Pages

Saturday, February 11, 2023

TANZANIA YASHIRIKI MKUTANO WA 18 WA BARAZA LA MAWAZIRI LA KISEKTA LA UCHUKUZI, MAWASILIANO NA HALI YA HEWA WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

 

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Fatma M. Rajabu (kushoto) akifuatilia Mkutano wa 8 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Uchukuzi, Mawasiliano na Hali ya Hewa (TCM) unaoendelea jijini Bujumbura, Burundi
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Fatma M. Rajabu (kushoto) akifuatilia Mkutano wa 8 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Uchukuzi, Mawasiliano na Hali ya Hewa (TCM) unaoendelea jijini Bujumbura, Burundi. Kulia ni Balozi wa Tanzania nchini humo Mhe. Balozi Jilly Maleko
Mkutano wa 18 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Uchukuzi, Mawasiliano na Hali ya Hewa (TCM) ukiendelea jijini Bujumbura, Burundi 

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeshiriki Mkutano wa 18 wa Baraza la Mawaziri la

Kisekta la Uchukuzi, Mawasiliano na Hali ya Hewa (TCM) unaofanyika jijini Bujumbura, Burundi

Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo umeongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Fatma M. Rajabu
Mkutano huo ulianza tarehe 6 - 8 February 2023 kwa ngazi ya wataalamu waandamizi, ulifuatiwa na kikao cha ngazi ya makatibu wakuu uliofanyika tarehe 9 Februari 2023 na utakamilishwa kwa kuwakutanisha Mawaziri katika kikao kitakachofanyika tarehe 10 Februari 2023 jijini humo.
Mkutano wa ngazi ya Makatibu Wakuu umepokea na kujadili taarifa za utekelezaji wa Programu na Miradi; Maamuzi; na Maagizo ya Mikutano ya awali katika sekta za Mawasiliano; Hali ya Hewa na Miundombinu ya Uchukuzi inayojumuisha sekta za Barabara, Vituo vya Huduma kwa pamoja Mipakani (OSBP), Reli, Usafiri wa anga na Bandari kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mkutano huo pia ulipokea taarifa ya utekelezaji wa Maagizo 12 kati 34 ya mikutano ya awali ya Baraza la Mawaziri wa sekta husika yaliyokamilika na maagizo mengine yaliyosalia utekelezaji wake upo katika hatua mbalimbali.
Mkutano huo unahudhuriwa na washiriki kutoka nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kupitia sekta za ujenzi, uchukuzi, mawasiliano na fedha.

No comments:

Post a Comment