Baba Mtakatifu Papa Francis akiwa katika mapokezi chini ya Rais Obama na familia yake
Kwa kawaida marais wa Marekani huwapokea
wageni rasmi Ikulu ya nchi hiyo, lakini alipowasili kwenye uwanja wa
ndege wa Kijeshi wa Andrews ulioko nje kidogo ya jiji la Washington,
Baba Mtakatifu alipata heshima ya kulakiwa na Rais Obama na familia
yake.
Mbali na gwaride la heshima, miongoni
mwa waliokuweko kwenye mapokezi hayo rasmi ni pamoja na Makamo wa Rais
wa Marekani Bwana Joe Biden na aila yake, watoto wa shule, na viongozi
wa Kanisa Katoliki.
Akiwa jijini Washington, Baba Francis
atafanya mazungumzo na Rais Obama, kukhutubia kikao cha pamoja cha
Mabaraza ya Bunge la Marekani pamoja na kuongoza Ibada mbalimbali.
Ziara yake hiyo ya siku sita, pia itamfikisha kwenye miji ya New York na Philladelphia.
Akiwa jijini New York, Baba Francis
ambaye ni kiongozi wa nne wa Vatican kuitembelea Marekani, atatembelea
Umoja Wa Mataifa na eneo la Kituo Cha Biashara kiclichoteketezwa kwenye
mashamulizi ya Septemba 11, 2001.
Kiongozi huyo wa Kanisa la Katoliki,
atamalizia ziara yake katika jiji la Philladelphia, ambako anatarajiwa
kuhudhuria kwenye Mkutano wa Familia wa Wakatoliki Duniani.
Miongoni mwa mambo yatakayopewa
kipaumbele katika mzungumzo na khotuba zake nchini humu, ni pamoja na
utoaji mimba, ndoa za jinsia moja, usawa katika maswala ya kiuchumi na
kijamii, mazingira na uhamiaji.
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi
CCM Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi katika mkutano wake
wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa shule ya Msingi Kalangalala
mjini Geita leo na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi.
Mgombea
Urais Huyo amewaambia wananchi wa Geita kuwa mara atakapoingia Ikulu,
moja ya changamoto anazotarajiwa kuzipa kipaumbele ni pamoja na suala la
kutatua mgogoro wa wachimbaji madini wadogo wadogo.
Magufuli
ameasema kuwa akiingia madarakani atawapa maeneo wachimbaji wadogo wa
madini nchini ikiwa ni pamoja na kuwakopesha mitaji na kuwapa vifaa vya
kisasa vya kufanyia kazi zao pamoja na mafunzo kwa ajili ya kuboresha
uchimabaji wao ili uwe wa kisasa zaidi na kupandisha kiwango
cha ufanisi wa kazi zao za uchimbaji.
Dkt.
Magufuli leo amehutubia mikutano katika miji ya Runzewe wilayani
Bukombe, Katoro wilayani Chato na Geita mjini akiendelea na kampeni zake
za kwaomba wananchi kumpa kura za ndiyo ili aweze kuingia Ikulu na
kuwafanyia kazi Watanzania kama kiongozi na Amiri Jeshi mkuu wa
Tanzania.
Sehemu
ya umati wa wakazi wa Geita na vitongoji vyake wakiwe kwenye mkutano wa
kampeni wa Dkt John Pombe Magufuli uliofanyika jioni ya leo mjini humo. PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-GEITA
Wananchi
wa mji wa Geita na vitongoji vyake wakiwa wamefurika kwenye uwanja wa
shule ya msingi ya Kalangalala,wakimsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania,kupitia chama cha Mapinduzi CCM Dkt John Pombe
Magufuli alipokuwa akijinadi na kumwaga sera zake mbele za wananchi hao
ikiwemo pia na kuwaomba ridhaa ya kuwa Rais kwa kushinda kura nyingi
ifikapo Oktoba 25 mwaka huu,ambapo uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika
Mgombea
Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwandani Wagombea Ubunge wa
jimbo la Busanda Mh.Lolensia Bukwimba na Dkt Meedad wa Chato mapema
mchana huu alipokuwa akiwahutubia wananchi wa mji mdogo wa Katoro mkoani
Geita, kwenye viwanja vya mnada wa Ng'ombe,katika mkutano wa hadhara wa
kampeni,ambapo maelfu ya Wananchi wamehudhuria.Dkt Magufuli atahutubia
jioni ya leo mjini Geita kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
Mgombea
Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa mji mdogo
wa Katoro mkoani Geita mapema leo mchana kwenye viwanja vya mnada wa
Ng'ombe,kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni,ambapo maelfu ya Wananchi
wamehudhuria.
