like land to boost cash flow and reduce its reliance on borrowing from banks. PHOTO | FILE
Uchumi Supermarkets branch in Kisumu. The retailer has started selling its non-core assets like land to boost cash flow and reduce its reliance on borrowing from banks. PHOTO | FILE 
By SIMON CIURI, sciuri@ke.nationmedia.com
In Summary
  • Uchumi had committed to open more than 20 outlets in Kenya in the mid-term and had reserved space in malls such as Centum-owned Two Rivers, Sarit Centre, Lake Basin Mall in Kisumu and Kenyatta University’s Unicity.
  • The payments now appear to have left the company with a huge legal battle that might take years to resolve.
  • The retailer has instructed its lawyers to serve the landlords with demand letters seeking refunds following the suspension of expansion plans.

Uchumi Supermarkets has opened a multi-pronged legal battle against landlords who pocketed hundreds of millions of shillings in down payments for proposed outlets in Kenya and neighbouring countries. 

National Bank tests liquidity ratios as MPs reject State cash injection

Money Markets
Despite the cash crunch, the bank more than doubled its profit in the nine months to September to Sh2.25 billion. PHOTO | FILE
Despite the cash crunch, the bank more than doubled its profit in the nine months to September to Sh2.25 billion. PHOTO | FILE 
By GEOFFREY IRUNGU
In Summary
  • National Bank’s liquidity ratio stands at 21.1pc against a minimum requirement of 20pc, leaving a 1.1pc headroom.
  • The bank’s capital ratios in relation to lending also remained tenuous with a headroom of only 0.9 percent above the minimum requirement of 14.5 per cent. This means that the institution must control the amount of lending going forward.
  • The Treasury is reported to be mulling merging NBK with state-sponsored Development Bank of Kenya and Consolidated Bank of Kenya.

National Bank of Kenya (NBK) has nearly reached the limit of its statutory ratios following Parliament’s rejection of the National Treasury’s plans to inject new cash into the institution.

Are you ready to rise and take your rightful place as a leader?

Only individuals who are ready to embrace the ever-changing environment emerge as leaders. PHOTO | FILE
Only individuals who are ready to embrace the ever-changing environment emerge as leaders. PHOTO | FILE 
By SERAPHINE RULIGIRWA-KAMARA

It is a very dynamic world that we live in. Only individuals who are ready to embrace the ever-changing environment emerge as leaders.

Defaulters on insurance premiums to be denied bank loans

Insured persons who fail to keep up with their insurance premiums will be listed with the credit reference bureaus beginning next year. PHOTO | FILE 
By GEORGE NGIGI
In Summary
  • Insurance companies usually pay their sales officers bulk commissions on initial phases of the policy contract. This means that when the premiums stop coming in the insurer is left in a loss position.

Insured persons who fail to keep up with their insurance premiums will be listed with the credit reference bureaus beginning next year, the Association of Kenya Insurance (AKI) has said.

Consumer prices harden for the fourth straight month


 
Duncan Kanyugo sells fruits at Nyeri municipal market on November 9, 2015. The cost of living in Kenya rose for the fourth straight month to 7.32pc in November from 6.72pc in October driven by higher food prices. Photo/ JOSEPH KANYI 
By RAWLINGS OTINI

The cost of living in Kenya rose to 7.32 per cent in November from 6.72 per cent in October driven by higher food prices sustaining a four month run that started in August, new inflation numbers show.
The prices of food and non-alcoholic drinks rallied to outweigh a decrease in the prices of cooking gas, electricity and housing.

Bilioni 4 za sherehe za uhuru kupanua barabara ya Mwenge-Moroco yenye urefu wa kilomita 4.3

index 
Sehemu  ambako utaanzia upanuzi wa barabara ya Mwenge hadi Morocco jijini Dar es salaam yenye urefu wa kilometa 4.3 kwa kuongeza njia mbili za barabara za lami kufuatia agizo la Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli la kutumia fedha shilingi bilioni  nne zilizopaswa kutumika kugharamia Shamrashamra za siku ya Uhuru Desemba 9, 2015 kutumika kufanya upanuzi wa barabara hiyo.
PICHA NA IKULU
…………………………………………………………………………………
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameamuru fedha zilizopaswa kutumika kugharamia shamra shamra za siku ya Uhuru ambazo zingefanyika tarehe 09 Desemba 2015, kutumika kufanya upanuzi wa barabara ya Mwenge hadi Morocco jijini Dar es Salaam yenye urefu wa kilometa 4.3 kwa kuongeza njia mbili za barabara za lami.
Tayari fedha hizo kiasi cha shilingi bilioni nne zimepelekwa kwa wakala wa barabara hapa nchini TANROADS kwa ajili ya utekelezaji wa agizo hilo, linalopaswa kuanza mara moja
Akizungumza na Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi PATRICK MFUGALE Ikulu Jijini Dar es Salaam, Dkt. Magufuli ametaka ujenzi wa barabara hiyo uanze haraka ili kukabiliana na adha ya msongamano wa magari katika barabara hiyo
Kujengwa kwa njia hizo kutaifanya barabara ya Morroco hadi Mwenge kuwa na njia tano.
Wakati huo huo, Rais John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti Mstaafu wa Chama Cha wananchi (CUF) Prof. Ibrahim Lipumba Ikulu Jijini Dar es salaam.
Katika Mazungumzo hayo Prof. Lipumba amempongeza Dkt. Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na pia kwa kutoa hotuba nzuri ya uzinduzi wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyokonga nyoyo za Watanzania.
Kwa Upande wake Rais Magufuli amempongeza Prof. Lipumba kwa msimamo wake thabiti wa kupinga ufisadi na amemtakia heri katika shughuli zake.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.
Dar es Salaam.
30 Novemba,2015

