Sehemu
ambako utaanzia upanuzi wa barabara ya Mwenge hadi Morocco jijini Dar
es salaam yenye urefu wa kilometa 4.3 kwa kuongeza njia mbili za
barabara za lami kufuatia agizo la Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli
la kutumia fedha shilingi bilioni nne zilizopaswa kutumika kugharamia
Shamrashamra za siku ya Uhuru Desemba 9, 2015 kutumika kufanya upanuzi
wa barabara hiyo.
PICHA NA IKULU
…………………………………………………………………………………
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameamuru fedha zilizopaswa kutumika
kugharamia shamra shamra za siku ya Uhuru ambazo zingefanyika tarehe 09
Desemba 2015, kutumika kufanya upanuzi wa barabara ya Mwenge hadi
Morocco jijini Dar es Salaam yenye urefu wa kilometa 4.3 kwa kuongeza
njia mbili za barabara za lami.
Tayari fedha hizo kiasi cha shilingi bilioni nne zimepelekwa kwa wakala wa barabara hapa nchini TANROADS kwa ajili ya utekelezaji wa agizo hilo, linalopaswa kuanza mara moja
Akizungumza na Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi PATRICK MFUGALE Ikulu Jijini Dar es Salaam, Dkt. Magufuli ametaka ujenzi wa barabara hiyo uanze haraka ili kukabiliana na adha ya msongamano wa magari katika barabara hiyo
Kujengwa kwa njia hizo kutaifanya barabara ya Morroco hadi Mwenge kuwa na njia tano.
Wakati huo huo, Rais John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti Mstaafu wa Chama Cha wananchi (CUF) Prof. Ibrahim Lipumba Ikulu Jijini Dar es salaam.
Katika Mazungumzo hayo Prof. Lipumba amempongeza Dkt. Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na pia kwa kutoa hotuba nzuri ya uzinduzi wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyokonga nyoyo za Watanzania.
Kwa Upande wake Rais Magufuli amempongeza Prof. Lipumba kwa msimamo wake thabiti wa kupinga ufisadi na amemtakia heri katika shughuli zake.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.
Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.
Dar es Salaam.
30 Novemba,2015
RAIS DKT. MAGUFULI, WAZIRI MKUU MAJALIWA, WAMTEMBELEA MAKAMU WA RAIS, MHE. SAMIA OFISINI KWAKE IKULU DAR.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, (kushoto)
akizungumza na Makamu wake, Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati) na
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa, wakati Rais na Waziri Mkuu
walipomtembelea Makamu Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Nov
30, 2015 kwa mazungumzo. Picha na OMR
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli (kushoto)
akiagana na Makamu wake, Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati) na Waziri
Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa (kulia) baada ya mazungumzo yao
yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaam, leo
Nov 30, 2015. Wa pili (kulia) ni Naibu Katibu wa Makamu wa Rais,
Mohamed Khamis. Picha na OMR
No comments:
Post a Comment