Rais
Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Balozi wa China hapa
nchini Dkt. Lu Youqing Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 30, 2015
Rais Dkt John Pombe Joseph
Magufuli akizungumza na Balozi wa China hapa nchini Dkt. Lu Youqing
Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 30, 2015
Rais
Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Balozi wa Korea ya
Kusini hapa nchini Mhe. Chung IL Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba
30, 2015. Balozi huyo pia alitumia nafasi hiyo kumuaga Rais kwa kuwa
muda wake wa kufanya kazi nchini umemalizika.
Rais
Dkt John Pombe Joseph Magufuli akizungumza na Balozi wa Korea ya Kusini
hapa nchini Mhe. Chung IL Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 30,
2015. Balozi huyo pia alitumia nafasi hiyo kumuaga Rais kwa kuwa muda
wake wa kufanya kazi nchini umemalizika.
Rais
Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na aliyekuwa Mwenyekiti wa
CUF Profesa Ibrahim Lipumba Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba.
Profesa Lipumba amempongeza Rais kwa kuchaguliwa kwake kwa kishindo na
pia ameipongeza hotuba ya Rais Magufuli aliyoitoa wakati wa kufungua
Bunge la 11 mjini Dodoma 30, 2015
Rais
Dkt John Pombe Joseph Magufuli akifanya mazungumzo na aliyekuwa
Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba Ikulu jijini Dar es salaam
leo Novemba. Profesa Lipumba amempondeza Rais kwa kuchaguliwa kwake kwa
kishindo na pia ameipongeza hotuba ya Rais Magufuli aliyoitoa wakati wa
kufungua Bunge la 11 mjini Dodoma 30, 2015
Rais
Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiagana na aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF
Profesa Ibrahim Lipumba Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba. Profesa
Lipumba amempondeza Rais kwa kuchaguliwa kwake kwa kishindo na pia
ameipongeza hotuba ya Rais Magufuli aliyoitoa wakati wa kufungua Bunge
la 11 mjini Dodoma 30, 2015
Jeshi la Polisi lawashikilia watuhumiwa kumi na mbili wa wizi wa Makontena.
Mkurugenzi
wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Bw.Diwani Athumani (CP) akizungumza na
waandishi wa habari ambao hawapo katika picha leo jijini Dar es Salaam
kuhusu uchunguzi wa sakata la watuhumiwa wa wizi wa makontena 329.
(Picha na Anitha Jonas) – MAELEZO
Baadhi ya waandishi wa habari
wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai
Bw.Diwani Athumani (CP) alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu uchunguzi wa
watuhumiwa wa wizi wa makontena kwa Mamlaka ya Bandari na Mamlaka ya
Mapato Tanzania.
…………………………………………………………………………………..
Na Nyakongo Manyama-Maelezo
Dar es Salaam.
Kufuatia agizo laWaziri Mkuu
Mhe. Kassim Majaliwa la kuwataka watuhumiwa wa wizi wa makontena 329
katika bandari ya Dar es salaam kuchukuliwa hatua na Jeshi la Polisi,
tayari Jeshi hilo limewashikilia watuhumiwa kumi na mbili wanaohusika na
wizi huo.
Akiongea na waandishi wa habari
leo Jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai
(CP) Diwani Athumani amesema kuwa, uchunguzi unaofanywa na wataalamu
waliobobea katika makosa ya uhalifu wa kifedha umeweza kuwabaini watu
kumi na mbili ambao wamehusika na wizi huo.
“Kati ya watuhumiwa hao kumi na
mbili, watano wanashikiliwa na Jeshi la Polisi na saba bado wapo katika
upepelezi na upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani,” alisema
Kamanda Athumani.
Wanaoshikiliwa kutokana na
tuhuma mbalimbali ni Kamishna wa Idara ya Forodha na Ushuru TRA Bw.
Tiagi Masamaki, Meneja Kitengo cha Huduma za Ushuru na Bi. Habib
Mponezia, Msimamizi Mkuu wa Kitengo cha Ushuru wa Forodha.
Watuhumiwa wengine ni pamoja na
Bi. Eliaichi Mrema, Msimamizi Kitengo cha Mawasiliano ya Kompyuta Bw.
Haroun Mpande na Mchambuzi Mwandamizi wa Masuala ya Biashara Bw. Hamis
Omary.
Aidha Kamanda Athumani amewaomba
wananchi wenye taarifa za ubadhilifu wa mali za Umma kuendelea
kulisaidia Jeshi la Polisi katika kutekeleza majukumu yake.
Watumishi wa Umma watakiwa kushiriki zoezi la usafi disemba 9
Na Shamimu Nyaki-Maelezo
Serikali imewaagiza watumishi wa umma
kushiriki zoezi la usafi wa nchi litakalofanyika tarehe 9 disemba
mwaka huu katika maeneo yao wanaoishi.
Agizo hilo limetolewa na Mkurugenzi wa Idara
ya Habari Bw Assah Mwambene alipokuwa akizungumza na waandishi wa
habari leo jijin Dar es salaam na kusema kwamba Watumishi wa Umma
wanatakiwa wabaki nyumbani na kufanya usafi katika maeneo yao na yale
watakayo pangiwa na viongozi wa mitaa wanayoishi.
