NA K-VIS MEDIA
CELINA
Ompeshi Kombani, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, (Utumishi), amefariki dunia
akiwa kwenye matibabu nchini India. Kwa mujibu wa Naibu Spika wa Bunge Job
Ndugai, Marehemu Kombani alipelekwa nchini India mwezi mmoja uliopita
akisumbuliwa na malaria iliyoambatana na homa kali.
Kwa
mjujibu wa Ndugai, Mh. Kombani ambaye mara ya mwisho alikuwa mbunge wa jimbo la
Ulanga Mashariki, amefariki jioni hii ya Septemba 24, 2015 na mwili wake
utawasili jijini Dar es Salaam, Jumamosi Septemba 26, 2015.
Mh.
Kombani aliyezaliwa 19 June 1959,
alipata
elimu yake ya msingi Kwiro kuanzia mwaka 1968 hadi 1975, na baadaye kujiunga na
shule ya sekondari Kilakala mwaka 1975 hadi 1978. Mnamo mwaka 1979 alijiunga na
shule ya sekondari ya wasichana ya Tabora, (Tabora Girls), na kuhitimu mwaka
1981.
Mwaka
1982, Mh. Kombani alijiunga na Chuo cha IDM Mzumbe na kujipatia shahada ya
Utawala wa Umma (B.A in Public Administration mnamo mwaka 1982 hadi 1985. Mwaka
1994 hadi mwaka 1995 Mh. Kombani alichukua shahada ya pili ya Utawala wa Umma, chuo
Kikuu ch Mzumbe
HOUSE GIRL ATOKOMEA NA MTOTO WA BOSI WAKE, HAIJULIKANI ALIKO NA MTOTO HUYO
Picha ya hivi karibuni ya mtoto Loveness C. Jullu |
Familia ya Jullu ya Wazo Hill kwa
Msabaha jijini Dar es Salaam inaomba msaada kutoka kwa raia wema ili
kufanikisha kumpata mtoto wao Loveness Coletha Jullu aliyepotea nyumbani
na msichana aliyekuwa akimlea na kusaidia shughuli za nyumbani.
Wawili hao hawajaonekana tangu juzi
Jumanne. Taarifa zimefikishwa katika kituo cha polisi na RPC wa mkoa wa
kipolisi wa Kinondoni amekiri kupata taarifa za tukio hilo.
Ikiwa una taarifa zozote zitakazosaidia kupatikana kwao tafadhali zitoa kupitia namba hizi: 0715797920 na 0786977615.
Asante.
Binti msaidizi wa kazi za nyumbani (house-girl) |
Picha ya awali ya mtoto |
Pichani kutoka kushoto ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Shekh. Khamis Haji Khamis, Rais wa Zanzibar, Dkt. Alhaj Ali Mohammed Shein, Waziri wa Sheria na Katiba wa Zanzibar,Abubar Khamis Bakary Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, na Rais mstaaffu wa
Zanzibar, Aman Abeid Karume, wakiwa kwenye baraza la Eid El Hajj, mjini
Zanzibar leo Septemba 24, 2015. Waislamu kote Duniani wanasherehekea
sikukuu ya Eid El Hajj
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Waziri wa katiba na
Sheria Mhe,Abubar Khamis Bakary mara alipowasili katika viwanja vya Chuo cha
Amali Mkokotoni katika Mkutano wa Baraza la Eid El Hajj akiwa mgeni rasmi
katika baraza hilo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Kamishna wa Polisi
Zanzibar Hamdani Omar Makame mara alipowasili katika viwanja vya Chuo cha Amali
Mkokotoni katika Mkutano wa Baraza la Eid El Hajj akiwa mgeni rasmi katika
baraza hilo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Kamishna wa Polisi Zanzibar
Hamdani Omar Makame mara alipowasili katika viwanja vya Chuo cha Amali
Mkokotoni katika Mkutano wa Baraza la Eid El Hajj akiwa mgeni rasmi katika
baraza hilo leo kabla ya kukagua gwaride rasmi la Sherehe hizo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein akipokea salamu ya heshma ya Gwaride la
KIKOSI cha Polisi FFU mara alipowasili katika viwanja vya Chuo cha Amali
Mkokotoni katika Mkutano wa Baraza la Eid El Hajj akiwa mgeni rasmi katika baraza
hilo leo (kushoto)Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamdani Omar Makame
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akitoa hutuba yake kwa wananchi
wa Zanzibar katika Baraza la Eid El Hajj lililofanyika leo katika Ukumbi wa
Chuo cha Amali Mkokotoni Wilaya ya Kaskazini A,Mkoa wa Kaskazini Unguja ikiwa ni katika sherehe za Sikukuu ya
Eid El Hajj
Mke wa Makamo wa Pili wa rais wa zanzibar Mama
Asha Suleiman Iddi (mwenye miwani) pamoja na Viongozi wengine mbali mbali
wakiwa katika ukumbi wa Chuo cha Amali
Mkokotoni katika Mkutano wa Baraza la Eid El Hajj lililofanyika leo,mgeni rasmi
katika baraza hilo akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein
Baadhi ya Viongozi na wananchi walioalikwa
katika mkurano wa Baraza la Eid El Hajj wakiwa katika ukumbi wa Chuo cha Amali
Mkokotoni Wialaya ya Kaskazini A mkoa wa kakskazini Unguja,palipofanyika
Baraza hilo katika kusherehekea Sikukuu ya
Eid El Hajj wakati mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein
IBADA YA HIJA ENEO LA MINA, NI WAKATI WA KUMRUSHIA MAWE SHETANI
KWA uchache Waislamu 717 wamefariki dunia kwa kukanyagana wakati wakitekeleza ibada ya Hija nje
kidogo ya Maka (Mecca).