RAIS DKT. MAGUFULI, WAZIRI MKUU MAJALIWA, WAMTEMBELEA MAKAMU WA RAIS, MHE. SAMIA OFISINI KWAKE IKULU DAR.

sa1 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, (kushoto) akizungumza na Makamu wake, Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati) na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa, wakati Rais na Waziri Mkuu walipomtembelea Makamu Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Nov 30, 2015 kwa mazungumzo. Picha na OMR
sa2 sa3 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli (kushoto) akiagana na  Makamu wake, Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati) na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa (kulia) baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Nov 30, 2015. Wa pili (kulia) ni Naibu Katibu wa Makamu wa Rais, Mohamed Khamis. Picha na OMR

RAIS MAGUFULI AONANA NA MABALOZI WA CHINA NA KOREA KUSINI, PROFESA LIPUMBA IKULU LEO ba1

ba1 
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana  na Balozi wa China hapa nchini Dkt. Lu Youqing Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 30, 2015
ba2
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akizungumza na Balozi wa China hapa nchini Dkt. Lu Youqing Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 30, 2015
ba4 
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana  na Balozi wa Korea ya Kusini  hapa nchini Mhe. Chung IL Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 30, 2015. Balozi huyo pia alitumia nafasi hiyo kumuaga Rais kwa kuwa muda wake wa kufanya kazi nchini umemalizika.
ba6 
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akizungumza na Balozi wa Korea ya Kusini  hapa nchini Mhe. Chung IL Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 30, 2015. Balozi huyo pia alitumia nafasi hiyo kumuaga Rais kwa kuwa muda wake wa kufanya kazi nchini umemalizika.
ba7 
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana  na aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba  Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba. Profesa Lipumba amempongeza Rais kwa kuchaguliwa kwake kwa kishindo na pia ameipongeza hotuba ya Rais Magufuli aliyoitoa wakati wa kufungua Bunge la 11 mjini Dodoma 30, 2015
ba9 
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akifanya mazungumzo na aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba  Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba. Profesa Lipumba amempondeza Rais kwa kuchaguliwa kwake kwa kishindo na pia ameipongeza hotuba ya Rais Magufuli aliyoitoa wakati wa kufungua Bunge la 11 mjini Dodoma 30, 2015
ba10 
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiagana na aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba  Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba. Profesa Lipumba amempondeza Rais kwa kuchaguliwa kwake kwa kishindo na pia ameipongeza hotuba ya Rais Magufuli aliyoitoa wakati wa kufungua Bunge la 11 mjini Dodoma 30, 2015

Jeshi la Polisi lawashikilia watuhumiwa kumi na mbili wa wizi wa Makontena.

po1 
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Bw.Diwani Athumani (CP) akizungumza na waandishi wa habari ambao hawapo katika picha leo jijini Dar es Salaam kuhusu uchunguzi wa sakata la watuhumiwa wa wizi wa makontena 329. (Picha na Anitha Jonas) – MAELEZO
po2
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Bw.Diwani Athumani (CP) alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu uchunguzi wa watuhumiwa wa wizi wa makontena kwa Mamlaka ya Bandari na Mamlaka ya Mapato Tanzania.
…………………………………………………………………………………..
 
Na Nyakongo Manyama-Maelezo
Dar es Salaam.
Kufuatia agizo laWaziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa la kuwataka watuhumiwa wa wizi wa makontena 329 katika bandari ya Dar es salaam kuchukuliwa hatua na Jeshi la Polisi, tayari Jeshi hilo limewashikilia watuhumiwa kumi na mbili wanaohusika na wizi huo.
Akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam,  Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (CP) Diwani Athumani amesema kuwa, uchunguzi unaofanywa na wataalamu waliobobea katika makosa ya uhalifu wa kifedha umeweza kuwabaini watu kumi na mbili  ambao wamehusika na wizi huo.
“Kati ya watuhumiwa hao kumi na mbili, watano wanashikiliwa na Jeshi la Polisi na saba bado wapo katika upepelezi na upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani,” alisema Kamanda Athumani.
Wanaoshikiliwa kutokana na tuhuma mbalimbali ni Kamishna wa Idara ya Forodha na Ushuru TRA Bw. Tiagi Masamaki, Meneja Kitengo cha Huduma za Ushuru  na Bi.  Habib Mponezia, Msimamizi Mkuu wa Kitengo cha Ushuru wa Forodha.
Watuhumiwa wengine ni pamoja na Bi. Eliaichi Mrema, Msimamizi Kitengo cha Mawasiliano ya Kompyuta  Bw. Haroun  Mpande na Mchambuzi Mwandamizi wa Masuala ya Biashara Bw. Hamis Omary.
Aidha Kamanda Athumani amewaomba wananchi wenye taarifa za ubadhilifu wa mali za Umma kuendelea kulisaidia Jeshi la Polisi katika kutekeleza majukumu yake.