“Kila mwananchi ahakikishe eneo lake ni safi”Alisema Mwambene.
Mkurugenzi ameongeza kuwa Watumishi wa Umma
hawataenda kazini badala yake watabaki nyumbani na kufanya usafi kwa
kushirikiana na wananchi kusafisha maeneo yanayozunguka mitaa wanayoishi
ikiwemo hospitali,kuzibua mitaro iliyoziba pamoja na kuzoa taka
zilizolundikana sehemu ambazo sio rasmi.
Ameongeza kuwa muongozo kuhusu namna zoezi
la usafi litakavyotekelezwa umeshatolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu
TAMISEMI kwa Uongozi wa Mikoa hadi Mitaa na kilichobaki ni utekelezaji
tuu wa agizo hilo kwa kila mwananchi sehemu anayoishi,anayofanyia
shughuli nyingine za kila siku kuhakikisha anafanya usafi.
Aidha Mkurugenzi amewataka viongozi wa kila
eneo kutengeneza utaratibu mzuri ambao utafanikisha zoezi la usafi
kufanikiwa kwa kuhakikisha wanasimamia kwa ukamilifu na kuwahimiza
wananchi kuwa na tabia ya kusafisha maeneo wanaoishi kwa kuwa ni wajibu
wao kufanya hivyo.
Hata hivyo tarehe tisa disemba kila mwaka
huwa ni siku ya kusherehekea Uhuru wa Tanganyika uliopatikana miaka
hamsini na nne iliyopita lakini kwa mwaka huu itaadhimishwa kwa kufanya
usafi nchi nzima.
NHIF YAKUTANA NA MADAKTARI KUTOKA ZAHANATI ZA MANISPAA YA KINONDONI,WATETA NAO KUHUSU HUDUMA YA (TIKA)
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa (NHIF) Bw, Rehani Athumani na Kaimu
Mkurugenzi Mkuu (NHIF) akifungua rasmi warsha ya siku moja ya waganga
wa zahanati na vituo vya afya vya Manispaa ya Kinondoni KuhusuMafunzo ya
TIKA kwa watoa huduma wa Manispaa ya Kinondoni kuhusu muundo na manufaa
ya mfuko wa bima ya afya ya jamii TIKA warsha iliyofanyika kwenye
ukumbi wa Manispaa ya Kinondoni leo jijini Dar es salaam, Kulia ni Mkurugenzi
wa Huduma na Uendeshaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ya Jamii
Tanzania, NHIF, Eugine Mikongoti na kushoto ni Mganga Mkuu wa Manispaa
ya Kinondoni Dk.Aziz Msuya
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa (NHIF) Bw, Rehani Athumani na Kaimu Mkurugenzi Mkuu (NHIF) na Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni Dk.Aziz Msuya kushoto wakiteta jambo wa kati wa warsha hiyo.
Mkurugenzi
wa Huduma na Uendeshaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ya Jamii
Tanzania, NHIF, Eugine Mikongoti akitoa mada katika warsha hiyo
iliyofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Kinondoni leo.
Baadhi ya washiriki wa Warsha hiyo wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa.
Ofisa Masoko na Elimu kwa Umma, Grace Michael NHIF kulia akiwa pamoja na washiriki wengine katika warsha hiyo.
Baadhi ya washiriki kutoka zahanati na vituo mbalimbali vya afya wilayani Kondondoni.
Bw Silvery Mgonza Meneja Mfuko wa
Afya ya Jamii akitoa mada kwa washiriki wa warsha hiyo iliyofanyika
kwenye ukumbi wa Manispaa ya Kinondoni leo.
Baadhi ya maofisa kutoka NHIF wakifuatilia Warsha hiyo.
Dola za Marekani Milioni 3.4 Zatengwa Kusaidia Wachimbaji Wadogo wa Madini Tanzania
Na. Lilian Lundo – Maelezo
Serikali kwa kushirikiana na Benki ya Dunia
imetenga jumla ya Dola za Marekani Milioni 3.4 kusaidia vikundi vya
wachimbaji wadogo na watoa huduma katika migodi nchini.
Akiongena
vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam, Msemaji wa Wizara ya Nishati
na Madini Badra Masoud amesema, hatua hii imekuja baada ya Serikali
kubaini kwamba wachimbaji wengi wadogo huchimba madini kwa kutumia zana
na vifaa duni kutokana na ukosefu wa fedha za kununulia vifaa vya
kisasa.
“Wachimbaji wadogo wengi hawawezi kukidhi
masharti ya kupata mikopo katika benki za biashara nchini, hivyo
Serikali inawajengea uwezo hatua kwa hatua hadi wafikie hatua ya kuweza
kukopesheka katika mabenki ya kibiashara,” alisema Badra.
Aidha, Badra alisema kuwa pesa hizo
zitatumika kwa miaka mitatu kuanzia mwaka huu wa fedha 2015/16 kwa ajili
ya kuwawezesha wachimbaji madini wadogo kupata ruzuku kwa awamu ya tatu
ili waweze kuchimba kisasa na kujiongezea vipato vyao na kuongeza pato
la Taifa.
