Pages

Wednesday, June 3, 2015

Mfuko wa Pensheni wa PSPF Wakabidhi Msaada kwa Wananchi wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar.


Mfuko wa Pensheni wa PSPF Wakabidhi Msaada kwa Wananchi wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar.


 Ofisa wa Mfuko wa Pensheni PSPF Tawi la Zanzibar Hazina Konde akimkabidhi msaada wa Magogoro Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Mhe Ame Perera kwa ajili ya Wananchi waliopata maafa yamvua na kuharibikiwa na mali zao, makabidhiano hayo yamefanyika katika viwanja vya skuli ya mabanda ya ngome chumbini Zanzibar.
 OFISA wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF Tawi la Zanzibar Hazina Konde akitowa maelezo kwa niaba ya
Mkufugenzi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi
msaada wa Magodoro kwa wananchi wa Jimbo la Chumbuni waliopata janga la mvua za
masika katika shehia tatu za jimbo hilo, Chumbuni. Karakana na Muembemakumbi
Zanzibar.
Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Mhe Perera Ame Silima akitowa shukrani kwa
uongozi wa Mfuko wa PSPF kwa msaada wao kwa Wananchi wa Jimbo lake wakati wa
makabidhiano hayo yaliofanyika katika viwanja vya skuli ya mabanda ya ngombe
chumbuni Zanzibar.Mhe Mbunge akiishukuru PSPF kwa kutumia sehemu ya pato lake
kwa kusaidia Jamii.
Sheha wa Shehia ya Karakana Ndg Bakari Makame akitowa shukrani kwa niaba ya
wananchi wake kwa Msaada wa Magodoro yaliotolewa na Mfuko wa PSPF kwa kujali
wananchi wakati wa maafa
  na kutowa
shukara hizo kwa Uongiozi huo wakati wa makabidhiano ya msaada huo yaliofanyika
katika viwanja vya Skuli ya Mabanda ya Ngome Chumbuni Zanzibar.
  WANANCHI wa Shehia tatu za Jimbo la Chumbuni Zanzibar
wakimsikiliza Ofisa wa Mfuko wa PSPF Tawi la Zanzibar Bi Zahazia Konde akitowa
maelezo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mfuko huo kwa wananchi wa Jimbo la Chum,buni
Zanzibar wakati wa kutowa msaada wa magodoro kwa wananchi waliopata maafa ya
mvua hivi karibuni.
Wananchi wa Shehia tatu za Jimbo la Chumbuni Zanzibar
wakimsikiliza Ofisa wa Mfuko wa PSPF Tawi la Zanzibar Bi Zahazia Konde akitowa
maelezo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mfuko huo kwa wananchi wa Jimbo la Chum,buni
Zanzibar wakati wa kutowa msaada wa magodoro kwa wananchi waliopata maafa ya
mvua hivi karibuni.

SHUGHULI MBALIMBALI ZA WAZIRI MKUU ARUSHA NA DODOMA

1
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na  Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Seif Rashid baada ya kuhudhuria sala na heshima za mwisho kwa aliyekuwa mbunge wa Ukonga, Egin Mwaiposa kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Juni 3, 2015.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
2

5
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Wakufunzi na watalaam wa mashine za kuandikisha wapiga kura za BVR wakati alipotembelea Kituo cha mafunzo ya BVR kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Juni 2, 2015.
6

Taswa FC kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya wafanyakazi wa shule ya sekondari ya Baobab ya Bagamoyo.

 2
 Mchezaji wa timu ya soka wa waandishi wa habari za michezo nchini (Taswa fc), Martin Peter (jezi ya kijani kulia) akipambana na mmoja wa wachezaji wa timu ya makipa, Ivo Mapunda.
1
kikosi cha baobab
……………………………………………………
Na Mwandishi wetu
TIMU ya soka ya waandishi wa habari za michezo nchini (Taswa FC) Ijumaa hii itacheza mchezo maalum wa kirafiki dhidi ya timu ya wafanyakazi wa shule ya sekondari ya Baobab ya Bagamoyo.
Mchezo huo umepangwa kuanza saa 10.00 jioni kwenye uwanja wa shule ya sekondari ya Baobab na tmgeni rasmi atakuwa mkurgugenzi wa shule hiyo, Hlafan Swai.
Mbali ya Swai, viongozi wengine wa shule hiyo watahudhuria mechi hiyo maalum kwa ajili ya kuhamasisha michezo shuleni hapo.
Mwenyekiti wa Taswa FC, Majuto Omary amesema kuwa awali walipanga kucheza mechi mbili, ya wanaume (mpira wa miguu) na wanawake (netiboli), hata hivyo wachezaji wa Taswa Queens hawakuweza kuanza mazoezi na hivyo kulazimika kufuta mechi hiyo.
Majuto alisema kuwa wamepokea maombi kutoka uongozi wa shule hiyo na hasa baada ya kutoa mwanafunzi bora kitaifa katika mtihani wa kidato cha nne, Nyakaho Marungu. Alisema kuwa wamehamasika kupata mwaliko huo ambapo mechi hiyo itakuwa kama sehemu ya sherehe ya kufunga shule.
Baadhi ya wachezaji wa Taswa FC wakataokuwepo katika mechi hiyo ni Ali Mkogwe, Wilbert Molandi, Salum Jaba, Deogratius “Super Deo” Maganga,  Julius Kihampa, Sweetbert Lukonge, Elius Kambili, Zahoro Mlanzi, Frank Balile, Mwarami Seif, Saidi Seif, Jose, Martin Peter, Athuman Jabir, Muhidi Sufiani na  Jabir Johnson.
Baadhi ya wachezaji wa  timu ya wafanyakazi wa shule hiyo ni John Kanakamfumu, Herry Morris (kocha wa timu ya wanafunzi), Renatus Kavishe, David Ntungi, Hadji Juma, Madata Lubigisa, Athuman Tippo na wengineo.
“Huu ni mchezo wa kudumisha ushirikiano wetu kwani sisi ni waandishi wa habari za michezo na pia ni wazazi, hivyo tunaweza kuwapeleka watoto wetu kusoma kaika shule hiyo bora, hivyo nawaomba wachezaji wote wafike kwa wingi ili kuona mechi hiyo ya aina yake,” alisema Majuto.

KONGAMANO LA KWANZA LA WANAWAKE WAFANYABIASHARA SOKONI TANZANIA LAFANYIKA JIJINI DAR LEO

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika Equality for  Growth (EfG), JaneMagigita akizungumza na waandishi wa Habari (Hawapo Pichani) wakati wa ufunguzi wa Kongamano hilo Dar es salaam leo.
Ofisa Programu Dawati la Uangalizi wa Serikali wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Hussein Sengu (kulia) akitoa mada katika Kongamano la siku mbili la Wanawake Wafanyabiashara Sokoni Tanzania lililofanyika Dar es Salaam leo. Kongamano hilo lililowahusisha wanawake kutoka mikoa tisa ya Tanzania Bara limeandaliwa na Shirika la Equality for Growth (EfG)
Mwezeshaji wa Kongamano hilo, Japhet Makongo akizungumza na Wanawake wafanyabiashara waliohudhuria Kongamano hilo.
Maofisa wa EfG, wakiwa kwenye Kongamano hilo. Kutoka kushoto ni Sarah Mambea na Brenda Kharono.
Maofisa wa EfG, wakiwa kwenye Kongamano hilo, kutoka kulia Mussa Mlawa,Susan Sitta na Munaa Abdalah.
Wafanyabiashara wanawake Masokoni wakiwa kwenye Kongano hilo.
……………………………………………………………………..
Na Dotto Mwaibale
MKURUGENZI Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti Tanzania (Repoa), Samwel Wangwe amewataka watanzania kuwawezesha wafanyabiashara wadogo wadogo hususani wanawake kwani wananafasi kubwa ya kuchangia pato la Taifa.
Akizunguza Dar es Salaam leo wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la kwanza la wanawake wafanyabiashara sokoni Tanzania, Wangwe alisema ni muhimu kuhakikisha wafanyabiashara hao wanawezeshwa na kuwajali katika uzalishaji na uendeshaji wa biashara zao.
Alisema kwa mujibu wa takwimu mbalimbali zinaonesha kuwa hali ya kiuchumi duniani katika sekta ya wafanyabiashara wadogo inaendelea kukua hivyo kutoa changamoto kubwa katika kuhakikisha inawekewa mazingira mazuri ya kisera.
“Wafanyabishara wadogo ni wengi sana hivyo wananafasi kubwa ya kuchangia pato la Taifa kutokana na uwepo wa asilimia 43 ya wajasiriamali wanawake Tanzania,” alisema Wangwe.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita, alisema  lengo la kongamano hilo ni kuwakutanisha wanawake wafanyabiashara walio sokoni kutoka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara kwa lengo la kuwajengea mshikamano na kujadili masuala muhimu yanayowahusu katika biashara zao.
Alisema kongamano hilo limehusisha wanawake 200 kutoka katika mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Mtwara, Lindi, Mara, Mbeya, Iringa, Dar es Salaam, na mkoani Tanga katika Wilaya ya Lushoto huku wakiongozwa na kauli mbiu isemayo ‘Sauti ya Mwanamke Sokoni’.
Alisema kauli hiyo inalenga kumkomboa mwanamke mfanyabiashara kwa kumjengea uwezo kutambua yeye ni nani na nafasi yake kama raia katika kuendesha shughuli biashara za shughuli za soko.
(Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com simu namba 0712-727062)

Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF lazindua jezi mpya za timu za Taifa pamoja na tovuti mpya

9
Jamal Malinzi, akisisitiza jambo wakati wa hafla hiyo.
2
Muonekano wa jezi mpya ya nyumbani.
3
Muonekano wa jezi mpya ya ugenini.
……………………………………………………
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF leo limezindua jezi mpya za timu za Taifa, zitakazokuwa zikitumika na timu za Taifa katika michuano mbali mbali itakayokua inazikabili.
Uzinduzi huo wa jezi mpya uliofanyika katika ukumbi wa Kilimanjaro jengo la Golden Jubilee uliambatana na uziduzi wa tovuti mpya ya shirikisho, uliongozwa na mgeni rasmi Mh. Said Mtanda, mbunge wa jimbo la Mchinga na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya jamii.
Katika uzinduzi huo, kulizunduliwa jezi aina tatu, ambazo ni jezi za ugenini, jezi za nyumbani na jezi zitakazokuwa zikitumika kwa ajili ya mazoezi.
Ifuatayo ni hotuba ya Rais wa TFF , Jamal Malinzi aliyoisoma wakati wa uzinduzi wa jezi mpya za timu za Taifa, uzinduzi wa tovuti mpya ya TFF na kutunuku vyeti kwa viongozi mbalimbali, makocha, wachezaji na wadhamini.
Mh Said Mtanda Mbunge wa Jimbo la Mchinga na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii
Mzee Said el Maamry Mwenyekiti Msataafu wa FAT
Ndugu Leodeger Tenga Mjumbe wa Kamati ya utendaji ya CAF na Rais mstaafu wa TFF
Ndugu wageni waalikwa
Ndugu waandishi wa habari
Mabibi na mabwana
Salam aleikum.
Nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kutufikisha hapa leo na kwa mafanikio mbali mbali ambayo tumekuwa tukiyapata.Ninakushukuru sana ndugu mgeni rasmi kwa kuacha shughuli zako kuja kujiunga nasi asubuhi hii katika shughuli hii.
Ndugu mgeni rasmi,tarehe 08 oktoba 1964 Tanzania ilipata uanachama rasmi wa shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA. TFF tuliona jambo zito kama hili hatuwezi kuliacha lipite hivi hivi.Hivyo mwaka jana tuliamua kuenzi  maadhimisho ya miaka 50 ya kujiunga na FIFA kwa kufanya mambo mambo matatu makubwa.
La kwanza ni kutoa vyeti maalum kwa watu binafsi na taasisi mbali mbali kwa kutambua mchango wao uliotukuka katika kuendeleza mpira wa miguu Tanzania.
Leo hii ndugu mgeni rasmi tutakuomba ukabidhi vyeti hivi kwa wawakilishi wa makundi kadhaa kwa niaba ya wenzao.Makundi haya ni pamoja na viongozi wa kitaifa wastaafu,mawaziri wa michezo wastaafu,viongozi waliopita wa TFF?
FAT,wakurugenzi wa idara ya michezo,wenyeviti na makatibu wa baraza la michezo la taifa,Timuya Taifa iliyocheza fainali za Afrika mwaka 1980,waamuzi,makocha,wachezaji wa timu ya Taifa na watangazaji mahiri wa michezo.Jumla tumetunuku vyeti 194. 
Kiuhalisia idadi hii ni ndogo sana ukilinganisha na wingi na uzito wa michango ya wadau mbali mbali wa mpira katika miaka 50 iliyopita. 
Tunaomba Watanzania wenzetu watuelewe katika hili kuwa hawa tutakaowatunuku vyeti hivi ni wawakalilisha wa wadau wote wa mpira Tanzania. 
Ninaomba tusimame kwa muda mfupi tuwaombe ewadau wenzetu na viongozi wa mpira wa miguu ambao wako katika orodha hii na wametangulia mbele ya haki. 
Ndugu mgeni rasmi katika kuenzi miaka 50 ya Tanzania kujiunga na FIFA leo hii pia tutatoa mchango wa fedha kwa makundi yenye mahitaji katika jamii. 
Pesa hizi zinatokana na makusanyo mbali mbali ikiwemo makusanyo ya mechi ya ngao ya hisani ifanyikayo kila mwaka. Makundi haya ni pamoja na walemavu wa viuongo,walemavu wa ngozi na wasioona. 
Kitendo hii ni moja ya juhudi za TFF kurudisha katika jamii kile tunachokusanya. Kila kundi litapewa shilingi milioni tano na tunaendelea kupokea maombi toka makundi mbali ya kijamii na tukiyapitisha tutaendelea kugawa fedha hizi.
Jambo la tatu tutakalolifanya leo litakuwa ni kuzindua rasmi tovuti mpya ya TFF (www.tff.or.tz). Tumeamua kufanya jamabo hili katika kuenzi miaka hamsini ya kujiunga na FIFA ili kutoa msisitizo kuwa sasa TFF na sisi tunajiunga Na kuendeleza mpira kisasa kulingana na teknolojia iliyopo. 
Kupitia tovuti hii wadau wa mpira watapata fursa ya kuhabarishwana kuelimishwa nkuhusu masuala mbali mbali yahusuyo mpira wa miguu. 
Tovuti hii itakuwa pia na sehemu ya kumbu kumbu (archive) zihusuzo historia ya mpira wa miguu na matukio mbali mbali katika historia ya mpira wetu. 
Tunaomba wadau wenye kumbu kumbu mbali za mpira kama picha,takwimu,vipande vya magazeti ya zamani na kadhalika mtuletee ili viingizwe katika tovuti yetu.
Tunaamini tovuti hii itakuwa ndio chanzo kikuu cha taarifa na rekodi mbali mbali za sasa na za zamani  zihusuzo mpira wa miguu.
Ndugu mgeni rasmi shughuli ya leo tutaihitimisha kwa kuzindua jezi mpya ya timu ya Taifa. Jezi hizi zitakuwa ni mbili moja ya ugenini na nyingine ya nyumbani.Tunawapongeza watanzania wote walioshiriki katika kubuni jezi na mwisho tuliunganisha ubunifu tofauti na kupata jezi itakayozinduliwa leo.
Ubunifu huu tayari umetafutiwa hati miliki Brela hivyo TFF tutalinda hakii hii kwa kuwakamata na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria wale wote watakaodiriki kuchapisha na kuuza kwa magendo jezi hizi.Utaratibu unafanyika kumpata msambaji mmoja halali atakayesambaza jezi hizi nchini kwa ajili ya wapenzi wa mpira wa miguu.Ukinunua jezi hii utakuwa umechangia maendeleo ya mpira wa miguu.
 TFF inawashukuru na kuwapongeza sana Tanzania Breweries ltd ambao ndio wazalishaji wa bia ya Kilimanjaro Lager kwa sapoti wanayoitia kwa timu ya Taifa na kutuwezesha kubuni na kuzalisha jezi hizi.Tunawashukuru sana.
Ndugu mgeni rasmi ninaomba nimalizie kwa kuzungumzia kwa kifupi program yetu ya mpira wa vijana.kwa kutambua umuhimu wa kuendeleza soka la vijana TFF tumejipanga vilivyo kwa mpambano wa hatua za awali za kucheza fainali za vijana za Afrika umri chini ya miaka 17 mwaka 2017. 
Mechi za ufaulu zitafanyika kati kati ya mwaka 2016.TFF tayari tumeunda kikosi cha awali cha vijana chini ya umri wa miaka 15 kujiandaa na michuano hii.Kikosi hiki kimetokana na michuano ya copa coca cola ya mwaka jana. 
Tunapenda tuchukue fursa hii kumshukuru Rais Dr Jakaya Mrisho Kikwete kwa kufanikisha nchi yetu ya Tanzania,kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hii,kupata uenyeji wa fainali za Afrika. Shirikisho la mpira wa miguu Afrika CAF limeipatia Tanzania uenyeji wa fainali za Afrika za vijana umri chini ya miaka 17 mwaka 2019.
Tunaomba Serikali itushike mkono katika hili ili tuweze kuandaa mashindano mazuri.Lakini haitakuwa vyema Tanzania kuandaa mashindano mazuri lakini tukatolewa hatua ya makundi.Siku ya jumapili tarehe 07/juni TFF tutazindua mashindano ya taifa ya vijana umri chini ya miaka 13 mjini mwanza.
 Wachezaji bora wa mashindano haya ndio wataunda kikosi cha awali cha Taifa kwa ajili ya kushiriki fainali za Afrika watoto umri chini ya miaka 17 mwaka 2109. 
Tunaomba Serikali pamoja na wadau wote tushirikiane katika kukilea kikosi hiki ili mwaka 2019 tuwe na timu nzuri.
Tunamshukuru Mh Dr Fennela Mukangara na wizara nzima ya habari vijana utamaduni na michezo kwa ushirikiano wanaotupatia katika hatua hizi na katika shughuli nyingine za kuendeleza mchezo wa mpira wa miguu.
Ndugu mgeni rasmi ninaomba sasa nikukaribishe uhutubie hafla  hii na pia utuongoze katika shughuli zitakazofuata.
Ahsate sana
Jamal Malinzi
Dar es salaam
03/juni/2015