Wananchi
wa Runzewe wilaya ya Mbongwe mkoani Geita wakimsikiliza kwa makini
Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akizinadi sera
zake na kuwaomba ridhaa ya kuiongoza Tanzania katika kipindi cha awamu
ya tano,kwenye viwanja vya mnada wa Ng'ombe,katika mkutano wa hadhara wa
kampeni,ambapo maelfu ya Wananchi wamehudhuria.
Wananchi wa Runzewe wakimsikiliza Dkt Magufuli alipokuwa akihutubia kwenye mkutano wa kampeni
Wananchi
wa Runzewe wakimshangilia Dkt Magufuli alipokuwa akijinadi na kuomba
kurra za ushindi ili aweze kuwa Rais wa Tanzania katika awamu ya tano
Wakiwa na mabango yao wakishangilia ujio wa Magufuli
Wananchi
wa Runzewe wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa
akijinadi na kuomba kurra za ushindi ili aweze kuwa Rais wa Tanzania
katika awamu ya tano.
Magufuli Style ilitikisa pia ndani ya Geita kwenye mkutano wa kampeni wa Dkt John Pombe Magufuli jioni ya leo
Mgombea
Urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi
CCM Dkt. John Pombe Magufuli akikumbatiana kwa furaha na kijana mlemavu
wa ngozi Albino Lazaro Malendeka ambaye alikuwa mtumishi wa kikundi cha
Red Briged cha Chadema baada ya kujiunga na CCM mjini Geita leo.
Mgombea
Urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi
CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwapokea mlemavu wa ngozi Albino Lazaro
Malendeka kushoto ambaye alikuwa mtumishi wa kikundi cha Red Briged cha
Chadema baada ya kujiunga na CCM mjini Geita leo na William Mabula
Msalaba aliyekuwa mgombea ubunge wa Chadema jimbo la Geita.
Mgombea
Urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi
CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwanadi wagembea ubunge wa mkoa wa Geita
katika mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Geita leo.
Wananchi wa Katoro wakiushangilia msafara wa Dkt Magufuli alipokuwa akielekea kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
Msafara wa Mgombea Urais ukielekea kwenye mkutano wa hadhara ndani ya mji Mdogo wa katoro mkoani Geita.
Nyomi
Mgombea
Urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi
CCM Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Geita Mama
Fatma Mwasa,pichani kati ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza na Mjumbe wa kamati ya ushindi ya CCM mjini Geita wakati wa mkutano wa kampeni leo
Wakazi wa Geita wakishangilia jambo kwenye mkutano huo wa kampeni.
Wananchi wa Geita mjini wakifuatilia mkutano wa kampeni
Mwenyekiti
wa CCM mkoa wa Geita na mgombea ubunge wa jimbo la Geita vijijini Ndugu
Joseph Kasheku a.k.a King Msukuma akihutubia malefu ya wananchi wa
Geita mjini kwenye mkutano wa kampeni wa Urais,ambapo Ndugu Joseph
aliwaomba wakazi wa Geita na vitongoji vyake kumchagua Dkt John Pombe
Magufuli awe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika awamu ya
tano,katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 25 mwaka.