Badra alizidi kufafanua kwa kusema kuwa,
ruzuku hii ni jitihada za Serikali katika kukwamua wachimbaji wadogo
kuondokana na umasikini kwa kuwajengea uwezo wa kufikia kuwa
wachimbaji wa kati.
Vilevile Serikali kupitia Wizara ya Nishati
na Madini, imetenga maeneo yenye ukubwa wa hekari 197,432 kwa ajili wa
wachimbaji wadogo ili kuendeleza uchimbaji wa madini mdogo nchini.
Serikali itaendelea kuwa karibu na
wachimbaji wadogo waliopatiwa ruzuku kuhakikisha fedha wanazopewa
wanazitumia kama ilivyokusudiwa na si vinginevyo, wachimbaji hao
watapewa elimu ya uchimbaji wa kisasa, utunzaji wa mazingira na namna ya
kuepuka ajali ndani ya migodi.
MAPACHA WANNE WALITEKA JIJI LA DAR ES SALAAM
Kiongozi
wa Bendi ya Twanga Pepeta Rwiza Mbutu akiwa jukwaani wakati wa shoo ya
uzinduzi baada ya kujiunga tena katika Bendi ya mapacha Wanne
Chazi
Baba kulia akiwa na Josee Mara wakiwa katika shoo iliyo wavutia wadau
wakati wa uzinduzi wa nyimbo yao ya usiku wa kuachwa iliyozinduliwa hivi
karibuni baada ya kusambaratika.
Mpenzi
wa Bend ya Mapacha wanne Fredicto Mupao ‘mwana tarime’ akimwagia mapesa
mwimbaji wa Bend ya Mapacha wanne Kalala Jonia (kulia) katika ukumbi wa
Mango Gaden wakati wa usiku wa nyimbo ya kuachwa iliyo zinduliwa hivi
karibuni Jijini Dar es Salaam
Rwiza Mutu akiwa Jukwaani
Mdau
achanganyikiwa kwa kumwagia mapesa Mwimbaji wa Bend wa ya Mapacha
wanne, KalalaJunia baada ya kuvutiwa na kipaji cha uimbaji wa mwimbaji
huyo nakujikuta anamwagia mapesa
Kuanzia kulia ni Chazz Baba, Haridi Chokora, Kalala Junia, Josee Mara
Kuanzi kulia ni Haridi Chokora, Kalala Jnia, Chazz Baba, Josee Mara
Wanasoka wanawake zaidi ya 400 washiriki tamasha la Live Your Goals
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole
Gabriel (wapili kushoto) akipokea zawadi ya vifaa vya michezo kutoka
FIFA vilivyokabidhiwa kwake na balozi alieteuliwa na FIFA kuhamasisha
mpira wa miguu wa wanawake nchini Bibi. Ester Chabuluma jana jijini Dar
es Salaam katika Viwanja vya Karume. Kushoto ni Mwenyekiti Kamati Soka
la Vijana Bw. Ayoub Nyenzi.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole
Gabriel (katikati mwenye koti la bluu) katika picha ya pamoja na
wanasoka wanawake kutoka katika shule 5 za msingi na vilabu 6 vya mpira
wa miguu wa wanawake baada ya kuhitimisha tamasha la Live Your Goals
lilifanyika jana jijini Dar es Salaam katika Viwanja vya Karume.
Baadhi
ya wanasoka wanawake kutoka katika vilabu mbalimbali vya mpira wa miguu
wakisakata kabumbu jana jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Karume
wakati wa tamasha la Live Your Goals kuhamasisha mpira wa miguu wa
wanawake lililoandaliwa na FIFA.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole
Gabriel (katikati) akifuatilia kabumbu ya wanawake iliyokua ikiendelea
wakati wa tamasha la Live Your Goals kuhamasisha mpira wa miguu wa
wanawake lililoandaliwa na FIFA jana jijini Dar es Salaam katika viwanja
vya Karume. Kulia ni Mkurugenzi wa Michezo Bw. Leonard Thadeo, na
kushoto ni Mwenyekiti Kamati Soka la Vijana Bw. Ayoub Nyenzi.
……………………………………………………………………………………………..
Na Genofeva Matemu – Maelezo
Watanzania wametakiwa kuibua vipaji vya michezo hasa mchezo wa mpira wa miguu kwa wanawake kwani michezo ni afya, biashara na ajira inayoheshimika katika jamii.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel jana wakati wa tamasha la Live Your Goals kuhamasisha mpira wa miguu wa wanawake lililoandaliwa na FIFA na kufanyika jana katika viwanja vya Karume Jijini Dar es Salaam.
Prof Gabriel amesema kuwa wazo la kuboresha michezo nchini linapaswa kuwekewa jitihada katika kila Mkoa kwa kuwa na timu ya mpira wa wanawake ili kuweza kuchuja lulu itakayotengenezwa na mikoa yote nchini hivyo kuinua vipaji vya michezo.
“Kama wazazi wote nchini wataweza kutambua vipaji vya watoto wao, kuviheshimu na kuviendeleza katika fani mbalilmbali ikiwemo michezo Tanzania itakua katika nafasi nzuri katika mashindano mbalimbali ya michezo duniani” alisema Prof. Gabriel.
