Pages

Saturday, February 11, 2023

WAZIRI NAPE AKUTANA NA MKURUGENZI WA KAMPUNI YA DAI KUTOKA MAREKANI

DODOMA

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Bw. Bill Garson, Mkurugenzi wa Miradi kutoka kampuni ya DAI Global ya Marekani katika ofisi za Bunge, jijini Dodoma, Feb. 10, 2023

Mazungumzo hayo yalilenga kuboresha mashirikiano katika maeneo ya Usalama Mtandao ikiwemo kujenga uelewa kwa wataalamu wa Taasisi za Umma na Jeshi la Polisi juu ya Usalama mtandaoni pamoja na kuendeleza kusambaa kwa Teknolojia ya 5G katika maeneo mbalimbali ya Tanzania. 





No comments:

Post a Comment