Mgombea
Ubunge wa jimbo la Shinyanga mjini Ndugu Steven Masele akimwombea kura
Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli kwa wakazi wa Geita
Nyomi la watu likishangilia
Wananchi wa Geita mjini wakimsikiliza Dkt Magufuli alipokuwa akiwahutubia jioni ya leo kwenye mkutano wa kampeni.
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha
Mapinduzi Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wa
Nyakahura,wilaya ya Biharamulo alipokuwa akielekea mkoani Gieta
kuendelea na kampeni zake.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Victoria
Mwakasege, ofisini kwake jijini Dar es salaam Septemba 23, 2015. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na
Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Victoria Mwakasege kabla ya mazunguzo yao
ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Septemba 23, 2015
Balozi wa China nchini Tanzania Bw. Lu
Youqing (wa pili kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Utangazaji Tanzania (TBC- wa kwanza kulia), Bw. Clement Mshana pamoja na
Makamu wa Rais wa Makampuni ya StarTimes, Bi. Guo Ziqi (wa kwanza
kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vyombo vya Habari,
Uchapishaji, Redio, Filamu na Luninga, Bi. Yang Peili (wa pili kulia)
wakifurahia zawadi za vitambaa vilivyonakshiwa na wabunifu wa Tanzania
wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Filamu na Tamthiliya za Beijing
kupitia kwenye Luninga ya mwaka 2015. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar
es Salaam mwishoni mwa wiki ikiwa ni jitihada za kukuza filamu pamoja
na uhusiano wa kiutamaduni baina ya nchi hizo mbili.
Makamu wa Rais wa Makampuni ya
StarTimes, Bi. Guo Ziqi (kushoto) akipokea zawadi ya kinyago
kilichochongwa na wasanii wa Tanzania kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa
Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC- wa kwanza kulia) Bw. Clement Mshana
wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Filamu na Tamthiliya za Beijing
kupitia kwenye Luninga ya mwaka 2015. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar
es Salaam mwishoni mwa wiki ikiwa ni jitihada za kukuza filamu pamoja
na uhusiano wa kiutamaduni baina ya nchi hizo mbili.
Balozi wa China nchini Tanzania Bw. Lu
Youqing (katikati) akifurahia jambo na Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa
Kampuni ya StarTimes Tanzania, Bw. Lanfang Liao (kulia) wakati wa
uzinduzi wa Maonyesho ya Filamu na Tamthiliya za Beijing kupitia kwenye
Luninga ya mwaka 2015. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam
mwishoni mwa wiki ikiwa ni jitihada za kukuza filamu pamoja na uhusiano
wa kiutamaduni baina ya nchi hizo mbili.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC- wa kwanza kulia) Bw. Clement Mshana (kulia), akikabidhiwa zawadi ya kinyago.
Hapa ni furaha tupu katika uzinduzi huo.
Waigizaji wa filamu ya’The Young Doctor’
Zhang Yi na Zhou Fang wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi wa
Maonyesho ya Filamu na Tamthiliya za Beijing kupitia kwenye Luninga ya
mwaka 2015. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa
wiki ikiwa ni jitihada za kukuza filamu pamoja na uhusiano wa
kiutamaduni baina ya nchi hizo mbili.
Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI ya StarTimes
Tanzania kwa kushirikiana na Mamlaka ya Vyombo vya Habari, Uchapishaji,
Redio, Filamu na Luninga ya Beijing wamezindua maonyesho ya mfululizo wa
filamu na tamthiliya mwaka 2015 ambayo yatajumuisha filamu na
tamthiliya za kusisimua za kichina barani Afrika.
Kuendelea kwa kukua kwa
muingiliano wa tamaduni baina ya watu wa Tanzania na China kumefanya
filamu na tamthiliya za China kwenye luninga zijizolee umaarufu mkubwa
na kuwa kichocheo kikubwa katika kukuza mahusiano baina ya nchi hizi
mbili.