Akizungumza wakati wa tamasha hilo Naodha wa Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu Wanawake Twiga Stars ambaye pia ni balozi wa tamasha la Live Your Goals Bibi. Sophia Edward amesema kuwa tamasha la Live Your Goals limekua na muitikio mkubwa kwani wasichana wapatao 400 wenye umri kati ya miaka 12 na kuendelea wameshiriki na kupatiwa nafasi ya kuonyesha vipaji vyao katika mchezo wa mpira wa miguu.
Bibi. Edward amesema kuwa tamasha lililofanyika jana katika viwanja vya Karume ni tamasha la pili baada ya kufanya tamasha la kwanza Mkoani Geita mwezi Julai na kuendelea kuhamashisha wanawake wote wenye vipaji nchini kujitokeza wanaposikia tamasha la mpira wa miguu kwa wanawake linafanyika kwani matarajio ya FIFA ni kufikia na kuibua vipaji vya wanawake nchini.
Naye Bibi. Pili Said mzazi wa mwanamke mwanasoka mwenye umri wa miaka 10 amekiri kujaribu kuzima ndoto ya mototo wake mara kadhaa baada ya kumzuia kucheza mpira wa miguu hivyo kuwataka wazazi wote nchini kutafakari na kuheshimu ndoto za vijana wao ili kuweza kutimiza azma zao.

MAHAFALI YA SHEREHE ZA FAROUK AKTASMUSLIM SCHOOL YAFANYIKA ZANZIBAR
Mkuu
wa Divisheni ya Elimu ya Msingi Zanzibar Ahmed Abdulmajid Shaabani
akivishwa shada la marumaru na wanafunzi Mwajuma haji na Raya Nasor kama
ishara ya kumkaribisha katika Mahafali ya Sherehe za Farouk Aktas
Muslim School iliofanyika katika ukumbi wa Taasisi ya kiswahili
(SUZA)mjini Zanzibar.PICHA NA -YUSSUF SIMAI -MAELEZO ZANZIBAR.
Wanafunzi
Zawadi Saidi kulia na Shufaa makame wakisoma Utenzi katika Mahafali ya
Sherehe za Farouk Aktas Muslim School iliofanyika katika ukumbi wa
Taasisi ya kiswahili (SUZA)mjini Zanzibar.
Baadhi
ya Wazazi waliohudhuria katika Mahafali ya Sherehe za Farouk Aktas
Muslim School iliofanyika katika ukumbi wa Taasisi ya kiswahili
(SUZA)mjini Zanzibar.
Wanafunzi
wa Farouk Aktas Muslim School wakionyesha mavazi la Kizanzibari katika
Mahafali ya Sherehe za Farouk Aktas Muslim School iliofanyika katika
ukumbi wa Taasisi ya kiswahili (SUZA)mjini Zanzibar.
Wanafunzi
wa Farouk Aktas Muslim School wakionyesha mavazi ya Kihindi katika
Mahafali ya Sherehe za Farouk Aktas Muslim School iliofanyika katika
ukumbi wa Taasisi ya kiswahili (SUZA)mjini Zanzibar.
Mkuuu
wa Divisheni ya Elimu ya Msingi Zanzibar Ahmed Abdulmajid akiwapa vyeti
wanafunzi wa Farouk Aktas Muslim School baada ya kumaliza Sherehe zao
zilizofanyika katika ukumbi wa Taasisi ya kiswahili (SUZA)mjini
Zanzibar.
KAMPUNI YA MSAMA PROMOTIONS YAMWAGA MISAADA VITUO 10 VYA YATIMA
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari.
……………………………………………………………………………….
KAMPUNI
ya Msama Promotions ya jijini Dar es Salaam chini ya Mkurugenzi wake,
Alex Msama, ilikabidhi misaada ya vitu mbalimbali kwa vituo 10 vya kulea
watoto yatima ikiwa ni sehemu ya mapato ya matamasha yaliyopita.

Akikabidhi
misaada hiyo kwa watoto hao, Msama alisema wamefanya hivyo kwa kutambua
nafasi yao katika jamii kwamba, watoto hao wanayo haki ya kupata
mahitaji muhimu katika makuzi kama wengine wenye wazazi wao.
misaada hiyo kwa watoto hao, Msama alisema wamefanya hivyo kwa kutambua
nafasi yao katika jamii kwamba, watoto hao wanayo haki ya kupata
mahitaji muhimu katika makuzi kama wengine wenye wazazi wao.
Msama
alisema msaada huo wenye thamani ya sh. milioni 7.5, ni sehemu ya fedha
ambazo zimekuwa zikipatikana kupitia matamasha ya muziki wa Injili
ambayo ni wakati wa Pasaka na Krismasi.
alisema msaada huo wenye thamani ya sh. milioni 7.5, ni sehemu ya fedha
ambazo zimekuwa zikipatikana kupitia matamasha ya muziki wa Injili
ambayo ni wakati wa Pasaka na Krismasi.