muonekano wa BUS LA ZIARA YA KINANA MKOA WA KAGERA

001 002

WASIFU WA KAMISHNA MKUU MSTAAFU WA JESHI LA MAGEREZA, MAREHEMU ONEL ELIAS MALISA

unnamedMarehemu alizaliwa mwaka 1944 katika kijiji cha Kidia, Old Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro. Alipata elimu ya msingi katika Shule ya Msingi Kidia mwaka 1951 – 1954 na baadae Shule ya Msingi Kidia Juu (Kidia Upper Primary School) mwaka1955 – 1958. Alihitimu Elimu ya Sekondari Kidato cha Nne mwaka 1974 katika Shule ya Sekondari Mawenzi akiwa mtahiniwa wa kujitegemea (Private Candate). Aidha, alisoma Cheti cha Sheria Chuo Kikuu cha D’Salaam mwaka 1975 – 1976 na baadaye Shahada ya Kwanza ya Sheria Chuo Kikuu cha D’Salaam mwaka 1977 – 1980.
Marehemu ajiunga na Jeshi la Magereza mwaka 1964 baada ya kuhitimu Mafunzo ya Awali ya Uaskari Magereza Chuo Ukonga, D’Salaam yaliyofanyika kuanzia Januari – Julai, 1964. Ndani ya utumishi, alipata fursa ya kuhudhuria Mafunzo ya Uongozi Daraja la Pili (Advance Course) Chuo Ukonga, D’Salaam kuanzia Aprili – Julai, 1967 na Mafunzo ya Uongozi wa Juu (Gazetted Course) kuanzia Februari – Mei, 1974.
Kutokana na utendaji wake wa kazi, marehemu aliwahi kutunukiwa vyeo mbalimbali kama ifuatavyo:-
• Afisa Magereza Daraja la Tatu mwaka 1964
• Afisa Magereza Daraja la Pili mwaka 1965
• Afisa Magereza Mkuu Daraja la Nne mwaka 1967
• Afisa Magereza Mkuu Daraja la Tatu mwaka 1971
• Mrakibu Msaidizi wa Magereza mwaka 1975
• Mrakibu wa Magereza mwaka 1976
• Mrakibu Mwandamizi wa Magereza mwaka 1978
• Kamishna Msaidizi wa Magereza mwaka 1982
• Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza mwaka 1984
• Kamishna wa Magereza mwaka 1992
• Kamishna Mkuu wa Magereza mwaka 1996 – 2002
Aliwahi kufanya kazi katika vituo mbalimbali vikiwemo Gereza Butimba – Mwanza, Isanga – Dodoma, Wami Vijana – Morogoro, Chuo cha Usalama Moshi, Gereza Songwe – Mbeya, Chuo Ukonga – D’Salaam na Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, D’Salaam.
Aidha, marehemu aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali ndani ya Jeshi la Magereza kama ifuatavyo:-
• Mkufunzi Mkuu Chuo Ukonga mwaka 1975
• Mkuu wa Chuo Msaidizi, Chuo Ukonga mwaka 1981
• Mkurugenzi Msaidizi wa Sheria na Urekebishaji, Makao Makuu mwaka 1983
• Mkurugenzi wa Sheria na Urekebishaji, Makao Makuu mwaka 1984
• Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Makao Makuu mwaka 1992
• Kamishna Mkuu wa Jeshi la Magereza mwaka 1996 – 2002 alipostaafu kazi.
Marehemu atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa alioutoa wakati wa utumishi wake. Baadhi ya mambo aliyoyafanya ni kama ifuatavyo:-
• Alianzisha na kuimarisha mahusiano baina ya Jeshi la Magereza na Magereza ya nchi nyingine Afrika na duniani.
• Alikuwa mmojawapo wa Makamishna wa Tume ya Marekebisho ya Sheria Nchini (Law Reform Commission)
• Alikuwa mshauri kwenye Maboresho ya Jeshi la Magereza pamoja na Sera ya Taifa ya Magereza.
• Kama hatua ya kupunguza msongamano wa wafungwa magerezani aliweza kushauri na kusimamia kutungwa kwa Sheria zifuatazo:-
– Sheria ya Bodi ya Parole
– Sheria ya Huduma kwa Jamii (Community Service)
Nishani alizotunukiwa akiwa kazini ni:-
• Nishani ya mstari wa nyuma
• Nishani ya Utumishi mrefu
• Nishani ya Utumishi uliotukuka
Hata baada ya kustaafu kazi, marehemu aliendelea kutoa mchango wake kwa kushauri mambo kadhaa pamoja na kushiriki kwenye matukio mbalimbali ya Jeshi na Taifa. Kutokana na mchango wake huo alitunukiwa Nishani ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Muungano Daraja la Nne na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 26 Aprili, 2015.
Kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Magereza na Watumishi wote wa Jeshi la Magereza, tunatoa salamu nyingi za rambirambi kwa Mke, Watoto na Ndugu wa Marehemu kwa msiba huo mkubwa uliotufika.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI, AMINA

Programu ya kukuza ajira zenye staha kwa vijana kuzinduliwa juni 5, 2015

 2
Mratibu wa Programu ya kukuza Ajira zenye Staha Dar es Salaam, kupitia Elimu ya Biashara na Maendeleo ya Ujasiriamali Bw. Dominic Ndunguru akiwasilisha mada kuhusu utekelezaji wa program hiyo jana jijini Dar es Salaam. Programu hii inaendeshwa kwa ubia wa asasi za kiraia za Tanzania Youth Vission Associataion (TYVA), Open Mind Tanzania (OMT) na Youth For Africa (YOA).
3
Mshauri wa maswala ya Sera na Miradi ya Maendeleo wa Tanzania Youth Vision Association Bw. Elly Ahimidiwe Imbyandumi akifafanua jambo kwa washiriki wa mkutano wa kutathmini utekelezaji wa Programu ya Kukuza Ajira zenye Staha katika jiji la Dar es Salaam (YEID jana katika ukumbi wa Kituo cha Vijana cha Don Bosco cha jijini Dar es Salaam.Programu hii inaendeshwa kwa ubia wa asasi za kiraia za Tanzania Youth Vission Associataion (TYVA), Open Mind Tanzania (OMT) na Youth For Africa (YOA).
6
Afisa Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Godfrey Nyaisa akielezea jambo wakati wa mkutano wa asasi za Vijana kujadili utekelezaji wa Programu ya Kukuza Ajira zenye Staha jijini Dar es Salaam (YEID) mradi huo unalenga kuwajengea uwezo vijana ili waweze kujiajiri na kuajirika. Programu hii inaendeshwa kwa ubia wa asasi za kiraia za Tanzania Youth Vission Associataion (TYVA), Open Mind Tanzania (OMT) na Youth For Africa (YOA).
7
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa asasi za vijana wakifuatilia mada zilizokuwa zinawasilishwa wakati wa mkutano wa asasi za Vijana uliofanyika jana jijini Dar es Salaam ili kujadili utekelezaji wa Programu ya Kukuza Ajira zenye Staha jijini Dar es Salaam (YEID) mradi huo unalenga kuwajengea uwezo vijana ili waweze kujiajiri na kuajirika. Programu hii inaendeshwa kwa ubia wa asasi za kiraia za Tanzania Youth Vission Associataion (TYVA), Open Mind Tanzania (OMT) na Youth For Africa (YOA).
1
Washiriki wa mkutano wa asasi za Vijana ILI kujadili utekelezaji wa Programu ya Kukuza Ajira zenye Staha jijini Dar es Salaam (YEID) wakiwa katika picha ya pamoja.
Picha na Frank Shija, WHVUM