Akizungumza na waandishi
wa habari wakati wa uzinduzi huo Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vyombo
vya Habari, Uchapishaji, Redio, Filamu na Luninga, Bi. Yang Peili
amebainisha kuwa Tanzania itabaki kuwa mshirika wake mkubwa na
wataendelea kuimarisha mahusiano yao ya kitamaduni kupitia matangazo ya
maudhui ambayo yana nafasi ya kipekee kuwafikia watu wengi zaidi.
”Maonyesho haya ambayo
kwa kawaida yatakuwa ni ya filamu na tamthiliya kutoka Beijing kwa kiasi
kikubwa yataonyeshwa nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla. Kwa
makadirio, jumla ya filamu na tamthiliya 30 za kwenye luninga
zitaonyeshwa nchini Tanzania na nchi nyingine za Afrika. Dhumuni kuu ni
kuimarisha muunganiko wa maingiliano ya kiutamaduni baina ya marafiki
zetu wa Afrika na watu wa China.” Alisema Bi. Peili
Mamlaka ya Vyombo vya
Habari, Uchapishaji, Redio, Filamu na Luninga itatoa fursa ya kipekee
kwa watazamaji wa barani Afrika kama vile Tanzania, Kenya na Afrika ya
Kusini kukutana na washiriki maarufu wa filamu ya ‘The Young Doctor’.
Pia wakurugenzi wa mamlaka hiyo watakuwa na wasaa wa kuzungumza na
kuyahoji makampuni ya kimataifa ya uzalishaji wa vipindi barani Afrika
kwa nchi hizo tatu.
Katika miaka ya hivi
karibuni tumeshuhudia ukuaji wa kasi wa tasnia ya filamu na tamthiliya
kwenye luninga na kunufaisha maisha ya watu huku masoko ya tasnia hizo
kwa nyumbani yakijulikana kimataifa na kuwa kiungo muhimu katika kukuza
muingiliano wa kiutamaduni baina ya nchi husika.
Kama sehemu ya chombo
cha uzinduzi wa Maonyesho ya Filamu na Tamthiliya za Beijing kupitia
kwenye Luninga ya mwaka 2015, sherehe za uzinduzi zitafanyika nchini
Afrika ya Kusini ambapo zitahudhuriwa na mamlaka ya bodi hiyo ya
Beijing.
“Maonyesho haya
yanafuatilia tukio kama hili ambalo lilifanyika mwaka jana na kuandaliwa
na Mamlaka ya Vyombo vya Habari, Uchapishaji, Redio, Filamu na Luninga
ambapo Mr. Guo Jinlong, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Mamlaka ya Kisiasa ya
CPC na Katibu wa Kamati ya Mamlaka ya Beijing alihudhuria sherehe ya
aina yake alipotembelea nchini Tanzania,” alisema Bi. Peili na
kumalizia, “Tamthiliya hizi za Kiingereza za kwenye luninga kama
zinavyojulikana miongoni mwa watazamaji wengi zimejizolea umaarufu
mkubwa burudani inayopendwa katika nchi nyingi za kiafrika na tunaamini
kwa pamoja tunaweza kuziunga mkono tasnia za uzalishaji wa vipindi za
nyumbani katika nchi husika ili kuweza kunufaika zaidi kwa pande zote
mbili.”
Uzinduzi wa Maonyesho ya
Filamu na Tamthiliya za Beijing kupitia kwenye Luninga ya mwaka 2015
utajumuisha vipindi vya luninga maarufu na filamu kama vile ‘The Young Doctor’, ‘The Sweet Burden’, ‘The Mi Family’s Marriage’, ‘Ordinary World’, ‘Love is Not Blind’, ’20 Once Again’, ‘A Wedding Invitation’, na ‘The Left Ear’ambazo zimepangwa kuonyeshwa nchini Tanzania ndani ya kipindi cha mwaka mzima.