“Msaada
huu ni sehemu ya fedha ambazo tumekuwa tukizipata kwa njia ya matamasha
ambayo tumekuwa tukifanya jijini Dar es Salaam na mikoani; Pasaka na
Krismasi,” alisema.
huu ni sehemu ya fedha ambazo tumekuwa tukizipata kwa njia ya matamasha
ambayo tumekuwa tukifanya jijini Dar es Salaam na mikoani; Pasaka na
Krismasi,” alisema.
Msama,
alisema wamekuwa wakisaidia watoto yatima na makundi mengine maalumu
katika jamii kwa kutambua kuwa huo ni wajibu wa kila mmoja na ametoa
wito kwa wengine kuwa na moyo wa kusaidia makundi hayo.
alisema wamekuwa wakisaidia watoto yatima na makundi mengine maalumu
katika jamii kwa kutambua kuwa huo ni wajibu wa kila mmoja na ametoa
wito kwa wengine kuwa na moyo wa kusaidia makundi hayo.
Vituo
vilivyopata misaada hiyo ni Umra, Zaidia, Hiari, Malaika, Maunga,
Mwandaliwa, Sifa, Honoratha, Chakuwama na Rahman vya jijini Dar es
Salaam.
vilivyopata misaada hiyo ni Umra, Zaidia, Hiari, Malaika, Maunga,
Mwandaliwa, Sifa, Honoratha, Chakuwama na Rahman vya jijini Dar es
Salaam.
Miongoni
mwa vitu vilivyokabidhiwa ni unga wa sembe, mchele, unga wa ngano,
sukari, sabuni, mafuta ya kupikia, mafuta ya kupaka, dawa za meno na
vinginevyo.Wakizungumza kwa nyakati tofauti baada ya kupokea misaada
hiyo ya kiutu, viongozi wa vituo hivyo walisema ni faraja kubwa kwao na
watoto hao wenye mahitaji maalumu.

Maombio
Jonas, mwakilishi wa Kituo cha Sifa Group Foundation cha Bunju, ametoa
shukrani kwa Msama kwa moyo wa kujitolea kusaidia watoto wenye mahitaji
na kutoa wito kwa wengine kuiga mfano wa moyo huo wa upendo.

Naye
Mkurugenzi wa Kituo cha Hiari cha Chang’ombe, Aminajat Klemia, alitoa
pongezi kwa Msama kutokana na misaada hiyo akisema ni faraja kubwa kwa
watoto hao ambao wanahitaji kuthaminiwa kama wengine.
Mkurugenzi wa Kituo cha Hiari cha Chang’ombe, Aminajat Klemia, alitoa
pongezi kwa Msama kutokana na misaada hiyo akisema ni faraja kubwa kwa
watoto hao ambao wanahitaji kuthaminiwa kama wengine.
Misaada
hiyo imetolewa wakati ambapo kampuni hiyo ipo katika maandalizi ya
Tamasha la Krimasi litakalofanyika Desemba 25 kwa ajili ya kuadhimisha
kuzaliwa kwa Yesu Kristo pia kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuijalia nchi
kuvuka salama katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25.

AZANIA BANK TAWI LA MOSHI YAKABIDHI VIFAA YA KUFANYIA USAFI KWA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MANISPAA YA MOSHI
Meneja wa Azania Bank ,Hajira Mmambe akitia saini katika kitabu cha wageni ofisini kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi.Jeshi Lupembe (kulia). |
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi,Jeshi Lupembe akipokea rasmi msaada kutoka benki ya Azania uliowasilishwa na Meneja wa benki hiyo ,Hajira mmambe kwa ajili ya kufanyia usafi. |
NHIF yakabidhiwa Kituo chake Dodoma
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF akionesha ufunguo wa kituo hicho baada ya
kukabidhiwa na baadae alikikabidhi rasmi katika uongozi wa Hospitali ya
Mkoa wa Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Michael Mhando
akikagua Kituo cha Kisasa cha Matibabu kilichopo katika Hospitali ya
Mkoa Dodoma. Kituo hicho kinatarajiwa kuanza kutumika mwishoni mwa mwaka
huu.
Kituo cha Matibabu cha Mfano cha NHIF Dodoma_sehemu ya mapokezi
…………………………………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umekabidhiwa kituo chake cha
matibabu cha mfano mara baada ya ujenzi wa kituo hicho kukamilika.
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umekabidhiwa kituo chake cha
matibabu cha mfano mara baada ya ujenzi wa kituo hicho kukamilika.
Makadhiano hayo yalifanyika mjini Dodoma mwishoni mwa wiki katika hafla fupi
iliyohudhuriwa na Uongozi wa NHIF, hospitali ya mkoa na timu ya
wakandarasi akiwemo mshauri mkuu wa mradi huo wa kampuni ya Nosuto
Associates.
iliyohudhuriwa na Uongozi wa NHIF, hospitali ya mkoa na timu ya
wakandarasi akiwemo mshauri mkuu wa mradi huo wa kampuni ya Nosuto
Associates.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Michael Mhando amesema kukamilika kwa
jengo hilo ni hatua kubwa iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu na kazi
iliyoko sasa ni ya ununuzi wa vifaa na samani za jengo ili lianze
kutoa huduma kabla ya sikukuu ya Krismasi.
jengo hilo ni hatua kubwa iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu na kazi
iliyoko sasa ni ya ununuzi wa vifaa na samani za jengo ili lianze
kutoa huduma kabla ya sikukuu ya Krismasi.