KINANA KUANZA ZIARA KESHO KUELEKEA KAGERA, GEITA ,MWANZA

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa, Nape Nnuye akizungumza na waandishi wa habari ambapo alizungumzia ratiba ya ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana katika mikoa mitatu ,Kagera,Geita na Mwanza itakayoanza tarehe 4 June.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akionyesha picha ya muonekano wa basi maalum litakalotumika kwenye ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa kuelekea mkoani Kagera.
………………………………………………………………………………..
NA HAFIDH KIDO, Dar es Salaam
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana anaanza ziara ya siku 28 leo katika mikoa mitatu ya Kagera, Geita na Mwanza kukamilisha mikoa yote 30 nchi nzima.
Ziara hizo zenye malengo ya kukagua utekelezwaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM mwaka 2010 na kuimarisha chama zimekuwa na mafanikio kwa kuondoa matatizo mbalimbali yanayowakumba wananchi hasa wa mikoani.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu wa NEC-CCM Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisema wataondoka jijini leo kwa basi maalumu ambapo watasimama njiani katika mikoa ya Morogoro, Dodoma, Singida na mengineyo kwa ajili ya kusalimia wananchi.
“Ziara rasmi itaanza June 4 katika Wilaya ya Nyakanazi mkoani Kagera, lakini kesho (leo) tutakunywa chai Morogoro chakula cha mchana tutakula Dodoma halafu tutasalimia wananchi katika Mikoa ya njiani kama Singida, Nzega na tumepanga kulala Kahama mkoani Shinyanga, tukiamka ziara ndio itaanza rasmi,” alisema Nape.
Aliongeza kuwa katika ziara hiyo watatembelea majimbo yote ya uchaguzi hivyo amewataka wana-CCM na wananchi wengine kujitokeza kwa wingi kumsikiliza Katibu Mkuu katika ziara hiyo ya kihistoria.
“Hii ni ziara ya kihistoria kwa sababu ya mambo matatu, kwanza tutatembelea visiwa vyote vya Ukerewe mabavyo ni nadra kutembelewa na viongozi, pili huu ni mwaka wa uchaguzi kuna masuala mengi yanahitaji ufafanuzi,” alisema.
Akitaaja ratiba ya ziara hiyo Nape alifafanua kuwa, “Kuanzia Juni 5 mpaka Juni 15 tutakuwa Mkoa wa Kagera, Juni 16 mpaka 21 tutakuwa Mkoa wa Geita na Juni 22 mapaka Julai 2 tutakuwa Mwanza kuhitimisha ziara ya nchi nzima kwa mkutano mkubwa wa kihistoria.”
Akijibu maswali ya waandishi wa habari kuhusu faida za ziara hizi Nape alisema kuna masuala mengi ya kimaendeleo yalisimama lakini alipopita Katibu Mkuu Kinana ufumbuzi umepaikana, akitolea mfano mashamba yaliyobinafsishwa bila kufuata utaratibu alisema Rais Jakaya Kikwete, amefuta hati nyingi za mashamba ya wawekezaji na kurudishwa kwa wananchi.
“Kuna baadhi ya maeneo kulikuwa na zahanati zimeshajengwa lakini hakuna vibali, nimepata taarifa kuwa vibali vimeshapatikana na huduma zinaendelea, kulikuwa na matatizo ya ardhi za wananchi kuchukuliwa na wawekezaji katika maeneo ya Tanga, Arusha, Babati na maeneo mengine lakini kila kitu kipo sawa sasa na wananchi wanamshukuru Kinana,” alisema.
Aliongeza kuwa, “Nisisitize kuwa tumesema tutaondoka na basi maalumu kwa sababu kama kuna mwingine atafanya hivyo atakuwa ametuiga, mkumbuke hili wazo la kuondoka na basi ni la Katibu Mkuu.”
Ikiwa ziara hizi zitamalizika salama Julai 2 mwaka huu, Kinana atakuwa Katibu Mkuu pekee wa CCM tangu kuanzishwa kwake Februari 5, 1977 kuzunguka nchi nzima kuangalia uhai wa chama na kusikiliza na kutatua kero za wananchi wote bila kujali itikadi za vyama.

TANZANIAN RAPPER FID Q ALBUM LISTENING PARTY AT NAIROBI RAPSODY – THUR JUNE 4TH

UC 2013 FB COVER 2

Maandalizi ya hafla ya Mh Samuel Sitta kutangaza nia ya kugombea urais yaiva!

Adama Fundikira akiwa na mama yake mdogo Mh Samuel Sitta aitwaye Ndisha Said Fundikira
Wayege wakicheza ngoma
Habari na picha kwa hisani ya 
Mkala Fundikira wa TBN central zone

Filamu ya MPANGO MBAYA kuzinduliwa ndani ya Ukumbi wa Mlimani City

MPANGO MBAYA ni filamu iliyochezwa na washiriki 10 waliofanikiwa kuingia katika Fainali ya shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) msimu wa kwanza 2014 na kushirikisha baadhi ya waigizaji mahiri kutoka katika kiwanda cha Filamu Tanzania.

Filamu ya Mpango Mbaya ni filamu ambayo imetengenezwa kwa viwango vya hali ya juu huku ikikidhi viwango vya kimataifa na ni filamu ambayo ina ubora wa hali ya juu kuanzia ubora wa picha, Sauti, rangi mpangilio wa matukio na upigwaji picha wake na ubora wa washiriki wa filamu hiyo

Filamu hii itazinduliwa mnamo tarehe 12 Juni 2015 Katika Ukumbi wa Mlimani City  na pia Filamu hii itaendelea kuonyeshwa kwa siku mbili mfululizo katika ukumbi huohuo.

Picha chini ni baadhi ya taswira za washiriki wa filamu hiyo

NASHINDWA NDANI YA DAR LIVE JUMAMOSI JUNI 6, 2015

TBL YAKABIDHI MSAADA WA KISIMA CHA MAJI KIJIJI CHA MAGOZA, MKURANGA

 Ofisa Elimu Wilaya ya Mkuranga, aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo,  Benjamin Majoya akikata utepe kuzindua rasmi kisima cha maji kilichojengwa kwa msaada wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kwa gharama ya sh. mil 56, katika Kijiji cha Magoza, Kata ya Kiparang’anda, Mkuranga, Mkoa wa Pwani. Kushoto ni Diwani wa Kata hiyo, Karu Karavina na Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL, Steve Kilindo (wa pili kulia).
 Ofisa Elimu Wilaya ya Mkuranga, aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo,  Benjamin Majoya (katikati) akiwa na Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo (kushoto kwake) pamoja na Diwani wa Kata ya Kiparang’anda, Karu Karavina (kushoto) wakifurahi baada kukabidhi mradi wa  kisima cha maji kwa wananchi wa Kijiji cha Magoza, wilayani Mkuranga mwishoni mwa wiki. Kisima hicho kimejengwa kwa msaada wa TBL gharama ya sh. mil. 56.
 Akina mama wakicheza kwa furaha wakati wa hafla ya kukabidhiwa kisima chas maji na TBL
 Ofisa Uhusiano wa TBL, Dorris Malulu akitoa utambulisho wakati wa hafla hiyo
 Ofisa Elimu Wilaya ya Mkuranga, aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo,  Benjamin Majoya akimtwisha ndoo ya maji Mama mkazi wa Kijiji cha Magoza, Kata ya Kiparang’anda, wilayani Mkuranga, Pwani, wakati wa hafla ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kukabidhi msaada wa kisima cha maji kilichojengwa kwa gharama ya sh. mil. 56 kijijini hapo. Makabidhiano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki.
 Mmoja wa akina mama akifurahia baada ya kuteka maji kwenye kisima hicho
 Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL, Steve Kilindo akielezea mikakati ya kuisaidia jamii katika uboreshaji wa sekta ya maji nchini kutoka  sehemu na faida inayopatikana katika mauzo ya vinywaji vyao
Diwani wa Kata ya Kiparang’anda, akitoa shukrani kwa TBL kwa kuwapatia msaada huo wa kisima.
 Wakifunua pazia kuzindua mradi huo wa kisima
 Mgeni rasmi, Benjamin Majoya akifungua maji ya bomba badaa ya kuzindua kisima hicho
 Steve Kilindo wa TBL, akinywa maji baada ya kuzindua kisima hicho
Akina mama wakazi wa Kijiji cha Magoza, Kata ya Kiparang’anda,Mkuranga, wakiwa wamebeba ndoo za maji waliyoteka katika Kisima cha maji kilichojengwa kwa msaada wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) katika Kijiji hicho kwa gharama ya sh. mil. 56. Hafla ya TBL kukabidhi kisima hicho cha maji ilifanyika mwishoni mwa wiki.