Shughuli za kukuza
maonyesho haya katika nchi zingine za barani Afrika zikiwemo Kenya na
Afrika ya Kusini zitafuatia kulingana na kampuni ya matangazo ya
dijitali ya StarTimes ambayo ina mpango wa kuzionyesha kupitia katika
ving’amuzi vyao vya antenna na madishi, na kwa uhakika itasaidia kwa
kiasi kikubwa itasaidia kukuza utamaduni wa China barani Afrika.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu
Dkt. Albina Chuwa akijibu baadhi ya maswali kutoka kwa wadau wakati wa kikao
cha kujadili rasimu ya Mkakati wa Usajili na Uhifadhi wa Takwimu za Matukio
Muhimu ya Binadamu katika ukumbi wa hoteli ya New Africa, Dar es Salaam leo Septemba 23, 2015
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Maimuna Tarishi (katikati) akiwa katika
picha ya pamoja na wadau mbalimbali baada ya kufunga kikao cha kujadili rasimu
ya Mkakati wa Usajili na Uhifadhi wa Takwimu za Matukio Muhimu ya Binadamu
katika ukumbi wa hoteli ya New Africa, Dar es Salaam.
Na Veronica Kazimoto wa MAELEZO
Usajili
wa Raia una jukumu la msingi katika kutekeleza matakwa ya utawala bora na
maendeleo ya kiuchumi katika taifa lolote lile duniani.
Hayo
yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Sheria na Katiba Maimuna Tarishi wakati
akifungua mkutano wa wadau wa kujadili Rasimu ya Mkakati wa Usajili na Uhifadhi
wa Takwimu za Matukio Muhimu ya Binadamu uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Tarishi
amesema Usajili wa Raia ni wajibu wa kisheria kwa kuwa unasaidia katika
upangaji wa mipango madhubuti ya maendeleo pamoja na kuiletea maendeleo jamiii
kulingana na Mkakati wa Kuondoa Umaskini na Kukuza Uchumi Tanzania (KUKUTA II).
Katibu
Mkuu huyo wa Wizara ya Katiba na Sheria amebainisha kuwa mfumo wa Usajili wa
Raia uliopo sasa Tanzania Bara umekuwa ukifanya kazi kwa kusuasua na hivyo
kusababisha baadhi ya wananchi kutotambulika katika kumbukumbu rasmi za
kiutawala.
“Kwa
mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi iliyofanyika mwaka 2012, ni asilimia 15 tu ya
watanzania ndio waliosajiliwa na kupata vyeti, hali inayowaacha wengi pasipo
kutambulika popote katika kumbukumbu rasmi za kiutawala,” amesema Tarishi.
Ameongeza
kuwa usajili ya vifo ndio uko katika hali mbaya zaidi ambapo ni matukio
machache ya vifo yanayoandikishwa na sababu za vifo hivyo hazibainishwi kwa
usahihi au hazibainishwi kabisa hali inayosababisha ugumu katika kutekeleza
majuku kwa upande wa sekta ya afya nchini.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa
ambaye ofisi yake ni mdau muhimu wa mfumo huu, amesema lengo la mkakati huu ni
kuanzisha mfumo wa Usajili wa Raia ambao unakidhi vigezo vya kimataifa ambao ni
wa kudumu na unaofikia watu wote katika kusajili matukio muhimu ya binadamu na
kuzalisha takwimu za matukio hayo katika namna ambayo ni endelevu na ya
kuaminika.
Dkt.
Chuwa amesema mfumo huu wa Usajili wa Raia ukikamilika utasaidia kupata huduma
zote za usajili katika sehemu moja kwa vituo vyote vya usajili nchini.
Nae
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili, Udhamini na Ufilisi (RITA) Emmy
Hudson amesema mfumo uliopo sasa uko mbali na wananchi walio wengi hasa wa
maeneo ya vijijini kwasababu ngazi ya chini ya usajili ni ofisi ya Katibu Tawala wa Wilaya.
Changamoto
hii na nyingine inasababisha huduma hii ya usajili kutofika kwa urahisi kwa
wananchi walio wengi hali ambayo inaleta uhitaji wa mabadiliko ambayo ili
tufanikiwe, RITA inahitaji peke yake haitamudu kuzikabili changamoto za mfumo
pasipo kuhusisha wadau mbalimbali katika kuboresha mfumo huu.
