Majengo
pacha yenye ghorofa 35 kila moja yaliyojengwa na mfuko wa pensheni wa hifadhi
ya jamii PSPF kama mojawapo ya vitega uchumi kwa kuwekeza kwa malengo ya
kulinda thamani ya michango ya wanachama, kupata fedha za uendeshaji wa
shughuli za mfuko, kuboresha mafao kwa wanachama na kuchangia juhudi za
serikali katika kuinuia uchumi wa nchi.
Na Christian Gaya Mwananchi alhamisi Septemba 24,2015
Wiki iliyopita tuliona baadhi ya changamoto
zinazoikabili mifumo ya mifuko ya pensheni ya hifadhi ya jamii hapa nchini. Na
kwamba mifuko hii ya hifadhi ya jamii mara nyingi imekuwa ikiwekeza kwenye
rasilimali ambazo haziwezi kuleta ongezeko bora zaidi, kama vile kwenye ujenzi
wa nyumba kwa malengo yanayoyajua wao wenyewe. Na uwekezaji umekuwa ukitolewa
kisiasa na siyo kiuakinifu wa miradi.
Kwa wakati fulani imesikika
kutoka katika vyombo vya habari mbalimbali ya kwamba kumekuwepo na gharama
kubwa zaidi kwa ajili ya kuendesha baadhi ya mifuko ya pensheni ya hifadhi ya
jamii na ukosefu wa vipingamizi vya matumizi ya utawala na hii imechangia
kupungua kwa fedha za akiba au limbiko la mfuko kwa ajili ya majanga na afya na
ustawi wa mfuko kwa hatarishi za sasa na siku za usoni
Ukija kwa upande wa
utoaji wa huduma bora kwa wateja ni sehemu ambayo imesababisha kutoridhika kwa
wanachama wengi na wadau wengine wa mifuko hii ya pensheni ya hifadhi ya jamii.
Na mara nyingi
malalamiko haya yamehusisha kwa mafao kidogo yanayotolewa kwa wanachama hasa
wastaafu, kuchelewesha kulipa mafao ya muda mfupi kwa wakati muafaka, kukosa
taarifa au kumbukumbu muhimu za wakati muafaka zinazohusu mfuko wa pensheni na
idadi ya michango iliyochangwa na wanachama na, kiasi cha pensheni na mafao
anayotakiwa kulipwa mwanachama au mrithi yaani maelezo ya akaunti ya mwanachama
ya uhakika yaani muamala. Mara nyingi kumbukumbu za michango zimekuwa
hazijakamilika na wala hazijawekwa kwenye kompyuta na pensheni kutokwenda na
mfumko wa gharama ya bei wakati huo inapolipwa.
Kwa upande wa chanya,
matumizi ya teknolojia ya habari na masiwasiliano na kampeni za uhamasishaji wa
umma juu ya mifuko ya pensheni ya hifadhi ya jamii inachangia sana katika kutoa
huduma za kijamii
Taratibu na kanuni za
mifuko ya pensheni ya hifadhi ya jamii zingeliweza kuchangia kiasi kikubwa
katika kulazimisha taasisi hizi za hifadhi ya jamii kufanya kazi kulingana na
viwango vinavyotakiwa na hivyo kujenga uaminifu wa taasisi hizi kwa wanachama
na wadau wengine wa sekta ya hifadhi ya jamii
Kanuni za mazingira ya
taasisi za umma na watu binafsi ni za muhimu sana katika kuongeza ukweli na
uwazi na kuwalinda wanachama na wadau wa mifuko hii ya hifadhi ya jamii. Pamoja
na hayo, kuna uzoefu mdogo sana wa mifuko ya pensheni ya hifadhi ya juu ya jambo
la uwazi na ukweli hapa nchini.
Kwa kawaida mifuko ya
pensheni ya hifadhi ya jamii imeshikiliwa na sheria na kuangaliwa na wizara
mama kama vile wizara ya fedha, wizara ya serikali za mitaa na wizara ya kazi
na ajira kama wizara mama ingawa zinatakiwa kuangaliwa na wizara moja kama vile
wizara ya kazi na ajira na kusimamiwa na kudhibitiwa na wakala wa serikali
kuhusiana na masuala yote ya sekta ya hifadhi ya jamii. Pamoja na hayo kuna
ongezeko wa mifano ya chambo cha usimamizi na mdhibiti kama vile mdhibiti na
msimamizi wa mifuko ya pensheni ya hifadhi ya jamii Tanzania (SSRA)
Pamoja na haya yote,
kuna vitu vingine vya msingi ambavyo vinatakiwa kufikiriwa ambavyo ni muhimu na
ambavyo vitachangia kuunda muundo wa mfumo wa kisasa na vinavyoweza kukubalika na
wanachama na wadau wengine wa sekta ya hifadhi ya jamii
Fikirio la kwanza
linahusiana na mahitaji ya kuwa na mfumo wa pensheni wa hifadhi ya jamii
unaohusisha pamoja kazi zisizo rasmi, hifadhi ya jamii isiyo rasmi, na kukinga
hatarishi zote kama vile mfumuko wa bei, kiwango cha riba ya uwekezaji, uzee, magonjwa, miaka
ya kuishi, kiwango cha kodi, ulemavu, msongo wa mawazo na mfumo wa hifadhi ya
jamii unaotekeleza kwa muda muafaka mahitaji yayohitajika kwa sasa na mlengwa
kwa haraka kinyume na kukinga majanga ya baadaye au mambo mengine ya hatarishi
au majanga, unahitajika mfumo wa hifadhi ya jamii unaojumuisha pamoja familia
zaidi ya moja na bila kuwepo mfumo dume.
Na jambo la pili
linalogusa na linalosababisha kuwagusa sana wachangiaji wa mifuko ya pensheni
ya hifadhi ya jamii ni pale wanapokuwa wanapoteza uanachama na kinga yao ya
hifadhi ya jamii pale wanaondoka au kuhamia mfuko mwingine wa pensheni ya
hifadhi ya jamii wakiwa ndani ya nchi na akivuka mpaka na kwenda nchi nyingine.
Christian Gaya
ni mwanzilishi wa kituo cha HakiPensheni Tanzania, mshauri na mtaalamu wa
masuala ya pensheni. Kwa maelezo zaidi wasiliana kwa barua pepe: gayagmc@yahoo.com na kwa habari zaidi za
kila siku juu ya HakiPensheni unaweza kutembelea tovuti www.hakipensheni simu namba +255 655 13 13 41
No comments:
Post a Comment