Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akikabidhi tuzo Mwenyekiti wa Kamati za Amani na Jumuiya ya Maridhiano Tanzania Sheikh Alhad Mussa Salum mara baada ya ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa la Maadili la Viongozi wa Dini wa Kamati za Amani na Jumuiya ya Maridhiano Tanzania linalofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam l
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiwa katika Picha ya pamoja na viongozi na wajumbe wa Kamati za Amani na Jumuiya ya Maridhiano Tanzania mara baada ya kufungua Kongamano la Kitaifa la Maadili la Viongozi wa Dini wa Kamati za Amani na Jumuiya ya Maridhiano Tanzania linalofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiwa katika Picha ya pamoja na mmoja wa washiriki (aliyekaa) wa Kongamano la Kitaifa la Maadili la Viongozi wa Dini wa Kamati za Amani na Jumuiya ya Maridhiano Tanzania linalofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiwaongoza kuimba wimbo wa Taifa viongozi na washiriki wa Kongamano la Kitaifa la Maadili la Viongozi wa Dini wa Kamati za Amani na Jumuiya ya Maridhiano Tanzania wakati wa Ufunguzi wa Kongamano hilo linalofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akihutubia viongozi na washiriki wa Kongamano la Kitaifa la Maadili la Viongozi wa Dini wa Kamati za Amani na Jumuiya ya Maridhiano Tanzania wakati wa Ufunguzi wa Kongamano hilo linalofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akisalimiana na Mwenyekiti wa Kamati za Amani na Jumuiya ya Maridhiano Tanzania Sheikh Alhad Mussa Salum wakati akiwasili katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam kufungua Kongamano la Kitaifa la Maadili la Viongozi wa Dini wa Kamati za Amani na Jumuiya ya Maridhiano Tanzania
……………………………..
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango ametoa wito kwa Viongozi wa dini zote, Viongozi wa Kimila na Wazee hapa nchini kusaidia kulea watoto na vijana kimaadili ili kuweka mustakabali wa taifa na
watu wake kwenye mikono salama.Makamu wa Rais amesema hayo wakati alipomwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika Ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa la Maadili la Viongozi wa Dini wa Kamati za Amani na Jumuiya ya Maridhiano Tanzania linalofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam. Ameongeza kwamba vijana wakifundishwa mila na desturi sahihi na kushika mafundisho ya dini, na wakawa na hofu ya Mwenyezi Mungu, maovu mengi yatapungua hapa nchini.
Makamu wa Rais amesema Serikali inatambua na kuthamini mchango wa Dini zote katika kujenga maadili mema ndani ya jamii ya watanzania. Amewasihi viongozi wa dini kuendelea kuliombea Taifa, viongozi na watumishi wa Serikali bila kuchoka ili kutekeleza vema mipango ya maendeleo ya nchi na watu wake.
Aidha Makamu wa Rais amekemea vikali ukatili na unyanyasaji dhidi ya watoto wa kike na kiume hapa nchini na kuviagiza vyombo vya dola kuongeza nguvu katika kupambana na ukatili huo. Aidha amewaasa walezi na wazazi kuweka mifumo imara ya ulinzi kwa watoto katika ngazi ya familia, mtaa, mashuleni, madrasa, vyuoni na sehemu nyingine ili kulinda haki na ustawi wa watoto na kuwaepusha na vitendo vya ukatili vinavyofanyika dhidi yao.
Pia amewakumbusha viongozi wa dini hapa nchini kukemea vitendo vya Rushwa na Ufisadi kupitia nyumba za ibada pamoja na kuwaelimisha wananchi madhara ya kutoa na kupokea rushwa na kushiriki kuhujumu mali za umma. Amesema Serikali itaendelea kuimarisha mifumo ya utoaji huduma ili kudhibiti vitendo vya rushwa na ufisadi pamoja na kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya mtu yeyote atakayejihusisha na vitendo hivi bila kujali cheo au nafasi yake katika jamii.
Halikadhalika Makamu wa Rais amewasihi wazazi na walezi kwa pamoja kushiriki katika mapambano ya kudhibiti matumizi ya dawa za kulevya kwa kutoa elimu kwa jamii pamoja na kutoa taarifa na kuwafichua wote wanajishughulisha na biashara hiyo haramu inayoathiri afya za vijana hapa nchini.
Katika hatua nyingine Makamu wa Rais amewaasa Viongozi wa dini kujiepusha na migogoro ndani ya Taasisi zao ambayo imekuwa ikisababishwa na uchu wa madaraka, ubinafsi, uchu wa fedha, matumizi mabaya ya mali za taasisi za dini na ukiukwaji wa katiba za taasisi za dini. Ametoa wito kwa viongozi hao wa dini kusuluhisha mapema migogoro ndani ya taasisi zao inapojitokeza kwa kuzingatia sheria, miongozo na taratibu zinazokubalika ili wawe mfano mzuri wa maadili kwa jamii ya watanzania.
Kwa Upande Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni amesema Wizara hiyo imeanzisha mfumo wa usajili na usimamizi wa jumuiya hpa nchini unaolenga kusaidia changamoto mbalimbali ambazo zilikua zikilalamikiwa ikiwemo ucheleweshaji wa usajili Jumuiya pamoja na kutopata taarifa mbalimbali. Amesema mfumo huo utaimarisha usalama nchini kwa kukabiliana na Jumuiya zinazotumia mgongo wa dini katika kufanya mambo ambayo ni kinyume na sheria za nchi.
Mwenyekiti wa Kamati za Amani na Jumuiya ya Maridhiano Tanzania Sheikh Alhad Mussa Salum amesema wataendelea kushirikiana na serikali katika kukabiliana na mmomonyoko wa maadili uliopo hapa nchini. Amesema Taifa lolote hubebwa na maadili kama heshima na utu wake katika uso wa dunia hivyo ni lazima viongozi wa dini kusimamia jambo hilo kadri serikali itakavyokuwa ikielekeza.
Awali akisoma Risala Katibu Mkuu, Jumuiya ya Maridhiano Tanzania Mchungaji Dkt. Israel Maasa amesema Jumuiya hiyo imeweza kufanya mambo mbalimbali ikiwemo kumaliza migogoro mbalimbali kati ya wakulima na wafugaji, kupambana na mila potofu pamoja na kupambana na ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na Watoto.
No comments:
Post a Comment