Usajili
wa Raia ulianzishwa na sheria ya kikoloni mnamo mwaka 1917. Kwa mujibu wa
sheria hiyo usajili ulikuwa ni lazima kwa wakazi wa Tanganyika na baada ya
uhuru, sheria hii ilirithiwa ambapo licha ya mabadiliko kadhaa ambayo yamekuwa
yakifanyika bado wananchi wamekuwa na kasumba ya kutokuona umuhimu wa Usajili
wa Raia nchini.
Mtakwimu Mkuu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu
Emilian Karugendo, akifafanua jambo wakati wa uwasilishaji wa mada iliyohusiana
na hatua za kuandaa Mkakati wa Usajili na Uhifadhi wa Takwimu za Matukio Muhimu
ya Binadamu wakati wa kikao cha wadau kilichofanyika katika ukumbi wa hoteli ya
New Africa, Dar es Salaam
Meneja
wa Usajili kutoka RITA Angela Anatory akiwasilisha rasimu ya Mkakati wa Usajili
na Uhifadhi wa Takwimu za Matukio Muhimu ya Binadamu katika kikao cha wadau
kilichofanyika katika ukumbi wa hoteli ya New Africa, Dar es Salaam.
Mwakilishi
wa Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO) Dkt. RufaroChatora akiongea kwa
niaba ya wawakilishi wengine wa mashirika ya Umoja wa Mataifa waliohudhuria
kikao cha wadau wa Usajili na Uhifadhi wa Takwimu za Matukio Muhimu ya Binadamu
katika ukumbi wa hoteli ya New Africa, Dar es Salaam.
Picha ya pamoja
Waziri
Mkuu wa zamani, Fredrick Sumaye, akionyesha kadi za wananchama 3000 wa Chama cha Mpinduzi(CCM)waliohamia
Chadema katika mkutano wa kampeni wa
Mgombea Urais wa anayeungwa mkono na Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa, (kulia), katika Jimbo la Mtama mkoani Mtwara leo
Jumatano Septemba 23, 2015
Mgombea
Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),
Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia Wananchi, katika Mkutano wa Kampeni
uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Pilipili,Lindi Mjini , leo
Septemba 23, 2015. (Picha na Othman Michuzi na Fidelis Felix).
Mfuasi wa CCM, akifurahia jambo wakati wa mkutano huo
Mgombea Urais wa anayeungwa mkono na Vyama
vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa),Edward Lowassa akiwa amekaa
kwenye kiti maalumu alichopewa kama zawadi
katika mkutano wa kampeni kwenye
jimbo la Mtama mkoani Mtwara
Wananchi wa Jimbo la Mtama, Mkoani Lindi
wakifatilia Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika
kwenye Uwanja wa Soko la Majengo, leo Septemba 23, 2015
Waziri Mkuu wa zamani, Fredrick Sumaye,
akihutubia wananchi katika mkutano wa kampeni
wa Mgombea Urais wa anayeungwa mkono na Vyama vinavyounda Umoja wa
Katiba ya Wananchi (Ukawa),Edward Lowassa(kulia) katika Jimbo la Mtama mkoani
Mtwara
Wabunge wa
jimbo la Mtama mkoani Mtwara, Isihaka Mchinjita (CUF) na Seleman
Luongo(chadema) kulia wakijinadi mbele ya mgombea Urais wa Ukawa, Edward
Lowassa
Umati
wa Wananchi wa Lindi Mjini, wakiwa katika Mkutano wa Kampeni za Mgombea
Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya
Msingi Pilipili, Mkoani Lindi leo Septemba 23, 2015.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI, LINDI.
Mgombea
Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia Wananchi, katika Mkutano wa
Kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Pilipili,Lindi
Mjini, leo Septemba 23, 2015.
