Na Pamela Mollel,Arusha
Taasisi ya Data science Afrika kwa kushirikina na chuo cha uhasibu Arusha (IAA) wametoa mafunzo ya sayansi ya data kwa lengo la kuwezesha wanafunzi, watafiti na wakufunzi kutatua matatizo kupitia teknolojia.
Mafunzo hayo yaliyofanyika kwa muda wa wiki moja, yamekutanisha watu kutoka mataifa mbalimbali kama Uganda, Kenya, Sudani, Nigeria, Malawi na wenyeji Tanzania.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo Dkt.Ciira Maina mwanzilishi wa taasisi ya Data science Afrika alisema tangu waanze mwaka 2015 wameweza kutatua changamoto za kilimo, Afya na mazingira kupitia teknolojia.
"Mpaka hivi sasa taasisi yetu inawanachama zaidi ya 600 Afrika nzima, hivyo tunahamasisha kila mmoja kujiunga ili tuweze kutatua matatizo yetu waafrika kwani sisi pekee ndio tuna yajua" alieleza.
Waziri wa nchi ofisi ya Rais serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Jamal Kassim Ali alisema mwelekeo wa nchi hivi sasa ni kufika uchumi wa juu wa kati na malengo hayo hayawezi kufikiwa kama teknolojia ya habari mawasiliano haitatiliwa mkazo.
"Ili tupige hatua kwenye masuala ya kilimo na afya ni vyema masuala ya "artificial intelligence" yakachukuliwa kwa uzito kwani ndio yanatatua matatizo na kuboresha huduma" aliongeza waziri Jamal
M/kiti wa bodi ya wakurugenzi chuoni hapo Dkt. Mwamini Tulli alisema mafunzo hayo yatawezesha wakufunzi wao katika maendeleo ya nyanja ya habari mawasiliano, hasa matumizi ya data.
"Tunaona ni kama tumependelewa kwa wakufunzi wetu kupata nafasi hii kwani nirahisi wakufunzi hawa kuandaa mitaala itakayo wajenga baadaye wanafunzi kutoka ngazi ya chini" alifafanua.
No comments:
Post a Comment