Watislamu
wengine 863 wamejeruhiwa kwenye kadhai hiyo iliyotokea wakati Waislamu
wanaoshiriki ibada ya Hija, walipokuwa wakitekeleza tendo la kumrushia mawe
shetani.
Mkanyagano
huo
ambao umetokea kwenye daraja la bonde la Minna, kilomita chache kutoka
mji
mtakatifu wa Maka nchini Saudi Arabia ambapo takriban mahema 160,000,
yanayohifadhi mamilioni ya waumini wa Kiislamu wanaoshiriki ibada ya
Hija
mwaka huu.
Tukio
hilo lilitokea wakati makundi makubwa mawili ya watu, waliokuwa wakijiandaa
kutekeleza moja ya matukio ya mwisho ya ibada yalipokutana kwenye “njia panda”
(makutano ya barabara), Maafisa wa Saudi Arabia wameviambia vyombo vya habari
leo Septemba 24, 2015
Mkanyagano
huo uliacha mlundikano wa maiti na majeruhi kwenye mitaa huku joto kali
likitawala eneo hilo, Picha za video zimeonyesha.
Zaidi
ya waokoaji 4,000 wamepelekwa eneo la tukio ili kusaidia shughulia za uokoaji
na kutoa huduma ya kwanza ambapo mamia ya watu waliojeruhiwea vibaya
walichukuliwa kwa helikopta na wengine kwenye mamia ya magari ya kubeba
wagonjwa.
Vifo
hivyo ni vingi mmno kutokea kwenye eneo hilo kwa wakati kama huu, ambapo mnamo
mwaka 1990, mahujaji 1,400 walifariki dunia baada ya kutokea mshtuko miongoni
mwa mahujaji wakiwa kwenye njia ya chini ya kupitia kuelekea eneo hilo la
kumrushia mawe shetani
Lakini
pia ni tukio la pili kutokea katika kipindi hiki cha hija, ambapo mwanzoni mwa
mwezi huu, zaidi ya watu 100 walipoteza maisha baada ya winchi kubwa lililokuwa
kwenye eneo la ujenzi kwenye msikiti mkuu wa Maka, kukatika na kuangukia
majengo na watu.
Watu
wengine zaidi ya 200 walijeruhiwa kwenye tukio hilo.
Profesa Ibrahim Lipumba, akisalimiana na Hujaji mwenzake kwenye msikiti mkuu wa Mecca, Saudi Arabia, wakati wa ibada ya Hija.
WAISLAMU WASALI SALA YA EID EL-HAJJ NCHINI
Waislamu wakiwa kwenye sala ya Eid al-Hajj kwenye uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma, leo Septemba 24, 2015.
Muumini wa Kiislamu, akichinja mbuzi,
ikiwa ni utekelezwaji wa sikukuu ya Eid Al-Hajj, amnbayo inawataka
Waislamu kutekeleza sherehe hiyo kwa kuchinja wanyama wanaoruhusiwa
kuliwa
Sheikh Abdu Kadri akiongoza swala ya
Idd El Haji katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke Dar es Salaam leo
asubuhi. Waislam wa Tanzania leo waliungana na wenzao duniani kote
kusherehekea Sikukuu ya Idd El Haji.