Watumishi wa Umma watakiwa kushiriki zoezi la usafi disemba 9

images
Na Shamimu Nyaki-Maelezo
Serikali imewaagiza watumishi wa umma kushiriki zoezi la usafi wa  nchi  litakalofanyika tarehe 9 disemba mwaka huu katika maeneo yao wanaoishi.
Agizo hilo limetolewa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Bw Assah Mwambene alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo jijin Dar es salaam na kusema kwamba Watumishi wa Umma  wanatakiwa wabaki nyumbani na kufanya usafi katika maeneo yao na  yale watakayo pangiwa na viongozi wa mitaa wanayoishi.
“Kila mwananchi ahakikishe eneo lake ni safi”Alisema Mwambene.
Mkurugenzi ameongeza kuwa Watumishi wa Umma hawataenda kazini badala yake  watabaki  nyumbani na kufanya usafi kwa kushirikiana na wananchi kusafisha maeneo yanayozunguka mitaa wanayoishi ikiwemo hospitali,kuzibua mitaro iliyoziba pamoja na kuzoa taka zilizolundikana sehemu ambazo sio rasmi.
Ameongeza kuwa muongozo kuhusu namna zoezi la usafi litakavyotekelezwa umeshatolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI  kwa Uongozi wa Mikoa hadi Mitaa na kilichobaki ni utekelezaji tuu wa agizo hilo kwa kila mwananchi sehemu anayoishi,anayofanyia shughuli nyingine za kila siku kuhakikisha anafanya usafi.
Aidha Mkurugenzi amewataka viongozi wa kila eneo kutengeneza utaratibu mzuri ambao utafanikisha zoezi la usafi  kufanikiwa kwa kuhakikisha wanasimamia kwa ukamilifu na kuwahimiza wananchi kuwa na tabia ya kusafisha maeneo wanaoishi kwa kuwa ni wajibu wao kufanya hivyo.
Hata hivyo tarehe tisa disemba kila mwaka huwa ni siku ya kusherehekea Uhuru wa Tanganyika uliopatikana miaka hamsini na nne iliyopita lakini kwa mwaka huu itaadhimishwa kwa kufanya usafi nchi nzima.

NHIF YAKUTANA NA MADAKTARI KUTOKA ZAHANATI ZA MANISPAA YA KINONDONI,WATETA NAO KUHUSU HUDUMA YA (TIKA)

2 
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa (NHIF) Bw, Rehani Athumani  na Kaimu Mkurugenzi Mkuu (NHIF) akifungua rasmi warsha ya siku moja ya waganga wa zahanati na vituo vya afya vya Manispaa ya Kinondoni KuhusuMafunzo ya TIKA kwa watoa huduma wa Manispaa ya Kinondoni kuhusu muundo na manufaa ya mfuko wa bima ya afya ya jamii TIKA warsha iliyofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Kinondoni leo jijini Dar es salaam, Kulia ni Mkurugenzi  wa Huduma na Uendeshaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ya Jamii Tanzania, NHIF, Eugine Mikongoti na kushoto ni Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni Dk.Aziz Msuya
3 
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa (NHIF) Bw, Rehani Athumani  na Kaimu Mkurugenzi Mkuu (NHIF) na Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni Dk.Aziz Msuya kushoto wakiteta jambo wa kati wa warsha hiyo.
4 
Mkurugenzi  wa Huduma na Uendeshaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ya Jamii Tanzania, NHIF, Eugine Mikongoti akitoa mada katika warsha hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Kinondoni leo.
5
Baadhi ya washiriki wa Warsha hiyo wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa.
6 
Ofisa Masoko na Elimu kwa Umma, Grace Michael  NHIF kulia akiwa pamoja na washiriki wengine katika warsha hiyo.
7
Baadhi ya washiriki kutoka zahanati na vituo mbalimbali vya afya wilayani Kondondoni.
8 9
Bw Silvery Mgonza Meneja Mfuko wa Afya ya Jamii akitoa mada kwa washiriki wa warsha hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Kinondoni leo.
10 
Baadhi ya maofisa kutoka NHIF wakifuatilia Warsha hiyo.

Wizara ya Nishati na madini yaendelea kutekeleza kwa vitendo ahadi za Rais Dkt. Magufuli.

Dola za Marekani Milioni 3.4 Zatengwa Kusaidia Wachimbaji Wadogo wa Madini Tanzania

images 
Na. Lilian Lundo – Maelezo
Serikali kwa kushirikiana na Benki ya Dunia imetenga jumla ya Dola za Marekani Milioni 3.4 kusaidia vikundi vya wachimbaji wadogo na watoa huduma  katika migodi nchini.
Akiongena vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam, Msemaji wa Wizara ya Nishati na Madini Badra Masoud amesema, hatua hii imekuja baada ya  Serikali kubaini kwamba wachimbaji wengi wadogo huchimba madini kwa kutumia zana na vifaa duni kutokana na ukosefu wa  fedha za kununulia vifaa vya kisasa.
“Wachimbaji wadogo wengi hawawezi kukidhi masharti ya kupata mikopo katika benki za biashara nchini, hivyo Serikali inawajengea uwezo hatua kwa hatua hadi wafikie hatua ya kuweza kukopesheka katika mabenki ya kibiashara,” alisema Badra.
Aidha, Badra alisema kuwa pesa hizo zitatumika kwa miaka mitatu kuanzia mwaka huu wa fedha 2015/16 kwa ajili ya kuwawezesha wachimbaji madini wadogo kupata ruzuku kwa awamu ya tatu ili waweze kuchimba kisasa na kujiongezea vipato vyao na kuongeza pato la Taifa.
Badra alizidi kufafanua  kwa kusema kuwa, ruzuku hii ni jitihada za Serikali katika kukwamua wachimbaji wadogo kuondokana na umasikini kwa kuwajengea uwezo  wa kufikia  kuwa wachimbaji wa kati.
Vilevile Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini, imetenga maeneo yenye ukubwa wa hekari 197,432 kwa ajili wa wachimbaji wadogo ili kuendeleza uchimbaji wa madini mdogo nchini.
Serikali itaendelea kuwa karibu na wachimbaji wadogo waliopatiwa ruzuku kuhakikisha fedha wanazopewa wanazitumia kama ilivyokusudiwa na si vinginevyo, wachimbaji hao watapewa elimu ya uchimbaji wa kisasa, utunzaji wa mazingira na namna ya kuepuka ajali ndani ya migodi.