Amesema timu ya wataalamu kutoka Sekteratarieti ya mkoa tayari iko
jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuchagua vifaa tiba mbalimbali
vitakavyotumika. Ameongeza kuwa vifaa vyote hivyo pamoja na samani za
jengo hili vitalipiwa na Mfuko wa NHIF.
jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuchagua vifaa tiba mbalimbali
vitakavyotumika. Ameongeza kuwa vifaa vyote hivyo pamoja na samani za
jengo hili vitalipiwa na Mfuko wa NHIF.
Kituo hicho cha matibabu cha kisasa kinayo mifumo mbalimbali ya TEHAMA
katika utoaji wake wa huduma ikiwemo miito kwa wauguzi, utayarishaji
wa madai na utambuzi wa wagonjwa.
katika utoaji wake wa huduma ikiwemo miito kwa wauguzi, utayarishaji
wa madai na utambuzi wa wagonjwa.
Amesema malengo makuu ya ujenzi wa kituo hicho ni kuwa na kituo cha
kisasa kitakachowezesha wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na
umma wa watanzania kwa ujumla kupata huduma bora za matibabu
wanapokuwa Dodoma katika shughuli mbalimbali za ujenzi wa Taifa.
kisasa kitakachowezesha wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na
umma wa watanzania kwa ujumla kupata huduma bora za matibabu
wanapokuwa Dodoma katika shughuli mbalimbali za ujenzi wa Taifa.
Naye Mkurugenzi wa fedha, Mipango na Uwekezaji wa NHIF Bw. Desudedit
Rutazaa amesema Kituo hicho vilevile kitasaidia kuwepo na watalamu
wenye uzoefu nchini kwani itakuwa ni sehemu ya kujifunzia kwa
wataalamu wa kada mbalimbali za udaktari na utabibu wawapo masomoni
katika mkoa wa Dodoma na mikoa mingine ya Tanzania.

MBUNGE WA JIMBO LA ILALA MUSSA ZUNGU
Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu (CCM) (mwenye kofia) akimkabidhi
nahodha wa timu ya Ferry Beach Boys, Selemani Ally ‘Kaseja’ nyaraka za
Pikipiki Dar es Salaam leo ambayo ilikuwa ni moja ya ahadi yake kwa
kikosi hicho wakati wa kampeni.(PICHA NA KHAMISI MUSSA)
Mbunge
wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu (CCM) (mwenye kofia) akimkabidhi nahodha
wa timu ya Ferry Beach Boys, Selemani Ally ‘Kaseja’ kibao cha namba za
Pikipiki Dar es Salaam leo.
Zungu
amesema ilikuwa ni moja ya ahadi yake kwa kikosi hicho wakati wa
kampeni alipofika kituoni hapo wakati alipopita kumuombea kura aliyekuwa
mgombea Urais Dk John Pombe Mgufuli kupitia Chama cha Mapinduzi CCM
ili iwasaidie kuongeza kipato.
Mbunge huyo aliendelea kusema ataendelea kusaidia maswala ya michezo ili
kuinua sekta hiyo kwa kusaidia vifaa vya michezo Zungu ameongeza na
kusema ” Leo nakusaidieni Pikipiki iwe mali ya timu si mali ya mtu,ya
wafanyabiashara wenyewe, na niliweka ahadi ya kuwawekea mahema kwenye
maeneo mnayouzia samaki, Nitatekeleza hilo kabla ya mwezi wa kumi na
mbili ili mfanye biashara kwa uhuru.
TAARIFA YA UPOTEVU WA MAKONTENA AZAM ICD TOKA SSB Group of Companies
Kumekuwa
na taarifa zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii kuwa kampuni ya
Bakhresa inahusika na upotevu wa Makontena 349 yaliyoripotiwa hivi
karibuni kuwa yametolewa bandarini bila kulipiwa ushuru.
Uchunguzi
wetu umeonyesha kuwa si kweli kuwa kuna makontena yenye bidhaa
zilizoingizwa na kampuni hiyo ama ni miongoni mwa makontena yaliyohusika
katika sakata hilo. Isipokuwa kumetokea upotevu wa makontena
yaliyoingizwa nchini na baadhi ya wafanyabiashara katika eneo la
kuhifadhia makontena(ICD) linalomilikiwa na kampuni hiyo la Azam ICD.
Aidha
imebainika kuwa kuna uchunguzi unaofanywa na mamlaka ya mapato nchini
TRA, huku kukiwa na ushirikiano na uongozi wa Kampuni hiyo (SSB Group of
Companies) kuhakikisha wale wote wanaohusika na upotevu huo
wanachukuliwa hatua na kodi yote ya serikali inalipwa na wamiliki wote
wa makontena yaliyohusika katika upotevu huo wanawajibishwa.