HIFADHI ZA TAIFA TANZANIA(TANAPA) KUPITIA UJIRANI MWEMA WAKABIDHI MRADI WA MAJI KATIKA KIJIJI CHA ASHIRA WILAYA YA MOSHI

Mkuu wa mkoa wa Kilimajaro,Leonidas Gama
akikaribishwa na Mhifadhi Mkuu Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro
(KINAPA)Erastus Rufungulo katika makabidhiano ya mradi wa maji wa
ujirani Mwema uliotolewa na hifadhi za taifa nchni
TANAPA.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Leonidas Gama
akikata utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi katika tanki la maji la mradi wa ujirani mwema uliotolewa na TANAPA kwa wananchi katika kijiji cha Ashira wilaya ya Moshi vijijini.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Leonidas Gama
akisoma kilichoandikwa katika vibao mara baada ya uzinduzi wa mradi
huo.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Leonidas Gama
kuashiria uzinduzi rasmi wa mradi huo.
RC ,Gama akinywa maji kwa kutumia mkono mara
baada ya kufungua bomba la maji katika kijiji cha Ashira wilaya ya
Moshi vijijini.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,akimtwisha ndoo
ya maji mmoja wa wakazi wa kijiji cha Ashira katika wilaya ya Moshi
ikiwa ni ishara ya kukabidhi mradi huo wa maji ulifadhiliwa na TANAPA
kupitia mradi wa ujirani mwema.
Tanki la Maji la mradi wa ujirani mwema
uliofadhiliwa na Hifadhi za Taifa ,Tanzania (TANAPA).
Mhifadhi mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima
Kilimanjaro (KINAPA) Erastus Rufungulo akiwasalimia wananchi katika kijiji cha Ashira wilaya ya Moshi wakati wa kukabidhi mradi wa maji wa ujirani mwema uliofadhiliwa na TANAPA.
Baadhi ya wananchi katika kijiji cha Ashira
wilaya ya Moshi vijijini.
Meneja Ujirani mwema wa Hifadhi za Taifa
,Tanzania(TANAPA) Ahmed Mbugi akizungumza kuhusu miradi ya ujirani mwema ambayo TANAPA imekuwa ikiitoa kwa jamii katika kijiji cha Ashira wilaya ya Moshi vijijini.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Ashira
katika wilaya ya Moshi .
Kaimu Mkurugenzi mkuu TANAPA,Ibrahim Musa
akitoa taarifa mbele ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama
kuhusu ujenzi wa mradi wa maji katika kijiji cha Ashira wilaya ya
Moshi ,
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga
akizungumza wakati wa makabidhiano ya mradi wa maji uliofadhiliwa na
TANAPA kwa ajili ya wananchi wa kijiji cha Ashira wilaya ya
Moshi.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Leonidas Gama
akiwahutubia wananchi waliofika katika makabidhiano ya mradi wa maji
katika kijiji cha Ashira wilaya ya Moshi ,uliofadhiliwa na hifadhi za
taifa Tanzania (TANAPA) .

Na Dixon Busagaga wa Globu ya
Jamii,Kanda ya Kaskazini, 

MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO LEONIDAS GAMA AZINDUA DUKA JIPYA LA KAMPUNI YA SIMU ZA MKONONI YA TIGO.

Duka jipya la kampuni ya mawasiliano ya simu
za mkononi,Tigo lafunguliwa mjini Moshi.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Leonidas Gama
akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa duka jipya la kampuni ya simu za mkononi ya Tigo.wengine wanaoshuhudia toka kulia ni mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga,Meneja huduma kwa wateja kanda ya
kaskazini,Gwamaka Mwakilembe na kushoto ni Meneneja wa Ubora wa Huduma ka wateja ,Mwangaza Matotola.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Leonidas Gama
akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka jipya la kampuni ya simu za mkononi ya Tigo lililozinduliwa mjini Moshi.
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga
akifuatilia kwa makini shughuli za uzinduzi wa duka la Tigo katika mji
wa Moshi.
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya simu za
mkononi ya Tigo,wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Leonidas
Gama wakati wa uzinduzi wa duka jipya la kampuni hiyo mjini
Moshi.
Meneja huduma kwa wateja kanda ya
Kaskazini,Gwamaka Mwakilembe akitoa maelezo kwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama wakati akitembelea vitengo mbalimbali ndani ya duka hilo.
Wafanyakazi wa kampuni ya Tigo wakiwa kazini.
Uuzaji wa simu za aina mbalimbali pia ulikuwa ukifanyika katika duka hilo.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Leonidas Gama
,akifurahia jambo mara baada ya kutembelea ndani ya duka hilo na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni hiyo ya Tigo.
Meneja huduma kwa wateja Kanda ya
Kaskazini,Gwamaka Mwakilembe akitoa neno la shukurani kwa mkuu wa mkoa
wa Kilimanjaro ,Leonidas Gama (hayupo pichani)mara baada ya uzinduzi
wa duka jipya la kampuni ya Tigo.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Leonidas Gama
akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni ya Tigo muda
mfupi mara baada ya uzinduzi wa duka hilo.
………………………………………….
Na Dixon
Busagaga wa Globu ya jamii Kanda ya Kaskazini.

NIAMBIE LIVE

Omby Nyongole, Dotto Maongo na Salma Moshi
Karibu kwenye kipindi hiki cha NIAMBIE LIVE
Kipindi kinachozungumzia mambo mbalimbali yaliyochukua nafasi za juu
kwenye mitandao ya kijamii. Pia kupata Tip ya siku / wiki kusaidia
kuboresha maisha yako.

PITIA VICHWA VYA MAGAZETI-JUNI 3,2015

1 2 3
6
  5
4
7 8 9
12
  11
10

UTAFITI WA KISIASA ULIOFANYWA NDANI YA MANISPAA YA IRINGA WAMBEBA FRANK KIBIKI

     
   frank kibiki akiongea na wananchi stand kuu ya mabas iringa.
 
wananchi wakimsikiza frank kibiki  alipokuwa maeneo ya stand kuu
 …………………………………….
na fredy mgunda,iringa
MATOKEO ya utafiti uliofanywa na taasisi ya Southern Highland Zone
Election Research (SHZER), katika jimbo la Iringa mjini umeonyesha kuwa nyota ya
Mwanahabari ,  Frank Kibiki aliyetangaza
nia kuwania Ubunge jimbo la Iringa mjini (CCM) inazidi kung’ara baada ya kuongoza
huku akichuana vikali na Mbunge wa sasa Mchungaji Peter Msigwa(CDM).
Utafiti huo uliofanywa kwa miezi minne tangu, kuwepo kwa
wimbi la watu wengi kutangaza nia ya kuwania ubunge katika jimbo la Iringa
mjini, wakiwemo makada lukuki wa CCM unaonyesha kuwa Nyota ya Frank Kibiki
inazidi kung’ara kutokana na kuungwa mkono na makundi mengi ya kijamii hasa
vijana,  wanawake, walemavu na wazee.
Akizungumza na mtandao huu, Mtafiti mkuu wa SHZER,  Patson William alisema utafiti huo umefanywa
katika kata 14 za jimbo la Iringa mjini huku wagombea vijana wakiwa ndio wanaoongoza
kupendwa ikilinganishwa na wagombea wenye umri kuanzia miaka 50 na kuendelea.
Kibiki anaongoza kwa asilimia 40.7, Mchungaji Msigwa 20.9,
Jesca Msambatavangu 11.7, Dr Yahaya Msigwa 7.6, Fredrick Mwakalebela 2.8, John Kiteve
2.4, Mahamoud Madenge 1.2 na wengine waliobaki wanagawana asilimia 12.7.
Utafiti huo unaonyesha kuwa, kinachomfanya Kibiki kuendelea
kung’ara ni siasa zake za kistaarabu, taaluma ya uana habari, uwezo mkubwa wa
kujenga na kujibu hoja anazokumbana nazo sambamba na uzoefu katika utendaji
wake wakati akiwa Katibu wa UVCCM katika wilaya mbalimbali alizowahi kufanya
kazi.
Alisema utafiti huo umefanywa kwa njia ya madodoso ambapo
watu 400 walijibu na maswali ya papo kwa papo ambapo watu 1000 waliyajibu.
Alitaja kata zilizohusishwa kuwa ni Makorongoni,
Miyomboni/kitanzini, Kihesa, Kwakilosa, Mlandege, Mivingeni, Gangilonga,
Kitwiru, Igumbilo, Nduli, Ruaha, Mkwawa, Mtwivila na Isakalilo.
Mambo ya msingi ambayo utafiti huo uliangalia ili kutafuta
majibu ni Changamoto za jimbo la Iringa mjini kwa sasa,sifa za Mbunge
anayetakiwa kukabiliana na changamoto hizo, mapendekezo ya jina la atakayesimamia
vizuri changamoto hizo na mazingira ya siasa za sasa za jimbo la Iringa mjini.
Hata hivyo CCM na Chadema ndiyo vyama pekee vinavyochuana
kwa kasi katika jimbo la Iringa mjini, tangu CDM iliponyakua jimbo hilo mwaka
2010.
Hata hivyo utafiti huo unaonyesha kuwa CCM itakuwa na
wakati mgumu ikiwa watateua jina la mtu asiyechaguo la wananchi jambo ambalo,
litampa Mchungaji Msigwa ushindi usio na jasho.
“Utafiti huu unaonyesha kuwa CCM inanafasi nzuri ya
kuchukua jimbo la Iringa mjini ikiwa tu watafuata nini wana Iringa wanasema
vinginevyo, nafasi ya Msigwa kuendelea itakuwa kubwa,”anasema