MAPACHA WANNE WALITEKA JIJI LA DAR ES SALAAM

 Kiongozi wa Bendi ya Twanga Pepeta Rwiza Mbutu akiwa jukwaani wakati wa shoo ya uzinduzi baada ya kujiunga tena katika Bendi ya  mapacha Wanne
 
 
 
 
 Chazi Baba kulia akiwa na Josee Mara wakiwa katika shoo iliyo wavutia wadau wakati wa uzinduzi wa nyimbo yao ya usiku wa kuachwa iliyozinduliwa hivi karibuni baada ya kusambaratika.
 Mpenzi wa Bend ya Mapacha wanne Fredicto Mupao ‘mwana tarime’ akimwagia mapesa mwimbaji wa Bend ya Mapacha wanne Kalala Jonia (kulia) katika ukumbi wa Mango Gaden wakati wa usiku wa nyimbo ya kuachwa iliyo zinduliwa hivi karibuni Jijini Dar es Salaam 
 Rwiza Mutu akiwa Jukwaani
 Mdau achanganyikiwa kwa kumwagia mapesa Mwimbaji wa Bend wa ya Mapacha wanne, KalalaJunia baada ya kuvutiwa na kipaji cha uimbaji wa mwimbaji huyo nakujikuta anamwagia mapesa
 Kuanzia kulia ni Chazz Baba, Haridi Chokora, Kalala Junia, Josee Mara
Kuanzi kulia ni Haridi Chokora, Kalala Jnia, Chazz Baba, Josee Mara

Wanasoka wanawake zaidi ya 400 washiriki tamasha la Live Your Goals

fo1 
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (wapili kushoto) akipokea zawadi ya vifaa vya michezo kutoka FIFA vilivyokabidhiwa kwake na balozi alieteuliwa na FIFA kuhamasisha mpira wa miguu wa wanawake nchini Bibi. Ester Chabuluma jana jijini Dar es Salaam katika Viwanja vya Karume. Kushoto ni Mwenyekiti Kamati Soka la Vijana Bw. Ayoub Nyenzi.
fo2 
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (katikati mwenye koti la bluu) katika picha ya pamoja na wanasoka wanawake kutoka katika shule 5 za msingi na vilabu 6 vya mpira wa miguu wa wanawake baada ya kuhitimisha tamasha la Live Your Goals lilifanyika jana jijini Dar es Salaam katika Viwanja vya Karume.
fo3 
Baadhi ya wanasoka wanawake kutoka katika vilabu mbalimbali vya mpira wa miguu wakisakata kabumbu jana jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Karume wakati wa tamasha la Live Your Goals kuhamasisha mpira wa miguu wa wanawake lililoandaliwa na FIFA.
fo4 
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (katikati) akifuatilia kabumbu ya wanawake iliyokua ikiendelea wakati wa tamasha la Live Your Goals kuhamasisha mpira wa miguu wa wanawake lililoandaliwa na FIFA jana jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Karume. Kulia ni Mkurugenzi wa Michezo Bw. Leonard Thadeo, na kushoto ni Mwenyekiti Kamati Soka la Vijana Bw. Ayoub Nyenzi.
……………………………………………………………………………………………..
Na Genofeva Matemu – Maelezo
Watanzania wametakiwa kuibua vipaji vya michezo hasa mchezo wa mpira wa miguu kwa wanawake kwani michezo ni afya, biashara na ajira inayoheshimika katika jamii.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel jana wakati wa tamasha la Live Your Goals kuhamasisha mpira wa miguu wa wanawake lililoandaliwa na FIFA na kufanyika jana katika viwanja vya Karume Jijini Dar es Salaam.
Prof Gabriel amesema kuwa wazo la kuboresha michezo nchini linapaswa kuwekewa jitihada katika kila Mkoa kwa kuwa na timu ya mpira wa wanawake ili kuweza kuchuja lulu itakayotengenezwa na mikoa yote nchini hivyo kuinua vipaji vya michezo.
“Kama wazazi wote nchini wataweza kutambua vipaji vya watoto wao, kuviheshimu na kuviendeleza katika fani mbalilmbali ikiwemo michezo Tanzania itakua katika nafasi nzuri katika mashindano mbalimbali ya michezo duniani” alisema Prof. Gabriel.
Akizungumza wakati wa tamasha hilo Naodha wa Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu Wanawake Twiga Stars ambaye pia ni balozi wa tamasha la Live Your Goals Bibi. Sophia Edward amesema kuwa tamasha la Live Your Goals limekua na muitikio mkubwa kwani wasichana wapatao 400 wenye umri kati ya miaka 12 na kuendelea wameshiriki na kupatiwa nafasi ya kuonyesha vipaji vyao katika mchezo wa mpira wa miguu.
Bibi. Edward amesema kuwa tamasha lililofanyika jana katika viwanja vya Karume ni tamasha la pili baada ya kufanya tamasha la kwanza Mkoani Geita mwezi Julai na kuendelea kuhamashisha wanawake wote wenye vipaji nchini kujitokeza wanaposikia tamasha la mpira wa miguu kwa wanawake linafanyika kwani matarajio ya FIFA ni kufikia na kuibua vipaji vya wanawake nchini.
Naye Bibi. Pili Said mzazi wa mwanamke mwanasoka mwenye umri wa miaka 10 amekiri kujaribu kuzima ndoto ya mototo wake mara kadhaa baada ya kumzuia kucheza mpira wa miguu hivyo kuwataka wazazi wote nchini kutafakari na kuheshimu ndoto za vijana wao ili kuweza kutimiza azma zao.

