Christian Gaya-HakiPensheni Centre
Benki Kuu ya Tanzania inasema ya kuwa shilingi ya Tanzania ndiyo fedha ya pekee inayoruhusiwa kutumika nchini. Hivyo hakuna mtu au kampuni yoyote inayoruhusiwa kuikataa kwa...
malipo yoyote halali.Kufuatana na maelezo hayo yaliyotolewa na Benki Kuu inasema
ya kwamba Serikali ilishatoa tamko kuhusu katazo la matumizi ya fedha za kigeni
kwa wakaazi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kulipia bidhaa na huduma
nchini.
“Hata hivyo, katika siku za karibuni imebainika kuwepo kwa
ukiukwaji wa Tamko hilo. Hivyo, Benki Kuu inapenda kuukumbusha umma kwamba
maagizo yaliyotolewa hapo awali kuhusu matumizi ya fedha za kigeni,”maelezo
yanaeleza.
Maelezo haya yanasisitiza ya kuwa bei zote hapa nchini
zitangazwe kwa shilingi ya Tanzania. “Bei hizi zinajumuisha kodi za kupangisha
ardhi, nyumba na ofisi; gharama za elimu; huduma za afya, vifaa tiba na
vitendanishi; gharama za usafiri, lojistiki na bandari; vifaa vya kielektroniki
na huduma za mitandao ya mawasiliano.
Maelezo ya Benki Kuu hayo yanasisitiza ya kuwa bei ambazo
walengwa wake wakuu ni watalii au wateja wasio wakaazi zinaweza kutangazwa kwa
fedha za kigeni na malipo yake yanaweza kufanyika kwa fedha za kigeni. Bei hizi
zinajumuisha gharama za hoteli, usafiri, gharama za viwanja vya ndege na viza
kwa wageni, usafirishaji kwenda nchi za nje kupitia Tanzania na gharama za
mizigo bandarini.
“Walipaji wanaotumia fedha za kigeni watambuliwe kwa
vitambulisho vyao kama pasi za kusafiria na nyaraka za usajili kwa makampuni”
Gavana anasema.
Anasema, viwango vya kubadilisha fedha vitakavyotumika katika
kuweka bei hizo viwekwe wazi na visizidi vile vya soko. Ifahamike wazi kuwa ni
benki na maduka ya kubadilisha fedha za kigeni pekee yanayoruhusiwa kupanga
viwango vya kubadilisha fedha kutokana na ushindani katika soko la fedha za
kigeni.
“Mkaazi yeyote wa Tanzania anapaswa kufanya malipo kwa
kutumia shilingi ya Tanzania pekee na hivyo asilazimishwe kulipia bidhaa au
huduma yoyote hapa nchini kwa kutumia fedha za kigeni,” anasisitiza.
No comments:
Post a Comment