Mgombea
Ubunge wa Jimbo la Lindi Mjini kwa tiketi ya Chama cha Wananchi CUF
kupitia Mwamvuli wa UKAWA, Salum Barwany, akimueleza Mgombea Urais wa
Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),
Mh. Edward Lowassa, changamoto mbalimbali za wananchi wa Lindi, katika
Mkutano wa Kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi
Pilipili,Lindi Mjini, leo Septemba 23, 2015.
Mgombea
Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Lindi
Mjini kwa tiketi ya Chama cha Wananchi CUF kupitia Mwamvuli wa UKAWA,
Salum Barwany, katika Mkutano wa Kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa
Shule ya Msingi Pilipili,Lindi Mjini, leo Septemba 23, 2015.
Mgombea
Ubunge wa Jimbo la Lindi Mjini kwa tiketi ya Chama cha Wananchi CUF
kupitia Mwamvuli wa UKAWA, Salum Barwany, akiwahutubia Wananchi wa Jimbo
lake hilo, katika Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa
UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward
Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Pilipili,Lindi
Mjini, leo Septemba 23, 2015.
Sehemu
ya Wananchi wa Jimbo la Lindi Mjini, wakimshangilia Mgombea Ubunge wao,
Salum Barwany, alipokuwa akihutubia na kukonga nyoyo zao kwa kugusa
moja kwa moja changamoto zinazowakabili na namna watakavyoweza kuzitatua
iwapo watapata ridhaa ya uongozi.
Mgombea
Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akifurahi jambo na Mgombea Ubunge wa
Jimbo la Lindi Mjini kwa tiketi ya Chama cha Wananchi CUF kupitia
Mwamvuli wa UKAWA, Salum Barwany.
Uwanja wa Pilipili ulikuwa ni shangwe tupu, muda wote wa Mkutano.
Waziri
Mkuu wa zamani, Mh. Fredrick Sumaye, akiwahutubia wananchi wa Jimbo la
Lindi Mjini, kabla ya kumkaribisha Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA
kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa,
katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi
Pilipili,Lindi Mjini, leo Septemba 23, 2015.
Sehemu
ya Wananchi wa Jimbo la Lindi Mjini, wakiwa katika Mkutano wa Kampeni
za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa
Shule ya Msingi Pilipili,Lindi Mjini, leo Septemba 23, 2015.
Wananchi
wa Jimbo la Mtama, Mkoani Lindi wakionyesha furaha yao kwa ujio wa
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, katika Mkutano wa Kampeni
uliofanyika kwenye Uwanja wa Soko la Majengo, leo Septemba 23, 2015.
Vinaja
wa Jimbo la Mtama Mkoani Lindi wakiishangilia Chopa anayoitumia Mgombea
Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, kawati ikiwasili kwenye eneo la Mkutano
uliofanyika kwenye Uwanja wa Soko la Majengo, leo Septemba 23, 2015.
Pipozzzzzzz........ Pawaaaaa......
Mgombea
Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia Wananchi wa Jimbo la Mtama,
Mkoani Lindi, katika Mkutano wa Kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa
Soko la Majengo, leo Septemba 23, 2015.
Wananchi
wa Jimbo la Mtama, Mkoani Lindi wakifatilia Mkutano wa Kampeni za
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa
Soko la Majengo, leo Septemba 23, 2015.
kadi
za wanancha wa CCM zaidi ya elfu tatu (3000) wa Jimbo la Mtama, Mkoani
Lindi walioamua kuunga mkono mabadiliko ya UKAWA, zikiwekwa kwenye
kiroba baada ya kukabidhiwa.
Mgombea
Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Waziri Mkuu wa zamani, Mh. Fredrick
Sumaye wakionyesha kwa wananchi wa Jimbo la Mtama, Mkoani Lindi, lundo
la kadi za wanancha wa CCM zaidi ya elfu tatu (3000) walioamua kuunga
mkono mabadiliko ya UKAWA, wakati wa Mkutano wa Kampeni za Mgombea huyo,
uliofanyika kwenye Uwanja wa Soko la Majengo, Mtama leo Septemba 23,
2015.
No comments:
Post a Comment