MAHAFALI YA SHEREHE ZA FAROUK AKTASMUSLIM SCHOOL YAFANYIKA ZANZIBAR

maa1 
Mkuu wa Divisheni ya Elimu ya Msingi Zanzibar Ahmed Abdulmajid Shaabani akivishwa shada la marumaru na wanafunzi Mwajuma haji na Raya Nasor kama ishara ya kumkaribisha katika Mahafali ya Sherehe za Farouk Aktas Muslim School iliofanyika katika ukumbi wa Taasisi ya kiswahili (SUZA)mjini Zanzibar.PICHA NA -YUSSUF SIMAI -MAELEZO ZANZIBAR.
maa2 
Wanafunzi Zawadi Saidi kulia na Shufaa makame wakisoma Utenzi katika Mahafali ya Sherehe za Farouk Aktas Muslim School iliofanyika katika ukumbi wa Taasisi ya kiswahili (SUZA)mjini Zanzibar.
maa3 
Baadhi ya Wazazi waliohudhuria katika Mahafali ya Sherehe za Farouk Aktas Muslim School iliofanyika katika ukumbi wa Taasisi ya kiswahili (SUZA)mjini Zanzibar.
maa4 
Wanafunzi wa Farouk Aktas Muslim School wakionyesha mavazi la Kizanzibari katika Mahafali ya Sherehe za Farouk Aktas Muslim School iliofanyika katika ukumbi wa Taasisi ya kiswahili (SUZA)mjini Zanzibar.
maa5 
Wanafunzi wa Farouk Aktas Muslim School wakionyesha mavazi ya Kihindi  katika Mahafali ya Sherehe za Farouk Aktas Muslim School iliofanyika katika ukumbi wa Taasisi ya kiswahili (SUZA)mjini Zanzibar.
maa6 
Mkuuu wa Divisheni ya Elimu ya Msingi Zanzibar Ahmed Abdulmajid akiwapa vyeti wanafunzi wa Farouk Aktas Muslim School baada ya kumaliza Sherehe zao zilizofanyika katika ukumbi wa Taasisi ya kiswahili (SUZA)mjini Zanzibar.

KAMPUNI YA MSAMA PROMOTIONS YAMWAGA MISAADA VITUO 10 VYA YATIMA

t12 
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari.
……………………………………………………………………………….
KAMPUNI
ya Msama Promotions ya jijini Dar es Salaam chini ya Mkurugenzi wake,
Alex Msama, ilikabidhi misaada ya vitu mbalimbali kwa vituo 10 vya kulea
watoto yatima ikiwa ni sehemu ya mapato ya matamasha yaliyopita.
Akikabidhi
misaada hiyo kwa watoto hao, Msama alisema wamefanya hivyo kwa kutambua
nafasi yao katika jamii kwamba, watoto hao wanayo haki ya kupata
mahitaji muhimu katika makuzi kama wengine wenye wazazi wao.
Msama
alisema msaada huo wenye thamani ya sh. milioni 7.5, ni sehemu ya fedha
ambazo zimekuwa zikipatikana kupitia matamasha ya muziki wa Injili
ambayo ni wakati wa Pasaka na Krismasi.
“Msaada
huu ni sehemu ya fedha ambazo tumekuwa tukizipata kwa njia ya matamasha
ambayo tumekuwa tukifanya jijini Dar es Salaam na mikoani; Pasaka na
Krismasi,” alisema.
Msama,
alisema wamekuwa wakisaidia watoto yatima na makundi mengine maalumu
katika jamii kwa kutambua kuwa huo ni wajibu wa kila mmoja na ametoa
wito kwa wengine kuwa na moyo wa kusaidia makundi hayo.
Vituo
vilivyopata misaada hiyo ni Umra, Zaidia, Hiari, Malaika, Maunga,
Mwandaliwa, Sifa, Honoratha, Chakuwama na Rahman vya jijini Dar es
Salaam.
Miongoni
mwa vitu vilivyokabidhiwa ni unga wa sembe, mchele, unga wa ngano,
sukari, sabuni, mafuta ya kupikia, mafuta ya kupaka, dawa za meno na
vinginevyo.Wakizungumza kwa nyakati tofauti baada ya kupokea misaada
hiyo ya kiutu, viongozi wa vituo hivyo walisema ni faraja kubwa kwao na
watoto hao wenye mahitaji maalumu.
Maombio
Jonas, mwakilishi wa Kituo cha Sifa Group Foundation cha Bunju, ametoa
shukrani kwa Msama kwa moyo wa kujitolea kusaidia watoto wenye mahitaji
na kutoa wito kwa wengine kuiga mfano wa moyo huo wa upendo.
Naye
Mkurugenzi wa Kituo cha Hiari cha Chang’ombe, Aminajat Klemia, alitoa
pongezi kwa Msama kutokana na misaada hiyo akisema ni faraja kubwa kwa
watoto hao ambao wanahitaji kuthaminiwa kama wengine.
Misaada
hiyo imetolewa wakati ambapo kampuni hiyo ipo katika maandalizi ya
Tamasha la Krimasi litakalofanyika Desemba 25 kwa ajili ya kuadhimisha
kuzaliwa kwa Yesu Kristo pia kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuijalia nchi
kuvuka salama katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25.