SSB Group of Companies
Corporate Affairs Department
November 29, 2015
OLE GABRIEL AFUNGA LIVE YOUR GOAL
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa
Elisante Ole Gabriel leo amefunga program ya Live Your Goal
iliyoandaliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) katika uwanja
wa Karume jijini Dar es salaam.
Ole Gabriel amewashukuru vijana
waliojitokeza kushiriki katika program hiyo na kuwaomba wazazi kuwarushu
watoto wa kike kujtokeza na kushiriki katika program hiyo ya
kuhamasisha wanawake kucheza mpira wa miguu.
Live Your Goal ni program
inayoendeshwa na TFF kwa msaada kutoka FIFA yenye lengo la kuwahamasisha
watoto wa kike, na wasichana kujitokeza kuucheza na kuupenda mpira wa
miguu.
Programu hii iliyomalizika leo
imejumuisha vilabu sita vya wanawake, kutoka wilaya za Ilala, Kinodoni
na Temeke, shule za msingi sita kutoka jijini Dar es salaam ambapo
washiriki walikua wanafunzi wenye umri kaunzia miaka 8 na kuendelea, na
ikifanyika kwa mara ya pili baada ya awalia mwezi Juni mwaka huu mkoani
Geita.
U15 YAKABIDHIWA BENDER YA TAIFA
Timu
ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U15) leo hii
imekabidhiwa bendera ya Taifa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel katika
hosteli za TFF zilizopo Karume jijini Dar es salaam.
Akiongea wakati wa kukabidhi
bendera kwa timu hiyo ya vijana, Ole Gabriel amewashukuru TFF kwa
kuwekeza katika soka la vijana, na kusema mafaniko yote yanandaliwa
chini, hivyo analipongeza Shirikisho kwa kuamua kuwalea na kuwaendeleza
vijana hawa wenye vipaji kwa manufaa ya taifa ya baadae.
Ole Gabriel amewataka vijana
waliochaguiwa katika kikosi hicho, kuitumia nafasi hiyo adimu ipasavyo
kuwawakilisha watanzania, kujituma katika mafunzo wanayopewa na waalimu
wao, nidhamu ndani na nje ya uwanja na kuonyesha uzalendo wao
wanapoiperesuha bendera ya Taifa.
Kikosi hicho cha vijana wenye umri
chini ya miaka 15 kinatarajiwa kuondoka kesho alfajiri (Jumatatu)
kuelekea jijini Mwanza kwa mchezo wa kirafiki na kombaini ya mkoa wa
Mwanza (U17), kisha kuelekea mkoani Kigoma kwa michezo miwili ya
kirafiki dhidi ya kombaini ya mkoa wa Kigoma (U17) na timu ya Taifa ya
Burundi (U17).
Baada ya michezo ya mkoani Kigoma,
U15 itaelekea Kigali Rwanda kwa michezo na timu ya taifa ya vijana
wenye umri chini ya miaka 17, kisha Jinja kucheza na timu ya taifa ya
vijana wenye umri chini ya miaka 17 ya Uganda, Nairobi itacheza na timu
ya taifa ya Kenya (U17) na kumalizia jijini Arusha kwa kucheza na
kombaini ya mkoa wa huo (U17).
Timu inatarajiwa kurejea jijini
Dar ess alaam Disemba 24 baada ya kuwa imecheza michezo kumi ya
kirafiki, mechi hizo zitampataia nafasi kocha mkuu Sebastiani Mkomwa
kuona maendeleo ya vijana wake, wakiajiandaa kucheza michezo ya kuwania
kufuzu kwa fainali za Mataifa Afrika U17 mwaka 2017 nchini Madagascar.
TUMEDHAMIRIA KUWATUMIKIA WATANZANIA – MAJALIWA
Waziri
Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya viongozi wa
kanisa la Africa Inland Church wakati alipohitimisha maadhimisho ya
miaka 20 tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo katika Dayosisi ya Pwani
yaliyofanyika kwenye ukumbi wa PTA katika uwanja wa maonyesho wa Mwalimu
Nyerere Kilwa Road jijini Dar es salaam Novemba 29, 2015. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akiwa na baadhi ya viongozi wa kanisa
la Africa Inland Church wakati alipohitimisha maadhimisho ya miaka 20
tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo katika Dayosisi ya Pwani yaliyofanyika
kwenye ukumbi wa PTA katika uwanja wa maonyesho wa Mwalimu Nyerere Kilwa
Road jijini Dar es salaam Novemba 29, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Waziri
Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipohitimisha
maadhimisho ya miaka 20 ya Kanisa la Africa Inland Church Dayosi ya
Pwani yaliyofanyika kwenye ukumbi wa PTA katika uwanja wa maonyesho wa
Mwalimu Nyerere Kilwa Road jijini Dar es salaam Novemba 29, 2015. (Picha
na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Majaliwa Kassim majaliwa akiwasha moja ya pikipiki tatu ili
kuashiria mkaka ti wa kueneza injili wakati alipohitimisha maadhimisho
ya miaka 20 ya kanisa la Africa Inland Church Dayosisi ya Pwani kwenye
ukumbi wa PTA katika uwanja wa maonyesho wa Mwalimu Nyerere, Kilwa Road
jijini Dar es salaam Novemba 29, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Waziri
Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akifurahia jambo na baadhi ya
viongozi wa kanisa la Africa Inland Church wakati alipohitimisha
maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo katika Dayosisi
ya Pwani yaliyofanyika kwenye ukumbi wa PTA katika uwanja wa maonyesho
wa Mwalimu Nyerere Kilwa Road jijini Dar es salaam Novemba 29, 2015.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
……………………………………………………………………………………………….