UBORESHWAJI DAFTARI LA MPIGA KURA MIKOA YA GEITA SIMIYU MWANZA NA SHINYANGA

unnamed

Profesa Sospeter Muhongo atangaza nia rasmi , MJINI Musoma

unnamedNA MWANDISHI WETU, MUSOMA
……………………………………………
WAZIRI wa zamani wa Nishati na Madini Sospeter Muhongo, ametangaza nia rasmi ya kuwaomba Wana CCM kumteua kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwezi Oktoba, huku akisema ni yeye pekee mwenye uwezo wa kuikwamua nchi katika hali mbaya ya umasikini na ukosefu wa wataalamu, hali inayoifanya nchi ishindwe kupiga hatua.
Pamoja na mambo mengine, Muhongo alitumia muda mwingi kutoa takwimu hali ya umasikini na utajiri kwa wananchi wa Tanzania, bila kusahau baadhi ya nchi ambazo zimeweza kupiga hatua kubwa kwa kujikita kwenye kuzalisha wataalamu na watafiti, akiwamo yeye, ambaye si tu ni Profesa, bali pia amebobea kwenye nishati kwa miaka mingi.
Akizungumza kwa kujiamini mbele ya wanachama wa CCM na Watanzania katika Ukumbi wa Chuo Kikuu Huria, Musoma Mjini, Profesa Muhongo alisema kwamba anayo tiba ya umasikini wa Watanzania kwa kuhakikisha kwamba anatumia utaalamu wake kwa kusimamia mambo ya gesi, mafuta, umeme, bila kusahau elimu kwa ajili ya kuwakwamua wananchi wake.
“Nchi ina upungufu mkubwa wa takwimu hali inayowafanya viongozi washindwe kujua namna gani wanaweza kuondoa umasikini na kero zinazowakumba wananchi wake, hivyo hata wale wanaosema wanataka uongozi, hawajui wangapi wenye uhitaji.
“Ukiacha takwimu ambayo kwa Dunia ya sasa ni lazima, nchi yetu lazima ijiamini, kuongeza ushindani, kuongeza upendo, bila kusahau rushwa ambayo kwa uhakika inapaswa kupigwa vita kwa vitendo ili nchi yetu isonge mbele,” alisema Muhongo.
Kuhusu uchumi, Profesa Muhongo alisema kwamba ni aibu Tanzania kupitwa kiuchumi na Mataifa waliyokuwa nayo sawa, akitolea mfano wan chi za Brazil, China, India na Kenya ambao wao wamewekeza kwa kiasi kikubwa kwenye elimu na utafiti.
Alisema nchi ikiwa na watafiti, wananchi wao hawataishi kwa mashaka, huku akisema endapo atapitishwa kuwania nafasi hiyo na kuwa rais wa Tanzania, atahakikisha kwamba anakuza uchumi wan chi kutoka asilimia 7.5 hadi asilimia 10 na 15 kwa kipindi cha miaka mitano hadi 10 ya urais wake.
“Nimeweza kufanya kazi ya gesi na mafuta kwa miaka kadhaa kwenye nchi mbalimbali, hivyo hakika kama chaguo ni wataalamu, basi mimi nastahili kwa sababu sioni mwingine mwenye uwezo wa kutangaza kuondoa kero za Watanzania na jinsi atakavyoziondoa.
“Ndio unaweza kusema utaondoa umasikini kwa wananchi au kuongeza mishahara, lakini ili hilo liweze kufanikiwa kwa vitendo, ni lazima pia katika kipindi cha uongozi wako uweze kukuza uchumi wako kwa kiasi kikubwa, bila hivyo hakuna kitu,” alisema Muhongo.
Aidha Profesa Muhongo alisema kwamba Duniani kote nchi zimepiga hatua kwa kuwekeza kwenye wataalamu na viwanda, hivyo Tanzania inapaswa kuangalia namna ya kuwekeza kwenye sekta hizo, bila kusahau sekta ya elimu yenye umuhimu mkubwa.
Katika hatua nyingine, Profesa Muhongo alisema kwamba akiwa Waziri wa Nishati na Madini, ndio mtu ambaye alifanikiwa kwa vitendo kutekeleza ilani ya CCM kwa kuhakikisha kwamba vijiji vingi vinapata umeme kwa kuongeza bajeti na kusimamia kwa vitendo wakala wa umeme vijijini (REA).
Alisema kusudio la kuhakikisha kwamba wananchi wake wanaendelea kupata umeme kwa bei nafuu ni kati ya mambo anayoona yanafaa kuongezewa chapuo na usimamizi wa aina yake, hivyo mwenye uwezo wa kulitatua hilo ni yeye.

SERIKALI YAMALIZA MGOGORO NA WAFANYABIASHARA.