AZANIA BANK TAWI LA MOSHI YAKABIDHI VIFAA YA KUFANYIA USAFI KWA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MANISPAA YA MOSHI

Meneja wa Azania Bank tawi la Moshi,Hajira Mmambe akisalimiana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi,Jeshi Lupembe alipofika ofisini kwake kuitikia wito wa rais John Magufuli ya kufanya usafi Desemba 9 kwa kuchangia vifaa vya kufanyia usafi.
Afisa afya mkuu wa manispaa ya Moshi,Mgeta Sebastian akisalimiana na Meneja wa Azania Bank tawi la Moshi ,Hajira Mmambe alipotembelea ofisi za halmashauri hiyo kutoa msaada wa vifaa vya kufanyia usafi.
Meneja wa Azania Bank ,Hajira Mmambe akitia saini katika kitabu cha wageni ofisini kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi.Jeshi Lupembe (kulia).
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi,Jeshi Lupembe akipokea rasmi msaada kutoka benki ya Azania uliowasilishwa na Meneja wa benki hiyo ,Hajira mmambe kwa ajili ya kufanyia usafi.
Wafanyakazi wa Azania Bank tawi la Moshi,wakishusha mifagio ,iliyotolewa na benki hiyo kwa ajili ya shughuli za usafi zitakazofanyika Desemba tisa mwaka huu,kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya manispaa ya Moshi ,Jeshi Lupembe.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi,Jeshi Lupembe akiwa ameongozana na Afisa afya mkuu wa manispaa hiyo,Mgeta Sebastian wakati wa kupokea msaada a vifaa vya kufanyia usafi kutoka Benki ya Azania tawi la Moshi.
Meneja wa Azania Bank tawi la Moshi ,Hajira Mmambe akikabidhi vifaa vya kufanya usafi kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi ,Jeshi Lupembe ,vifaa hivyo vimetolewa kwa ajili ya kutekeleza agizo la rais Magufuli la kufanyika wa usafi siku ya Desemba 9. Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

NHIF yakabidhiwa Kituo chake Dodoma

mi01 
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF akionesha ufunguo wa kituo hicho baada ya kukabidhiwa na baadae alikikabidhi rasmi katika uongozi wa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma.
mi1 
 Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Michael Mhando akikagua Kituo cha Kisasa cha Matibabu kilichopo katika Hospitali ya Mkoa Dodoma. Kituo hicho kinatarajiwa kuanza kutumika mwishoni mwa mwaka huu.
mi2 
Kituo cha Matibabu cha Mfano cha NHIF Dodoma_sehemu ya mapokezi
…………………………………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umekabidhiwa kituo chake cha
matibabu cha mfano mara baada ya ujenzi wa kituo hicho kukamilika.
Makadhiano hayo yalifanyika mjini Dodoma mwishoni mwa wiki katika hafla fupi
iliyohudhuriwa na Uongozi wa NHIF, hospitali ya mkoa na timu ya
wakandarasi akiwemo mshauri mkuu wa mradi huo wa kampuni ya Nosuto
Associates.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Michael Mhando amesema kukamilika kwa
jengo hilo ni hatua kubwa iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu na kazi
iliyoko sasa ni ya ununuzi wa vifaa na samani za jengo ili lianze
kutoa huduma kabla ya sikukuu ya Krismasi.
Amesema timu ya wataalamu kutoka Sekteratarieti ya mkoa tayari iko
jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuchagua vifaa tiba mbalimbali
vitakavyotumika. Ameongeza kuwa vifaa vyote hivyo pamoja na samani za
jengo hili vitalipiwa na Mfuko wa NHIF.
Kituo hicho cha matibabu cha kisasa kinayo mifumo mbalimbali ya TEHAMA
katika utoaji wake wa huduma ikiwemo miito kwa wauguzi, utayarishaji
wa madai na utambuzi wa wagonjwa.
Amesema malengo makuu ya ujenzi wa kituo hicho ni kuwa na kituo cha
kisasa kitakachowezesha wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na
umma wa watanzania kwa ujumla kupata huduma bora za matibabu
wanapokuwa Dodoma katika shughuli mbalimbali za ujenzi wa Taifa.
Naye Mkurugenzi wa fedha, Mipango na Uwekezaji wa NHIF Bw. Desudedit
Rutazaa amesema Kituo hicho vilevile kitasaidia kuwepo na watalamu
wenye uzoefu nchini kwani itakuwa ni sehemu ya kujifunzia kwa
wataalamu wa kada mbalimbali za udaktari na utabibu wawapo masomoni
katika mkoa wa Dodoma na mikoa mingine ya Tanzania.

MBUNGE WA JIMBO LA ILALA MUSSA ZUNGU 

  Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu (CCM) (mwenye kofia) akimkabidhi nahodha wa timu ya Ferry Beach Boys, Selemani Ally ‘Kaseja’ nyaraka za  Pikipiki  Dar es Salaam leo ambayo ilikuwa ni moja ya ahadi yake kwa kikosi hicho wakati wa kampeni.(PICHA NA  KHAMISI MUSSA)
 Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu (CCM) (mwenye kofia) akimkabidhi nahodha wa timu ya Ferry Beach Boys, Selemani Ally ‘Kaseja’ kibao cha namba za Pikipiki Dar es Salaam leo.  
 
 Zungu amesema  ilikuwa ni moja ya ahadi yake kwa kikosi hicho wakati wa kampeni alipofika kituoni hapo wakati alipopita kumuombea kura aliyekuwa mgombea  Urais Dk John Pombe Mgufuli  kupitia Chama cha Mapinduzi  CCM  ili iwasaidie kuongeza  kipato.
Mbunge huyo aliendelea kusema ataendelea kusaidia maswala ya michezo ili kuinua sekta hiyo kwa kusaidia vifaa  vya michezo Zungu ameongeza na kusema ” Leo nakusaidieni Pikipiki iwe mali ya timu si mali ya mtu,ya  wafanyabiashara wenyewe, na niliweka ahadi ya kuwawekea mahema kwenye maeneo mnayouzia samaki,  Nitatekeleza hilo  kabla ya mwezi wa kumi na mbili ili mfanye  biashara kwa uhuru.