*Asema Serikali hii siyo ya watu wapole
WAZIRI MKUU Majaliwa Kassim
Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuhakikisha kila
kinachokusanywa kama mapato ya nchi kinatumika kwa maslahi ya Watanzania
wote na si kwa manufaa ya wachache.
Ametoa kauli hiyo leo mchana
(Jumapili, Novemba 29, 2015) wakati akifunga maadhimisho ya miaka 20 ya
Dayosisi ya Pwani ya Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT)
kwenye ukumbi wa PTA, viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
“Serikali imeanza kukabiliana na
upotevu wa mapato ya Serikali na kuepuka matumizi yasiyo ya lazima ya
fedha za umma. Nia yetu ni kuhakikisha kila kinachopaswa kukusanywa kama
mapato ya nchi, kikusanywe na kitumike kwa masuala ya msingi kwa ustawi
wa Watanzania wote na si kwa watu wachache,” alisema.
Akifunga maadhimisho hayo kwa
niaba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Waziri Mkuu alisema Serikali
imedhamiria kupambana na maovu yote na kuondoa kero zinazowaumiza
wananchi wa kawaida. “Wako watu wanaoamini kwamba hatuwezi, nawaomba
waondoe hiyo dhana. Wako watu wanaodhani kwamba kwamba utawala huu ni wa
watu wapole, nao pia waondoe hiyo dhana,” alisema huku akishangiliwa na
mamia ya waumini waliohudhuria sherehe hizo zilizoanza Novemba 27,
2015.
“Tunawaomba Watanzania wote
mtuunge mkono kwenye vita hii na mtuwezeshe kuifanya kazi hiyo. Tunaomba
waumini wote mtuombee katika sala zenu za kila siku ili tuweze kuongoza
kwa haki na kuwaletea Watanzania wote maendeleo,” aliongeza.
Akinukuu kitabu cha Mithali sura
ya 29 mstari wa pili, Waziri Mkuu alisema: “Wenye haki wakiwa na amri,
watu hufurahi, bali mwovu atawalapo, watu huugua. Mtuombee viongozi wenu
tuwe waadilifu na wenye kutenda haki. Nasi tutaendelea kuwa waadilifu
ili watu wetu wasigue,” alisema.
Aliwataka viongozi wa kanisa hilo
waendelee kuisaidia Serikali katika kujenga kundi la watu wenye maadili
mema ili walisaidie Taifa kuwa na watu waadilifu na hivyo kupunguza kero
nyingi zinazoikabili jamii.
Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu
kuzungumza na waumini wa kanisa la hilo kutoka mikoa mbalimbali, Askofu
Mkuu wa Kanisa la AICT, Askofu Silas Kezakubi alisema Kanisa hilo
litaendelea kumuombea Rais Dkt Magufuli na viongozi wenzake ili wawe na
afya njema, wawe na hekima na kuahidi kwamba wataendelea kuwaweka chini
ya ulinzi wa Mungu siku zote.
Alisema wao kama kanisa wanaamini
kwamba Serikali ya awamu ya tano ina nia ya kuwatumikia wananchi kwa
bidii na uadilifu lakini akasisitiza kuwa siri ya bidii na uadilifu
inapatikana kwenye neno la Mungu.
Akisoma risala ya kanisa hilo,
Askofu wa AICT Dayosisi ya Kibaha, Askofu Charles Salalah alisema kanisa
halina budi kushirikiana na Serikali kwa sababu wote wanawahudumia watu
walewale isipokuwa katika malengo tofauti.
Alisema kanisa hilo linahubiri
maadili mema na bidii katika kazi kwa vile linaamini kuwa maendeleo
hayadondoki kutoka juu wala hayaoti kama uyoga bali yanapatikana kwa
watu kufanya kazi.
Akisisitiza kuhusu uadilifu,
aliwataka wazazi kudumisha ndoa zao ili watoto wapate malezi mema kutoka
kwa baba na mama na kwamba baba na mama wasipokaa vizuri, watoto
hawawezi kuwa waadilifu.
“Wazazi tunao wajibu wa kupanda
mbegu bora ya uzalendo kwa watoto wetu. Endapo tutapanda mbegu mbaya ya
kuwagawa watoto wetu kwa itikadi tofauti, ni lazima tujue kuwa tutavuna
tunachopanda.”
“Tukumbuke kuwa tunalo Taifa moja
tu la Tanzania. Hata kama watoto wetu watakuwa na upenzi na vyama vyao,
ni lazima tuwalee katika misingi ili wakue wakijua Taifa letu ni moja
tu. Ndiyo maana tunaweka mkazo kwenye familia kwa sababu maadili mema
yanaanzia nyumbani,” alisisitiza.
No comments:
Post a Comment