1
Waziri wa Fedha Mh. Saada Mkuya Salum akiwaeleza wafanya biashara kuendelea kutoa ushirikiano, utakaojenga uhusiano wa kudumu kati yao na Serikali kwa maslahi na maendeleo ya Taifa, wakati akitoa Taarifa ya muafaka uliofikiwa kati ya wafanyabiashara na serikali juu ya Matumizi ya Mashine za kielektroniki (EFDs) leo Jijini Dar es Salaam.
2
2- Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Rished Bade akimshukuru Waziri wa Fedha kwa ushirikiano wanaoendelea kuuonyesha kwa mamlaka hiyo hasa katika kukabiliana na changamoto mbalimbali katika suala la ukusanyaji Kodi nchini.
3
3- Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabishara Bw. Johnson Minja akimueleza Waziri wa Fedha Mh. Saada Mkuya Salum kuridhishwa na utendaji wa serikali katika utatuzi wa changamoto za wafanyabiashara na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano ili kwa pamoja waweze kufikia malengo ya taifa ya kuwa na uchumi imara kupitia ukusanyaji wa Kodi.
4
4- Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mzee Benard Mchovu akipongeza kazi iliyofanywa Kamati ya uhamasishaji wa matumizi ya mashine za kielektroniki(EFDs) na kuwaasa kuendelea kutoa ushirikiano kwa maslahi ya Taifa kwa Ujumla.
5
 Waziri wa Fedha Mh. Saada Mkuya Salum akiwa katika picha ya pamoja wafanyabiashara alipotoa Taarifa ya muafaka uliofikiwa kati ya wafanyabiashara na serikali juu ya Matumizi ya Mashine za kielektroniki (EFDs) leo Jijini Dar es Salaam, Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabishara Bw. Johnson Minja na Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mzee Benard Mchovu.
…………………………………………………………..
Na Anitha Jonas – MAELEZO.
Serikali yafikia muafaka katika mgogoro wake na wafanyabiashara juu ya matumizi ya mashine za kieletroniniki EFD’s.
Hayo ameyasema jana Waziri wa Fedha Mhe.Saada Mkuya alipokuwa akitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari juu ya Serikali kufikia muafaka wa makubaliano yaliyofanyika kwa ushirikiano wa Kamati kuu ya Taifa iliyoshirikisha wajumbe kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na Viongozi wa Jumuiya ya wafanyabiashara katika ngazi ya Taifa.
“Matumizi ya mashine za EFD yalipoanza yalileta changamoto kwa wafanyabiashara ,hivyo niliunda kamati ya kitaifa pamoja na kamati katika ngazi za Mikoa na Wilaya pamoja na wenyeviti wakuu wa mikoa kutafuta suluhu la suala hili”alisema Mhe.Mkuya.
Waziri Mkuya aliendelea kusema Kamati imetoa mapendekezo mbalimbali kwa Serikali ikiwemo ya muda mfupi ambayo wameshaanza kuyafanyia kazi na mengine ni yakisera ambayo yatahitaji muda mrefu yatafuata utaratibu unaopaswa katika utekelezaji wake,kwa ufuatiliaji na ushirikiano wa karibu,kupitia kamati ya Kitaifa itakayodumu kwa kipindi cha miaka miwili.
Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara nchini Bw.Johnson Minja aliipongeza serikali kwa kubali kukaa meza moja na wafanyabiashara katika kutatua mgogoro huo uliyokuwepo katika matumizi ya mashine za EFD na kuakukubali kupokea changamoto za wafanyabiashara na kuahidi kuzifanyia kazi.
“Serikali imekubali kupitia mfumo wa utozwaji kodi kuanzia ngazi ya bandarini na kuongeza uwazi ilikuleta uelewa kwa wafanyabiashara na kuepuka kutozwa kodi kubwa kutoka na kukosa uelewa wa gharama za ulipaji kodi”,alisema Bw.Minja.
Aidha Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo ya wafanyabiashara aliendelea kusema ni wajibu wa kila mmoja kulipa kodi na hii ni kwa maendeleo ya nchi na pia ni kosa kwa mfanyabiashara yoyote kuendesha biashara yake bila kuwa na namba ya utambulisho wa mlipakodi (Tin Number),tunataka namba ya walipakodi iendelee kuongezeka na kuondoa kabisa wafanyabiashara wasio lipa kodi.
Mbali na hayo nae Kamishana Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Rished Bade aliipongeza kamati kwa kuweza kufika mwafaka na kuweza kuzitambua changamoto mbalimbali zilizokuwa zikiwasumbua wafanyabiashara na ameahidi ,kuwa ofisi yake itaendelea kuwawajibisha watu wote wanao kiuka taratibu za ulipaji kodi.

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda AISIFU mifuko ya hifadhi za jamii

unnamed 
NA Mahmoud Ahmad,ARUSHA.
………………………………………………
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amesifu juhudi za mifuko ya hifadhi ya jamii nchini inayomilikiwa na serikali kwa kazi nzuri iliyofanya ikiwemo ujenzi wa vyuo vikuu mbalimbali kikiwemo cha Dodoma,Nelson Mandela pamoja na jengo la Bunge la jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Waziri Mkuu Pinda alitoa pongezi hizo alipokua akifungua mkutano wa tano wa wanachama wa mfuko wa jamii wa NSSF unaoendelea mkoani Arusha na kushirikisha viongozi wa mifuko mingine ya ndani ya nchi na ile ya nje ya nchi.
Alisema pasipo kuwepo kwa mifuko hiyo mambo mbalimbali ya maendeleo yakiwemo ya ujenzi huo kamwe yasingefanyika kutokana na ufinyu wa bajeti ya serikali jambo ambalo lilisababisha serikali kuitumia mifuko hiyo kwa makubaliano ya kulipa deni litakalotokana na shughuli hizo za maendeleo.
Alisema mbali na mchango huo wa ujenzi wa miundo mbinu pia mifuko hiyo imeweza kuchangia pato la taifa kwa kiasi cha asilimia 11 tofauti na sekta zingine ambazo bado zina michango midogo katika pato la taifa mbali na ile ya utalii na madini.
Pia alisema hadi hivi sasa mifuko hiyo ina mtaji wa kiasi cha shilingi trilioni tano na milioni miambili na arobaini na mbili mtaji ambao unampa uhakika wa kuendelea kuwepo kwa mifuko hiyo na kamwe haiwezi kutetereka kwa namna yoyote hata kutokana na misukosuko mbalimbali inayoonekana.
Aliahidi serikali kurejesha madeni yote yanayodaiwa na mifuko hiyo kutokana na kazi mbalimbali za maendeleo zilizofanywa nayo ili kuwezesha mifuko hiyo kuendelea kukua na kutoa michango yake katika ukuaji wa uchumi na maendeleo ya nchi.
Naye mkurugenzi mkuu wa NSSF Ramadhan Dau alisema mwaka huu shirika lake limekaa na kutathimini changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii ya watanzania na kuja na kauli mbiu ya Hifadhi ya jamii na ujasiriamali yenye mikakati mbalimbali ya kuiondoa jamii dhidi ya changamoto hizo.
Alizitaja changamoto hizo kuwa ni ukosefu wa mikopo toka taasisi mbalimbali za kifedha kutokana na na kukosekana kwa mali za kuweka kama dhamana ambapo tayari shirika lake limeanza kutoa mikop yenye masharti na riba naafuu ya kiasi cha shilingi bilioni 55.6 ambapo watu 7000 mpaka sasa wameshanufaika.
Alitaja changamoto nyingine kuwa ni ukosefu wa ujuzi na nidhamu ya biashara kwa wajasiriamali kutokana na ukosefu wa elimu ambapo shirika lake tayari limeanza mazungumzo na taasisi za serikali ikiwemo Veta,Sido na nyinginezo ili kuweza kutoa mafunzo hayo kwa wajasiriamali hao.
Pia alitaja changamoto nyingine kuwa ni ukosefu wa uthubutu na woga kwa wajasiriamali katika kuanzisha biashara na kujiajiri ambapo katika mkutano huo wamewaalika watu mbalimbali ambao watatoa ushuhuda wao wa maisha yao ya kujiajiri kama chachu ya wajasiriamali kujiamini na kutuhubutu kufanya biashara.
Aliwataja watu waliowaalika kuwa ni pamoja na mfanyabiashara Patrick Mfugale anayemiliki kampuni za Pickkork,mfanyabiashara Salim Salum Bakhresa na mfanyabiashara maarufu afrika raia wa Nigeria Alhaj Aliko Dangote.
Pia alitaja mafanikio mbalimbali yaliyofikiwa na shirika lake hilo ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya wanachama,ujenzi wa majengo mbalimbali ya kitega uchumi ambapo pia aliweza kutaja matarajio yao mbalimbali ikiwemo ujenzi wa hospitali ya Apollo katika mji ya Kigamboni jijini Dar es salaam.
Pia alitaja mradi mwingine wanaotaraji kuufanya ni ule wa ujenzi wa kituo cha michezo,ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme wa megawati 1000 utakaochangia katika gridi ya taifa utakaofanyika katika mji wa Kibaha mkoani Pwani pamoja na ujenzi wa viwanda vya bidhaa zitakazotumia rasilimali mbalimbali zitokanazo na wanyama na mimea.

BUNGE LAAHIRISHWA KUFUATIA KIFO CHA MBUNGE WA UKONGA EUGEN MWAIPOSA

Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Ukonga marehemu Bi. Eugen Mwaiposa ambaye amefariki usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake mjini Dodoma. Taarifa za kifo chake zimetangazwa wakati bunge likiendelea na mjadala wa bajeti ya wizara ya afya hivyo kupelekea bunge hilo kuahirishwa hadi tarehe 4 mwezi huu.
1
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Mhe. Dkt Seif Rashid akiwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2015/2016 leo mjini Dodoma.
2
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge Mhe. Jenista Mhagama (mwenye nguo nyekundu) akimfariji Mwenyekiti wa Bunge Bi. Lediana Mng’ong’o mara baada ya bunge kuahirishwa kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Ukonga Bi. Eugen Mwaiposa. Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora Bi. Mary Nagu na kushoto ni wabunge James Mbatia na Goodluck Ole Medeye.
3
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Anjela Kairuki (kushoto) akitoka nje ya ukumbi wa bunge akiwa ameambatana na wabunge Bi. Mary Mwanjelwa na Rita Kabati baada ya bunge hilo kuahirishwa kufuatia kifo cha Mbunge wa Ukonga Bi. Eugen Mwaiposa.
4 5
Baadhi ya wabunge wakiwa kwenye hali ya simanzi baada ya kutangazwa kifo cha aliyekuwa mbunge wa Ukonga Bi. Eugen Mwaiposa kilichotokea usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake mjini Dodoma.
6