TAARIFA YA UPOTEVU WA MAKONTENA AZAM ICD TOKA SSB Group of Companies

Kumekuwa na taarifa zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii kuwa kampuni ya Bakhresa inahusika na upotevu wa Makontena 349 yaliyoripotiwa hivi karibuni kuwa yametolewa bandarini bila kulipiwa ushuru.

Uchunguzi wetu umeonyesha kuwa si kweli kuwa kuna makontena yenye bidhaa zilizoingizwa na kampuni hiyo ama ni miongoni mwa makontena yaliyohusika katika sakata hilo. Isipokuwa kumetokea upotevu wa makontena yaliyoingizwa nchini na baadhi ya wafanyabiashara katika eneo la kuhifadhia makontena(ICD) linalomilikiwa na kampuni hiyo la Azam ICD.

Aidha imebainika kuwa kuna uchunguzi unaofanywa na mamlaka ya mapato nchini TRA, huku kukiwa na ushirikiano na uongozi wa Kampuni hiyo (SSB Group of Companies) kuhakikisha wale wote wanaohusika na upotevu huo wanachukuliwa hatua na kodi yote ya serikali inalipwa na wamiliki wote wa makontena yaliyohusika katika upotevu huo wanawajibishwa.
SSB Group of Companies
Corporate Affairs Department
November 29, 2015

OLE GABRIEL AFUNGA LIVE YOUR GOAL

gab1 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel leo amefunga program ya Live Your Goal iliyoandaliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.
Ole Gabriel amewashukuru vijana waliojitokeza kushiriki katika program hiyo na kuwaomba wazazi kuwarushu watoto wa kike kujtokeza na kushiriki katika program hiyo ya kuhamasisha wanawake kucheza mpira wa miguu.
Live Your Goal ni program inayoendeshwa na TFF kwa msaada kutoka FIFA yenye lengo la kuwahamasisha watoto wa kike, na wasichana kujitokeza kuucheza na kuupenda mpira wa miguu.
Programu hii iliyomalizika leo imejumuisha vilabu sita vya wanawake, kutoka wilaya za Ilala, Kinodoni na Temeke, shule za msingi sita kutoka jijini Dar es salaam ambapo washiriki walikua wanafunzi wenye umri kaunzia miaka 8 na kuendelea, na ikifanyika kwa mara ya pili baada ya awalia mwezi Juni mwaka huu mkoani Geita.

U15 YAKABIDHIWA BENDER YA TAIFA

u15
Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U15) leo hii imekabidhiwa bendera ya Taifa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel katika hosteli za TFF zilizopo Karume jijini Dar es salaam.
Akiongea wakati wa kukabidhi bendera kwa timu hiyo ya vijana, Ole Gabriel amewashukuru TFF kwa kuwekeza katika soka la vijana, na kusema mafaniko yote yanandaliwa chini, hivyo analipongeza Shirikisho kwa kuamua kuwalea na kuwaendeleza vijana hawa wenye vipaji kwa manufaa ya taifa ya baadae.
Ole Gabriel amewataka vijana waliochaguiwa katika kikosi hicho, kuitumia nafasi hiyo adimu ipasavyo kuwawakilisha watanzania, kujituma katika mafunzo wanayopewa na waalimu wao, nidhamu ndani na nje ya uwanja na kuonyesha uzalendo wao wanapoiperesuha bendera ya Taifa.
Kikosi hicho cha vijana wenye umri chini ya miaka 15 kinatarajiwa kuondoka kesho alfajiri (Jumatatu) kuelekea jijini Mwanza kwa mchezo wa kirafiki na kombaini ya mkoa wa Mwanza (U17), kisha kuelekea mkoani Kigoma kwa michezo miwili ya kirafiki dhidi ya kombaini ya mkoa wa Kigoma (U17) na timu ya Taifa ya Burundi (U17).
Baada ya michezo ya mkoani Kigoma, U15 itaelekea Kigali Rwanda kwa michezo na timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17, kisha Jinja kucheza na timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 ya Uganda, Nairobi itacheza na timu ya taifa ya Kenya (U17) na kumalizia jijini Arusha kwa kucheza na kombaini ya mkoa wa huo (U17).
Timu inatarajiwa kurejea jijini Dar ess alaam Disemba 24 baada ya kuwa imecheza michezo kumi ya kirafiki, mechi hizo zitampataia nafasi kocha mkuu Sebastiani Mkomwa kuona maendeleo ya vijana wake, wakiajiandaa kucheza michezo ya kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa Afrika U17 mwaka 2017 nchini Madagascar.