Sheikh Nurudin Kishki alitohotuba baada ya swala hiyo.
Sheikh Othman Dishi akitoa maelekezo kabla ya kuanza kwa swala hiyo.
Waumini wa dini ya kiislam wakiwa katika swala.
Wanawake na watoto wakiwa kwenye swala hiyo.
Mazuria ya kuswalia yakitandikwa kabla ya kuanza ibada.
Hapa wakitawaza kabla ya kuinza kwa swala hiyo.
Abdurahi Suleiman (kulia), akiuza mafuta na manukato mbalimbali katika viwanja hivyo.
Ibada ya swala ya Idd El Haji ikiendelea.
Biashara ya Balaghashia ikiendelea katika viwanja vyao.
Swala ikiendelea katika viwanja hivyo.
Pikipiki na baiskeli zikiwa zimewekwa kwa pamoja kwa ajili ya usalama.
Mwanahabari akichukua picha katika ibada hiyo.
Waumini wa kiislam wakiwa katika viwanja hivyo wakati wa ibada hiyo.
Hapa salamu zikiendelea.
Sheikh Othmani Dishi (kushoto), akisalimiana na Sheikh Abdu Kadri kabla ya kuanza kwa swala hiyo.
Swala ikifanyika katika viwanja hivyo.
Swala ikifanyika kwa unyenyekevu mkubwa.
Shirika
la Maendeleo Tarime SHIMATA chini ya ufadhiri wa Taasisi ya TWAWEZA
kupitia mradi wake wa UWEZO ambao umelenga kufanya kazi ya kutathimini
hali ya kielimu katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda linatarajia
kufanya tathimini kwa watoto (Wanafunzi na wasio wanafunzi) walio na
umri kati ya miaka saba hadi 16 katika Wilaya ya Tarime Mkoani Mara kwa
lengo la kubaini hali ya kielimu na changamoto zake ilivyo wilayani
humo.
Na:Binagi Media Group
Ili
kufanikisha zoezi hilo, SHIMATA imetoa semina kwa wahojaji watakaofanya
tathimini hiyo ambayo pia itawafikia wenyeviti wa Mitaa na Vijiji
pamoja na Wanakaya pamoja na kupima kiwango cha madini joto katika kaya
hizo.
Akifunga
semina hiyo iliyoanza juzi Septemba 22,2015 na kutamatika jana Septemba
23,2015 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime, Kaimu Katibu
Tawala Wilaya ya Tarime John Marwa ambae alimwakilisha Mkuu wa Wilaya
hiyo aliwataka washiriki wa semina hiyo (wahojaji) kuhakikisha wanafanya
tathimini hiyo kwa ukweli na uwazi ili kupata majibu sahihi ya kiwango
cha elimu katika Wilaya hiyo.
Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Tarime John Marwa
Mwenyekiti wa SHIMATA Joseph Magabe akizungumza katika semina hiyo
Baada ya semina, mgeni rasmi alikabidhi vyeti vya ushiriki kwa wanasemina
Baada ya semina, mgeni rasmi alikabidhi vyeti vya ushiriki kwa wanasemina
Baada ya semina, mgeni rasmi alikabidhi vyeti vya ushiriki kwa wanasemina
Baada ya semina, mgeni rasmi alikabidhi vyeti vya ushiriki kwa wanasemina
Baada ya semina, mgeni rasmi alikabidhi vyeti vya ushiriki kwa wanasemina
Baada ya semina, mgeni rasmi alikabidhi vyeti vya ushiriki kwa wanasemina
Baada ya semina, mgeni rasmi alikabidhi vyeti vya ushiriki kwa wanasemina
Baada ya semina, mgeni rasmi alikabidhi vyeti vya ushiriki kwa wanasemina
Baada ya semina, mgeni rasmi alikabidhi vyeti vya ushiriki kwa wanasemina
Baada ya semina, mgeni rasmi alikabidhi vyeti vya ushiriki kwa wanasemina
Mratibu wa Twaweza Wilayani Tarime akipokea Cheti cha utambuzi kutoka TWAWEZA
Mwenyekiti wa SHIMATA akipokea cheti cha utambuzi kutoka TWAWEZA
Picha ya pamoja kati ya washiriki wa semina na mgeni rasmi
Picha ya pamoja kati ya washiriki wa semina na mgeni rasmi
Viongozi na Wajumbe wa SHIMATA
No comments:
Post a Comment