Kubomoka kwa tuta la Kijiji cha Jombwe Mkoa wa Kusini Pemba kunatokana na mabadiliko ya tabia nchi

Na Mwanaisha  Moh’d  Na Kijakazi Abdallah -Madownload (7)elezo Zanzibar
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema sababu ya kubomoka kwa tuta Kijiji cha Jombwe Mkoa wa Kusini Pemba ni kupanda kwa kina cha maji kinachotokana na athari za mabadiliko ya tabia ya Nchi na baadhi ya  Wananachi walivunja mawe yaliyokuweko kwenye tuta hilo.
Hayo yameelezwa huko Baraza la Wawakilishi Chukwani Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Fatma Abdulhabibu Fereji wakati alipokuwa akijibu suala  la Mh. Saleh Nasouro Juma (Jimbo la Wawi).
Alisema kuwa tuta hilo lipo Mkoa wa Kusini Pemba  Kijiji cha Jombwe na Sipwese Wananchi waliweza kulitumia tuta hilo ni kama njia ya kwenda Muambe pia wanafunzi walilitumia kwa ajili ya kwendea Skuli hiyo  mnamo mwaka 2010 tuta hilo lilianza kubomoka na kurahisisha njia ya maji ya chumvi  kupita na kuelekea  Kijiji  cha Sipwese hadi Chuo cha Mafunzo Kengeja.
Alifahamisha kuwa tuta hilo zaidi ya urefu wa mita 100  mbali ya kuwani kizuizi cha maji ya chumvi yanayoingia katika maeneo hayo  kwani  tuta hilo limetumika zaidi kama kivuko katika maeneo hayo.
Aidha alisema uingiaji wa maji ulianza mwaka 2002 wakati tuta hilo lilijengwa mwaka 2004  kutokana na kutumiwa vibaya halikuweza kuchukuwa muda mrecu likabomoka.
 Hata hivyo Serikali kwa sasa haijasaidia kujenga tuta hilo bali Mpango huo ndio utakao toa dira ya kushughulikia maeneo yalioingia maji ya chumvi ambayo yapo (145) Uguja na Pemba.
Sambamba na hayo Waziri huyo amesema juhudi za kupunguza maji ya chumvi kuelekea maeneo hayo Serikali ikishirikiana na wananchi kupitia Ushirika wa (Green Peace and Enveronmetal Conservation- GPEC) imeweza kupanda miti ikiwemo Mikoko,Mikandaa yenye urefu wa heka tatu za miti hiyo zimepandwa eneo hilo na imeweza kuendelea kustawi vizuuri kuhifadhi mazingira .

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA UONGOZI WA CHAMA CHA WAFUGAJI LEO.

lib1

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na wajumbe wa Kamati ya uongozi wa Chama cha Wafugaji Tanzania, wakati walipomtembelea Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo Juni 02,2015.
………………………………………………………………….
Na Mwandishi Maalum
Asema :Jitahidini kuepusha migogoro-Dkt. Bilal awaasa wafugaji .
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal amewataka wafugaji nchini kuhakikisha wanafuata sheria na kuachana na tabia ya kuchukua sheria mkononi ili kuhakikisha usalama wao na watu wanaopakana nao unakuwepo wakati wote. Mheshimiwa Makamu wa Rais amezungumza hayo leo Ikulu jijini Dar es Salaam baada ya kupokea ujumbe kutoka Chama cha Wafugaji Tanzania ulioongozwa na Mwernyekiti wao Ally Hamis Lumiye.
Makamu wa Rais alisema, si busara kwa wafugaji kujichukulia sheria mkononi na kwamba matatizo yanayowakabili wafugaji ni muhimu yakatatuliwa kwa kufuata sheria za nchi. “Jitahidini kuepusha migogoro hasa ile inayosababisha watu kupoteza maisha. Tusichukue sheria mkononi, sote lazima tuwe watii wa sheria,” Makamu wa Rais alisema.
Awali akizungumza kwa niaba ya Baraza la Wazee wa Chama cha Wafugaji Tanzania, Mwenyekiti wa Chama hicho Ally Hamis Lumiye alisema, chama cha wafugaji kwa sasa kinakabiliwa na changamopto kubwa hasa baada ya kuwepo mgawanyiko unaolenga kukimomonyoa chama hicho hasa kufuatia kujitokeza baadhi ya wafugaji kuamua kupora madaraka ya chama hicho na hivyo akaitaka serikali kuungana nao katika kuzima nguvu za waporaji hao.
“Mheshimiwa Makamu wa Rais leo hii tumekuja kwako kwa jambo moja nyeti. Wapo baadhi yetu wasiotaka kuona wafugaji tunajikomboa kwa kuwa na umoja kama huu. Wamefikia hatua ya kupora chama hiki na jitihada zetu za kutaka kuwadhibiti zinaonekana kuwa ngumu kufuatia baadhi ya viongozi wa serikali kuwatambua waporaji hao,” alisema mwenyekiti huyo.
Mheshimiwa Makamu wa Rais alisisitiza kuwa jambo la uporaji wa chama kamwe haliwezi kuachwa kimya kwa kuwa wafugaji na chama chao kimesajiliwa hivyo wafuate sheria hizo hizo ili kupata haki yao kama inaonekana kutokuwepo. Pili alisisitiza kuwa atalifanyia kazi suala hilo kupitia nafasi ziliozpo chini yake na kulipatia ufuimbuzi wa haraka.
“Mimi nami ni mfugaji, chama hiki ni muhimu kwa maslahi ya wafugaji. Kwa kuwa tuna katiba inayokiongoza na kwamba tunazo sheria ambazo zilifuatwa hadi kukipatia chama hiki usajili, basi hakuna haja ya kusikitika sana. Tutumie taratibu hizi hizi ili kuondokana na hao wanaotaka kupora mamlaka ya chama hiki,” alisema na kuongeza:
“Ni muhimu kiwepo chama imara kwa maslahi ya wafugaji wote. Chama hiki kinaweza kuwasaidia sana katika kukabiliana na changamoto mlizonazo maana kwa kuwa wamoja ni nguvu.”

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA MKURUGENZI WA SHIRIKA LA UTANGAZAJI TBC

li1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muuangano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Taifa, TBC, Clement Kiondo, wakati alipofika na ujumbe wake Ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Juni 2, 2015 kwa mazungumzo. Picha na OMR
li2
li3
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya Kombe kutoka kwa Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Taifa, TBC, Clement Mshana, ikiwa ni sehemu ya shukrani kutoka Kituo cha kuelelea watoto waishio katika mazingira magumu kilichopo Kigamboni, kinachosimamiwa na TBC. Mshana alifika na ujumbe wake Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar esSalaam, leo kwa ajili ya mazungumzo na kumkabidhi zawadi hizo. Picha na OMR
li4
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya Saa ya ukutani kutoka kwa Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Taifa, TBC, Clement Mshana, ikiwa ni sehemu ya shukrani baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini Kwa Makamu, Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Juni 2, 2015. Picha na OMR
li5
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya Khanga zenye Nembo ya TBC na zinazotangaza Utalii wa ndani  kutoka kwa Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Taifa, TBC, Clement Mshana, ikiwa ni sehemu ya shukrani baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini Kwa Makamu, Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Juni 2, 2015. Picha na OMR
li6
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya Tisheti  kutoka kwa Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Taifa, TBC, Clement Mshana, ikiwa ni sehemu ya shukrani baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini Kwa Makamu, Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Juni 2, 2015. Picha na OMR
li7
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,  Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Taifa, TBC, Clement Mshana, wakiwa katika picha ya pamoja ya kumbukumbi na baadhi ya wafanyakazi wa Kituo cha kulelea Watoto waishio katika mazingira magumu, kilichopo Kigamboni baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
li8
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib BIlal, akiagana na wajumbe walioongozana na Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Taifa, TBC, Clement Kiondo, Omar Rajab (kushoto) na Maico Rugendo, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo. Picha na OMR

Rais Dk.Shein aondoka Nchini leo

sh1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein wakisalimiana na Viongozi mbali mbali wa Serikali katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume leo wakati wakiondoka chini kwa ziara ya kikazi nchini ujerumani.[Picha na Ikulu.]
sh2
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiagana Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idii   katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume leo wakati akiondoka chini kwa ziara ya kikazi nchini ujerumani pamoja na Ujumbe wa Viongozi mbali mbali.[Picha na Ikulu.]

No comments:

Post a Comment