TUMEDHAMIRIA KUWATUMIKIA WATANZANIA – MAJALIWA

ks1 
Waziri  Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa  akisalimiana na baadhi ya viongozi wa kanisa la Africa Inland Church  wakati alipohitimisha maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo katika Dayosisi ya Pwani yaliyofanyika kwenye ukumbi wa PTA katika uwanja wa maonyesho wa Mwalimu Nyerere Kilwa Road jijini Dar es salaam Novemba 29, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
ks2 
Waziri  Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa  akiwa na  baadhi ya viongozi wa kanisa la Africa Inland Church  wakati alipohitimisha maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo katika Dayosisi ya Pwani yaliyofanyika kwenye ukumbi wa PTA katika uwanja wa maonyesho wa Mwalimu Nyerere Kilwa Road jijini Dar es salaam Novemba 29, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
ks3 
Waziri  Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa  akizungumza  wakati alipohitimisha maadhimisho ya miaka 20 ya Kanisa la Africa Inland Church Dayosi ya Pwani yaliyofanyika kwenye ukumbi wa PTA katika uwanja wa maonyesho wa Mwalimu Nyerere Kilwa Road jijini Dar es salaam Novemba 29, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
ks5 
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim majaliwa akiwasha moja ya pikipiki tatu ili kuashiria mkaka ti wa kueneza injili wakati alipohitimisha  maadhimisho ya miaka 20 ya kanisa la Africa Inland Church Dayosisi ya Pwani kwenye  ukumbi wa PTA katika uwanja wa maonyesho wa Mwalimu Nyerere, Kilwa Road jijini Dar es salaam Novemba 29, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu. 
ks6
Waziri  Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa  akifurahia jambo  na baadhi ya viongozi wa kanisa la Africa Inland Church  wakati alipohitimisha maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo katika Dayosisi ya Pwani yaliyofanyika kwenye ukumbi wa PTA katika uwanja wa maonyesho wa Mwalimu Nyerere Kilwa Road jijini Dar es salaam Novemba 29, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
……………………………………………………………………………………………….
*Asema Serikali hii siyo ya watu wapole
WAZIRI MKUU Majaliwa Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuhakikisha kila kinachokusanywa kama mapato ya nchi kinatumika kwa maslahi ya Watanzania wote na si kwa manufaa ya wachache.
Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumapili, Novemba 29, 2015) wakati akifunga maadhimisho ya miaka 20 ya Dayosisi ya Pwani ya Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) kwenye ukumbi wa PTA, viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
“Serikali imeanza kukabiliana na upotevu wa mapato ya Serikali na kuepuka matumizi yasiyo ya lazima ya fedha za umma. Nia yetu ni kuhakikisha kila kinachopaswa kukusanywa kama mapato ya nchi, kikusanywe na kitumike kwa masuala ya msingi kwa ustawi wa Watanzania wote na si kwa watu wachache,” alisema.
Akifunga maadhimisho hayo kwa niaba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Waziri Mkuu alisema Serikali imedhamiria kupambana na maovu yote na kuondoa kero zinazowaumiza wananchi wa kawaida. “Wako watu wanaoamini kwamba hatuwezi, nawaomba waondoe hiyo dhana. Wako watu wanaodhani kwamba kwamba utawala huu ni wa watu wapole, nao pia waondoe hiyo dhana,” alisema huku akishangiliwa na mamia ya waumini waliohudhuria sherehe hizo zilizoanza Novemba 27, 2015.
“Tunawaomba Watanzania wote mtuunge mkono kwenye vita hii na mtuwezeshe kuifanya kazi hiyo. Tunaomba waumini wote mtuombee katika sala zenu za kila siku ili tuweze kuongoza kwa haki na kuwaletea Watanzania wote maendeleo,” aliongeza.
Akinukuu kitabu cha Mithali sura ya 29 mstari wa pili, Waziri Mkuu alisema: “Wenye haki wakiwa na amri, watu hufurahi, bali mwovu atawalapo, watu huugua. Mtuombee viongozi wenu tuwe waadilifu na wenye kutenda haki. Nasi tutaendelea kuwa waadilifu ili watu wetu wasigue,” alisema.
Aliwataka viongozi wa kanisa hilo waendelee kuisaidia Serikali katika kujenga kundi la watu wenye maadili mema ili walisaidie Taifa kuwa na watu waadilifu na hivyo kupunguza kero nyingi zinazoikabili jamii.
Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na waumini wa kanisa la hilo kutoka mikoa mbalimbali, Askofu Mkuu wa Kanisa la AICT, Askofu Silas Kezakubi alisema Kanisa hilo litaendelea kumuombea Rais Dkt Magufuli na viongozi wenzake ili wawe na afya njema, wawe na hekima na kuahidi kwamba wataendelea kuwaweka chini ya ulinzi wa Mungu siku zote.
Alisema wao kama kanisa wanaamini kwamba Serikali ya awamu ya tano ina nia ya kuwatumikia wananchi kwa bidii na uadilifu lakini akasisitiza kuwa siri ya bidii na uadilifu inapatikana kwenye neno la Mungu.
Akisoma risala ya kanisa hilo, Askofu wa AICT Dayosisi ya Kibaha, Askofu Charles Salalah alisema kanisa halina budi kushirikiana na Serikali kwa sababu wote wanawahudumia watu walewale isipokuwa katika malengo tofauti.
Alisema kanisa hilo linahubiri maadili mema na bidii katika kazi kwa vile linaamini kuwa maendeleo hayadondoki kutoka juu wala hayaoti kama uyoga bali yanapatikana kwa watu kufanya kazi.
Akisisitiza kuhusu uadilifu, aliwataka wazazi kudumisha ndoa zao ili watoto wapate malezi mema kutoka kwa baba na mama na kwamba baba na mama wasipokaa vizuri, watoto hawawezi kuwa waadilifu.
“Wazazi tunao wajibu wa kupanda mbegu bora ya uzalendo kwa watoto wetu. Endapo tutapanda mbegu mbaya ya kuwagawa watoto wetu kwa itikadi tofauti, ni lazima tujue kuwa tutavuna tunachopanda.”
“Tukumbuke kuwa tunalo Taifa moja tu la Tanzania. Hata kama watoto wetu watakuwa na upenzi na vyama vyao, ni lazima tuwalee katika misingi ili wakue wakijua Taifa letu ni moja tu. Ndiyo maana tunaweka mkazo kwenye familia kwa sababu maadili mema yanaanzia nyumbani,” alisisitiza.